Mbowe, Slaa na Zitto tuvusheni 2015 salama

masanjasb

JF-Expert Member
Joined
Aug 11, 2011
Posts
2,364
Reaction score
869
Salaam wana janvi?

Kunamekuwepo na majibizano mengi ndani ya mitandao ya kijamii kuhusiana na uchaguzi ndani ya chama cha maendeleo na demokrasia (chadema) wengi wa wachangiaji wakidai ni vyema kufanya uchaguzi kwa sasa na wengine wakisema ni bora tubadilishe uongozi wa juu hasa wanachama wa chama cha mapinduzi (ccm) ndiyo wanaopigia kelele swala hili.

Ukiangalia kwa undani na kwa jicho pevu utagundua kuwa kuna mapinduzi baridi yanayotaka kufanywa na viongozi ndani ya chadema kwa maelekezo toka ccm ili kuuondoka uongozo wa ngazi ya taifa hasa slaa na mh mbowe, hawa ndiyo target kubwa kwani watu hawa wamekosanishwa kwa njia tofauti ila bado wamesimama imara, na hii imepelekea ccm kutumia kila aibu ya umafia kuwatoa hawa watu hapo walipo ili waweke viongoizi laini (soft leader) watakao fanya kazi kwa maelekezo ya ccm.

Sisi wanachama wa cdm hatutaki uchaguzi ndani ya chama ufanyike leo wala kesho bali ufanyike baada ya uchaguzi mkuu 2015 chakushangaza mashabiki na wanachama wa ccm wanataka chadema ifanye uchaguzi wa ndani na tena mh mbowe na slaa wasiogombee kwani vipindi vyao vimekwisha, hii sio tabia nzuri, cdm haiwezi kuwa sawa na ccm, nyie kama mnafanya uchaguzi wenu kila baada ya miezi 6 acha iwe hivyo kwenu ila kwa cdm haiko hivyo na hatutaki kufanana na ccm hata kiutendaji au kiuendeshaji wa taasisi hii.

Endapo uchaguzi utafanyika kwa sasa kuna hatari kubwa ya ccm kuingiza masalia yake ndani ya cdm, ambayo kwa sasa yameanza kujitokeza tena, nakiomba sana chama changu pendwa kisikie kilio chetu sisi wanachama hai kuwa hatutaki uchaguzi ndani ya chama chetu kwa sasa bali ufanyike mwaka 2015.

Mbowe, dr slaa, zitto tuvusheni salama na kama tutafika salama bs mtapumzika wakuu zetu tofauti na hapo mtatupoteza, mpeni zito kijiti baada ya uchaguzi wa 2014/15, tunataka tumtathimini kupitia chaguzi zote ili tumpe chama kikiwa kamili na sio vipande vipande kama wanavyotaka wanachama wa ccm:

Shabiki, mwanachama wa cdm pls paza sauti isikike kwa viongozi wetu hawa
 
Hata kama uchaguzi utafanyika leo.CHADEMA hakitaweza kuongozwa kqlwa Maelekezo kutoka Lumumba au Ikulu.

Hakuna kibaraka wa CCM atakayeongoza CHADEMA

Kuliko CHADEMA kiongozwe na mamluki ni bora CCM kiendelee kuongoza na nitakua wa kwanza kujitoa

Kama CCM wana watu wanaowataka wachukue uongozi ndani ya CHADEMA basi wawachukue wakagombee huko CCM.Hakuna kuendekeza wanafiki na wasaliti ambao Mwenyekiti aliwaonya juzi

Infact ningejiskia ashamed sana kama mpinzani ninapoona CCM ndio wanaonipigia kampeni na kunisifia.Ni aibu

Fisi anamshauri mbuzi jinsi ya kuilinda familia yake?It's a tricky affair!

NB:Uongozi wa CHADEMA sio wa kupewa bali ni kuomba ridhaa kwa wapiga kura ambao ni wanachama

Asipogombea Mbowe anaweza kuwa yeyote.Kuna Lissu,Mnyika na wengineo.No silver plate....
 
