Mbowe, Slaa na Zitto tuvusheni 2015 salama

Mbowe, Slaa na Zitto tuvusheni 2015 salama

salaam wana janvi?

Kunamekuwepo na majibizano mengi ndani ya mitandao ya kijamii kuhusiana na uchaguzi ndani ya chama cha maendeleo na demokrasia (chadema) wengi wa wachangiaji wakidai ni vyema kufanya uchaguzi kwa sasa na wengine wakisema ni bora tubadilishe uongozi wa juu hasa wanachama wa chama cha mapinduzi (ccm) ndiyo wanaopigia kelele swala hili.

Ukiangalia kwa undani na kwa jicho pevu utagundua kuwa kuna mapinduzi baridi yanayotaka kufanywa na viongozi ndani ya chadema kwa maelekezo toka ccm ili kuuondoka uongozo wa ngazi ya taifa hasa slaa na mh mbowe, hawa ndiyo target kubwa kwani watu hawa wamekosanishwa kwa njia tofauti ila bado wamesimama imara, na hii imepelekea ccm kutumia kila aibu ya umafia kuwatoa hawa watu hapo walipo ili waweke viongoizi laini (soft leader) watakao fanya kazi kwa maelekezo ya ccm.

Sisi wanachama wa cdm hatutaki uchaguzi ndani ya chama ufanyike leo wala kesho bali ufanyike baada ya uchaguzi mkuu 2015 chakushangaza mashabiki na wanachama wa ccm wanataka chadema ifanye uchaguzi wa ndani na tena mh mbowe na slaa wasiogombee kwani vipindi vyao vimekwisha, hii sio tabia nzuri, cdm haiwezi kuwa sawa na ccm, nyie kama mnafanya uchaguzi wenu kila baada ya miezi 6 acha iwe hivyo kwenu ila kwa cdm haiko hivyo na hatutaki kufanana na ccm hata kiutendaji au kiuendeshaji wa taasisi hii.

Endapo uchaguzi utafanyika kwa sasa kuna hatari kubwa ya ccm kuingiza masalia yake ndani ya cdm, ambayo kwa sasa yameanza kujitokeza tena, nakiomba sana chama changu pendwa kisikie kilio chetu sisi wanachama hai kuwa hatutaki uchaguzi ndani ya chama chetu kwa sasa bali ufanyike mwaka 2015.

Mbowe, dr slaa, zitto tuvusheni salama na kama tutafika salama bs mtapumzika wakuu zetu tofauti na hapo mtatupoteza, mpeni zito kijiti baada ya uchaguzi wa 2014/15, tunataka tumtathimini kupitia chaguzi zote ili tumpe chama kikiwa kamili na sio vipande vipande kama wanavyotaka wanachama wa ccm:

Shabiki, mwanachama wa cdm pls paza sauti isikike kwa viongozi wetu hawa

lakini wanasema zito ni gamba.
 
Hii habari ilikuwemo humu ikatolewa

[wanabidii] UFISADI WA ZITTO ZUBERI KABWE

Wednesday, October 30, 2013​
kauli yake inadhihirsha tabia zake za kisaliti.​
anataka kuficha maovu yake ya kupokea Million 250 CRDB na zile Dolla laki 2 na ushee kupitia German.​
Huyu bwana ni msaliti na kwa wajuzi wa mambo mtaona ni kwanini hakuandamana na dr slaa wakati wa kampeni za urais​
CCM wana mtumia na walishamtumia siku nyingi na innafaa atemwe cheo chake kabla ya 2015 atakiangamiza chama.​
Zito your finished man, nlikuamini lakini baada ya kusoma post inayokuhusu wewe sina imani nawe kanisa​
Umethamini hela kuliko maisha ya sisi walalahoi tunaotegemea ukombozi wa kweli......​

​
Riporti ya siri inaeleza ukweli 23/6/2008 saa 07:52 ulikutana na kina Wassira na mtu wa usalama wa Taifa sea cliff​
30/6/2008 Ulipokea mshiko wako CRDB Bank kiasi 250Tsh Million.​
Kisha Jumatano ya tarehe 16/12/2009 majira ya saa 13:12 za mchana​
kwa Ujerumani akaunti namba .............................,​
ziliingizwa dola za kimarekani 266,000 pesa hizi katika​
uchunguzi zimebainika kuwa zilitoka Tanzania katika Benki ya​
NMB Dar katika akaunti namba​
.............................. ... yenye jina la TSA,​

