Mbowe 'awekewa kisu' shingoni na Lowassa

Mbowe 'awekewa kisu' shingoni na Lowassa

DuppyConqueror

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2014
Posts
9,466
Reaction score
6,970
Taarifa zilizonifikia ni kwamba CHADEMA ipo kwenye wakati mgumu sana baada ya Lowasa kuweka masharti (conditions) kuwa ACT WAZALENDO lazima iwe sehemu ya UKAWA ili kuongeza nguvu katika umoja huo.

Inasemekana kuwa upinzani mkubwa umetoka kwa Mh. Mbowe ambaye ametafsiri sharti hilo kuwa ni sawa na kuwekewa kisu shingoni na Team Lowassa na wala kamwe hayupo tayari kurudia matapishiyake.

Inasemekana kuwa baada ya mvutano mkubwa, Mh amesikika akitishia kuingiza document ya Memorandum of Understanding kwenye 'Shredder' (Machine ambazo hutumiwa maofsini kuharibu documents/karatasi zenye taatifa za siri).
Wazee/washauri wakuu wa chama wamelalamikia jambo la Mh. Mbowe kushindwa kuweka "personal issues" pembeni kwa maslahi mapana ya chama.

Swali la kujiuliza: Hizi siasa za vinyongo na uhasama zitaisha lini?

Karibuni tujadili haya mambo muhimu kwa mustakabali wa Taifa.
 
DuppyConqueror

Hizi habari sio za kweli. Ni mwendelezo wa siasa za kitapeli, kilaghai na kipuuzi ambazo kwa muda mrefu sasa zimekuwa zinaenezwa na CCM-ACT na mawakala wake. CHADEMA wanaendelea na kura za maoni kuanzia leo wakijandaa na vyama washirika ndani ya UKAWA kuchukua nchi October, 2015. Mleta uzi km huu ni tapeli, muongo na mnafiki. Tutakufuatilia tujue uko sehemu gani tukushughulikie. Mods wawe wanawapa ban wahuni kama hawa ambao kazi yao ni kueneza uongo na uzushi. Hiyo ACT sio chama cha siasa, ni genge la wahuni, majizi, matapeli, walaghai na wasaliti. ACT=CCM
 
Last edited by a moderator:
DuppyConqueror

Kama walimuona Lowassa hafai hapo awali na sasa anafaa, iweje kwa Zitto isiwe vivyo hivyo? Wanasahau kuwa kwenye negotiations maadui huwa wanaweka common ground ili wote kufaidika.
 
Last edited by a moderator:
Huwa naamini katika siasa hakuna rafiki wala adui wa kudumu,lolote linaweza kutokea labda kama kuna uadui binafsi baina ya wanasiasa.
 
Hizi habari sio za kweli. Ni mwendelezo wa siasa za kitapeli, kilaghai na kipuuzi ambazo kwa muda mrefu sasa zimekuwa zinaenezwa na CCM-ACT na mawakala wake. CHADEMA wanaendelea na kura za maoni kuanzia leo wakijandaa na vyama washirika ndani ya UKAWA kuchukua nchi October, 2015. Mleta uzi km huu ni tapeli, muongo na mnafiki. Tutakufuatilia tujue uko sehemu gani tukushughulikie. Mods wawe wanawapa ban wahuni kama hawa ambao kazi yao ni kueneza uongo na uzushi. Hiyo ACT sio chama cha siasa, ni genge la wahuni, majizi, matapeli, walaghai na wasaliti. ACT=CCM

Umenifurahisha hapo ulivyosema utanifuatilia unishughulikie...Nakuamuru uwe makini kibao kisije kukugeukiwa wewe mwenyewe!
 
asante kwa taarifa nzuri
 
Wakati zito anamuuliza Lowasa 'mzee vipi!? Mbona kila anayechomoka anaelekea CDM? Hii inaniua mzee!'
Maana hata machali alihakikishiwa kuwa jamaa yupo njiani kujiunga nayo.
 
Umenifurahisha hapo ulivyosema utanifuatilia unishughulikie...Nakuamuru uwe makini kibao kisije kukugeukiwa wewe mwenyewe!

Huwezi hata kidogo. Siwezi kuwa makini na tapeli hata siku moja. Wewe ndio utashughulikiwa. Utaletaje hbr za upuuziiii mtupu jamvini? Hilo genge lenu la wahuni & matapeli linatafuta tu promo kwa migongo ya wengine. CHADEMA wanaendelea na kura za maoni nchi nzima kuanzia leo hadi tar.25 July. Wambie na genge lenu la ACT-TANZANIA / WAZALENDO; a.k.a genge la wahuni & wasaliti wafanye kura za maoni tuone kama wana ubavu
 
Uebu anayejua kinacho endelea atujuze acheni propaganda ambazo hazina maana. Nikwel lowasa leo ndo anaongea na waandishi wa habar?
 
Mbowe atafakari umuhimu wa Zito kwenye umoja huo .
Kama ni kweli basi chadema kisipoangalia kitaendelea kuwa chama cha upinzani milele.Kwenye siasa za demokrasia hakuna adui. Hapo ni hoja tu hakuana vita za msituni ya kutumia bunduki hivyo hakuna haja ya kujenga chuki.Sisi wote ni watanzana.
Wapinzani inabidi waanze kwanza kwa kuitoa CCM madarakani kwa kura baada ya hapo wajipange kuleta maendeleo kwa kushika nyadhifa zote muhimu kuanzia wakurugenzi ,wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,mawaziri,mabalozi na wakuu wa idara mbalimbali.Huko ndiko wanapoumizwa wananchi. Uraisi wamwachie Lowasa.
 
Back
Top Bottom