Khaa!! wewe vipi mbona una akili isiyofika mbali? Unaoanisha uhai wa chama na mtu binafsi? Weka akili yako vizuri kama leo Mungu akiwapenda zaidi Mbowe na Dr Slaa ndiyo uwe mwisho wa Chadema? Au baada ya 2015 Ridh1 wa mbowe atakuwa amekuakua kidogo?
 
Nadhani chadema ni zaidi ya mbowe, slaa na zitto. Chadema ni wanachama
 
Unatokwa povu kweli soma tena mstari wa kwanza ulichoaandika sasa naamini maovu mliyofanya yanawarudi mmevurugwa.
 
Tangu lini zito akae chungu moja na watu wanaomwinda kila siku kwa mabaya halafu leo akae nao thubutu.
 
Nadhani chadema ni zaidi ya mbowe, slaa na zitto. Chadema ni wanachama

Naongelea uongozi hapa mkuu, uongozi wao umetufikisha hapa tulipo leo kwa nini leo tunawabeza kwa msasda wa ccm?
 
Inaniuma sana ninapoona majemedali wetu wanaingizwa kwenye mitego midogo sana ya kisiasa nao wanaelekea kuingia. Nawazungumzia viongozi wakuu waandamizi; Mbowe, Slaa na Zitto.

Labda niseme tu CCM wanakesha kila siku kutafuta wataalamu wakusaidia kutafuta njia za kuiangamiza CHADEMA, wao kwa sasa wameamua kuwekeza zaidi huko. Na hawajaona mahala pengine pa kuyafanya hayo zaidi ya humu kwenye mitandao ya jamii hasa jamii forums.

Viongozi wangu hawa watu ni wa kuwapuuza wote tena kwa nguvu zote, hakuna sababu ya kufuata na kuzicheza ngoma wanazozipiga. Wao wanapotuona tunakinzana wanafurahi kwani tunapoteza muda mwingi sana kujadili mambo wanayoyatengeneza kuliko mipango ya chama.

Mara nyingi wanapozusha mada za kichonganishi hapa jamii forums huzaa mizozo mingi sana na lawama kwa wanachama na wapenzi wa chadema, hili linazaa ugonjwa sugu katika chama na kama hatutakuwa makini tutavurugana katika chama.

Nitoe mfano mmoja, binafsi nafahamu mchango mkubwa wa Naibu katibu mkuu Zitto Kabwe katika kuifanya chadema kufika hapa ilipo leo. Ni kutokana na mambo ambayo hayakuwa na sababu za kubishana kupitia mitandaoni kulikofanywa na Zitto na makada wengine wa chadema kulikopelekea watu wengi waanze kumtukana Zitto leo hii huku wakisahau mchango wake katika chama. Lakini haya yote yalikuja baada ya kuendekeza mijadala isiyo na tija kwa mustakbari mwema kwa chadema.

Nilihudhuria kongamano la chadema kanda ya kaskazini la tarehe 26/10/2013. Mheshimiwa Mbowe aliongea mambo ya busara sana, kwamba chadema kimejengwa kwa takribani miaka 20 mpaka kikawa imara hivi na kama kikifa leo itachukua miaka mingine ishirini kutokea chama pinzani imara chenye mfano wa chadema.

Nataka niseme miongoni mwa mambo ambayo yatapelekea kukwamisha jitihada za chadema itakuwa ni viongozi wa chadema na makada wao mitandaoni.

Anaesimamishwa uongozi chadema kwa vithibitisho vya usaliti kama Mwigamba lisitufanye tuifanye kama mada na tukasahau wajibu wetu kama wanachama wa chadema. Vivo hivyo sioni sababu ya baadhi ya makada kujenga taswira za kumshutumu Zitto Kabwe wakati tunaona jitihada anazofanya za kuimarisha chama katika kanda ya magharibi ikiwa ni mwendelezo wa ujenzi wa chama wa muda mrefu ambao Zitto anamchango nao.

