Baada ya uchaguzi mdogo wa Madiwani kumalizika na kukipa ushindi wa kishindo CCM, huku CHADEMA kikiambulia Kata 3 ikiwemo ile ya SOMBETINI iliyoko Arusha mjini, Imeibuka minong'ono kuwa Sababu kubwa ya MWENYEKITI WA CHADEMA FREEMAN MBOWE kutopenda kuona uongozi wa juu wa CHAMA hicho ukibadilika na hasa kutoka watu wa kasakzini na kwenda kwa wanachama wanaotokea mikoa ya Kanda zingine ni hofu ya mikoa hiyo ya kaskazini kupoteza nafasi za kiutawala kama vile Udiwani na ubunge. MBOWE ni mbunge wa jimbo la HAI mkoani Kilimanjaro
Viongozi wengine wa CHADEMA wanaotokea kaskazini wenye hofu hiyo ni pamoja na Mbunge wa Arumeru Mashariki, JOSHUA NASSARI, Katibu Mkuu wa CHADEMA , WILBROAD SLAA anayetokea jimbo la Karatu ambalo halmashauri inaongozwa na upinzani(CHADEMA), Mbunge wa Arusha Mjini, GODBLESS LEMA wa arusha mjini.
Wachunguzi wa mambo ya siasa wanasema pamoja na PHILEMON NDEASAMBURO kuwa mzee sana, lakini ndiye anaweza kuwa na uhakika wa kushinda endapo uongozi wa CHADEMA taifa utabadilika na kwenda kwa watu ambao siyo wakazi wa mikoa ya Kaskazini.