Mbowe, Jipime kwa mustakabali wa CHADEMA, Kinusuru Chama

Mbowe, Jipime kwa mustakabali wa CHADEMA, Kinusuru Chama

Kifyatu

JF-Expert Member
Joined
Oct 12, 2010
Posts
3,382
Reaction score
3,226
Kwa kweli nimesikitishwa sana namna chama mahiri cha upinzani kama CDM kudhalilika kiasi hiki katika uchaguzi huu mkuu. Niliipenda CDM-Asilia lakini ilipoingiliwa na wana CDM-Maslahi niliamua kuitosa na kumpigia debe Magufuli.

Uchaguzi umekwisha na tunae Raisi.

Je Tunao Upinzani Mahiri Tena?
Kwa kweli CDM imeathirika sana na inaweza kumeguka vipande vipande. Kwa sasa naona ACT-Wazalendo wanaweza kupata wafuasi wengi sana na kuwa chama kikuu cha upinzani ifikapo 2020. Sidhani kama tuna upinzani mahiri tena kwa sasa.

CDM Wafanye Nini Sasa:
Cha kwanza ni kumng'oa haraka sana yule rubani aliebadilisha gia angani na kukiangamiza CHOMBO.

YES, lazima mheshimiwa Mbowe awajibike haraka sana kama wana CDM watakuwa na imani tena na chama chao, la sivyo itakuwa ni mafuriko kuelekea ACT, au CCM. Leadership ethics zinamshinikiza Mbowe aachie kiti.

Utabiri wangu uchwara ni kuwa sidhani CDM inaweza kuji-rehabilitate tena katika miaka mitano ijayo. Pengine ni mpaka 2025 ndio wanaweza kuwa na nafasi ya kuwania uraisi ikiwa tu mabadiliko katika ngazi za juu yawe yalishafanyika jana.

Katika mabadiliko haya ya ngazi za juu ni muhimu CDM wasiwape waTanzania hisia ya kuwa hiki ni chama cha watu wa kanda ya kaskazini - itawagharimu sana.

Tanzania haiwezi kusonga mbele kama chama tawala hakiwezi kuogopa kuwa kuna upinzani mahiri. Kwa anguko hili la CDM na UKAWA, Tanzania hakuna upinzani tena, trust me.

Sheikh Mbowe mdogo wangu, kiongozi wangu, jipime halafu ukinusuru chama. Bado muda upo lakini hii window of opportunity ni fupi sana.

Please do the needful.
 
Chama kikishindwa uchaguzi huwa vinabadilisha viongozi.CHADEMA Sijui muulizeni Mzee MTEI.
 
Kweli. Chadema si ajabu kikawa ni chama kizuri ila wengine tukimuangalia Mbowe, au Lema tuna conclude ni genge la wahuni illiterate.
Ni kweli, a new chairman is needed. Angalizo... Asiwe Mchaga wala mwenye undugu na Mtei, Mbowe.
 
Upinzani utashamiri tu ikiwa katiba mpya itapatikana yenye kuondoa umungu mtu na tume huru ya uchaguzi na muungano ufumuliwe na kusukwa upya ikiwa bado twauhitaji anyway. Dola iongezewe watu wenye fahamu kwa kufanya intake zao zipate watu wenye pass za hali ya juu na siyo failures. Hapo ndiyo ubabe utakoma na uchaguzi utakuwa huru na haki..
 
Thubutu uone. Unajua nini kilimkuta Zitto? CHAgaDEMA ina wenyewe
 
chama cha ba mkwe aende wapi,tatizo ni nyinyi wafuasi hamuelewi.hicho chama cha kibiashara zaidi,siasa ni mojawao tu ya kukifanya kiwe hai
 
Kama wewe ulisha hamia kwa Magufuli haya ya Chadema yanakuhusu nini tena? Fanya kazi uchakachuzi umekwisha tumepata rais wa kichina.
 
Huu ni upuuzi mkubwa sana.... Mbowe hawezi kujiuzulu...kwa lipi???? Ninyi mnafikiri Slaa angeshinda eeeh???, Nani alikuambia kuwa CCM itashindwa kwenye sanduku la kura???? Goli mkono lilishasemwa???,

Ulitaka Mbowe afanyeje???

Huku ni kufikiri kiccm kuwa Mbowe ajiuzulu!!! Mimi nasema hapana, hapana, hapana!!!

Ndani ya CDM hakuna ana uwezo kumfikia Mbowe kwa sasa!!!

Zito asingeasi na akawa na subira angeweza lakini ndo ivo!!!
 
Binafsi nilikuwa fan wa CHADEMA O.G ila baada ya Mbowe kuleta upuuzi wa gia angani sikuona jipya zaidi ya kubaki CCM O.G
 
Mazwazwa ya lumumba yanamshauri kamanda mbowe..hahahah
 
BIG UP UKAWA mmefanya kazi kubwa sana hata watawala wanafahamu, hakuna kulala tunahitaji katiba mpya. Bila katiba mpya ni ndoto kushinda uchaguzi au kupata maendeleo ya ukweli. Mbowe usibabaishwe na watu wenye malengo ya kuua upinzani Tanzania. Vijana wengi bado wana imani na UKAWA, anzeni kuandaa timu kubwa zaidi ya vijana wazalendo, wachunguzeni watu mnaowapa madaraka. Wapo bado watu wenye mapenzi ya kweli ya nchi hii na tunawaamini.
 
Kwa sasa tujiandae kuona mpambano wa bwana toka mashariki na bwana toka magharibi kwa mwanamwali bikira asiyemjua mume. Vizawadi vimeanza kutolewa, majigambo na tambo vimeanza. Maskini mwanamwali bikira wala hajisumbui kutafakali mustakabali wake
 
Hapana Mkuu, ACT unayoisema inapata wapi ongezeko la wanachama ilhali ina Mbunge mmoja tu !! Mbowe kafanya mengi katika kikijenga chama, katika uchaguzi huu amefanikiwa kviweka pamoja vyama vinne vyenye itikadi tofauti na wote tumeshuhudia kilichoendelea na idadi ya wabunge wa upinzani walipatikana pamoja na mazingira yasiyo sawa ambayo wamekabiliana nayo.

Hata kama CDM haijashinda Urais, lakini kuna chembe ya mbegu imepandwa kwa Watanzani na itaendele akuchipuka taratibu miyoni mwao ili mradi tu wabunge wa UKAWA waisimamie Serikali ipasavyo. Pamoja na mazuri aliyofanya Mhe. Mbowe bado kuna umuhimu wa kufanya Uongozi wa Chama uwe wa Kitaifa ambao wananchi wa Tanzania wanajiona kama sehemu ya chama kupitia viongozi kutoka maeneo yao.

Kwa mfano chama kama ccm Mwenyekiti anatoka Pwani, Makamu - Iringa, Itikadi na Uenezi - Mtwara; Katibu Mkuu - Arusha; Meneja Kampeni - Mara. Unaona kabisa kuwa chama kina utaifa na hao watu wanaisadia kuoneza hicho chama katika maeneo hayo. Bulembo akismama kuongea, watu wa Mara wanaona kuwa wanawakilishwa katika hicho chama.

Sasa bila kumumunya maneno angali nyumba ya pili (CHADEMA) ambayo wanategewa kuwatoa kimasomaso husasan Uongozi wakati wa kampeni ulikuwaje: Mwenyekiti - Arusha; Mgombea - Jirani; Meneja Kampeni- Jirani; Mkurugenzi wa Fedha - Jirani; Mwenyekiti Mwenza aliyekuwa anaongea sana na vyomba vya habari-Jirani.

Katika hali kama hiyo mwananchi. Katika hali kama hii, chama kinawezaje kushika nchi ? Hebu fanyeni chama kuwa cha Kitaifa acha kulalamika ilihali mnajidhoofisha wenyewe.

Mnategemea kweli mwananchi wa kawaida kutoka kijijini akiambiwa kuwa hiki chama ni cha Kikanda atashindwaje kuamini kama kipewa mifano hiyo !!!
 
Back
Top Bottom