​
Fedha hizo alizichukua ili kutoa taarifa za siri za chadema na aliezipokea kwa niaba yake huko germani ni mwana mama alisoma nae nae akapewa Dola 25,000 kama ahsante...kweli tanzania hatuna wazalendo​

​
wakatoa na evidence hii Mfano tarehe 7/9/2010 siku ya jumanne saa 11:21 asubuhi,​
...............kupitia namba yake ya simu ya kiganjani​
......................, alimpigia Zitto kupitia simu ya kiganjani namba​
.............................. waliongea mambo mengi japo kwa muda mfupi, na​
jambo kubwa lilikuwa ni "vipi kuna kipya ndani ya Chadema?"​
Zitto alijibu "yapo mengi lakini hayana impact kwa ccm"​

​
LISEMWALO LIPO NA KAMA HALIPO LAJA.

​
NIWAULIZE MOOD KWANINI WALITOA HABARI NZIMA ISIACHWE IKASOMWA NA JF TUKAMPIMA ZITO????

​
nlibahatika kukariri chache.
​

kwa sasa ipo WANABIDII BLOG: [wanabidii] UFISADI WA ZITTO ZUBERI KABWE
 
Wasiokitakia mema chama cha CHADEMA ndo wanaoshabikia suala la uchaguzi wa viongozi ndani ya cdm.SASA HIVI HIVI HAKUNA HITAJI LA UONGOZI MPYA NGAZI YA TAIFA NDANI YA CHADEMA.Kikubwa kinacho takiwa ni kuendelea kuimarisha chama na kujipanga kwa ajili ya Uchaguzi mkuu 2015.Siyo kupotezewa muda na mamuluki wa CCM.Kwanza vingozi mnatakiwa mjiulize kitu kimoja kwamba mbona wawakomlie nyie wakati chama cha CUF Kina viongozi ambao wako madalakani toka chama kanzishwe.NYERERE PIA ALIKAA MUDA MREFU SANA MADARAKANI KWA KUHOFIA MAMURUKI WA WAKOLONI WASIIUZE NCHI ila baada ya kuondoka matokeo yake yanaendelea kuonekana,NCHI IMEGEUZWA KUWA SHAMBA LA BIBI, WATU WANAUZA RASLIMALI ZETU KAMA VILE PIPI.Viongozi wa ngazi ya juu CDM kuweni makini sana na hii ajenda ya uchaguzi haina umuhimu wowote kwa sasa.
 
lakini wanasema zito ni gamba.

Ni yeye pekee anaeweza jua kama yeye ni gamba au gwanda, siwezi usemea moyo wake
Nachokijua mie ni naibu katibu mkuu wa chama changu na pia ni mbunge wa kigoma kwa tiketi ya cdm das it
 
Iko hivi........ Mbowe.......Slaa........Zitto hawa mmoja anatazama kusini mwingine kaskazini na mwingine mashariki hawawezi kutazamana na itakuwa vigumu kuwavusha wana cdm. ......... Katiba gani ambayo imeandikwa na watu watatu na inabadilishwa na kiongozi yeyote anapojisikia kuendelea kuwa madarakani halafu mtegemee kushika dola.
 
nimekuwa nikifatilia kwakaribu kinachoendelea ndani ya cdm na hasa madai ya kwamba mwenyekiti wake ni kiongozi dicteta na hampedi kabisa naibu katibu mkuu wa cdm na kwamba anaendesha chama kimabavu.Hebu tutafakari yanayoendelea katika vyama vingine;1)CUF; Sharrif alimfukuza Hamad Rashid pamoja na kwamba alisota naye gerezani lakini wote wakiitwa waaini, CDM haijamfukuza Shibuda wala ZITTO pamoja na yote yanayoendelea ila inaendelea kuwafundisah siasa za ki CDM na hata kafululila hakufukuzwauanachama ila alisimamishwa uongozi tu. ndani ya nccr alifukuzwa ndani ya mda mfupi.

Ndani ya CDM kuna kundi dogo ambalo linaendekeza majungu ama kwa uchu wao wa madaraka au kwa kutumiwa na watuau taasisi inje ya chama na baati mbaya sana ni kwamba hawa hawaonekani kufanya kazi yoyote ya kukijenga chama zaidi ya kuibua migogoro kila kukicha

.Tatizo linaonekana kukua tunapokalibia uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo tulitegemea viongozi wangelikuwa vijijini badala ya kufikilia mambo ya uongozi wakiimarisha chama.

Kuhusu ruzuku hivi kuna chama ambacho kimefanya mikutano kama cdm na vipi vyama vingine kama cuf, nccr, na ccm mbona havishutumiwi kuhusu hili.

Lengo la haya yote ni ili CCM iendelee kubugia keke ya taifa huku wananchi wakiedelea kutaabika bila kupigiwa kelele na mtu yeyote, Hivi kama nccr mageuzi isingesambaratika ufisadi wote ulifanyika ungefanyika na nani angenufaika kama sio watu wa kawaida Je kuna nguvu ya mafisadi nyuma ya haya
KAZA BUTI KAMANDA MBOWE.
 
Alishabadili katiba na kujiongezea mda baada ya kuchakachua katiba so hakuana kipya alishajiongezea.
 
Umevulugwa?,ana miaka mingapi madarakani?,mwenyekiti hupatikana kwa kupigiwa kura,na siyo kuongezewa muda kiholela,wacha democrasia ipewe nafasi mkuu.
 
Inasemekana kwamba kama CDM wakishinda uchaguzi mkuu wa 2015 watafanya mabadiliko ya muda wa kukaa madarakani kwa viongozi wa kuchaguliwa wa serikali kutoka miaka mitano iliyopo sasa hadi miaka saba!
Lengo la kufanya hivyo ni ili viongozi hao wapate muda zaidi wakushughulikia Kero za wananchi!
 
tehetehetehe, naona mwisho wa siku wataondoa kabisa ukomo wa uongozi ili waendelee kutawala milele
 
...vikaragosi vya Lumumba vikisikia jina "MBOWE" ma------ yanatikisika!...
 
Mkuu weka kura yangu - huwezi kubadilisha wana anga wakati ndege imesha-takeoff.
 
nimekuwa nikifatilia kwakaribu kinachoendelea ndani ya cdm na hasa madai ya kwamba mwenyekiti wake ni kiongozi dicteta na hampedi kabisa naibu katibu mkuu wa cdm na kwamba anaendesha chama kimabavu.Hebu tutafakari yanayoendelea katika vyama vingine;1)CUF; Sharrif alimfukuza Hamad Rashid pamoja na kwamba alisota naye gerezani lakini wote wakiitwa waaini, CDM haijamfukuza Shibuda wala ZITTO pamoja na yote yanayoendelea ila inaendelea kuwafundisah siasa za ki CDM na hata kafululila hakufukuzwauanachama ila alisimamishwa uongozi tu. ndani ya nccr alifukuzwa ndani ya mda mfupi.

Ndani ya CDM kuna kundi dogo ambalo linaendekeza majungu ama kwa uchu wao wa madaraka au kwa kutumiwa na watuau taasisi inje ya chama na baati mbaya sana ni kwamba hawa hawaonekani kufanya kazi yoyote ya kukijenga chama zaidi ya kuibua migogoro kila kukicha

.Tatizo linaonekana kukua tunapokalibia uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo tulitegemea viongozi wangelikuwa vijijini badala ya kufikilia mambo ya uongozi wakiimarisha chama.

Kuhusu ruzuku hivi kuna chama ambacho kimefanya mikutano kama cdm na vipi vyama vingine kama cuf, nccr, na ccm mbona havishutumiwi kuhusu hili.

Lengo la haya yote ni ili CCM iendelee kubugia keke ya taifa huku wananchi wakiedelea kutaabika bila kupigiwa kelele na mtu yeyote, Hivi kama nccr mageuzi isingesambaratika ufisadi wote ulifanyika ungefanyika na nani angenufaika kama sio watu wa kawaida Je kuna nguvu ya mafisadi nyuma ya haya
KAZA BUTI KAMANDA MBOWE.

Tusonge mbele.Kwa hatua hii ya kuelekea lala salama ya harakati hizi za ukombozi,It's either you are with us or against us.No Middle ground hata kama Dunia ni three dimension!
 
Back
Top Bottom