Mbowe atolewa nje ya bunge

Mbowe atolewa nje ya bunge

cjui unaongelea wilaya ipi hai kuna kila kitu maji shule zahanati mbunge wetu aligawa komputa kila shule ya sekondari bado tunamwamini sana mbunge wetu tunamwini sana tunamwombea aendelee na harakati za kuikomboa tz sisi wa hai tushakombolwe


Hakuna lolote nenda hai day pale uambiwe wanafunzi wangapi wanasoma tarakilishi..
 
hayo matatizo ya ukosefu wa maji, ajira na matatizo mengine unayoyasema ni common ktk majimbo yote ya uchaguzi tz، siyo hai tu, kama ungekuwa na kumbukumbu hata kidogo (kitu ambacho hauna) maana umeanza kujistukia kuwa utatukanwa kwakujua kuwa uko less imformed kwenye matatizo yanayoikabili nchi hii, utatuzi wa matitizo ya nchi hii hayawezi kutatuliwa na mbunge, na ukumbuke 2005-2010 mbowe hakuwa mbunge wa hai je huyo aliyekwepo kwann hakutatua hayo matatizo ya maji na ajira?
Tukiacha ushabiki nchi hii inarudishwa nyuma na watendaji wa serikali kuanzia taifa mpaka halmashauri.

mbowe ametembea nchi nzima na chopa akiwahamasisha watanzania kuhakikisha swala la maji limeingia kwenye katiba mpya.unataka nini tena???watanzania wengine jamani?????
 
Katika Tanzania una uzoefu na wapi ambako utakuta vitu vilivyoko Hai utafikuta uko. Wilaya ya hai kwa majimbo mengine ni Ulaya ndogo. Wewe shukuru kuzaliwa Hai ole wako ungezaliwa Mtwara, Lindi, Songea, Rukwa, Singida kwa Mwigula husingekuwa unapayuka hivyo.
Mimi kwangu Wilaya na jimbo la Hai liko juu kama Ulaya ndogo wewe kalia majungu wenzako tunalinea wivu tunatamani lingekuwa jimbo letu na tungekuwa na Mbunge kama Mbowe.

Katika maendeleo sinaga upambe mtu akiboronga kama kawaida...tunampasulia wazi wazi sipendagi undumilakuwili...
 
Tatizo mojawapo la technology ni hili maana kuna watu wasioona shida kupoteza muda na hicho ndicho anafanya mleta hoja, ingelikuwa kuandika haya inahusisha kalamu/wino na karatasi kadhaa naamini usingelikuja kihivi!
 
Katika maendeleo sinaga upambe mtu akiboronga kama kawaida...tunampasulia wazi wazi sipendagi undumilakuwili...
Mkuu kunawatu hawatakinkuambiwa ukweli hata kama wanamapungufu kitu ambacho ni hatari sana kwa ustawi wa jamii.
 
mbowe ametembea nchi nzima na chopa akiwahamasisha watanzania kuhakikisha swala la maji limeingia kwenye katiba mpya.unataka nini tena???watanzania wengine jamani?????

Kama wilaya tu imemshinda ataweza nchi nzima?
 
Kuna sauti za wabunge wa CCM zinasikika zikisema "KAMA ASKARI WAMESHINDWA WAWAACHIE WABUNGE WENYEWE". Hali ni tete kiukweli wabunge wanasukumana na askari

Taabu ya kuchagua mijitu mihuni kama wawakilishi wetu ndiyo matunda yake haya
 
Peopleeeeeeee!!!!!!

Sina shaka wengi mtaniona hamnazo lakini mimi nina dukuduku la moyoni na sina pa kusemea ni hapahapa jamvini potelea mbali mkinitukana ninaandika.

