Mbowe vs Chifupa + CHADEMA vs Family Business

Status
Not open for further replies.
Mkandara Heshima na kwako pia,

Kwenye sera ya majimbo kutakuwa na serekali za majimbo na wilaya, sioni ni kwa jinsi gani tutatua miji mingine na kutengeneza mmoja. Kwa sababu ya mgawanyo muafaka wa mapato ya rasiliamli na ushiriki wa wananchi, ambapo watakuwa na nguvu ya kuwajibisha viongozi wanaofanya vibaya miji mingi itasonga zaidi.

Nisichokubaliana na wewe ni kwamba Tz ilikuwa na Ukabila, Tukirejea mfano wako wa Afrika kusuni, weupe waliwabagua weusi. Je hapa Tz, kabla ya Nyerere kubadili jina toka Jimbo mpaka mkoa(maana aleendeleza mfumo ule ule wa wakoloni) nani alikuwa anabagua mwingine? Kabila gani lilikuwa linabaguliwa na jingine?

Je Nyerere angeibuka na sera ya majimbo kubalisha mfumo wa kichifu ukabila ungekuwepo Tanzania?

Mimi siamini wala sishawishiki kwamba Tanzania ilikuwa na ukabila, ila wapo watu wachache wabifsi wenye kupenda ukabila.

Nyerere alitaka Nchi iwe na muelekeo mmoja, mfumo mmoja wa utawala. watu wenye ukabila wasingekubali kirahisi kupoteza mamlaka yao na mamlaka yao kupewa watu wengine! Wangepinga na wafuasi wao wangepinga sana.Tungesikia machifu kazaa wamewekwa kizuizini, kwa maana makabila yaliendelea kuwepo na machifu bado waliendelea kuheshimika sana kwenye jamii zao. Nashindawa kuona ukabila uliokuwepo Tanzania, ambao ilikuja kuondolewa na MaDC na maRC!

Pia zilikuwepo fursa nyingi za ukabila kuchomoza wakati ule, kulikuwa na fursa ya vyama vingi,kabla ya kufutwa, vyama vingapi vilikuwa na mguso wa makabila? Kwanini hawa machifu waliondekeza ukabila wasingejiunga au kuanzisha vyama vya kikabila vikitetea maslahi ya makabila yao? Mbona ilikuwa raisi hivyo kuondoa ukabila?

Mchanganyiko baina ya makabila utakayoletwa na mgawanyo mzuri wa mapato ya rasilimali ndio suluhisho la "hofu" ya "ukabila".

Hulka pia huchangia watu kutengeneza sera na mifumo ya kibaguzi. Makaburu walimuona mtu mweusi ni kiumbe dhaifu na anapaswa kuwatumikia kwa sulubu ndio maana wakabuni mfumo wa kikandamizaji.Mifumo hubuniwa na watu kwa maksudio fulani, kama una hulka ya ubinafsi utajenga mfumo wa kufanikisha lengo.Ndio maana Serekali inakuwa ngumu kubadili katiba kwa maana wanafaidikia na mfumo mbovu wa sasa.

Hoja ya kusema Mzaramo hataweza kuwa Gavana wa kanda ya ziwa haina mantiki, kwani leo hii Mzaramo anaweza kugombea na kushinda u meya au ubunge Bariadi? Je kwanini Halmashauri ya zisitunge sheria ndogo za kibaguzi/kikabila! Mbona kuna mianya mingi tu ya kuweza kuendeleza ukabila katika mfumo wa sasa? Watanzania wangekuwa wakabila wasingeshindwa kutumia mianya hii,ukabila si tatizo la msingi Tanzania na mabo ya msingi yataposhugulikiwa litajimaliza.

Naendelea kusisitiza kuwa umoja wa watanzania upo hatarini kila siku, ubinafisi na ufisadi unalishambilia vibaya taifa kila siku.
 
Eric Ongara,

Labda sasa nibadilishe jinsi ya kutoa majibu yangu inaweza kukusaidia zaidi kuelewa. issue by issue na tafadhali jaribu kutenganisha maswala tunalojadili hapa.
Kwenye sera ya majimbo kutakuwa na serekali za majimbo na wilaya, sioni ni kwa jinsi gani tutatua miji mingine na kutengeneza mmoja. Kwa sababu ya mgawanyo muafaka wa mapato ya rasiliamli na ushiriki wa wananchi, ambapo watakuwa na nguvu ya kuwajibisha viongozi wanaofanya vibaya miji mingi itasonga zaidi.

Sijakataa kabisa kuwepo na mgao muafaka wa mapato.. swala ni mapato ya kiuchumi ama mapato ya rasilimali?
Nakwama kuelewa mgao wa mapato ya rasilimali - hapa inaonyesha wazi kwamba swala hili sio uzalishaji Kiuchumi) ila kugombania kile mwenyezi mungu alichotupa kwa majimbo yake.

Ndio nikasema ni sawa na kugawana mirathi kila mtoto atafaidikika na mali aliyoacha marehemu baba yao kwa sababu - wajomba (viongozi) ndio wanaofaidika. Why, msichukue tu mali toka kwa wajomba na kuiweka mikononi mwa watoto! Je, ni lazima kuigawa na kama ni kuigawa kumbukeni kuna watoto wengine wameachiwa mirathi ya banda la kuku (mikoa maskini).

Upooo?
Pili, ikiwa bado mnasisitiza bado ugawanaji wa mapato ya maliasili zetu, Je mkoa wa Arusha ambao sasa hivi ni tajiri mkubwa hawawezi kujiona kuwa wanabeba mikoa mingine kwa maliasili zao?..Leo hii tunaona baadhi ya mikoa haifaidiki na maliasili zao ndio sababu yenu kuweka majimbo ati hawafaidiki kwa sababu nchi ni kubwa, well hapa unaposema nchi ni kubwa ina maana kuna mikoa haina kitu inapewa mali hizi lakini hili sio kweli kabisa. Mikoa yenye maliasili haifaidiki kwa sababu wajomba (viongozi) ndio wezi wa mali zetu. maliasili hazimsaidii Mtanzania yeyote ila baadhi ya watu walioshika madaraka na matajiri wenye uwezo wa kutoa RUSHWA.

Hata kama dhana yenu ni ugawaji wa maliasili kwa sababu nchi ni kubwa, kesho bado baadhi ya mikoa hiyohiyo (yenye maliasili) pamoja na faida kuwepo bado wataona hakuna sababu ya kugawia mikoa mingine maskini chini ya mfumo wa majimbo ambayo hai contribute sawa na wao ktk jimbo moja.

Kumbuka tu jimbo ni mfumo mpya watu wataanza ku-question nini hasa lengo la mfumo huu na huwezi kuondoa kirahisi akilini mwao mipaka ya mikoa yao. Ikija ku hit akilini kuwa sababu ya majimbo ni uchumi basi kila mtu atavuta kwake kwanza.. Arusha watasema ingekuwa bado Arusha ni mkoa, tungekuwa mbali sana, na how come Moshi imekuwa NewYork badala ya Arusha?

Ndio maana nikashauri economic zones ambayo itawasaidia wananchi kuendesha miradi kila mkoa kulingana na utajiri, vipaji asili na mazingira yake ktk uzalishaji wa biashara.

Mikoa yenye mifugo itapewa wataalam na mashamba ya mifugo pia kuanzisha legal union na viwanda (wawekeshaji) vinavyohusiana na malighafi inayozalishwa sehemu hizo. Wafugaji vilevile, wakulima wa mazao pia watashughulikiwa kulingana na zao bora linaloweza kuzalishwa sehemu hiyo. Masoko yatatafutwa kitaifa ama kimkoa inategemea na soko la finished product yenyewe.

