Mbowe na Slaa wamesusiwa chama?

iron finger

JF-Expert Member
Sep 27, 2011
339
225
Habari za jioni wakuu,

nimeona nidondoke upya tena hapa jukwaani kueleza kwa kina hasa yale yaliyo moyoni na pia yanayokisibu chama changu pendwa CHADEMA

Kama ni mtafiti huru wa siasa za nchi yetu utaweka fikra zako juu ya mustakabali wa CHADEMA na kama ni mkweli na huru wa fikra hutakawia kujua anguko zito ambalo CHADEMA wasipobadilika litawakumba

Tukianzia bungeni wabunge wengi wa CHADEMA wameanza kujisahau na hasa kusahau kilichowapeleka bungeni na kushindwa kutetea maslahi na maendeleo ya majimbo yao,wengi sasa wamejikita katika kuendesha hoja zao binasfi na sio za chama tena hapa nawazungumzia wale machachari kama Zitto, Mnyika, Wenje, Sugu na wasemaji wengine. Kazi ya kubeba chama imebaki kwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni Mh. Mbowe ambaye peke yake ndio anapigania maslahi ya chama, pia wapo wabunge wa chama ambao hawana msaada wowote katika kazi na hata hoja za chama bungeni wao wameshashindwa na wanasubiri tu mwaka ujao wa uchaguzi wakabidhi majimbo kwa CCM hawa ni kama kina Machemli, Kasulumabayi, Dr Mbasa na profesa Kahigi wakiwepo pia wengi wa viti maalum ambao hawabebi ajenda yeyote ya chama bungeni hivyo kuifanya sasa CHADEMA ionekane ya kawaida sana bungeni kwa hiyo kwa upande wa bunge ni kama wabunge wote wa CHADEMA wamemsusia Mbowe na kumfanya yeye peke yake abebe chama akisaidiwa kidogo na Mh Lissu

Katika kazi za nje za chama napo kuna mgomo baridi kwa mtazamo wangu kawa sasa kurugenzi zote za chama zimelala pono nahisi ni hangover za uchaguzi uliopita wakuregenzi wengi hasa baada ya kukabidhiwa mashangingi wapo busy kuandaa majimbo ya uchaguzi na kusahau shughuli za kujenga chama hali ambayo inamfanya katibu mkuu Dr Slaa awe peke yake katika kubeba ajenda za chama hapa wakurugenzi walio kwenye mgomo ni kama kina Kigaila, Lwakatare, Mrema na Komu, wote sasa hawafikirii chama na badala yake wanawaza hatma zao kisiasa.

Nasema hayo kwa uchungu mkubwa na ndio maana nikaleta utafiti huu hapa jamvini ili wajitekebishe na kuokoa chama chetu pendwa dhidi ya anguko linalokuja na tuache kuwasusia Mbowe na Slaa wao peke yao ndio wabebe ajenda za chama

Nitasema ukweli daima
 
MARCKO

JF-Expert Member
Jun 10, 2011
2,261
0
Kichwa cha habari ni kikali kama wembe wakati ndani ni (ubabe wa 'idealism' ) , hakuna chamsingi sana mbali na kukumbusha tuuu!
 
Fpam

JF-Expert Member
Apr 28, 2011
290
0
kuhusu bungeni hilo halina ukweli kinachojulikana ni kwamba wabunge wa Chadema wapo so active japo sio wote na haitakuja kutokea wote wakawa active.

Hoja binafsi ni kitu kinachohusu suala binafsi kama inavyojionyesha kuwa ni hoja binafsi lakini haivui dhamana ya mtoa hoja kuwa anasimama kwa kimvuli cha chama chake na ndivyo tunavyojua,

Kumbuka huo utafiti kuhusu bungeni bila shaka unahusu bunge lililopita ambalo lilikuwa ni fupi sana so tusingetegemea kila mbunge afanyiwe publicity ya kutosha hata hivyo wale wachache waliopata nafasi wametumia vizuri kwa manufaa ya chama
 
DALLAI LAMA

JF-Expert Member
Jan 31, 2012
8,614
2,000
Huna jipya..wakizunguka mnaanza kudai chadema wanavuruga amani.KESHO UTAISOMA KARAGWE.
 