Mapungufu huwa yanaotokea, madhaifu huwa yapo kwa mwanadamu. Yawezekana ni kweli Zitto kuna maeneo aliteleza lakini kama mngepima mwenendo wake katika chama kwa sasa, hasa ujenzi wa chama sidhani kama itakuwa busara kumjadili Zitto kwa namna ambayo huwa naiona inaendelea humu mitandaoni. Leo hii kanda ya magharibi tumepata wafuasi wengi sana kutokana na mchango wake, Tabora na kwingineko tumepata wafuasi wengi sana na ngome nyingi za CCM zimekuwa zikivunjwa kutokana na ziara za Mheshimiwa Zitto Kabwe.

Mimi naamini viongozi wa chadema hawana shida isipokuwa ni makada wa chadema humu mitandaoni. Niwaombe tuwe pamoja tutoe ushirikiano wa kutosha kwa viongozi wetu katika wakati huu mgunu wenye majaribu mengi sana. Tuache kushiriki katika mijadala yenye lengo la kutuvuruga hasa kwa kuwashutumu viongozi wetu wakuu wa chama. Kwa kufanya hivyo tutafikia malengo tuliyojiwekea.
 
Hata kama uchaguzi utafanyika leo.CHADEMA hakitaweza kuongozwa kqlwa Maelekezo kutoka Lumumba au Ikulu.

Hakuna kibaraka wa CCM atakayeongoza CHADEMA

Kuliko CHADEMA kiongozwe na mamluki ni bora CCM kiendelee kuongoza na nitakua wa kwanza kujitoa

Kama CCM wana watu wanaowataka wachukue uongozi ndani ya CHADEMA basi wawachukue wakagombee huko CCM.Hakuna kuendekeza wanafiki na wasaliti ambao Mwenyekiti aliwaonya juzi

Infact ningejiskia ashamed sana kama mpinzani ninapoona CCM ndio wanaonipigia kampeni na kunisifia.Ni aibu

Fisi anamshauri mbuzi jinsi ya kuilinda familia yake?It's a tricky affair!

NB:Uongozi wa CHADEMA sio wa kupewa bali ni kuomba ridhaa kwa wapiga kura ambao ni wanachama

Asipogombea Mbowe anaweza kuwa yeyote.Kuna Lissu,Mnyika na wengineo.No silver plate....

Ben nimekupata na kukuelewa vzr ila wito wangu pia uzingatie kwani ccm wana kila nyenzo yakufanikisha matakwa yao, najua kabisa tunajiamini ila ya nini twende kwenye uchaguzi wakati tunajua huo uchaguzi utatuacha na makovu makubwa?
 
Khaa!! wewe vipi mbona una akili isiyofika mbali? Unaoanisha uhai wa chama na mtu binafsi? Weka akili yako vizuri kama leo Mungu akiwapenda zaidi Mbowe na Dr Slaa ndiyo uwe mwisho wa Chadema? Au baada ya 2015 Ridh1 wa mbowe atakuwa amekuakua kidogo?

Hapo ndio wanaponichanganya WanaCHADEMA wanaposema akiondoka Mbowe na Dr Slaa CHADEMA itakufa sina uhakika kama wanafahamu wanachokiongea?Khaa!Kwa lugha nyingine hawa watu hawakipendi Chama ila wanawapenda akina Mbowe tu,Pia hawaiamini CHADEMA kama Taasisi iliyokamilika yenye muundo na mfumo makini wenye kutoa muongozo wa namna Chama kiendeshe vipi shughuli zake za kisiasa na namna gani Chama kinaweza kukabiliana na misuko suko ya nje ikiwemo dhidi ya njama za Wapinzani wake wakubwa kisiasa kama CCM.Kama hoja za WanaCHADEMA zina ukweli wowote again Mbowe na wenzie walaumiwe kwa kuijenga Taasisi dhaifu inayowategemea watu wachache ku-survive kisiasa.
 
Nimekosa maneno mazuri ya tumia ili kuwaenzi viongozi wangu wakuu wa chama(Dr wilbrod Slaa na kamanda freeman Mbowe.
Tangu kuanza kwa vuguvugu la uchaguzi wa ndani ya chama kila mwenye jambo analofikiri liko sahihi(kwa mtazamo wake ambao nami sipingani nao) amekuwa akilitupa hapa ili wadau wachangie kwa kutoa mawazo yao.

