Mbowe kuwania tena uenyekiti CHADEMA

Mbowe kuwania tena uenyekiti CHADEMA

Aisee ...

Hii sasa chama cha siasa au kampuni binafsi..

Oneni aibu basi hata wagombea wengine waruhusiwe hata kama ni Mbowe na Lema (maigizo)

Nawasikitia wanachama na wachangiaji wa mfuko huu wa kanda maalum

Msichoke ..kama kwa kakobe mnaweza kutoa nini chadema ..
 
Kama chama bado ni kichanga kwanini kinataka kipewe nchi?

Mbowe atapita bila kupingwa maana zitto hayupo.

Mbowe ni muoga sana hakika.

Hata hivyo uenyekiti wa chadema ni wa mbowe milele hakuna cha kuwania.

mbona uenyekiti wa vyama vingine hamuutolei povu kama huu wa CHADEMA?
 
Mbowe lazima agombee ana hisa kubwa sana ndani ya NGO hiyo. Na yeyote atakayempinga ajiandae kufukuzwa.

TANZANIA DAIMA + DAIMA=MBOWE DAIMA
 
Bravo kamanda wa Anga.. wasaliti wote chali.. CHADEMA daima hadi mtanganyika akombolewe!

Ndiyo mkuu , kama Mbowe siyo mwiba mchungu kwao , kwanini walitaka kumuua pale soweto Arusha?

hii imekula kwa magamba.......
 
Mbowe anafaa kuwa mwenyekiti wa CDM. Ni jabali la kisiasa lisiloweza kuhongeka! Salaam ziwafikia vibaka wote wa CCM!
 
Story kama za LEMA hizi. anusurike kuuwawa kwa lipi hasa? anamtishia nani? mtu mwenyewe hata hoja hajui kuzipanga, hata elimu ya kushindana kwenye nyadhifa mbalimbali hana, yeye ashukuru baba mkwe wake amempa huo ulaji.

Vpi umeshatoka Msalani kunya?Je umetawaza vzr maana nahc harufu kali unaitoa!
 
Katika hatua nyingine, Mwenyekiti wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amesema

kuwa kamwe hatakiacha chama hicho katika uchanga wa harakati za kulikomboa taifa kama kiongozi wake wa juu.


Akihutubia katika mikutano ya Operesheni M4C Pamoja Daima katika sehemu mbalimbali mkoani Morogoro jana,

mwenyekiti huyo alisisitiza kuwa, bado atagombea nafasi ya uenyekiti kwa lengo la kuendeleza harakati za ukombozi

wa pili wa taifa hili.

Halima Mdee anguruma
Naye Mbunge wa Kawe, Halima Mdee, ambaye yuko katika msafara wa mwenyekiti huyo, alisema vijana wengi wanaochipukia katika

siasa kupitia chama hicho, wamelelewa na Mbowe, ambao leo wamekuwa chachu ya mabadiliko nchini.


"Ukweli ni kwamba kamanda huyu wa anga (Mbowe), ndiye ametulea vijana wengi nikiwemo mimi, tena wengine hatukuwa na ujasiri

tulionao sasa, asiwadanganye mtu, hasa sisi vijana kwamba tuliingia CHADEMA na umaarufu, hawapo hao, tumelelewa na huyo

kamanda," alisisitiza huku akipigiwa makofi.



Bila kutaja jina, Mbowe alionya kuwa wenye fikra za kuachiwa chama hicho kikiwa katikati ya ukombozi huo

hawatapata nafasi, kwa sababu hawana nia thabiti ya kukiendeleza, bali wana nia ya kukibomoa kwa kutumiwa na

wapinzani wa CHADEMA.


"Makamanda, kumbukeni kuwa chama hiki na sisi viongozi wake tumepita katika majaribu makubwa na hata

kukoswakoswa kuuawa. Mimi nimekoswakoswa kuuawa kwa bomu huko Arusha, lakini pia kuna watu wamepoteza

maisha, wamefungwa jela, wengine wamekuwa vilema, halafu watu wengine wanatusaliti kwa kupewa visenti ili

wakivuruge chama na wanataka tuwape chama. Huu ni uendawazimu," alisema.