  • Thanks
Reactions: PSM

adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,195
2,000
habari za jioni wakuuuuuu
nimeona nidondoke upya tena hapa jukwaani kueleza kwa kina hasa yale yaliyo moyoni na pia yanayokisibu chama changu pendwa chadema

kama ni mtafiti huru wa siasa za nchi yetu utaweka fikra zako juu ya mustakabali wa chadema na kama ni mkweli na huru wa fikra hutakawia kujua anguko zito ambalo cdm wasipobadilika litawakumba

tukianzia bungeni wabunge wengi wa chadema wameanza kujisahau na hasa kusahau kilichowapeleka bungeni na kushindwa kutetea maslahi na maendeleo ya majimbo yao,wengi sasa wamejikita katika kuendesha hoja zao binasfi na sio za chama tena hapa nawazungumzia wale machachari kama zito mnyika wenje sugu na wasemaji wengine kzi ya kubeba chama imebaki kwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni mh mbowe ambaye peke yake ndio anapigania maslahi ya chama,pia wapo wa wabunge wa chama ambao hawana msaada wowote katika kazi na hata hoja za chama bungeni wao wameshashindwa na wanasubiri tu mwaka ujao wa uchaguzi wakabidhi majimbo kwa ccm hawa ni kama kina machemli kasulumabayi dr mbasa na profesa kahigi wakiwepo pia wengi wa viti maalum ambao hawabebi ajenda yeyote ya chama bungeni hivyo kuifanya sasa chadema ionekane ya kawaida sana bungeni kwa hiyo kwa upande wa bunge ni kama wabunge wote wa cdm wamemsusia mbowe na kumfanya yeye peke yake abebe chama akisaidiwa kidogo na mh lisukatika kazi za nje za chama napo kuna mgomo baridi kwa mtazamo wangu kawa sasa kurugenzi zote za chama zimelala pono nahisi ni hangover za uchaguzi uliopita wakuregenzi wengi hasa baada ya kukabidhiwa mashangingi wapo busy kuandaa majimbo ya uchaguzi na kusahau shughuli za kujenga chama hali ambayo inamfanya katibu mkuu dr slaa awe peke yake katika kubeba ajenda za chama hapa wakurugenzi walio kwemye mgomo ni kama kina kigaila lwakatare mrema na komu wote sasa hawafikirii chama na badala yake wanawaza hatma zo kisiasa.

Nasema hayo kwa uchungu mkubwa na ndio maana nikaleta utafiti huu hapa jamvini ili wajitekebishe na kuokoa chama chetu pendwa dhidi ya anguko linalokuja na tuache kuwasusia mbowe na slaa wao peke yao ndio wabebe ajenda za chama

nitasema ukweli daima

Asante mkuu kwa utafiti wako.

Umetumia ainagani ya utafiti, maana hujaweka ni vipi umekusanya taarifa na kufikia conclusion.

umeandika kwa mtazamo wako unaona kunamgomo baridi (yaan wewe binafsi) Je kwa mtazamo wa wangine unasemaje? (please takwimu)

Umeweza kutaja majina machache ya wabunge unaodai hawafanyi chochote bungeni, Je umejaribu kuangalia kwa mtazamo wa michango ya wabunge against idad yao bungen ukalinganisha kwa maana hiyohiyo kwa upande wa vyama vingine tupe utafiti wako kwa data.

Sion tatizo katika maelezo yako mkuu nimtazamo wako ila mimi naomba unisaidie tu kunielewesha kama nilivouliza hapo juu.
 
kiLimIlire

JF-Expert Member
Apr 8, 2012
282
1,000
mbona tunaohitaji kuendeleza mapambano tupo wengi,watakaosusa watuachie gap tuendeleze mapambano dhidi ya nduli ccm
 
Molemo

JF-Expert Member
Sep 24, 2010
14,098
2,000
habari za jioni wakuuuuuu
nimeona nidondoke upya tena hapa jukwaani kueleza kwa kina hasa yale yaliyo moyoni na pia yanayokisibu chama changu pendwa chadema

kama ni mtafiti huru wa siasa za nchi yetu utaweka fikra zako juu ya mustakabali wa chadema na kama ni mkweli na huru wa fikra hutakawia kujua anguko zito ambalo cdm wasipobadilika litawakumba

tukianzia bungeni wabunge wengi wa chadema wameanza kujisahau na hasa kusahau kilichowapeleka bungeni na kushindwa kutetea maslahi na maendeleo ya majimbo yao,wengi sasa wamejikita katika kuendesha hoja zao binasfi na sio za chama tena hapa nawazungumzia wale machachari kama zito mnyika wenje sugu na wasemaji wengine kzi ya kubeba chama imebaki kwa kiongozi wa kambi ya upinzani bungeni mh mbowe ambaye peke yake ndio anapigania maslahi ya chama,pia wapo wa wabunge wa chama ambao hawana msaada wowote katika kazi na hata hoja za chama bungeni wao wameshashindwa na wanasubiri tu mwaka ujao wa uchaguzi wakabidhi majimbo kwa ccm hawa ni kama kina machemli kasulumabayi dr mbasa na profesa kahigi wakiwepo pia wengi wa viti maalum ambao hawabebi ajenda yeyote ya chama bungeni hivyo kuifanya sasa chadema ionekane ya kawaida sana bungeni kwa hiyo kwa upande wa bunge ni kama wabunge wote wa cdm wamemsusia mbowe na kumfanya yeye peke yake abebe chama akisaidiwa kidogo na mh lisukatika kazi za nje za chama napo kuna mgomo baridi kwa mtazamo wangu kawa sasa kurugenzi zote za chama zimelala pono nahisi ni hangover za uchaguzi uliopita wakuregenzi wengi hasa baada ya kukabidhiwa mashangingi wapo busy kuandaa majimbo ya uchaguzi na kusahau shughuli za kujenga chama hali ambayo inamfanya katibu mkuu dr slaa awe peke yake katika kubeba ajenda za chama hapa wakurugenzi walio kwemye mgomo ni kama kina kigaila lwakatare mrema na komu wote sasa hawafikirii chama na badala yake wanawaza hatma zo kisiasa.