Kwa hiyo dawa ya kiuchumi bado itakuwa sawa kabisa na ile ya Chadema isipokuwa ukubwa wa pill ndio tofauti yenyewe.
Brother, the same leaders ambao leo wameuza nchi kwa asilimia 10 wanaweza kuwa hao hao Magavana na hata mkija mfukuza huyu mtu tayari kesha vuta share zake New York exchange kupitia Barricks - You can do nothing!.. kesha invest huko.

After 5 years hakuchaguliwa hawezi kujali kama wasivyojali akina Mkapa. Hapa zinatakiwa policy nzito kabisa ambazo hazitoi mwanya kwa viongozi kutoa uamuzi wa uwekezaji bila bunge iwe leo ktk mfumo huu ama mfumo wowote ule. Mikapa haiwezi kuzuia rushwa ila policy (sheria) ndio chombo pekee kinachoweza ku deal na real problem ya UWAJIBIKAJI sio mikapa, mamlaka ya mbunge, gavana wala RC ama DC. Hili ni swala zima peke yake nje ya kila kitu.

Kinachotakiwa ni kuwepo kwa mfumo bora wa hizi contracts (Contract zitazamwe Upya), kisha taifa letu liweze kuwa na share kubwa badala ya kutegemea ruzuku. Ruzuku iwe inatolewa kwa mkoa/wilaya yenye maliasili hizo. Ile share ya taifa itatumika kujenga nchi nzima, iwe ktk elimu, Afya ama ustawi wa jamii kwa uwazi.

Nisichokubaliana na wewe ni kwamba Tz ilikuwa na Ukabila, Tukirejea mfano wako wa Afrika kusuni, weupe waliwabagua weusi. Je hapa Tz, kabla ya Nyerere kubadili jina toka Jimbo mpaka mkoa(maana aleendeleza mfumo ule ule wa wakoloni) nani alikuwa anabagua mwingine? Kabila gani lilikuwa linabaguliwa na jingine?

Nitarudia kusema kuwa South Afrika ilikuwa kukuonyesha source ya Ukabila kuwa sio hulka ila ni mfumo. mfumo wa Apartheid ndicho chanzo cha ubaguzi SA..hao hao wazungu wapo USA na Europe lakini hawana nafasi ya kuyafanya hayo kama mfumo hauruhusu. Hapa nikimaanisha Ubaguzi wa rangi na sio ubaguzi wa kikabila. Ukabila ni moja kati ya Ubaguzi kama vile dini, rangi, gender n.k .

Sasa wewe mwenzangu hapo juu amechanganya Ubaguzi wa rangi na kuuliza swali ukitumia ubaguzi wa kikabila ili kupata jawabu la Ukabila... Haiwezekani ni sawa na kuuliza kuwa if 2+2=4, how come 2 mangos plus 2 oranges isn't 4 oranges pamoja na kwamba yote haya ni matunda.
Nitarudia kusema kuwa mfumo wa Nyerere ndio uliondoa cheche za Ukabila nchini.. na nilisema pia Ukabila ni sawa na Volcano iliyolala.

Hivi sasa mwenyewe unaona kuwa Udini nchini hakuna lakini brother usije danganywa. Udini ni valcano iliyolala bila mfumo bora udini unaweza kufumka vibaya vibaya na hakuna wa kuuzuia.

Kama tanzania ingeendelea kuwa ktk majimbo lakini mfumo wa RC na DC bado umetekelezwa nadhani matokeo yasingekuwa tofauti sana na leo..(UKABILA), ila kumbuka hapa tunachotaka kuondoa ni RC na hao DC. trust me Eric machief hawakuwa na power kabisa kama hawana madaraka, swala la kuheshimika ni nje kabisa ya kuongoza. Akina Warioba, Salim, Mwakawago, Fundikira, wote hawa bado wanaheshimika kama viongozi wetu waliopita lakini leo hii hawana nguvu ya kusema kitu kikasikiwa. Once Ur out of power ndio imetoka hiyo!.

Machief wote wakubwa walitupwa balozi za nje. Marealle alijitahidi sana wakati tukigombea uhuru hata kwenda Uingereza kuomba Uhuru wa JIMBO lake... sijui kama unafahamu hili, lakini nguvu ya kura hakuwa nayo. Na leo hii bado anaheshimika lakini hana power kabisa. marealle anaweza kutiwa ndani tena Keko akalazwa na walalahoi lakini Dito kapewa chumba chake mwenyewe.

Wale machief waliokubali kujiunga na TANU walipewa madaraka tofauti kabisa na Uchief wa majimbo ama mikoa yao, tena sio nafasi ya juu ktk Uongozi wa kitaifa.

Eric,
Hulka haibadiliki hata siku moja.. kila binadamu ni mbinafsi kwa hali fulani. Hata sisi waafrika tunapenda sana tuwe juu..na kama mfumo ni mbovu basi ubaguzi utakuwepo, ndio hiyo mifano ya Rwanda, sijui wewe unataka kunambia nani pale mwenye hulka ya Ukabila au ndio watu woteee!, kenya sijui nani wenye hulka hiyo.

Na ikiwa kweli kaburu anayo hulka ya Ubaguzi mbona toka mfumo huu wa utawala uwekwe kashindwa kuendeleza apartheid?.. hapa ina maana pamoja na kuwa kila mtu hupenda kujinufaisha yeye mfumo wowote ule ni lazima uwe na kinga ya kuzuia nature hii ya binadamu...KUJIBAGUA.

Hata kuzaliwa kwa hii EAC umeona matatizo yanajitokeza kwa sababu kila mtu anataka kuvuta kwake na ni mfumo bora peke yake unaoweza kuleta amani ktk hii EAC....
tena nakuombeni sana Chadema kuna watu ndani ya chama chenu ni magugu yaliyooteshwa ambayo ni hatari kubwa sana ya udini na Ukabila. I came to learn that. J.J Mnyika, Freeman, mwanasiasa ni watu fresh ile mbaya ila kuna hawa walokole fake watakuja haribu kabisa malengo yenu.. labda ndio hulka hiyo unayozungumzia.

Mkiwapa Uongozi hawa watu tumekwisha, iwe majimbo, mikoa ama wilaya... tumekwishaaa! Hawa hawataiba mali za umma tu bali watatugawa vibaya sana.. hawa watu wamo humu humu JF.

Anyway, swala la mzaramo kugombea Ugavana lazima ulitazame kwa mapana yake. nakuomba soma vizuri maelezo yangu kisha chambua kama karanga (Bi. Kaloli alisema)
Leo hii mzaramo hawezi kushinda Bariadi kweli lakini haina mgogoro kwa sababu Msukuma wa bariadi ndiye mshindi na siku zote ataendelea kuwa mshindi kuwakilisha wasukuma wa Bariadi... up to now hatuna shida kabisa na wala mimi sijali kwani mgeni siku zote ndiye hujibadilisha kulingana na mazingira aliyoyakuta.

Katika mfumo wa majimbo, hapa kila JIMBO litakuwa na makabila makubwa sio chini ya matatu. Now, matokeo yake ni Mzaramo hawezi kushinda, Mhaya hawezi na hata Mjita hawezi kushinda kwa sababu Msukuma atatawala JIMBO zima nje ya mikapa yake kutokana na hesabu kubwa ya wasukuma ktk jimbo...trust me, hakuna msukuma atakaye mchagua Mhaya ama Mhaya kumchagua msukuma kuongoza mwinziwe.. hii ndio hulka ya binadamu.

Baada ya muda watu hawa wanaoshindwa kila mara watachoka kuona msukuma tu ndiye anawaongoza nenda rudi pamoja na kwamba sheria inasema wengi wape (demokrasia).