Mwenyekiti huyo alisema CCM imekuwa ikifanya jitihada za kuihujumu CHADEMA kwa mbinu mbalimbali, zikiwemo za

kupandikiza migogoro, jambo ambalo limeshindwa kufanikiwa kwani Mungu ameweka mkono wake ili kisisambaratike.


"Harakati hizi tunazofanya za kuwakomboa Watanzania mjue tunahatarisha maisha yetu, tumejaribiwa kushawishiwa

ndani na nje ya Bunge ili tuwe kondoo, tumekataa. CCM wamekuja na mbinu za kupandikiza migogoro wameshindwa na

sasa wanaomba nife wakifikiri nikifa na CHADEMA itakufa. Nawaambia CHADEMA haifi kwa kuwa tumezalisha

makamanda wengi, watakiendeleza," aliongeza Mbowe.


Akielezea kwa mara ya kwanza kwa undani zaidi kuhusu mauaji ya Arusha, mwenyekiti huyo alisema wana ushahidi wa

kutosha kwamba polisi walihusika na mauaji hayo na kuongeza kuwa waliohusika ni polisi wa kutoka mkoani Morogoro.


"Kwa mara ya kwanza niliseme hili, mauaji ya Arusha yaliyofanyika kwa kurusha bomu katika mkutano wa kampeni za

CHADEMA, yalifanywa na polisi ambao walitoka mkoani Morogoro. Ndiyo maana tunaendelea kumwambia Rais Jakaya

Kikwete aunde tume ya kimahakama ili kupata ukweli wa jambo hili," alisema.

My Take: Sina, habari imejitosheleza

- Wallahi this is biggest joke of mylife!!

Le Mutuz
 
Hilo bomu alilitengeneza yy mwenyewe ili iwe ndo kauli yake kuwa alinusurika kuuawa na bomu shame on his face,kawauwa raia wasio na hatia ili aendeleee kukalia kitu,n Mungu alivo wa ajabu ataendelea paskia ikulu kwenye gazet la Tanzania Daima tuuuu
 
Mbowe hana tofauti na Mugabe au Museven au PK kwa sababu huwa wanahisi hamna mzalendo au mtu mtu mkomavu wa kushika hatamu ya viti vyao(Uroho wa madaraka),wote hao watatu wanahistoria ya kuchachua katiba kwa kuondoa ukomo wa madaraka(like PK.MU7,Mugabe)
Sipati picha angekalia ikulu na dola lake jinsi kulivyo kutamu sijui kama angeachia madaraka!!
Hao ndo type ya viongozi wahafidhina wa kiafrika(angekua yeye ni Madiba au Nyerere sijui ingekuaje?)
 
huyu jamaa mpaka afe, cdm ni ujasiliamali unaomuingizia hela nyng mbowe hawez kuacha ufalme wake kirahis hiv hivi
UDP toka ianzishwe Mwenyekiti ni Cheyo tuu, CUF kwa vipindi vitatu sasa Lipumba ni Mwenyekiti, CCM sasa inabadilisha tu wazee toka huku kwenda kule na bado vyama hivi vyote vimezorota na vinaelekea KUFA. Hilo hulijadil bali chadema inayoimarika kila kukicha chini ya Kamanda Mbowe ndiyo mnaipa ushauri wa kipuuzi, hebu endeleeni na shughuli nyingine; tunashukuru kwa ushauri wenu wa ovyo lakini TUMEUKATAA!!!!!!!!!
 
vyama vya ukombozi huwa makini sana na mamluki kama ifanyavyo sasa cdm! hatuwezi kuwakabidhi chama fisi waliojaa tamaa!!!
 
kweli kamanda,ia naamini kabisa msaliti mkubwa wa chadema ni zitto kabwe,huyu kijana ni mbaya sana,yaani ni kibaraka wa ccm,eee mungu tuepushe na wasaliti wengine kama zitto anaetumiwa na ccm,peoples powerrrr
 
Ni upuuzi kumuacha mwenyekiti mwenye mafanikio na kumpa uenyekiti msaliti
 
Dhana ya Mwenyekiti lazima awe na association na Mzee mtei acha iendelee
Mbowe ndo chama kitamfia mikononi
 
Back
Top Bottom