UFUNUO WA TANZANIA
JF-Expert Member
- Apr 7, 2013
- 471
- 166
Acha vitisho visivyo na mashiko. Amin amin hao uliowataja watapita, na wewe utapita lakini CHADEMA itabaki. Saa 24 umetoa nyingi sana. Halafu pia wewe nauna madhara. Ni nyoka wa kijani
Najiuliza tu, hivi hiki chama chetu si kina mwenyekiti, na katibu? Haiingii akilini Zitto naibu katibu anashambuliwa na Lema na baadhi ya wanaoitwa makada wa chadema then mwenyekiti na katibu hawasemi lolote. Hivi angekuwa amesemwa John Mnyika, Josephine Mushumbusi ama Slaa si matamko yangetolewa? Mungekaa Kimya?
Binafsi nina matatizo na mwenendo wa Zitto, lakini katika hali ya kawaida uongozi wa chadema mmechemsha, badala ya kujibu hoja mnaleta risiti zinazomhusu Zitto sasa hizo risiti tuzifanyeje?
Ninachotaka kuona ni maamuzi yasiyo na double standard. Yaani hiki chama kimekuwa cha ajabu sana yani kwa mfano wapo vijana kama Yericko Nyerere anatoa matamko utafikiri chadema ni chama cha shangazi yake (naongea kama wanachama wanavyosema huku mitaani) na haoni madhara ya anayoyaandika humu.
Natoa saa 24 Mbowe na Dr Slaa najua mtasoma hii post, mchukue hatua na kuhakikisha Zitto hashambuliwi katika taratibu zisizo sahihi, laa sivyo nitaungana na wanachama wa kanda yangu tutatoa tamko latakalofuatiwa na kujitoa katika shughuli zote za kichama. Tunaweza!
More updates
--------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------------
Sasa hivi ni saa sita mchana..Mpaka sasa yamebaki Masaa Tisa. Bado nasubiri kusikia Tamko la Mwenyekiti wa chama, ama Katibu... Laa sivyo tutachukua maamuzi magumu.
Sizgates, Vipi ..?? Saa 24 bado hazijatimia ili 'uondoke' kama ulivyosema..??
Sipati picha utakavyobebwa juu-juu kwenye mkutano wa hadhara...!!
FaizaFoxy atakuwepo mkutanoni akipiga vigele-gele..??
![]()
Acha vitisho visivyo na mashiko. Amin amin hao uliowataja watapita, na wewe utapita lakini CHADEMA itabaki. Saa 24 umetoa nyingi sana. Halafu pia wewe nauna madhara. Ni nyoka wa kijani
Yamebaki masaa sita.
Mwambie Slaa asifanye mzaha na makamanda kama Sixgates, ohoooo shauri yenu.
Hapana.
Mwambie sixgates ajiandae kubebwa mgongoni..??
Na alivyo ki-mbau-mbau, atarushwa-rushwa angani kama shujaa...!!
Kikwete atakuwepo...Vipi 'utatia' timu kwenye mkutano huo wiki ijayo..??
Unashangaza sana, unampa nani saa 24, unadhani Chama ni familia, siyo kila kitu kichojadiliwa kwenye mitandao nicha kutolea tamko.. Mnyika mkurugenzi wa Habari na Uenezi alishatoa tamko na alishwakemea viongozi wasiotumia vikao kutoa hoja zao, yanayosemwa na wananchama hakuna wa kuyazuia hata wewe huwezi, wanaoleta risit za Zitto siyo viongozi wa chadema ni wanachama tu, na hawakilishi uongozi wa chadema!
Jamani tuwe wahalisia;Mnataka Mbowe ama Slaa watoe tamko la nn? Wamkemee Lema kisa Zitto ni naibu katibu mkuu? Angekuwa anawathamini hao mnaotaka wamkingie kifua ingepasa wafanye hivo.Kama mtu anahangaika kukupindua uongozini utamteteaje? Hapa msiniulize mapinduzi yaliyopangwa na kina Zitto na masalia wengine,muulize Mamuya,Saanane,Mwampamba ama dada yetu Juliana Shonza.
Zitto angetumia siasa safi kuhusu malengo yake,angekuja kuwa kiongozi mzuri sana wa nchi yetu.
Huwa najiuliza,hii haraka na papara ya Zitto ni ya nini?
Zitto ajibu hizo nyaraka na ushahidi wa akina Nassary,aache kuomba huruma ya watu kwa kujifananisha na viongozi wa MALASYIA NA India
Ufunuo asante kwa kumpa za uso, huwezi kumpa saa 24 Dr Slaa kwa lipi?
Moja ya jambo linalokera ni kutaka kumfanya Dr slaa kama mungu wa chadema. Yeye kama anakosea akosolewe, mara nyingi anakosea na tunamkosoa. Sasa mimi sio fuata upepo.
Hapana.
Mwambie sixgates ajiandae kubebwa mgongoni..??
Na alivyo ki-mbau-mbau, atarushwa-rushwa angani kama shujaa...!!
Kikwete atakuwepo...Vipi 'utatia' timu kwenye mkutano huo wiki ijayo..??
We bana ondoka tu chadema,usiwatishe viongozi. Inaonesha una chuki binafsi. Toka nenda ccm. Kwa nini hata kwa aliyeleta rist(YERICKO NYERERE) unawatuhumu viongozi wa chama? Kwani Yericko anacheo gani makao makuu?.unaposema wameishia kuleta rist,ina maana Yericko angekemea ndio ungemuelewa kama kiongozi? Nimeshakwambia Mnyika(msemaji wa chama) alishalitolea ufafanuzi hilo.tafuta uzi wa Pasco usemao, lema kumshambulia zitto,ni ushujaa wake au udhaifu wa viongozi wa juu?(kimsingi kauli ya Mnyika ndio kauli ya chama-ndio kauli ya Mbowe-ndio kauli ya dr slaa). Unachokitaka ni kitu kisichowezekana. Binafsi sitaki kuona Mbowe,dr au mwingine yeyote akiingilia kazi ya Mnyika tena kwa jambo ambalo alishalitolea ufafanuzi. LENGO lako ni kuondoka chadema,toka tena uwahi bungeni ukatambulishwe kabla vikao havijaisha.kafanyiwe kama walivyofanyiwa wenzako kina Shenzi na Stella.