UncleBen
JF-Expert Member
- Oct 27, 2014
- 9,693
- 12,320
Nimegundua tu kuwa watanzania ni waongo sana
Sasa kwenye siasa kuna ukweli mkuu ?
Nimegundua tu kuwa watanzania ni waongo sana
Huwezi hata kidogo. Siwezi kuwa makini na tapeli hata siku moja. Wewe ndio utashughulikiwa. Utaletaje hbr za upuuziiii mtupu jamvini? Hilo genge lenu la wahuni & matapeli linatafuta tu promo kwa migongo ya wengine. CHADEMA wanaendelea na kura za maoni nchi nzima kuanzia leo hadi tar.25 July. Wambie na genge lenu la ACT-TANZANIA / WAZALENDO; a.k.a genge la wahuni & wasaliti wafanye kura za maoni tuone kama wana ubavu
Ni haki ya Mbowe kufanya hivyo kwani anajua vizuri chama kilikotoka, kilikopitia na pia zitto alidiroki kumtukana mbowe matusi ya nguoni na utu wake wakati Mbowe ndie aliyemfikisha zitto alipo. Nami namuunga mkono kumkazia zitto kama VP lowasa akaungane na zitto kwenye chama cha Asasi ya Chama Tawala
Hata ningekuwa mimi nisingekubali kwa Zitto kuwa sehemu ya Ukawa jamani, Edo aje lakini ACT hapana
Kwa ujinga wako huu upinzani usingekuwepo mileleKwa ujinga huu CCM ina haki ya kutawala milele.
My instinct tells me something...
Mkuu kwa suala la Zitto itakuwa ngumu. Chadema ndio chama kinachojua gharama na athari za utukutu na ubinafsi wa Zitto, Na mtu ambaye amejisikia vibaya sana kutokana na dharau na usahaulifu wa Zitto ni Mbowe. Kwa hiyo Chadema haipo tayari kurudi ilikotoka na kama Zitto ana nguvu kiasi mnachokisema basi Lowassa aungane na Zitto ili tuone kama watachukua nchi. Na sio Mbowe pekee asiyetaka Uhusiano wowote baina ya chadema na Zitto bali kuna wanachadema wengi zaidi tusiotaka kuona Zitto anahusiana na Chadema. Jamaa alikuwa ni pasua kichwa sana ndani ya chama. Tupo wengi tunaoamini Zitto ni mnafiki na mbinafsi sana na hawezi kutushawishi kuwa eti ana dhamira ya kweli ya kuiondoa ccm madarakani.Mbowe atafakari umuhimu wa Zito kwenye umoja huo .
Kama ni kweli basi chadema kisipoangalia kitaendelea kuwa chama cha upinzani milele.Kwenye siasa za demokrasia hakuna adui. Hapo ni hoja tu hakuana vita za msituni ya kutumia bunduki hivyo hakuna haja ya kujenga chuki.Sisi wote ni watanzana.
Wapinzani inabidi waanze kwanza kwa kuitoa CCM madarakani kwa kura baada ya hapo wajipange kuleta maendeleo kwa kushika nyadhifa zote muhimu kuanzia wakurugenzi ,wakuu wa wilaya,wakuu wa mikoa,mawaziri,mabalozi na wakuu wa idara mbalimbali.Huko ndiko wanapoumizwa wananchi. Uraisi wamwachie Lowasa.
Taarifa zilizonifikia ni kwamba CHADEMA ipo kwenye wakati mgumu sana baada ya Lowasa kuweka masharti (conditions) kuwa ACT WAZALENDO lazima iwe sehemu ya UKAWA ili kuongeza nguvu katika umoja huo.
Inasemekana kuwa upinzani mkubwa umetoka kwa Mh. Mbowe ambaye ametafsiri sharti hilo kuwa ni sawa na kuwekewa kisu shingoni na Team Lowassa na wala kamwe hayupo tayari kurudia matapishiyake.
Inasemekana kuwa baada ya mvutano mkubwa, Mh amesikika akitishia kuingiza document ya Memorandum of Understanding kwenye 'Shredder' (Machine ambazo hutumiwa maofsini kuharibu documents/karatasi zenye taatifa za siri).
Wazee/washauri wakuu wa chama wamelalamikia jambo la Mh. Mbowe kushindwa kuweka "personal issues" pembeni kwa maslahi mapana ya chama.
Swali la kujiuliza: Hizi siasa za vinyongo na uhasama zitaisha lini?
Karibuni tujadili haya mambo muhimu kwa mustakabali wa Taifa.
DuppyConqueror
Hizi habari sio za kweli. Ni mwendelezo wa siasa za kitapeli, kilaghai na kipuuzi ambazo kwa muda mrefu sasa zimekuwa zinaenezwa na CCM-ACT na mawakala wake. CHADEMA wanaendelea na kura za maoni kuanzia leo wakijandaa na vyama washirika ndani ya UKAWA kuchukua nchi October, 2015. Mleta uzi km huu ni tapeli, muongo na mnafiki. Tutakufuatilia tujue uko sehemu gani tukushughulikie. Mods wawe wanawapa ban wahuni kama hawa ambao kazi yao ni kueneza uongo na uzushi. Hiyo ACT sio chama cha siasa, ni genge la wahuni, majizi, matapeli, walaghai na wasaliti. ACT=CCM