Wengi wao(ambao siamini sana kama ni wanachama halisi wa CDM) wamekuwa wakitoa malalamiko na kashfa kedekede kuwatuhumu Mh Freeman Mbowe( mbunge wa hai pia mwenyekiti wa kambi rasmi ya upinzani bungeni) pamoja na Dr wilbrod Slaa( katibu mkuu wa CDM, ambayo pia namwombea kwa Mungu maisha marefu awe ndie mgombea urais 2015-pendekezo langu).

Tuhuma hizi kimantiki zinaonekana zinafanywa na watu waliotumwa na watu fulani ambao either wako ndani ya chama kwa maslahi yao ama wametumwa na watu walio nje ya chama kwa kuhofia nguvu walizonazo viongozi hawa pamoja na misimamo yao mikali juu ya kukemea maovu yanayofanywa na baadhi ya vigogo na wanasiasa wakubwa wa nchi hii.

Siko vizuri sana katika historia lakini kumbukumbu zangu zinajaribu kunirudisha nyuma na kuangalia idadi ya vyama vilivyowahi kuanzishwa tangu kuanza kwa vyama vingi vya siasa nchini(1992) na vyama vilivyobaki huku vikiwa na nguvu na mvuto mkubwa mbele wa wananchi.

Sababu kuu ya kupotelea hewani kwa vyama hivi ni pamoja na kutokuwa na viongozi makini na wasio na misimamo thabiti juu ya mambo wanayoyaamini. pamoja na sababu hii lakini ipo nyinginge ambayo ni ya kusadikika tu mwamba vingi vilianzishwa na chama tawala ilikupunguza nguvu ya upinzani hasa nyakati za chaguzi sababu iliyopelekea vipotee ghafla baada ya chaguzi kuu kupita.

Tanzania imeonekana kufika hapa kwasababu ya KIONGOZI MKUU WA NCHI ambaye ndiye msimamizi wa shughuli zote zinaohusu maendeleo ya watanzania.

CHADEMA hatuwezi kusita wala kumung'unya maneno kwamba uimara wa chama ni kwa sababu ya misingi imara iliyojengwa na viongozi wetu ambao ndio wanakiongoza chama kitaifa na anayesita kuyasema haya ana chuki za kwake binafsi ambazo hatuwezi kuziondoa sisi kama binadamu wa kawaida labda mpaka Mwenyezi Mungu aingilie kati. Rais wa nchi alipokuwa akiwatahadhalisha wanachama wake juu ya kung'oka mwaka 2015 hakuwa anamaanisha kung'olewa na chama kingine chochote bali hofu yake aliyokuwa nayo juu ya CDM ambayo viongozi wake wameonyesha kuwa na msimamo mkali sana hivyo haoni namna ya kuwatisha wala kuwarubuni.

Safari yetu bado ni ngumu na tunahitaji viongozi wanaoendana na ugumu wa safari hii(pamoja na uzoefu wa kuongoza) na baada ya kuvuka kipindi hiki ambacho watanzania wengi wanategemea kubadilika kwa historia ya Tanzania yeyote anayedhani anaweza kushika nafasi yoyote anaweza kufanya maamuzi hayo lakini kwa sasa barabara bado ni mbovu tunahofia gari kupindukia njiani..

DR SLAA, FREEMAN MBOWE ARE CUSTODIANS OF POLITICAL SUCCESS
 
Wana JF.

Wahenga walisema, "hakuna jambo lisilo na mwisho na hakuna marefu yasiyo na ncha" vivyo hivyo kila jambo na wakati wake na ndege mwelevu hufichama mbawa zake........... Ni baadhi ya misemo kati ya mingi iliyopo katika hazina ya lugha yetu TAMU ya KISWAHILI ambayo imenigusa na kunishawishi kufungua kumpyuta mpakato yangu na kuja moja kwa moja humu jamvini na kuanza kuandika "UZI" huu "USHAURI WANGU"

Ushauri wangu uwaendee moja kwa moja na uwafikie popote walipo viongozi wa CHADEMA ngazi ya Taifa, Mkoa, Wilaya na hata kata/shina. Haijalishi katiba imechakachuliwa au haijachakachuliwa, inakikomo cha uongozi au haina...... ni busara kubwa ukajipa ukomo wa kuongoza kabla unaowaongoza hawajakuengua kwa nguvu kupitia chaguzi mbalimbali.

