Huu ulafi wa madaraka wa Mbowe sasa umepitiliza yaani jamaa hataki kukubali kabisa kwamba ukomo wake wa kiuongozi ndio umekomea hapo na hakuna jipya atakalolileta ndani ya Chama,Mbowe hataki kuamini kuwa Chadema sio kichanga tena Chama kimeshakuwa sasa na kina Makada wengi wenye uwezo mkubwa wa kuongoza kushinda hata yeye sasa kwanini hataki kuwapa nafasi na wengine wagombee?Halafu kwakweli hakuna kitu muhimu kama elimu ya juu kwasababu inapanua upeo wako wa kufikiri na kuyatafakari mambo kabla ya kuyaongelea au kuyatenda.Ebu mwangalie Mbowe anasema hawezi akakiachia Chama sasa kwasababu bado ni kichanga,Je aliwahi kufikiria Makada wengine watajisikiaje pale wanapoonekana hawaaminiwi na yeye wazi wazi si watajiona kama hawana thamani yoyote katika Chama na hii ndio sababu migogoro Chadema haitakoma kwasababu Mwenyekiti haoni kama wengine wana haki ya kugombea nafasi yake.Hii ndio Demokrasia ambayo amekuwa akiipigania katika majukwaa ya kisiasa wakati yeye mwenyewe anaikandamiza katika Chama chake?Kweli Mbowe?