Mbowe na Slaa kutikisa Zanzibar kesho

Mbowe na Slaa kutikisa Zanzibar kesho

Ninawajua vizuri watu wa Uzini, ndio walioanzisha joto la Mapinduzi, na ndipo maandalizi yalioongozwa na John Okello yalipotimia, ni waafrika wuesi pure na hawababaishwa na mhindi kama Raza wa CCM, watampa yeyote wale, hata awe Chadema ilmradi wajitambulishe vizuri, na wawashika watu wa maana jimboni, mi baadhi ninao, lakini niko mbali, ningeisaidia Chadema.
Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CDM) kesho kitazindua kwa kishindo kampeni za Uchaguzi mdogo wa Uwakilishi jimbo la Uzini ambapo chama hicho kimejizatiti kuchukua kiti hicho na kuandika historia mpya ya chama hicho huko Zanzibar.

Taarifa ya CDM imesema vinara wakuu wa chama hicho Freeman Mbowe na Dr Wilbroad Slaa watawaongoza maelfu ya wanachama wake wa Zanzibar hapo kesho katika uzinduzi unaotarajiwa kuwa wa kihistoria.

Taarifa zaidi kutoka Zanzibar zinasema tayari Dr Slaa amewasili tangu jana kupanga mikakati ya mwisho mwisho.Pia kuna taarifa kwamba kuna shamrashamra za hapa na pale za wafuasi wa CDM.

Habari zaidi:Tanzania Daima.
 
Kazi kweli kweli kwani Padre alikuwa na kikao kifupi na askofu mkuu wa jimbo katoliki nZnz kuweka mambo sawa ili waumini wote wakitoka tu kanisani waelekee uzini.

kazi kwenu.
Soma sainecha yangu hapa chini
 
Feedback,
Hiyo picha imechukuliwa Lushoto Tanga na sio Zanzibar..Mkuu umeamini sasa Utabiri wangu ujio wa chama kipya - CCK kimesajiliwa niliyasema ukatukana sana.. Leo yako wapi?

Mkandara CCK imekushtua nini? Mbona kuna kingine tena kipo hatua za mwisho kusajiliwa? Kwa siasa zetu hata vikifikia 50 si hoja.
 
Sababu za Chadema KUSHINDWA Uzini .
1. Mgombea wao hana makazi Unguja
2. Chadema hawajawahi kupeleka fedha za ruzuku Unguja
3. Viongozi wa Chadema wafikapo Unguja wanalala katika hosteli zinazomilikiwa na kanisa
4. Katika bunge la Muungano matamko ya akina Lissu ni kukebehi Zanzibar

HIZO NI SABABU TOSHA ZA Chadema kukalia pua UZINI!!!!!
:crutch:

Mkuu MAFILILI,
Tena Chadema kama watampeleka Tundu Lissu, Zanzibar wataambulia kura mbili tu ya Mgombea na ya mke wake.
 
Nimeishasema Chadema wakishinda uwakilishi mie tatembea bila nguo kutoka Posta mpaka Kimara bonyokwa na kurudi baada ya apo nakunywa sumu nakufa.
Mkuu anza kupiga jaramba ikiwa ni pamoja na kujiandalia sanduku-ili usiwasumbue ndugu zako
 
Hao wanachama wa CDM maelfu wametoka wapi zanzibar? Au mwandishi alikuwa naandika tu kujifurahisha?

Wapo mkuu hata kama hawatafika hayo maelfu,wakati wa kampeni last 2010 niliona kiasi flani japo still wana kauoga kakutotaka kujionyesha hadharani,inakuwa ni kama hali ile ilikuwepo bara enzi zile upinzani ndo unaanza,watu hawakutaka kujionyesha,au kama lilivo kwa watumishi wengi wa umma leo wanapenda upinzani ila hawataki kujitokeza kiviiiile!
 
kila jambo ni kuamua;hata mbuyu uliota kama mchicha:nendeni hakuna chama kilicho na hati miliki ya jimbo
 
Lakini nyie CDM si ndio mnapinga muungano sasa mnataka nini Zanzibar?
Kwanza CHADEMA hawapingi muungano na ndiyo maana wana wanachama mpaka Unguja na pemba na hata huyo mgombea wao ni mwanachama wao pia, au naye si Mzanzibar kwa sababu tu anagombea kupitia CHADEMA?

Pili hata wagombea wa vyama vingine viwili (CCM + CUF = wavurugaji) nao pia wakichaguliwa watakwenda kuapishiwa Dodoma na wala si Kibanda Maiti au Maisara. Nafasi inayoombwa ni kwa ajili ya Watanzania na wala si kwa ajili ya Wanzibar na CHADEMA imekidhi vigezo vyote vya kuweka mgombea kwenye uchaguzi huo.

CHADEMA haipingi Muungano bali haikubaliani na aina ya Muungano tulio nao wa upande mmoja kuwa na Serikali yake na Upande Mwingine kuwa na serikali inayochangiwa na watu wa Upande mwingine kwa kisingizio cha Serikali ya Muungano. Watanganyika hawana chuki na Wazanzibar na wala Wazanzibr hawana chuki na Watanganyika bali kuna Mabazazi wachache ndiyo wanaochochea chuki dhidi ya watanganyika kwa faida yao!!
 
