Mbowe na Slaa kutikisa Zanzibar kesho

Mbowe na Slaa kutikisa Zanzibar kesho

Hao wanachama wa CDM maelfu wametoka wapi zanzibar? Au mwandishi alikuwa naandika tu kujifurahisha?

Na mbona usingojee hadi hadi hayo maelfu ya watu yakosakane kwanza ndipo uje na post yako?
 
Najua nimepig nyuki ndimu lakini kua na ustahmilivu mkuu! Kumbuka Watanganyika sio sawa na Wanzanzibari, huko ikifika Uchaguzi ukiwa na vijipesa unaweza kuwahadaa watu kwa; pombe, kanga, pilau, ubwabwa, 'Sadaka', takrima, 'kifuta machofu' na kulichukua jimbo kiurahisi na ama kuwapata wananchi wengi wa kukuwekea kura lakini tofauti kwa Wazanzibari.

Wazanzibari kwao siasa ni Ukombozi na hawakubali kununuliwa kiurahisi kwa vitu vya kimaajabu majabu, kwao wao siasa imo ndani ya damu yao! Kitu chengine umesema yule mama alivuliwa mtandio na sio hijabu! Hoja sio hijabu mtandio au kilemba bali ni jinsi walivyomkashifu yule mwanamama!

@mpemba mbishi, hapo kwenye red, Maalim Seif kanunuliwa kwa kiasi gani? Hata mtoto wa darasa la nne anaweza kukuambia kuwa aliyeshinda 2010 ni Maalim na sio Shein. Mtafute Zitto akupe mkanda wote. Utakatifu ni mgumu sana. Kama ambavyo kuna watu wananunulika Tanganyika hivyo hivyo Zanzibar nako wapo watu wanaonunulika.
 
Sijui kama ni wakati muafaka au la, lakini kama wataona inafaa CHADEMA wangetumia fursa hii huko Pemba kueleza aina ya Muungano wanaotaka. Yale aliyosema Lissu bungeni kwa kiasi kikubwa ndio watu wa Zanzibar na hasa Pemba wanataka lakini kwa sababu CCM waligeuza bunge kuwa sehemu ya mipasho hoja ya Lissu ilipotoshwa vibaya sana. Sasa wawaeleze wananchi nini hasa wanashauri kuhusu Muungano.
 
Mwenyezi Mungu awatangulie watetezi wa watanzania na hiyo ndiyo ibada kuu.for the first time zanzibar itapata ukombozi wa kweli, na huo ndo utakuwa mwanzo wa maandalizi ya kuchukua nchi 2015.
 
Wewe umeshawahi kuja Pemba au unaropokwa hapa mtandaoni tu!
 
@mpemba mbishi, hapo kwenye red, Maalim Seif kanunuliwa kwa kiasi gani? Hata mtoto wa darasa la nne anaweza kukuambia kuwa aliyeshinda 2010 ni Maalim na sio Shein. Mtafute Zitto akupe mkanda wote. Utakatifu ni mgumu sana. Kama ambavyo kuna watu wananunulika Tanganyika hivyo hivyo Zanzibar nako wapo watu wanaonunulika.

Pale uliangaliwa Uzanzibari kwanza, siasa za vita kwa sasa hazina nafasi tena kwetu sisi. Au wewe ulitaka tuanze kufanyiana vurugu muje na vifaru mutumalize! Wewe hujasikia kama Mkapa na Mwinyi walishajipark Bwawani kwa kwa ajili ya kuanzisha fujo?
 
Mwenyezi Mungu awatangulie watetezi wa watanzania na hiyo ndiyo ibada kuu.for the first time zanzibar itapata ukombozi wa kweli, na huo ndo utakuwa mwanzo wa maandalizi ya kuchukua nchi 2015.

Mkuu wambie Wanyamwezi wenzako waombe Wazanzibari waukatae Muungano ili CHADEMA muchukue madaraka 2015. Na pengine Tanganyika yenu itakua imeshafufuka, ingawa sina uhakika kama mutaita jina hili tena kwani mzimu wa Nyerere unawahangaisha!
 
Mabadiliko ya siasa ya vyama vingi yameanza rasmi Zenji baada ya CUF na CCM kushindwa kuonyesha hilo
 
CDM kweli wapambanaji. Wameamua hasa kuhakikisha wanachukua na Zenji, kazi kweli kweli
 
mwaka huu lazima kieleweke watasema sana ila moto utawaunguza tu, unajua hawa wanao wapinga Chadema wanaogopa madhambi waliyo yafanya kuwekwa peupe, wananchi kuambiwa ukweli
 
Mlioko uwanja wa mapambano mturushie live na picha.Nimeambiwa na jamaa yangu aliyeko huko kuna heka heka kubwa huko za maelfu ya wanachama wa CDM
 
hawana mtaji

WanaJF,
Niko uzini leo siku ya Tatu. Naomba niwahakikishie wanachadema na wapenzi wenu kuwa tutafanya mpaka kieleweke. Uzini wananchi ni waelewa sana. Wanapenda hoja na si porojo. Wanaopiga porojo kwenye jamvi hili au hawajui kinachoendelea on the ground au wanasukumwa na ushabiki tu kama walivyozoea. Uzini na Zanzibar iko tayari kwa mabadiliko makubwa. Uzini tofauti na watu wanavyofikiri Chadema ina matawi sasa kila Shehia katika Shehia (sawa na vijiji au mitaa bara). Jana nimezindua ofisi, matawi,maskani 7 katika majimbo mbalimbali nje ya Uzini mathalan Mfenesini,Magogoni, Bububu na kadhalika. Kwa hakika moto utakaowaka kutokea Bambi(Uzini) tunakozindulia Kampeni yetu kwa hakika utaunguza Zanzibar yote. Kwa bahati mbaya ndani ya Uzini hakuna network isipokuwa Zantel na hata hivyo hakuna mtandao (internet hadi uende mjinZanzibar. Ndio maana hakuna taarifa. Tunaomba radhi. Lakini kuanzia leo waandishi wa habari watakuwepo ambapo jioni wanaweza kuleta habari wakirejea mjini.
Narudia tena wananchi ni wakarimu sana. Kwa kuwa hakuna guesti kabisa wananchi wamewapokea timu yetu ya Kampein kwenye nyumba zao. Hii ni dalili njema. Tunawashukuru sana.
 
Asante baba na Rais wetu wa moyoni
Nimefurahi sana kwa taarifa hii nzuri na ya kutia matumaini.Tunawatakia kila la kheri na Mungu yuko upande wetu.
 
Back
Top Bottom