Mbowe, Slaa na Zitto tuvusheni 2015 salama

Mbowe, Slaa na Zitto tuvusheni 2015 salama

Ukiangalia kwa makini siasa za Tz tangu kuanzishwa kwa vyama vingi utagundua kuwa ccm kina fikra za kuliongoza taifa hili milele na baadhi ya viongozi waandamizi wa ccm na serikali wamejitokeza hadharan kutangaza kuwa ccm itatawla milele. Kwa kufanikisha kusudio hilo ccm kimekuwa kikitumia pesa nyingi kuvuruga vyama vya upinzani vinavyojitokeza kuwa na nguvu kwa kupandikiza vibaraka. walifanikiwa kwa nccr-magauzi, na baadaye wakafanikiwa kuivuruga TLP , wakafanikiwa kwa cuf baada ya kufunga nao ndoa ya mkeka. mwanzoni mwa mwaka huu ccm kupitia wasira na wenzake wakajitokeza na kuutangazia umma wa Tanzania kuwa watahakikisha chadema kinakufa mwaka huu. Baada ya kauli hiyo tukasikia mengi mara chadema ni magaidi, wakarudia nyimbo za ukanda, udini, ukabila vyote hivyo vikashindikana na hii ni kutokana na uongozi imara na thabiti wa viongozi wa cdm chini ya Mbowe na Dr slaa.Sasa wamekuja na staili ya kutaka kuwapangia wacdm safu za uongozi ndan ya chama na wanacdm wasipokuwa makini na kuingia ktk mkenge huu watakivuruga chama.katika azma yao ya kuua cdm mwaka huu utaona gazeti la ccm uhuru linakuja na vichwa vya habari kama mwisho wa cdm umetimia pamoja na magazeti mengi corrupted na kulipa watu kukichafua chama kupitia mitandao ya kijamii. Lkn chini ya uongozi wa mbowe na Dr slaa hili nalo litapita.

Natoa rai kwa wanacdm kuwa makini ili lengo la kusimika misingi nchi nzima lisiharibiwe na propaganda chafu za maccm.Na yale yaliyotolewa na mwigamba ambayo ni ya msingi yafanyiwe kazi ili tusitoe loop hole kwa wanaotumiwa , wasipate pa kuzungumzia. kwa kufanya hivyo cdm iataendelea kuimalika cku hata siku.

Nakubaliana kwa kiasi kikubwa na post hii mkuu
 
kuna post Ngongo jana alitoa soma hapa chini
Hii inanikumbusha enzi za NCCR
Mageuzi ilianza hivi hivi.
Ni wazi kabisa CCM haijazoea
kukabiliana na upinzani mkubwa /
mkali kwa mwongo mmoja(vipindi
viwili vya uchaguzi).Mwaka 1995
NCCR Mageuzi waliisumbua sana CCM
walichofanya ni kuisambaratisha
kabla ya uchaguzi wa mwaka
2000.Mwaka 2010 Dr Slaa wa CDM
aliwasumbua sana wasingependa
kuingia uchaguzi wa mwaka 2015 huku
CDM wakizidi kujitanua kila uchao
wakijua wazi watakuwa na mgombea
mpya asikuwa na nguvu za kidola
ambaye anaweza kupambana na mgombea
mwenye rekodi nzuri na mwenye mtaji
mkubwa wa kura za mwaka 2010.CCM
wanajua wazi baada ya uchaguzi mkuu
uliopita CDM haikulala bali
walianzisha programs maalum M4C
ambayo ilihakikisha inawafikia
wapiga kura wengi kabla ya uchaguzi
mkuu ujao.
CDM wakiweza kushinda mtihani ulio
mbele yao ni wazi uchaguzi mkuu
ujao itabidi CCM wajiandae kwa
kumweka mgombea mwenye rekodi nzuri
ya uadilifu.CCM isingependa
kuchagua mgombea mzuri kwasababu ya
kitisho cha CDM kuzidi kujiongezea
umaharufu.Warasimu wa CCM
wangependa kumchagua mgombea
atakayelinda uchafu (maslahi) wao
ili linaweza kuepukwa iwapo CDM
itasambaratishwa.
Kwa afya na ustawi wa taifa letu
tusikubali CDM ikasambaratishwa
itatuchukua miaka mingine 15 kujenga
upinzani mwingine wenye nguvu huku
tukiwaachia walafi/wezi wakitafuna
na kutuibia rasilimali
zetu.Tusisahau Mzee Mkapa
alivyofanya baada ya kusambaratika
kwa NCCR Mageuzi.Mabenk yaliuzwa
kwa bei ya kutupa,madini,mashirika
ya umma,EPA,Meremeta zote
zilisababishwa na ukosefu wa
upinzani wa maana ulioanza
kujengeka enzi hizo.

Maneno mazito sana haya
 
Last edited by a moderator:
Na huwezi kubadilisha rubani wakati ndege ndio kwanza inapaa;;;;»»»»»»»»»»»>>>>>>
 
Na huwezi kubadilisha rubani wakati ndege ndio kwanza inapaa;;;;»»»»»»»»»»»>>>>>>
that is a point, tena unapita kwenye sehemu yenye mgandamizo mkubwa wa hali ya hewa - lazima dege ulibwage chini.
 
Ni watu wachache wawaweza kuelewa haya.Na ndio maana kwa upande wangu naunga mkono kusiwe na uchaguzi CDM kwa sasa mpaka baada ya uchaguzi wa 2015.Bado najiuliza kwa nini Mabere Marando ,kwenye vyama anavyoeenda mgogoro wa kiuongozi hujitokeza?
 
Mleta mada anajitahidi kupulizia pafyumu kwenye kinyesi, ngoja tuone km hakitanuka
 
Hakuna kulala mpaka Kieleweke! Na hatufanyi uchaguzi mpaka tukomboe Nchi!
 
Kwanza andikeni katiba inayotokana na wanachama, sio katiba ya kukidhi mahitaji ya Mtei.

Mtei alimuandaa binti yake Lilian kuwa Mwenyekiti wa Chadema baada ya Mbowe. Binti huyo alipokataa ikabidi Mtei aagize kipengele cha kuweka ukomo wa mihula ya uongozi kiondolewe ili Mbowe aendelee kuwa Mwenyekiti.

Chadema ni chama kinachoendeshwa katika misingi ya kilaghai.
 
Chama chochote hakiwezi kusimama kama hamna mkakati wa kuandaa viongozi ulio wazi na kueleweka!!!!!

Mengine mnajidanganya tu kwa faida binafsi!!!!!

Haiingii akilini kusema unataka nchi wakati uwezo wa ndani tu kuwa na watu reliable with high level of integrity haupo na kushuku kuwa flani akiondoka basi hili litakuwa hivi na lile vile as if haikuwa inafahamika kuwa watu wanazeeka na kuchoka na wengine wanakua!!!!!

Nature will take care of weaknesses,just a matter of time!!!!!!
 
Ila nadhani kama CDM wako makini hali hii nadhani waliitegemea.Usitegemee CCM kuondoka madarakani kirahisi rahisi hata kama Umma wa watz uko nyuma ya CDM.Bado kuna kai kubwa na makubwa zaidi yatajitokeza.Kwa upande wa CDM ni wakati wa kuendeleza M4C maana ,kukaa kwenu Idle ndio kunawafanya wasio na kazi kupata muda wa kuhongwa na kufanya ujinga.Inabidi muwakeep busy viongozi wenu muda wote.Kwani "an Idle mind is a home of devil".
 
Ni watu wachache wawaweza kuelewa haya.Na ndio maana kwa upande wangu naunga mkono kusiwe na uchaguzi CDM kwa sasa mpaka baada ya uchaguzi wa 2015.Bado najiuliza kwa nini Mabere Marando ,kwenye vyama anavyoeenda mgogoro wa kiuongozi hujitokeza?

Kwa hio unadhani marando ndio tatizo chadema???
Historia ya marando inajulikana hakika, Mwanzo alikua Usalama wa taifa kabla ya kujiunga na Nccr-Mageuzi na baadae Chadema, Labda tuanzia hapa ni nini kilimtoa usalama wa taifa???
 
Chama chochote hakiwezi kusimama kama hamna mkakati wa kuandaa viongozi ulio wazi na kueleweka!!!!!

Mengine mnajidanganya tu kwa faida binafsi!!!!!

Haiingii akilini kusema unataka nchi wakati uwezo wa ndani tu kuwa na watu reliable with high level of integrity haupo na kushuku kuwa flani akiondoka basi hili litakuwa hivi na lile vile as if haikuwa inafahamika kuwa watu wanazeeka na kuchoka na wengine wanakua!!!!!

Nature will take care of weaknesses,just a matter of time!!!!!!

Hilo unaloliongea linawezekana kama mazingira na kila kitu kiko sawa.Huwezi anza kuongelea habari za uongozi wakati hali iko tetenamna hii."one step at a time"
 
Urais 2015 unawachanganya CCM.
Mkuu, siumesikia kelele za lile jinga lao lenye tumbo kana kwamba linajisaidia ndani kwa ndani lilivyokosa haya kutangaza kuwa mzee wa Richmond ndie raisi ajae kupitia chama lao la rushwa?
 
Ukiangalia kwa makini siasa za Tz tangu kuanzishwa kwa vyama vingi utagundua kuwa CCM kina fikra za kuliongoza taifa hili milele na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM na serikali wamejitokeza hadharan kutangaza kuwa CCM itatawala milele.

Kwa kufanikisha kusudio hilo CCM kimekuwa kikitumia pesa nyingi kuvuruga vyama vya upinzani vinavyojitokeza kuwa na nguvu kwa kupandikiza vibaraka.

Walifanikiwa kwa NCCR-magauzi, na baadaye wakafanikiwa kuivuruga TLP , wakafanikiwa kwa CUF baada ya kufunga nao ndoa ya mkeka.

Mwanzoni mwa mwaka huu CCM kupitia Wasira na wenzake wakajitokeza na kuutangazia umma wa Tanzania kuwa watahakikisha CHADEMA kinakufa mwaka huu.

Baada ya kauli hiyo tukasikia mengi mara CHADEMA ni magaidi, wakarudia nyimbo za ukanda, udini, ukabila vyote hivyo vikashindikana na hii ni kutokana na uongozi imara na thabiti wa viongozi wa CHADEMA chini ya Mbowe na Dr slaa.

Sasa wamekuja na staili ya kutaka kuwapangia CHADEMA safu za uongozi ndani ya chama na wanaCHADEMA wasipokuwa makini na kuingia ktk mkenge huu watakivuruga chama.

Katika azma yao ya kuua CHADEMA mwaka huu utaona gazeti la CCM 'Uhuru' linakuja na vichwa vya habari kama mwisho wa CHADEMA umetimia pamoja na magazeti mengi corrupted na kulipa watu kukichafua chama kupitia mitandao ya kijamii. Lkn chini ya uongozi wa mbowe na Dr slaa hili nalo litapita.

Natoa rai kwa wanaCHADEMA kuwa makini ili lengo la kusimika misingi nchi nzima lisiharibiwe na propaganda chafu za CCM.

Na yale yaliyotolewa na Mwigamba ambayo ni ya msingi yafanyiwe kazi ili tusitoe loop hole kwa wanaotumiwa , wasipate pa kuzungumzia.

Kwa kufanya hivyo CHADEMA iataendelea kuimalika siku hadi siku.

M4c nayo haijulikani imefia wapi.
 
Hata jeneza na sanduku la maiti hunakshiwa kwa pambo zote za kuvutia lakini huwa haliondoi ukweli kuwa ndani kuna maiti
 
Back
Top Bottom