Kila la heri,
Wananchi siku hizi wameshatambua ukombozi wa kwel wa Mtanzania utatoka wapi, hasa wanavyoona kazi ya CDM. Zanzibar kwa sasa hakuna chama kikubwa cha upinzani CDM kwa sababu CCM = ccm+cuf.
 
Kwanza CHADEMA hawapingi muungano na ndiyo maana wana wanachama mpaka Unguja na pemba na hata huyo mgombea wao ni mwanachama wao pia, au naye si Mzanzibar kwa sababu tu anagombea kupitia CHADEMA?

Pili hata wagombea wa vyama vingine viwili (CCM + CUF = wavurugaji) nao pia wakichaguliwa watakwenda kuapishiwa Dodoma na wala si Kibanda Maiti au Maisara. Nafasi inayoombwa ni kwa ajili ya Watanzania na wala si kwa ajili ya Wanzibar na CHADEMA imekidhi vigezo vyote vya kuweka mgombea kwenye uchaguzi huo.

CHADEMA haipingi Muungano bali haikubaliani na aina ya Muungano tulio nao wa upande mmoja kuwa na Serikali yake na Upande Mwingine kuwa na serikali inayochangiwa na watu wa Upande mwingine kwa kisingizio cha Serikali ya Muungano. Watanganyika hawana chuki na Wazanzibar na wala Wazanzibr hawana chuki na Watanganyika bali kuna Mabazazi wachache ndiyo wanaochochea chuki dhidi ya watanganyika kwa faida yao!!
Umenena maneno mazuri sana!....lakini subiri uone Viwavi jeshi vya magamba vitakavyokushambulia. Big up Kigarama!
 
anaepinga muungano ni jusa na seif;wasiyotaka hata upanuzi wa mipaka yetu ya baharini
 
Kumbe hiki ni chama cha watu wawili..nilikuwa silifahamu hili!
Wanataka kufanya kila kitu wao, hawataki kuwapa wengine nafasi! Kwa mtindo huu chama kitakua?

Hujapata Bwana we Bweg.e naona Full astellia
 
TIME WILL TELL...

NANI ALIDHANI cdm WANGEWEZA KUWA NA WABUNGE KWENYE MIKOA MBALIMBALI NCHINI NJE YA KANDA YA ZIWA NA KASKAZINI KAMA MAGAMBA YALIVYO HUBIRI?

chadema NI MASHINE TATA!!!

Na ukumbuke kanda ya ziwa ilikua ni ngome imara ya magamba,baada ya elimu hawataki tena kusikia tena uchafu huo!cuf imewaangusha wa znz,kwa hiyo dhambi hii inaanza kuwatafuna!wazanzibar ni waelewa
 
It is a good start....nadhani hapo CCM wanakaa kimya sasa,maana walikuwa wanasema CDM haipo Zenji..lol!!
 
Lakini nyie CDM si ndio mnapinga muungano sasa mnataka nini Zanzibar?

Wewe na we kichwa maji! Chadema wanataka muungano wa serikali tatu ambao utakuwa na maslahi Sawa kwa pande zote. Kwa taarifa yako chadema ndo wanaowatetea wanzanzibari ili wapate haki yao ila kwa sababu ya udini wenu mtaendelea kung'ang'ania magamba yenu hata kama yanawanyonya. Kwa taarifa yenu uchaguzi unaokuja shilingi itageuka sijui mtaSema nini tena maana watu wanaowatetea mnawaona makafiri ila wanaowatumia kama toliet paper mnawaona wanawafaa kisa Mnashare imani poleni maana maumivu yenu yataendelea sana bado kama hamtakubali kuachana na mtazamo hasi Kwa wasiokuwa wa imani yenu. Poleni maana Mungu akisema ndiyo hakuna kati yenu atakayeweza kuibadilisha ikawa hapana! Mungu huwaheshimu wale wampendao na kumtumikia kwa uaminifu. Dr. Slaa na Mbowe na wananchama wengine wa chadema wanawatumikia wananchi kwa uaminifu na Mungu atawaheshimu na mtashangaa mambo makubwa yatatokea kupitia watu hawa.
 
Sababu za Chadema KUSHINDWA Uzini .
1. Mgombea wao hana makazi Unguja
2. Chadema hawajawahi kupeleka fedha za ruzuku Unguja
3. Viongozi wa Chadema wafikapo Unguja wanalala katika hosteli zinazomilikiwa na kanisa
4. Katika bunge la Muungano matamko ya akina Lissu ni kukebehi Zanzibar

HIZO NI SABABU TOSHA ZA Chadema kukalia pua UZINI!!!!!
:crutch:

Amekuwa vipi mgombea huko wakati hakai huko , maana navyojua mimi hakuna sehemu ambayo hawataki masiala kwenye hilo klama znz, huko kupiga kura tu, lazima huwe huko for more that 3/5 years!
 
Back
Top Bottom