USHAURI WANGU wa pekee uwafikie M/kiti, Katibu Mkuu,na M/Katibu Mkuu wa CHADEMA Taifa. Ni ukweli uliotukuka ya kuwa chini ya uongozi wenu mmefanya kazi kubwa mkishirikiana na viongozi wengine na wanachama kwa ujumla, ya kukitoa CHADEMA kutoka chama vha 4 cha upinzani na kuwa CHAMA KIKUU na namba 1 upinzani. Ni mafanikoi makubwa yaliyopatikana ndani ya Miaka 10 tu.......... HONGERENI SANA. Mafanikio haya mmeandika historia ndani ya CHADEMA ambayo vizazi vijavyo vitaisoma kama si kusimuliwa. Lakini ni ukweli uliowazi ya kuwa ni wakati muafaka wa nyinyi kudhihirisha maana halisi na pana ya maneno "CHAMA CHA DEMOKRASIA NA MAENDELEO". Ni wakati muafaka wa nyinyi kufanya maamuzi magumu, yenye busara kubwa na yatakayo wadhihirishia wanachama na watanzania wote kuwa "CHADEMA ni zaidi ya nyinyi. Ni muda muafaka wa nyinyi kutogombea nafasi zenu za sasa pasipo kujali katiba inawaruhusu au haiwaruhusu.

Ni ukweli siofichika kuwa CHADEMA kwa sasa kinapita katika wakati mgumu wa kuhujumiwa kwa kila aina ya mbinu kutoka kila pande ya Dunia, lakini hili peke yake halitoshi kuwa sababu ya kuamini kuwa hakuna wanachama wengine ndani ya CHADEMA wenye uwezo na waoaminika kuweza kuongoza nafasi mlizo nazo. Pia sio sababu ya kuwa na hofu ya kufanya uchaguzi wa chama, kwani kufanya hivyo ni kuendelea kukuza majeraha yatokanayo na uchaguzi huku ikiwa imebaki muda mfupi kuelekea uchaguzi mkuu.

Ninapenda kuona CHADEMA ikiwa na mshikamano kuanzia viongozi ngazi ya Taifa mpaka tawi/shina. Hizi tuhuma za ukomo wa uongozi ni nzito na zinaharibu sifa na muonekano wa chama. Msizichukulie kisiasa na kuanza kuja na majibu mepesi mepesi, bali mzitafakari katika mantiki ya "DEMOKRASIA NA MAENDELEO". Ni muda muafaka wa nyinyi kujitofautisha na vyama vingine katika safu ya Uongozi Taifa.

Aluta kontinuawa......................
 
Infact ningejiskia ashamed sana kama mpinzani ninapoona CCM ndio wanaonipigia kampeni na kunisifia.Ni aibu

Fisi anamshauri mbuzi jinsi ya kuilinda familia yake?It's a tricky affair!...
hapa ndipo panapo tushangaza wengi tunaoitakia mema CDM.
 
Naongelea uongozi hapa mkuu, uongozi wao umetufikisha hapa tulipo leo kwa nini leo tunawabeza kwa msasda wa ccm?

Wanaowabeza ni CCM, by th way wanawaogopa. Chadema ni chama kinachokuwa kwa kasi sana. Hayo ni mafanikio makubwa
 
Hapo ndio wanaponichanganya WanaCHADEMA wanaposema akiondoka Mbowe na Dr Slaa CHADEMA itakufa sina uhakika kama wanafahamu wanachokiongea?Khaa!Kwa lugha nyingine hawa watu hawakipendi Chama ila wanawapenda akina Mbowe tu,Pia hawaiamini CHADEMA kama Taasisi iliyokamilika yenye muundo na mfumo makini wenye kutoa muongozo wa namna Chama kiendeshe vipi shughuli zake za kisiasa na namna gani Chama kinaweza kukabiliana na misuko suko ya nje ikiwemo dhidi ya njama za Wapinzani wake wakubwa kisiasa kama CCM.Kama hoja za WanaCHADEMA zina ukweli wowote again Mbowe na wenzie walaumiwe kwa kuijenga Taasisi dhaifu inayowategemea watu wachache ku-survive kisiasa.