Nasema hayo kwa uchungu mkubwa na ndio maana nikaleta utafiti huu hapa jamvini ili wajitekebishe na kuokoa chama chetu pendwa dhidi ya anguko linalokuja na tuache kuwasusia mbowe na slaa wao peke yao ndio wabebe ajenda za chama

nitasema ukweli daima
Majitaka at works...!
 
adolay

JF-Expert Member
Dec 8, 2011
11,195
2,000
mbona huyu mleta hoja hajitokezi kutuelewesha yanayotusibu katika uzi wake?
 
MgungaMiba

JF-Expert Member
Aug 28, 2011
975
1,000
Mtoa mada pengine una nia njema lakini inaelekea u mvivu wa kufuatilia, wakurugenzi uliowataja mbona wanajituma sana, angalia Benson Kigaila, hekaheka zote za M4C yuko mstari wa mbele na dhahama zote zinamfika, hata nyumbani kwake sidhani kama ana muda, Mrema si mtu wa makelele sana lakini anajituma sana, hata Arumeru aliongoza yeye, Lwakatare anapugania sana Red Brigade mpaka iko effective, sijaona Mkurugenzi aliyezubaa. Bungeni kuna utaratibu wa kuongea si kila mbunge atapata nafasi, cha msingi kaangalie majimboni mwao Kama wanawajibika ipasavyo au la, kuongea tu Bungeni pekee hakutoshi kumpa ushindi Mbunge. Mwenyekiti Mbowe kwakuwa ni KUB anapewa nafasi ya kipekee kuongea ndo maana unamsikia sana.
 
Domy

JF-Expert Member
Dec 12, 2011
4,698
1,195
Fuatilia karagwe kesho.ndipo utakapojua CHADEMA ni chama bora Africa.
 
Thanda

JF-Expert Member
Apr 6, 2012
1,915
0
Majitaka at works...!
Mkuu Molemo tusimshambulie huyu jamaa. huo ni mtazamo wake hivyo tunapaswa kuuheshimu.....Being critical by point ni nzuri sana na haipaswi kuwaacha kuwasemasema hawa wabunge wetu kwani ni kweli wameanza kujisahau wakati 2015 bado ni mbali....Ni mtazamo tu.
 
TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
2,000
Mbowe kasusiwa chama????
Yawezekana ndio sababu ya mbowe kuanza kumuta sumaye aje amsaidie???
Duuuh mbowe naye kwa hasira ameamua kupeleka nguvu zake kwa kikwete yaani amenyoosha mikono juu na kusema kikwete wewe ndiye rais pekee niliyekuona tangu nianze siasa.
Dr.slaa yeye kazi yake ni kutoa matamko tu siku hizi tena akiwa amejifungia ofisini
dr.slaa yeye amevunjika moyo jabisa baada ya kubamizwa kwenye chaguzi za kata alipoambulia patupu kata zote alizopewa atembelee na kufanya mikutano
 
Tukundane

JF-Expert Member
Apr 17, 2012
10,566
2,000
Kwa majimbo ambayo wabunge wake ni kutoka chadema kama wanapwaya katika majimbo hayo hayatakabidhiwa kwa ccm kama ulivyoeleza.wanaopwaya katika majimbo hayo ni kama vile askari anavyo kufa vitani au kuchoka vitani watawekwe pembeni na wengine watasonga mbele ndani ya cdm hihii. tunao askari wengi waakiba wanasubiri nafasi ili wasonge mbele.
 
TUNTEMEKE

JF-Expert Member
Jun 15, 2009
4,587
2,000
mkuu molemo tusimshambulie huyu jamaa. Huo ni mtazamo wake hivyo tunapaswa kuuheshimu.....being critical by point ni nzuri sana na haipaswi kuwaacha kuwasemasema hawa wabunge wetu kwani ni kweli wameanza kujisahau wakati 2015 bado ni mbali....ni mtazamo tu.
kazi ya molemo ni kutibua tibua yaani yeye hanaga hoja hata siku moja...ataishia kulialia tu kwamba mnamsema mbowe na dr.slaa
molemo uwezo wake wa kuchambua hoja na kuzijibu accordingly ni nusu kaputi.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom