Mbowe: Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote CHADEMA

Mbowe: Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote CHADEMA

Mimi nilishangaa mbowe ulipo paza sauti unataka kwenda mahakamani kwa kuwa tu masha amekatwa kwenye ubunge wa east africa,unataka kuwapa moyo wanachama watiifu!
 
Mbowe ili mtu awe msaada kwa CHADEMA anataka apewe hela yupo kibiashara zaidi
CHADEMA Mbowe peke yake ndo siyo mzigo. Wengine wote mizigo tupu!!!

Hata akina Mgeja, Sumaye, Lembeli na hata Lowasa nao ni mizigo tu. Hata Nyarandu ajiangalie sana asije akawa mzigo. Mianasiasa !!!
 
Anakuja mtu anakuambia nchi hii ina Upinzani!
Inachekesha sana
Mbowe Kaisha changanyikiwa si yeye
 
uchaguzi wa TLS?? masha did well

insipiration to new members..

mbowe akae kimya, kuna siku atahama.na yy wenzake watasema alikuwa mzigo
Chadema ni kama bahari samaki mkubwa anawala samaki wadogo na kipindi samaki mdogo anapokuwa mkubwa naye anawala wale wadogo.
 
Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amesema aliyekuwa mwanachama wao ndugu Masha hakuwahi kuwa na msaada wowote ndani ya chama chao tokea alipojiunga akitokea CCM.

Chanzo: Gazeti la Nipashe!

My take:
"Sizitaki mbichi hizi", Sungura akagumia
Kama hakuwa na msaada, ilikuwaje ndiye akaonekana bora zaidi ndani ya CHADEMA, hadi skate ukiwa na kugombea ubunge wa Afrika Mashariki, akiwa na Wenje?
 
masha alitoa mchango gani kuhusu yale mambo alioyaona kuwa chadema haijafanya vizuri ?
 
TLS sio chadema
Naona wengi sana mmetumia nguvu kubwa sana kutuaminisha kuwa tls sio chadema.

Hivi nani ambaye hajui kuwa tls sio chadema?

Tunajua vizuri sana.

Nyie endeleeni kujipumbaza na kuzungusha mikono na viuno.
Ila ukweli utabaki pale pale kuwa mwenyekiti Mbowe kaishiwa hoja.

Hawezi kuwezesha chama kushika dola.

Sikutegemea mwenyekiti mbowe amjibu masha vile.
Angetumia busara sana kama Anemshukuru Masha na angechukua ushauri wa Masha na angemuahidi kuuganyia kazi.

Alichofanya mwenyekiti ni kujibu kiwema sepetu sepetu.

Mwenyekiti hana nia ya kuongoza dola.
Ajitafakari na akae pembeni.

Wenye uwezo wa kuongoza chama wapo wengi.

Ninavyoona imefika muda sasa aweke wazi tu kuwa chadema ni saccos.
Kwa sababu saccos kazi yake ni kutengeneza profit.
 
Kweli kamanda amechoka naye. Watu tunajua jinsi alivyosimama na kutetea demokrasia. Na zaidi ya kusaidia sana TL kuwa rais wa Chama cha Wanasheria Tanzania, amesota sana Lumande kule Sumbawanga muda fulani kwa sababu ya kujenga chama.
 
Masha ni mbahili tofauti na Lowasa, Masha kashindwa kutoa mpunga kwa mangi Mbowe. Ni haki yake kusema hakuwa msaada wowote, mangi Mbowe yuko kimaslahi zaidi.
 
sasa yeriko nyerere na masha nani ana impact kwenye siasa za nchi hii ???

au yule bananga na masha nani ana impact kwenye siasa za nchi hii

basi kama masha hana impact hao niliowalinganisha nae ndo hovyo kabisa kama huyo bananga anajionaga kama rais vile kumbe mpuuz mmoja tuu


chadema mlimtumia masha ili mpate ushawishi kanda ya ziwa lakini haikua riziki
 
Back
Top Bottom