Kwa sasa ccm wanataka mbowe na slaa watoke pale walipo na sisi kama wanachana tunasema hatutaki watoke, ila chama kama cham kikiamua kwenda kwenye uchaguzi wa ndani hatuna budi kukiunga mkono japo kwa ushauri wangu haya yafanyike baada ya uchaguzi mkuu wa 2015; kama unatutakia mema utanielewa ila kama wataka chama kife bs endeleza porojo zako mkuu
 
Nadhani chadema ni zaidi ya mbowe, slaa na zitto. Chadema ni wanachama

Nashukuru kama umeutambua uwepo wetu ila pamoja na yote uongozi wa hao watu ndiyo umetufikisha hapa tulipo na bado tunauhitaji walau utuvushe hapa tulipo ili wakamlishe ngwe yao vzr sana
 
Hata kama uchaguzi utafanyika leo.CHADEMA hakitaweza kuongozwa kqlwa Maelekezo kutoka Lumumba au Ikulu.

Hakuna kibaraka wa CCM atakayeongoza CHADEMA

Kuliko CHADEMA kiongozwe na mamluki ni bora CCM kiendelee kuongoza na nitakua wa kwanza kujitoa

Kama CCM wana watu wanaowataka wachukue uongozi ndani ya CHADEMA basi wawachukue wakagombee huko CCM.Hakuna kuendekeza wanafiki na wasaliti ambao Mwenyekiti aliwaonya juzi

Infact ningejiskia ashamed sana kama mpinzani ninapoona CCM ndio wanaonipigia kampeni na kunisifia.Ni aibu

Fisi anamshauri mbuzi jinsi ya kuilinda familia yake?It's a tricky affair!

NB:Uongozi wa CHADEMA sio wa kupewa bali ni kuomba ridhaa kwa wapiga kura ambao ni wanachama

Asipogombea Mbowe anaweza kuwa yeyote.Kuna Lissu,Mnyika na wengineo.No silver plate....

Lakini pia ukumbuke kuwa maneno yako haya yanaweza kutushawishi tuamini kuwa kuwa na wewe unafanyaka kazi hiyo hiyo ya UKIBARAKA ndani ya chama. Haiwezekani mtu anafanya chama kuwa mali yake na watu wanapohoji wanaitwa vibaraka wa CCM.
 
Khaa!! wewe vipi mbona una akili isiyofika mbali? Unaoanisha uhai wa chama na mtu binafsi? Weka akili yako vizuri kama leo Mungu akiwapenda zaidi Mbowe na Dr Slaa ndiyo uwe mwisho wa Chadema? Au baada ya 2015 Ridh1 wa mbowe atakuwa amekuakua kidogo?

Hayo nitayaita mapenzi ya Mungu ila sitaki watoke pale kwa mapenzi ya ccm, vita tunayopigana ni kubwa ajabu sema hauko msatari wa mbele ndiyo maana unalaumu andiko langu.....
 
Ukiangalia kwa makini siasa za Tz tangu kuanzishwa kwa vyama vingi utagundua kuwa CCM kina fikra za kuliongoza taifa hili milele na baadhi ya viongozi waandamizi wa CCM na serikali wamejitokeza hadharan kutangaza kuwa CCM itatawala milele.

Kwa kufanikisha kusudio hilo CCM kimekuwa kikitumia pesa nyingi kuvuruga vyama vya upinzani vinavyojitokeza kuwa na nguvu kwa kupandikiza vibaraka.

Walifanikiwa kwa NCCR-magauzi, na baadaye wakafanikiwa kuivuruga TLP , wakafanikiwa kwa CUF baada ya kufunga nao ndoa ya mkeka.

Mwanzoni mwa mwaka huu CCM kupitia Wasira na wenzake wakajitokeza na kuutangazia umma wa Tanzania kuwa watahakikisha CHADEMA kinakufa mwaka huu.

Baada ya kauli hiyo tukasikia mengi mara CHADEMA ni magaidi, wakarudia nyimbo za ukanda, udini, ukabila vyote hivyo vikashindikana na hii ni kutokana na uongozi imara na thabiti wa viongozi wa CHADEMA chini ya Mbowe na Dr slaa.

Sasa wamekuja na staili ya kutaka kuwapangia CHADEMA safu za uongozi ndani ya chama na wanaCHADEMA wasipokuwa makini na kuingia ktk mkenge huu watakivuruga chama.

Katika azma yao ya kuua CHADEMA mwaka huu utaona gazeti la CCM 'Uhuru' linakuja na vichwa vya habari kama mwisho wa CHADEMA umetimia pamoja na magazeti mengi corrupted na kulipa watu kukichafua chama kupitia mitandao ya kijamii. Lkn chini ya uongozi wa mbowe na Dr slaa hili nalo litapita.

Natoa rai kwa wanaCHADEMA kuwa makini ili lengo la kusimika misingi nchi nzima lisiharibiwe na propaganda chafu za CCM.

Na yale yaliyotolewa na Mwigamba ambayo ni ya msingi yafanyiwe kazi ili tusitoe loop hole kwa wanaotumiwa , wasipate pa kuzungumzia.

Kwa kufanya hivyo CHADEMA iataendelea kuimalika siku hadi siku.
 
Salaam wana janvi?

Kunamekuwepo na majibizano mengi ndani ya mitandao ya kijamii kuhusiana na uchaguzi ndani ya chama cha maendeleo na demokrasia (chadema) wengi wa wachangiaji wakidai ni vyema kufanya uchaguzi kwa sasa na wengine wakisema ni bora tubadilishe uongozi wa juu hasa wanachama wa chama cha mapinduzi (ccm) ndiyo wanaopigia kelele swala hili.

Ukiangalia kwa undani na kwa jicho pevu utagundua kuwa kuna mapinduzi baridi yanayotaka kufanywa na viongozi ndani ya chadema kwa maelekezo toka ccm ili kuuondoka uongozo wa ngazi ya taifa hasa slaa na mh mbowe, hawa ndiyo target kubwa kwani watu hawa wamekosanishwa kwa njia tofauti ila bado wamesimama imara, na hii imepelekea ccm kutumia kila aibu ya umafia kuwatoa hawa watu hapo walipo ili waweke viongoizi laini (soft leader) watakao fanya kazi kwa maelekezo ya ccm.

Sisi wanachama wa cdm hatutaki uchaguzi ndani ya chama ufanyike leo wala kesho bali ufanyike baada ya uchaguzi mkuu 2015 chakushangaza mashabiki na wanachama wa ccm wanataka chadema ifanye uchaguzi wa ndani na tena mh mbowe na slaa wasiogombee kwani vipindi vyao vimekwisha, hii sio tabia nzuri, cdm haiwezi kuwa sawa na ccm, nyie kama mnafanya uchaguzi wenu kila baada ya miezi 6 acha iwe hivyo kwenu ila kwa cdm haiko hivyo na hatutaki kufanana na ccm hata kiutendaji au kiuendeshaji wa taasisi hii.

Endapo uchaguzi utafanyika kwa sasa kuna hatari kubwa ya ccm kuingiza masalia yake ndani ya cdm, ambayo kwa sasa yameanza kujitokeza tena, nakiomba sana chama changu pendwa kisikie kilio chetu sisi wanachama hai kuwa hatutaki uchaguzi ndani ya chama chetu kwa sasa bali ufanyike mwaka 2015.

Mbowe, dr slaa, zitto tuvusheni salama na kama tutafika salama bs mtapumzika wakuu zetu tofauti na hapo mtatupoteza, mpeni zito kijiti baada ya uchaguzi wa 2014/15, tunataka tumtathimini kupitia chaguzi zote ili tumpe chama kikiwa kamili na sio vipande vipande kama wanavyotaka wanachama wa ccm:

Shabiki, mwanachama wa cdm pls paza sauti isikike kwa viongozi wetu hawa

Umeandika vizuri, ila natofautiana na wewe kuwa mapinduzi yanapata maelekezo toka CCM, unataka kutuaminisha kuwa yaliyosemwa na MWIGAMBA hayana ukweli?
 
Back
Top Bottom