Je, kuna mbinu gani Chadema mnayo kuhakikisha kuwepo kwa usawa ktk chaguzi hizo?.. ubaya wako hutajibu ila utageuza kuwa swali jingine.

Eric, nadhani maelezo yangu wazi brother kinachoshindikana kueleweka nini hasa!
 
Eric Ongara,

Bado upoooo!...

Summary yangu:-

Nyerere alitupa chanjo ya dawa kukinga - Ukabila. Unapokinga kitu ina maana maradhi hayo yapo lakini hayajamuathiri mtu...

Leo hii, Chadema mnatupa dawa ya gonjwa hili la umaskini - Uchumi.,

Sasa naomba tuzungumzie tu hizi dawa zenu na ukubwa wa hiyo pill yenyewe kuliko kuzunguka huku na huko, tunapoteza mwelekeo!
 
Ndugu Mkandara Nipo

Summary yangu: Majimbo ni muhimu kwa mtazamo kwamba:
1. Itachochea ushiriki na uwezo wa wananchi kuwawajibishi viongozi wao
2. Mgawanyo muafaka wa mapato ya rasilimali(serekali kuu itachukua sehemu na kugawanya sehemu nyingime na maeneo ya vipaumbele kwa nchi)
3.Itapunguza ukiritimba wa kutugemea maamuzi yote yatoke Dar
4. Itaondoa viongozi wa kuteuliwa wasio na uwezo wa maono ya kimaendeleo katika maeneo husika
5. Itapunguza utitiri wa viongozi kwenye ngazi ya mkoa na wilaya
6. Itaimarisha umoja wa kitaifa baina watu kutokana na muingiliano wa makabila utakao jitokeza
7. Utaliokoa taifa kutokuingia kwenye gharama nyingi za kiutawala kutokana na ongezeko la wilaya la kila siku kutokana na mfumo wa sasa kushindwa
8. Tutapata mfumo unaoendana na siasa ya vyama vyingi(rejea Halmashauri zilizo chini ya vyama vya upinzani vikiwa na mkuu wa wilaya anaesimamia maslahi ya CCM)
9.utachochea ushindani wa kimaendeleo baina ya serekali za wilaya na majimbo
10. Itapoanaua uwanja wa mawazo, taifa litanufaika mijadala chanya na mawazo mbadala yatakayo jitokeza kutokana na ongezeko la ushiriki wa wananchi na kuwa na tawala za kidemokrasia badala ya tawala zilizo simikwa toka Dar

Sawa tujadile juu ya maeneo haya kwanza kwa maana suala la ukabila yaelekea tunakubaliana katika kutokukubaliana! Tuweke hoja ya ukabila kiporo na pengine watachangia zaidi badae sasa tujikite kwenye mantiki ya sera ya majimbo. Moja baada ya nyingine

Tupo pamoja
 
Eric Ongara,
Wala sikuchukua muda kusoma maelezo yako na kugundua kuwa bado HUJIBU SWALI langu ila unajaribu kuuza na kuijenga dhana ya imani ktk majimbo.

Toka nyuma kila ulosema hapa nimekupa solution zake kutokana na mfumo uliopo sasa hivi.

1. KATIBA.
Marekebisho ya katiba kulingana na Mwanasiasa ni dawa tosha kabisa ambayo itajibu maswali yako mengi sana na hasa pale ukiwaondoa viongozi wateule hao ma RC na DC na kukabidhi madaraka yao kwa Wabunge waliochaguliwa wakishilikiana na Halmashauri za miji

(waliochaguliwa)utakuwa umeondoa matatizo yote ya Utawala na kasoro za serikali kuu ziliyopo.

2. kuwepo kwa serikali za majimbo bado hakuondoi serikali kuu na utitiri wa viongozi wake bali utaongeza hesabu ya viongozi kwa ujumla.
a) Serikali kuu bado itakuwa na wizara zake makao makuu iwe Dar ama Dodoma na mikoa/wilaya zitawakilishwa ktk jimbo. Bado mikoa na wilaya zitakuwa na idara zote za serikali ya jimbo. Hivyo kutakuwepo na muundo mpya wa wizara kuu za kila jimbo.

Na Gavana atakuwa rais mdogo ambaye sii muhimu kama katiba imebadilika kuondoa nguvu ya rais na kukabidhiwa wabunge wawakilishi wa wananchi.

b) Kuundwa kwa majimbo, watumishi wa serikali hizi watakuwa na mipaka ya kuhudumia jimbo hali nchi yetu ina wataalam wachache. Lugha ipi itatumika ktk mgogoro kati ya waziri wa maliasili wa serikali kuu na yule wa jimbo ambaye katoa maamuzi ya uwekezaji. Mathlan...jimbo la ziwa wanataka kutaifisha machimbo yote ya dhahabu ama mradi wa umeme hali serikali kuu imekubali mkataba wa wawekeshaji! - Who has the upper hand?

c) Mipaka ya jimbo itaathiri pia viongozi, sidhani kama Gavana wa ziwa aliyeshindwa anaweza kusimama ktk uchaguzi baadaye jimbo la kaskazini. Na Je, hawa Magavana wagombea watateuliwa na vyama vyao toka kila Mkoa/Wilaya ama mkoa mmoja unaweza kutoa wagombea finalist? -kumbuka ile side effect!

3. Uchumi ni somo langu na kila napotazama kuwa maliasili ziwe ktk majimbo yake hii ina maana tunagawana mirathi.. kubali usikubali.
Matatizo haya yanatukuta ktk muungano wetu na Zanzibar kwa sababu kuna uvutano wa nani mwenye mali kati ya serikali ya visiwani na serikali kuu.

Matatizo ya mgao wa mapato unatokana na kuwepo na mipaka ya ardhi na sii kweli kuwa serikali ya Zanzibar akiwa ndio mwenye sauti ya mali visiwani basi wananchi wake watafaidika na mapato..

WEZI wa mali ya Zanzibar ni viongozi hawa wajomba, iwe wanatoka bara ama visiwani kwa hiyo kumkabidhi mali baba mdogo ama mjomba hakuwezi kuleta tofauti yeyote ikiwa wote hawa wana tamaa ya utajiri wako. Ni sawa kabisa na kumhamisha mla rushwa toka wizara moja kuhamia wizara nyingine.

4. Kwa mfano huo huo wa Zanzibar na hata leo EAC utakuta muungano wa mikoa utakuwa na matatizo ktk uchaguzi wa viongozi. Nani ana -qualify kuwa Gavana?.. leo hii tunayaona Zanzibar wanapochagua viongozi wao na hata sasa hivi kasheshe kubwa lipo ktk nani atakuwa rais wa jumuiya hii!

Je, kweli wewe unaamini rais akiwa M7 itakubalika kama ulivyosema hapo juu nambari 6?.. Je watanzania watakubali ikiwa kila mwaka rais atakuwa Mganda kwa sababu ya wingi wa wapiga kura toka Uganda?

Afadhali EAC tunaweza kuteua viongozi na bado ikakubalika lakini hatuwezi kufanya hivyo kwa magavana kwa sababu tunataka viongozi waliochaguliwa na wananchi. Mikoa na makabila yenye Population kubwa ndiyo yatakayo chukua nafasi kila uchaguzi.

Nitarudia kusema hakuna Mhaya atakaye mpigia kura msukuma kushika Ugavana wala msukuma kumchagua Mhaya.. Huu ni ukweli usioweza kuepukwa na balaa litakalo zuka hapo - Mungu pekee ndiye anayefahamu.

Problem kubwa pia ya Majimbo, hai-deal na real issue hapa kwani face zitakazo shika madaraka ni zile zile tunazozichagua kila siku kwani hawa watu wanakumbatiwa bado na vyama na ndio pekee tutakao pewa kuchagua. Richmonduli atakuwa kanda ya juu, Mwaki nani vile kanda ya na Ngosha Kinehe - ziwa.

Kwa sababu hawa wote wanaoiba leo hii ni watu ambao wamepita katika kila chaguzi za majimbo yao. DEAL na RUSHWA kwanza kabla ya ya mapendekezo mengine ya mfumo wa mipaka kitaifa.

Nitamalizia kwa kuuliza tena Chadema wana mbinu gani kuhakikisha yote hayo hapo juu hayawezi tokea!
 
Mkandara, hii mada ipo!
Haijaondolewa. Sema iko ukurasa wa pili. Ukiiihcangia inarudi tena kuwa top!
 
Shukran sana mzee mwenzangu... na samahani sana unajua uzee tena!

Sikuona kitu kikaanza kubabaika maanake Eric na J.J Mnyika nawasubiri kwa hamu, ndio chama pekee kilichokubali kujadili maswala nyeti ambayo hawana ulazima wa kuyajadili na mtu yeyote zaidi ya wananchama wake....
 
Jana Jumapili nilifanya Mahojiano na Mheshimiwa Mhonga Said wa CHADEMA.Amejibu baadhi ya maswali yenu ya jinsi gani walivyochaguliwa kwenye hivyo viti maalum vya wanawake.

Mnaweza kuja kumsikiliza hapa:

www.RadioButiama.com
 
Wale wanaofuatilia mjadala wa majimbo nadhani habari hii ina mchango pia...

Kwa mfano, suala la mgawanyo wa gharama za kuendesha serikali kuu na serikali za majimbo utakuwaje etc etc.

Pia wataalam wetu nchini wa masuala ya fedha, menejimenti nk wanasemaje?

Gharama za kuendesha Muungano ni kubwa - Tume

Na Dunstan Bahai

Tume ya pamoja ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, imebaini kuwepo kwa gharama kubwa za uendeshaji wa Serikali ya Jamhuri.

Kauli hiyo ilitolewa jana na Katibu wa Tume hiyo, Bw. Khamis Ali Ame, mara baada ya ufunguzi wa warsha ya siku nne ya tume hiyo, inayoendelea jijini Dar es Salaam.

Warsha hiyo iliyofunguliwa na Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Abdisalaam Issa Khatibu, inaendeshwa na wataalamu kutoka Chuo Kikuu cha Georgia, nchini Marekani.

Bw. Ame alisema, gharama hizo ambazo zimekuwa zikiongezeka na kupungua, ongezeko lake linatokana na kuwepo kwa taasisi zinazofanya kazi za muungano na zile ambazo si za muungano, lakini zinafanya kazi za Muungano.

Alisema, tangu kuundwa kwa tume hiyo mwaka 2003, katika utafiti wao wamegundua mambo mbalimbali yenye dosari katika makusanyo na mgao wa mapato.

Katibu huyo wa Tume ya Pamoja, alisema tangu kuanza kwa tume hiyo, wameshindwa kujua gharama halisi za matumizi ya undeshaji wa Serikali ya Muungano kutokana na muingiliano wa kazi wa taasisi hizo.

Kuhusu malalamiko ya upande mmoja wa Muungano kufaidika kuliko upande mwingine, alisema katika muda mfupi wa kuwepo kwa tume hiyo, wametoa mapendekezo mbalimbali kwa serikali ambayo yamekwishaanza kufanyiwa kazi.
Hata hivyo, alikataa kutaja mapendekezo hayo kwa madai kwamba, sheria za tume hiyo haziruhusu hadi idhini maalum.

Kuhusu mafunzo hayo, alisema wataalamu kutoka Marekani, wameitwa ili kutoa elimu kutokana na uzoefu wao katika nchi zenye Muungano kama wa Tanzania jinsi zinavyoshirikiana katika masuala ya kifedha.

Kwa mujibu wa Katibu huyo, baada ya warsha hiyo, watakuwa na upeo mkubwa kuhusu uendeshwaji wa masuala ya fedha na baadaye watatoa mapendekezo yao kwa serikali.

Naibu Waziri wa Fedha, Bw. Khatibu, akifungua warsha hiyo alisema, tume imefanya kazi nzuri tangu kuundwa kwake na kwamba, Agosti, mwaka jana, ilimaliza utafiti wake na kukabidhi mapendekezo yao serikalini.

Alisema, lengo la utafiti huo ni kubaini dosari na matatizo mbalimbali na kisha kuzishauri serikali zote mbili za Muungano na ile ya Mapinduzi Zanzibar kuhusu masuala ya fedha.

Bw. Khatibu alisema, serikali imeleta wataalamu hao ili kufundisha uzoefu wao wa masuala ya fedha katika serikali za muungano na kwamba warsha hiyo pia itatoa fursa kwa wadau kujadili mambo mbalimbali yaliyoandaliwa kwenye warsha hiyo.

``Warsha hii ndiyo itapanua wigo kwa wataalamu wetu kuelewa uendeshaji wa serikali ya Muungano na ile ya Mapinduzi katika masuala ya kifedha, hali ambayo inaweza kupunguza malalamiko ya upande mmoja kupendelewa,`` alisema Naibu Waziri.

Aidha, alisema itasaidia pia kuweza kuangalia kila upande kuwa unapata mapato kwa mujibu wa mipango iliyoandaliwa.

Tume ya Pamoja ya Fedha ya Jamhuri ya Muungano, ni chombo cha pamoja cha fedha cha Tanzania Bara na Visiwani. Chombo hiki kipo kwa mujibu wa Katiba.

SOURCE: Nipashe Januari 30, 2007
 
Eric Ongara,
Wala sikuchukua muda kusoma maelezo yako na kugundua kuwa bado HUJIBU SWALI langu ila unajaribu kuuza na kuijenga dhana ya imani ktk majimbo.
Toka nyuma kila ulosema hapa nimekupa solution zake kutokana na mfumo uliopo sasa hivi.
1. KATIBA.
Marekebisho ya katiba kulingana na Mwanasiasa ni dawa tosha kabisa ambayo itajibu maswali yako mengi sana na hasa pale ukiwaondoa viongozi wateule hao ma RC na DC na kukabidhi madaraka yao kwa Wabunge waliochaguliwa wakishilikiana na Halmashauri za miji (waliochaguliwa)utakuwa umeondoa matatizo yote ya Utawala na kasoro za serikali kuu ziliyopo.

Nakubaliana na umuhimu wa kuwa na Katiba mpya. Hapa tupo pamoja kabisa. Hata CHADEMA inaponadi sera ya majimbo huwa inasema jambo la kwanza ni kubadili katiba kabla ya kuipeleka sera ya majimbo kwa wananchi. Ni kweli kwamba katiba yetu ina mapungufu mengi na inahitaji mabadiliko hili ni dhahiri.

Ni kweli baada ya mabadiliko ya katiba, tutakuwa tumeondoa viongozi wa kuteuliwa. Hivyo kwenye ngazi ya wilaya kiongozi mkuu kiutawala atakuwa meya. Wabunge na Madiwani wataendelea na kazi ya ya asali ya kusimamia utendaji wa viongozi kuanzia wilaya, jimbo na taifa.

Tofauti na wilaya, mkoa hakuna viongozi wa kuchaguliwa, tukiondoa mkuu wa mkoa na kumuweka wa kuchaguliwa na kusema tuunde wizara katika ngazi ya mkoa, tutakuwa na uongozi mpana sana kwa mikoa 26 ya nchi yetu. Hapa kuna mambo mawili ama tuwe na serekali ya za wilaya na Taifa pekee au tuwe na serekali katika ngazi za wilaya, jimbo na Taifa. Jimbo linakuja kuziba pengo litakaloachwa na mikoa baada ya kuondoa viongozi wa kuteuliwa. Jimbo linakuja kuunganisha mikoa na kubeba majukumu yatakayopunguzwa toka serekali kuu.


2. kuwepo kwa serikali za majimbo bado hakuondoi serikali kuu na utitiri wa viongozi wake bali utaongeza hesabu ya viongozi kwa ujumla.

Utititiri utapungua, na si utitiri pekee, kuna utitiri na mgongano wa kimajukumu baina ya viongozi wa kuchaguliwa na wale wa kuteuliwa. Rejea mchango wangu wa siku za nyuma juu ya uongozi katika ngazi ya wilaya. Hapa tutakuwa tumeondoa kabisa idadi ya viongozi na kubakiza wa kuchaguliwa pekee.

a) Serikali kuu bado itakuwa na wizara zake makao makuu iwe Dar ama Dodoma na mikoa/wilaya zitawakilishwa ktk jimbo. Bado mikoa na wilaya zitakuwa na idara zote za serikali ya jimbo. Hivyo kutakuwepo na muundo mpya wa wizara kuu za kila jimbo. Na Gavana atakuwa rais mdogo ambaye sii muhimu kama katiba imebadilika kuondoa nguvu ya rais na kukabidhiwa wabunge wawakilishi wa wananchi.

Kumbuka kuwa, kwenye sera ya majimbo, utawala katika ngazi ya mkoa hautakuwepo. Tutakuwa na serekali katika ngazi za Wilaya, Jimbo na serekali kuu. Jimbo linachukua nafasi ya mikoa.

Pia kutakuwa na mgawanyo wa kimajukumu baina ya serekali katika ngazi hizi tatu, hivyo hakutakuwa na sababu ya kuwa na wizara hizo hizo katika ngazi ya serekali kuu na jimbo.

Wabunge wanasimamia viongozi, hawawezi kubeba majukumu/mamlaka tutayapunguza toka kwa rais. Watakaopekewa majukumu/mamlaka ni magavana na mameya.


b) Kuundwa kwa majimbo, watumishi wa serikali hizi watakuwa na mipaka ya kuhudumia jimbo hali nchi yetu ina wataalam wachache. Lugha ipi itatumika ktk mgogoro kati ya waziri wa maliasili wa serikali kuu na yule wa jimbo ambaye katoa maamuzi ya uwekezaji. Mathlan...jimbo la ziwa wanataka kutaifisha machimbo yote ya dhahabu ama mradi wa umeme hali serikali kuu imekubali mkataba wa wawekeshaji! - Who has the upper hand?

Si kweli nchi yetu ina wataalam wachache. Wataalam wapo wengi sana na michango yao mara nyingi inapuuzwa.

Hakuta kuwa na mgogoro, lazima pande zote mbili zikubalianae, hapa ndio tutaongeza ushiriki wa wananchi kuwa na maamuzi juu ya rasilimali zao. Si vyema watu wa serekali kuu ndio wakawa na maamuzi pekee juu ya rasilimali za nchi yetu. Kumekuwa na hoja za mara kwa mara za kushirikishi wanachi katika ngzi za chini kushiriki katika maamuzi ya rasilimali zao. Hivyo utemi wa serekali kuu kukurupuka kufanya maamuzi pasipo kushirikisha wananchi/serekali za ngazi ya china hakutakuwepo kutakoma. Tunapunguza matatizo ya watu wachache kuwa na maamuzi juu ya rasiliamali za nchi. Sote ni wahanga wa matatizo haya.


c) Mipaka ya jimbo itaathiri pia viongozi, sidhani kama Gavana wa ziwa aliyeshindwa anaweza kusimama ktk uchaguzi baadaye jimbo la kaskazini. Na Je, hawa Magavana wagombea watateuliwa na vyama vyao toka kila Mkoa/Wilaya ama mkoa mmoja unaweza kutoa wagombea finalist? -kumbuka ile side effect!

Hapa unaongelea ukabila au ukaaazi? Mfano: Hata John Mnyika asingeweza kugombea na kutetemesha kama angombea kwao Mwanza kama alivyuofanya ubungo. Lipo suala la ukaazi, umekaa eneo fulani, mahusiano yako na jamii ya eneo husika na pengine mtandao. Mnyika pamoja na kuwa Msukuma asingefanya vizuri mwanza kama alivyofanya ubungo.

Wagombea watogombea kama raia, wananchi ndio watakaoamua
.


3. Uchumi ni somo langu na kila napotazama kuwa maliasili ziwe ktk majimbo yake hii ina maana tunagawana mirathi.. kubali usikubali.
Matatizo haya yanatukuta ktk muungano wetu na Zanzibar kwa sababu kuna uvutano wa nani mwenye mali kati ya serikali ya visiwani na serikali kuu. Matatizo ya mgao wa mapato unatokana na kuwepo na mipaka ya ardhi na sii kweli kuwa serikali ya Zanzibar akiwa ndio mwenye sauti ya mali visiwani basi wananchi wake watafaidika na mapato.. WEZI wa mali ya Zanzibar ni viongozi hawa wajomba, iwe wanatoka bara ama visiwani kwa hiyo kumkabidhi mali baba mdogo ama mjomba hakuwezi kuleta tofauti yeyote ikiwa wote hawa wana tamaa ya utajiri wako. Ni sawa kabisa na kumhamisha mla rushwa toka wizara moja kuhamia wizara nyingine.

Hapa tuanongelea mabadiliko ya mfumo, uwezo wa wananchi kuwawajibisha viongozi hata kabla ya viongozi(power of recall). Viongozi wa sasa mafisadi wanalewa na udaifu wa kimfumo/kikatiba. Mfumo unawapendelea wao, tume iko mikononi mwao na wanatumia rasilimali za dola kujirudisha madarakani. Mfumo wa kidemokrasia(kama sera ya majimbo) ndio suluhisho la kupamba na viongozi dhaifu na mafisadi.

Naamini wananchi wakiwa na satu ya kutosha kuwajibisha viongozi wao, rasilimali zinaweza kabisa kunufaisha wanachi wa maeneo husika.


4. Kwa mfano huo huo wa Zanzibar na hata leo EAC utakuta muungano wa mikoa utakuwa na matatizo ktk uchaguzi wa viongozi. Nani ana -qualify kuwa Gavana?.. leo hii tunayaona Zanzibar wanapochagua viongozi wao na hata sasa hivi kasheshe kubwa lipo ktk nani atakuwa rais wa jumuiya hii!..
Je, kweli wewe unaamini rais akiwa M7 itakubalika kama ulivyosema hapo juu nambari 6?.. Je watanzania watakubali ikiwa kila mwaka rais atakuwa Mganda kwa sababu ya wingi wa wapiga kura toka Uganda?... Afadhali EAC tunaweza kuteua viongozi na bado ikakubalika lakini hatuwezi kufanya hivyo kwa magavana kwa sababu tunataka viongozi waliochaguliwa na wananchi. Mikoa na makabila yenye Population kubwa ndiyo yatakayo chukua nafasi kila uchaguzi..

Sina imani kabisa na Museveni, Kibaki na Kikwete, wote kwa ujumla wao. Na wala sikubaliani na namna wanavyoendesha zoezi zima la shirikisho la Afrika mashariki. Wananchi wamezarauliwa kwa kiasi kikubwa. Kama wananci watakuwa bado wanapiga kura kwa mtazamo wa kinchi na sio hoja hakuna haja ya kuwa na shirikisho, muda wake utakuwa bado.

Watanzania hawana hali mbaya kiasi hicho ya ukabila. Kama ndivyo kwenye uchaguzi wa uraisi tungeone mgawanyo wa kura kwa wale wagombea 10 kwa mtazamo wa kimkoa au kikanda. Kwa Kilimajaro kwa mfano Kikwete alipaswa apitwe na Mbowe, Mrema, Mvungi n.k


Nitarudia kusema hakuna Mhaya atakaye mpigia kura msukuma kushika Ugavana wala msukuma kumchagua Mhaya.. Huu ni ukweli usioweza kuepukwa na balaa litakalo zuka hapo - Mungu pekee ndiye anayefahamu.

Kuna mchanganyiko mkubwa baina ya makabila utakaoletwa na majimbo. Hili ni jambo la kufikirika zaidi.Watanzania wamegawanyika kikabila, kidini, kivyama, kimkoa na kadahilika, migawanyiko hii inamalizana yenyewe kwa yenyewe hivyo hakuna udini wala ukabila! Na pia kama hali itakuwa hivyo kwa kiasi kidigo, iko mikoa ya akiba kama Mara ambayo itaweza kudilute matatizo kama hayo.

Problem kubwa pia ya Majimbo, hai-deal na real issue hapa kwani face zitakazo shika madaraka ni zile zile tunazozichagua kila siku kwani hawa watu wanakumbatiwa bado na vyama na ndio pekee tutakao pewa kuchagua. Richmonduli atakuwa kanda ya juu, Mwaki nani vile kanda ya na Ngosha Kinehe - ziwa. Kwa sababu hawa wote wanaoiba leo hii ni watu ambao wamepita katika kila chaguzi za majimbo yao. DEAL na RUSHWA kwanza kabla ya ya mapendekezo mengine ya mfumo wa mipaka kitaifa.

kama nilivyo eleza hapo juu, tutaondokana na viongozi mafisadi kwa kuwa na mfumo unampa sauti mwananchi. Nguvu ya umma ndio suluhisho.
Nitamalizia kwa kuuliza tena Chadema wana mbinu gani kuhakikisha yote hayo hapo juu hayawezi tokea!

Kama nilivyo anisha hapo juu, matatizo ya msingi yakipatiwa ufumbuzi, matatizo madogo yanajiondo yenyewe.
 
Eric Ongara,
Ningependa kufahamu kama haya majibu yako yametoka kwa niaba ya Chadema ama unazungumza mawazo yako mwenyewe.

Utanisamehe kwa kuuliza hivyo maanake navyoona mimi tunazunguka mbuyu mara 18 sasa hivi na bado hujanieleza KINGA.

Kwa mukhtasari nitaweza hapa tena maelezo yangu kwa ufupi ambavyo sii kawaida yangu.

1. Ikiwa Meya ndiye atakuwa kiongozi mkuu wa kiutawala, huyu atakuwa anawakilisha nani tofauti na RC ama DC kama sii kuchaguliwa ama kuteuliwa. Ikiwa ni mbunge anayekwenda bungeni kuwakilisha wananchi wake kwa nini kumtumia mtu ambaye hutoa ahadi hewa (Meya)akitegemea kile watakachomkatia!.

Meya siku zote ni watu wanaotoa ahadi hewa kwa sababu Halmashauri za miji hutegemea fungu toka serikalini kujiendesha..Je, Meya ndiye atakuwa mwakilishi wa vikao vya bunge la jimbo chini ya Gavana!

Hadi hapa sielewi uhusiano wa sheria za kijimbo kati ya Gavana, Meya au Mbunge.

2. Sikusema tuunde wizara ktk ngazi ya mikoa.. mfumo huo haupo hata sasa hivi. Kuna wizara 26 na hizi wizara hazipo mikoani ila idara za wizara hizo chini ya RC na DC. Kwa hiyo umeongeza hoja ambayo haipo, haikuwepo wala hatuihitaji kabisa.

Nitafafanua nilichosema.
Kwa mfano, tuseme mkoa wa Mwanza leo hii una idara 120 za serikali ktk wilaya 5 toka wizara 26 za serikali kuu. Chini ya majimbo bado wilaya hizo 5 zitahitaji idara hizo hizo 120 kufanya kazi zake iwe chini ya meya au nani. walioondoka hapa ni RC, DC na neno mkoa kwani Mwanza mjini pia ni wilaya yenye idara za serikali.

kwa upana wa mtazamo wa majimbo kitaifa utakuta kumezuka zaidi wizara 26 ktk Majimbo 4, a total of 104 Ministries maanake kila jimbo litajitegemea na kuna wizara nyingine 26 za kitaifa, jumla Tanzania itakuwa na wizara 130.

Hii ni hesabu ya haraka haraka, unless unataka kusema hapatakuwepo na wizara ktk majimbo, hapa bado kabisa hatujazungumzia swala la ukubwa wa bunge za kila jimbo ambazo zitapanga budget ya serikali zao. Kama TZ leo ina wabunge 200 basi with majimbo tutegemee wabunge mara 4 na jingine la kitaifa.

3. Umezungumzia habari ya J.J Mnyika kugombea Ubungo hali ukijua ya kwamba Ubungo ni wilaya iliyojaa wahamiaji. Asilimia 90 ya wapiga kura ni wahamiaji tofauti kabisa na mikoani. Na wala siwezi kuamini kama J.J Mnyika hataweza kufanya vizuri kama akigombea kwao na mshindani toka makabila nyingine.

JK kamshinda Freeman au Mrema ktk uchaguzi wa kitaifa! tofauti kabisa kama JK angeshindana na Mbowe kwa nafasi ya kuongoza Kilimanjaro iliyotenganishwa. Na kwa sababu hiyo hiyo siamini kama JK anaweza kumshinda hata karume ktk uchaguzi wa Zanzibar ama Karume kumshinda Kabouru ktk uchaguzi wa kuongoza bara. Yote hii inatokana na kuwepo mipaka.

Kofi aliweza kushinda UN lakini huyo huyo Kofi hawezi kushinda uchaguzi wa aina yeyote unaohusu maslahi ya Notrh America tu!

4. Wataalam niliozungumzia sio wataalam wa maoni na michango ya mawazo, laa hasha bali wataalam wa utendaji kazi. Kwa mfano leo hii Tanzania ina madaktari wa cancer mangapi?....tena basi hapo hujaondoa wale ambao wanafanya kazi ktk mashirika ya watu binafsi.

Hao wachache waliobaki serikalini ndio madaktari wasiokuwa na border leo wakienda kila kona ama kupokea wagonjwa toka kila kona. Tukisha weka majimbo hakuna jimbo litakalo kubali kupokea wagonjwa wengi toka jimbo jingine lenye uhaba wa madaktari na pengine watu kutokuwa na uwezo kumudu private hospital. Kumbuka kuna mashindano ya kiuchumi kama ulivyosema.

Kuna kila possibility ktk nchi maskini kuanguka ktk mfumo ambao umefanikiwa nchi za Ulaya kwani Ulaya asilimia kubwa ya wananchi wake wana uwezo, hawana kikorosho wala makabila na hesabu ya wataalam wao ni kubwa. Huu ndio muhimu na msisitizo wa kuwepo elimu mbele... wataalam ktk utendaji kazi.

Nitaendelea siku nyingine kama kuna swala bandika!... usiku mkubwa tena.
 
Ndugu Mkandara,

Ninayoandika si Msimamo au Majibu ya CHADEMA. Naandika ninayoamini na kuelewa juu ya sera murua ya Majimbo.

1.Meya ni kiongozi, sijaelewa ahadi hewa una maanisha nini: Ahadi hewa inaweza kutolewa na Meya, Mbunge na hata raisi. Suala ni kudhibiti viongozi wanoatoa ahadi hewa. Katiba mpya inaweza kuweka kipengele cha wananchi kuwajibisha viongozi hawa(Power of recall).

Meya ndio kiongozi mkuu wa kiutawala, mbunge hawezi kuchukua nafasi ya kuitawala yeye kama walivyo madiwani wataendelea na kazi yao ya asili.Meya anachaguliwa na wananchi ajenda zake zitakubaliwa na wananchi, na atakuwa na rasilimali za kuweza kutekeleza ahadi zake, wawakilishi wanakuja kuangalia anavyofanya kazi(Checks and Balance).

2. Hesabu zako juu ya wizara zina hitilafu. Sera ya majimbo itabainisha vizuri mgawanyo wa majukumu baina serekali hizi tatu. Hivyo haitegemewi majimbo kwa mfano, kuwa na wizara ya mambo ya nje na ushirikiano wa kimataifa! Yapo majakumu ya serekali kuu amabayo hatakuwepo kwenye serekali za majimbo hali kadhalika yapo majukumu ya serekali za majimbo ambayo hayatukuwepo kwenye serekali za wilaya. Kinachosisitizwa ni mgawanyo wa majukumu na Kimamlaka koandokana na utaratibu mbovu wa sasa wa kurundika majukumu na mamlaka sehemu moja.

Wabunge wataweza kuhudhuria mabunge ya majimbo na yale ya serekali kuu kama wanavyofanya sasa kuhudhuria mabaraza ya madiwani(Kumbuka mbunge ni diwani pia).

3. Mipaka sijui unaifikiriaje, sasa hivi mbona tuna mipaka ya mikoa na wilaya na haina athati hizo? Haizui maingiliano ya watu ndivyo itakavyo kuwa mipaka ya majimbo. Unapovuka Mkoa wa Dar-es-salaam kwenda Pwani hukakuguliwi wala kudaiwa passport una swaga tu, kitambulisho pekee kitachokuonyesha upo mkoa mwingine pengine ni mabango, hupotezi utu wako wala haki zako unapovuko eneo moja la kiutawala kwenda jingine na ndivyo itakavyokuwa kwenye majimbo, hatutengenezi nchi zingine ndani ya nchi moja, sijui unaelewaje juu ya mipaka ya utawala, au unachanganya na mipaka biana ya nchi na nchi?


4. Hoja ya wataalam ina mambo mengi, wataalam wapo ila wanakatishwa tamaa na maslahi duni, wanakimbia nchi kusaka maslahi na sehemu ambapo michango na mawazo yao itathaminiwa. Na bado tunaendelea kutengeneza wataalam kila uchao.

Mfano wako wa kwamba hakuna jimbo litakalopokea wagonjwa toka jimbo jingine haina mshiko. Bado una tasfsiri ya mipaka ya kinchi badala ya kiutawala! Leo ukiwa mkazi wa Dar na ukasafiri kwenda mkoa wa mbeya kwa kazi na bahati mbaya ukaugua huko hospitali ya rufaa ya mbeya haiwezi kukutaa kwa madai wewe ni mgonjwa wa Dar! Ndivyo itakavyokuwa kwenye hospitali za Kiwilaya, kijimbo na kitaifa!
 
Ni sawa na kusema simba na fisi nani ana nguvu zaidi kwa vile wote ni wanyama wa porini, wanakula nyama na wanaweza kutoa makelele; halafu ukatumia kigezo cha kwamba kwa vile fisi anaweza kutoa makelele mengi inawezekana yeye akawa ni zaidi.................................

Pamoja na mimi kuwa ninavyo vidigrii kadhaa tena vya nguvu kweli kweli, huwa ninasema kuwa uongozi wa kisiasa siyo wa madigrii. Kinachotakiwa kwa kiongozi wa kisiasa ni kujua vizuri shida za jamii na jinsi ya kuzipatia ufumbuzi ili kuleta maisha mazuri kwa jamii hiyo. Kiongozi mzuri atafanya kazi ya kuwapanga wataalamu mablimbali ili kutatua matatizo ya jamii, siyo kwamba yeye ndiyo atakayetatua matatizo hayo kwa mkono wake.

Machifu wetu kama akina Mkwawa, Milambo na wengineo hawakuwa na digrii yoyote lakini tunajuwa jinsi walivyopigania wananchi wao.

Ninapoona wanasiasa wetu wanajipachika madigrii lukuki wakati wakiwa kwenye madaraka ya kisiasa na kutaka watambuliwa kwa madigrii hayo huwa ninakereka sana kwa sababu inaonyesha jinsi gani wasivyojiamini na wasivyojua wajibu wao kama wanasiasa. Ni kutokana na kutojua wajibu wao, huwa wanaishia kufanya kazi ambazo zilitakiwa zifanywe na wataalamu lakini wao wanasiasa wanajipachika utaalamu huo na matokeo yake ndiyo tunayoona hivi sasa. Tanzania sasa hivi inaweza kuwa inaongoza kwa kuwa na wansiasa wengi madokta wakiwa wamepta udokta wao madarakaini na wote wanataka watambulike kwa udakitari wao huo: Dr. Malecela, Dr. Mzindakaya, Dr. Nchimbi, Dr. Kamala, Dr. Mary Nagu, Dr. Masaburi, Dr. Makongoro Mahanga, Dr. George Nangale, Dr. Waryoba, na wengine wengi wenye masters lukuki zote zilizopatikana kimkatomkato. Mmoja wao ana masters 2 na bachelors 2 zote zikiwa zimepatikana kwa mpigo katika kipindi cha miaka mitatu tu wakati akiwa ni ofisa wa kibalozi.

Ukiangalia katika nchi za wenzetu, utashangaa kuwa viongozi kama John Major hakuwa msomi na wala hakujipachika madigrii baada ya kuwa madarakani. Vile vile madokta halisi kama akina Paul Wolfowitz, Condoleeza Rice, Madeline Albright, Gordon Brown, Newt Gingrich, na marehemu Paul Wellstone hawatumii title za udakitari wao katika shughuli za kisiasa ingawa wote wameingia kwenye siasa wakiwa na Ph.D. na wengi wao waliwahi kuwa maprofesa kwenye vyuo vikuu. Wanajali zaidi utendaji wa kisiasa kuliko sifa za kuwa wasomi.

SIJAONA ULICHOONGEA NDUGU YANGU, UMEJITAHIDI SANA KUONGEA LAKINI KUMBUKA TANZANIA NI NCHI KAMA ILIVYO MAREKANI AU UINGEREZA. NAONA UNAANGALIA KWA JICHO LA USUDA TU ILA KUMBUKA KWAMBA NDIYO STYLE ZA WANASIASA WETU. MAANA NAONA MH.MBOWE NAYE ANAKAMUA MBILI KWAMMPIGO. MOJA TOKA MAREKANI NA NYENGINE UINGERENZA. BRAVO MZEE MBOWE LAKINI MNATAKIWA MBADILIKE.

NIKUELEKEZE KITU, WENGI WA CCM NI WATU AMBAO WAMEPEWA ZA HESHIMA KUTOKANA NA JUHUDI ZAO KATIKA MAENEO FULANI. INAWEZEKANA IKAWA KWAMBA WAMEGUSHI BAADHI YAO LAKINI ASIKWAMBIE MTU CCM NI BABA NA KWAMBA WEWE NA HUYO MREMA KAMA UNAMUAMINI NA DEGREE YAKE YA UCHAGUZI ALIYOPEWA KIRARACHA NAONA MLALE MBELE.

NAPENDA KUTOA HOJA...

PIA SIJAWAHI ONA MTU UNAYEONGEA OVYO KAMA WEWE.POLE SANA
 
Eric Ongara,

Nashukuru kwamba umenifahamisha vizuri kuhusu maelezo unayoyatoa.

Kinachoshangaza zaidi ni pale mnapotumia vigezo vya mfumo huu uliopo kupitisha mfumo wa majimbo -, hali ni mfumo huu huu mnaoupiga vita ubadilishwe.

Kwa mfano, kila mara umeuliza mbona leo hakuna Ukabila..Mnyika kaweza kugombea Ubungo na sasa umerudi ukiuliza mbona leo kuna mipaka ya mikoa na wilaya!

Labda nirudie kusema kuwa hiyo ndiyo CHANJO ya Nyerere aliyotupa na ndio maana unaona mafanikio ktk sehemu hizo. Mfumo wa Nyerere alikuwa na mazuri yake na ajabu unayatumia hayo mazuri kunipa sababu za kuwepo mabadiriko.

Mipaka ya mikoa na wilaya zimetuwezesha kuona viongozi wengi, wataalam hata hao RC na DC wakihamishwa kila kona ya nchi jambo ambalo haliwezi kufanyika ktk majimbo. Hii tofauti moja tu tosha kabisa kukupa picha kile nachozungumzia. Sasa basi mbali na mazuri ya mfumo huu wa sasa, athari za kutokuwepo mikapa hiyo ya kiutawala tumeziona ktk Uchumi.

Kwa kupitia utafiti tumegundua kuwa hawa watu RC na DC ni wateule wa rais ambao hawawakilishi wananchi. Hii sababu nimekubaliana nayo kuwa waondolewe lakini tunapotafuta fidia ya nafasi hizo lazima tuangalie pale makosa yalipofanyika - kuongoza ktk maswala ya UCHUMI.

Binafsi sikatai wala kupinga uwezo wa hawa wachaguliwa ikiwa kuna aina fulani ya kuwa monitor. City council ndio sehemu za mission town miji yote Tanzania. Ma meya ndio wauza deal zote ndogo ndogo (ukoko) miji yote na hasa wakati huu wa milango wazi. Mwenyewe umeyasikia ya Coco beach, Wa machinga na kadhalika na ndio watoa vibali vya ujenzi na kubomoa. Imagine huyu mtu anakuwa na uwezo zaidi kuwa chief exerctive administrator wa serikali za wilaya!

Sina la kusema kuongezea isipokuwa kuwapa ma meya nafasi kubwa zaidi za huduma za miji ambazo wameshindwa ni sawa na kuondoa bango la Dc mezani na kuweka linalosema Meya wakati mtu ni yuleyule.

Ndio maana kila kukicha nawaomba mnipe KINGA zenu, sioni kitu hadi sasa hivi.

Kuhusu utitiri wa viongozi zile wizara 26 zilikuwa ni mfano tu. nachojaribu kusema ni kuwa kila jimbo litakuwa na wizara zake (executive council) iwe 10 ama 20 hizi zote ni ongezeko la viongozi. Kinachonishangaza pia ni hapo unaposema kuwa mbunge atakuwa akishiriki ktk bunge la jimbo na lile la serikali kuu.

Hii ndio kwanza naisikia Eric, na nimeshindwa kabisa kuelewa kwa nini huyu mbunge awe sehemu mbili ambazo zinaweza kuwa moja tu kuondoa mkorogano wa vikao.
Huyu mbunge wa Ukerewe mwakilishi ktk jimbo na serikali kuu ambaye pia ni diwani mbona kazii!..sijawahi kuona wala kusikia mfumo huu.

Hata hivyo Eric, kutakuwepo na wizara nyingi sana TZ , kwa uchache kabisa tuseme 100.

Sasa nakuuliza wewe mbona JK kaongeza wizara kufikia 26 tu watu wote tumepiga kelele hali JK ametoa madai sawa na ya kwenu?.. je, ni kweli ufanisi wa kazi umeongezeka! HAPANA!
Kuhusu mipaka ndugu yangu, naishi nchi yenye mipaka ndani na sheria za kila jimbo ni tofauti hasa ktk maswala ya ustawi wa jamii zao. Hayo ya kusafiri kwenda Mbeya yapo hivyo kwa sababu leo hii hakuna majimbo ndugu Eric. Majimbo ni mipaka ya kiutawala tofauti na mikoa ambayo ni administration regions!

Ukisha weka majimbo swala hili halitatazamika hivyo tena! Hospital zinajengwa kwa kodi ya watu wa jimbo fulani, wameondoa baadhi ya kodi, wameweka bimaza afya leo utoke huko na Ukimwi wako mjazane ktk jimbo letu hali hamkulipa kodi?... mshikaji sidhani unless unataka kusema itakuwepo sheria kuhusu sehemu zote za huduma kuwa chini ya serikali kuu. na ukisha fanya hivyo nini basi maana ya kuwepo majimbo ikiwa vita ya kupunguza umaskini bado itakuwa chini ya serikali kuu. hayo mapato mtakayo pewa mtayatumia kwa kitu gani?
 
Haya Ndugu Wapenzi Wapenda Maendeleo, Narudi Tena Sasa Katika Mjadala Wa Kiutendaji....ongara Nambie Kijana Wa Tyva?
 
Eric, Ongara,

Je, Chadema mnapokea ushauri toka nje jinsi ya kutayarisha muundo wa kiutawala NJE ya haya Majimbo ama ndio kitabu kilisha fungwa!
 
Ndugu Mkandara,
nafahamu kuwa CHADEMA ni chama mbadala, kinapokea maoni, utafanya vyema ukiyawasilisha

Nipo, nitajibu mchango wako wa mwisho
 
Eric, Ongara,

Sio maneno mangi nayotaka kusema ila naomba uwakilishe hoja hii kuwa MAJIMBO ni swala la kitaifa ktk katiba ya taifa. Sidhani kama ni jambo zuri chama cha kisiasa kuweka ama kutunga mfumo wa kiutawala ktk serikali inaweza kuwa pendekezo isiyojumuisha mrengo wa chama.

Ni sawa na pale vyama vya upinzani vinapotoa ahadi ya kuundwa kwa serikali TATU badala ya hizi tulizokuwa nazo kwa sababu ambazo wananchi wanaelewa kuwa zinatokana na Utendaji kazi mbaya wa viongozi toka chama tawala.

Chadema, TLP NCCR-mageuzi ama CUF zinaweza kuwapa haki Wazanzibar kiasi kwamba mfumo huu uliopo ukafanya kazi vizuri kwa sababu kosa ni Utawala wa chama CCM sio mipaka ya nchi zetu. Na ikiwa tutabadilisha mipaka yetu bado haitasaidia kitu kwa sababu wanaowafunga Zanzibar ni Wazanzibar wenyewe kwa kutumia jina la CCM.

Marekebisho yanatakiwa ndani ya viongozi wenyewe kupewa mipaka ya madaraka yao na sio mikapa ya nchi kurekebisha Utawala mbovu.
Unapobadilisha mipaka ya nchi kiutawala ina maana kuwa kosa ni mipaka sio viongozi wa CCM jambo ambalo kwa wenye upeo mkubwa watasema oooh! kwa hiyo viongozi wa CCM ni wazuri ila problem ipo ktk mikapa ya kiutawala.

Haya yote mawili ni maswala nyeti ya kitaifa (KATIBA) ambayo yanatakiwa kuwashirikisha wananchi wote au vyama vyote, jambo ambalo sioni faida yake kusimama ndani ya malengo ya chama. Na kuna uwezekano mkubwa wa maswala haya kugongana huko mbeleni ikiwa kutakuwepo na serikali ya majimbo na pia serikali tatu.

Ni bora mara Elfu kutazama viongozi wetu kiutawala kwa sababu tunaweza kubeba uzito wa makosa yake kuliko makosa yatakayo tokana na mikapa ya kiutawala.
 
Status
Not open for further replies.

Similar Discussions

Back
Top Bottom