Kwa mbunge wetu wa wilaya ya hai kwa kweli navunjika moyo sana kwa sababu ni wilaya iliyonyuma sana kimaendeleo mkoani kilimanjaro kwa sababu zifuatazo:-

1. Kwa kipindi hiki hakuna maji. Hakuna hata juhudi za mbunge kuhamasisha uchimbaji visima maji safi yapo ardhini.
2. Sehemu kadhaa hazina umeme na hakuna sababu, pesa tunazo huduma hakuna na kuna utashi wa kisiasa katika hili. Pale kwa wasomali wana umeme mpaka kwenye nyumba za mabati matupu!
3.Hakuna hata kiwanda kimoja kwa ajili ya kutoa ajira kwa vijana/ Labda bajaj na bodaboda ambao kwangu hiyo ni kama upepo na majanga kwa vijana.
4. Mbunge wetu akija jimboni ni kwa taabu sana na akija lazima FFU tuwategemee hata kwa hotuba ambazo hazina joto la uchaguzi ni kusema CCM na CUF wakati maendeleo hatuyaoni. Sidhani kama siasa za namna hii tunazihitaji.
5. Tabia ya kutuma wabunge waje kukusafisha eti unamajukumu mengi ya kitaifa hoja hiyo ni tasa, mngetupa mtu wa kurutumikia.
6. Sina hakika kama unaofisi jimboni kwako.
7. Tabia ya kuja Hai na kupanda miti wakati wa jua kali na kundi la Chembe kidevu hatukuelewi hata kidogo kwamba ni sisi wananchi wa hai ndio tuliokuchagua ama Chembe kidevu.

Vyovyote inavyodhaniwa ama kusema ukienda jimbo lingine utachaguliwa ni hoja dhaifu tena haina uwajibikaji. Tunataka mrudi majimboni mtuletee maendeleo sio maandamano ama vurugu maana kwa miaka hii tuliyowapa dhamana sijaona mafanikio.

Kama kuna mtu anania ya kuwa mbunge hai aje tumsikilize hatuangalii chama tunaangalia mtu kwa kuwa sie sio wanywa viroba. Ninasikitikia sana uamuzi wangu wa kumpigia kura mtu huyu.

Je unambunge wa chadema amefanya nini jimboni kwako? unajua sera za chama chako?

Peopleeeee!

KUB, mwenyekekiti wa Chama Taifa, Mbunge na vyeo kadhaa, bado anafanya mambo ya kitoto kama yale ya bungeni leo? jamani leo nimeamini bora ukawa maskini lakini ukapata utajiri wa elimu.
 
Afadhali nyinyi huko hai umeme mnaupata, tuulizeni sisi tuliopo huku mbinga, umeme ni msamiati vijijini, barabara za lami ni msamiati, sasa hivi bei ya kahawa ipo chini sana na wakulima wanahangaika sana! Na majimbo yetu yanaongozwa na chama tawala tangu uhuru!
 
Naibu spika J. Ndugai ametoa amri Mbowe atolewe nje baada ya Mbowe kuomba muongozo ila Job Ndugai akamuamuru akae chini na asiongee chochote ndipo Mbowe akakataa kukaa mpaka asikilizwe anachotaka kusema.

Wabunge wa upinzani wamegoma Mbowe kutolewa nje na kinachoendelea ni kupigana kati ya askari na wabunge wa CHADEMA.

kiukweli ndugai hafai hata kuongoza kikao cha familia tuu. nikiona tu yupo pale mbele bungeni nahamisha station nacheki kbc au citizen tv bunge la kenya lina radha nzuri kuliko la tz la kizamani sana. hadi sasa inaonesha kama hata wabunge wa Ccm hawaujui mswada wenyewe kwa vile wanaonesha kutogusa chochote kwa mswada badala yake wanashambulia upinzani tuu. kwa hyo wapinzani wasingetia ngumu CCM wangekaa kimya bungeni ovyoooooo ccm
 
Kinachofanyika bungeni ni kutisha watu waione chadema haina mantiki iliccm iendelee kutawala na kujilimbikizia mali kama ilivyo kama katiba ya serikali mbili itapita kama ccm wanavyotaka basi ccm watakuwa wanatawala kiimla na hapa wanataka kupunguza idadi ya wajumbe kutoka zanzibar wa bunge la katiba ilisuport ya serikali tatu ipungue kwenye bunge la katiba.
 
Mimi naishi hai lete uongo wako hapa..
Mkuu naona kichwa chako kimechoka na hujasoma vizuri,

mimi nimesema hivi wewe umetutoa data nzuri ukaonesha jinsi mbunge wa hai ambavyo hajafanya kitu,

lakini akaja mtu mmoja hapa akaanza kukutukana bila hoja wala mifano hata data hana anakwambia linganisha iramba na isimani lakini hajatoa data zozote,

mimi nikamwambia mbona anakutukana bure wala hajatoa hoja yoyote ya msingi sasa mkuu mbona umeshindwa kunielewa.
 
Afadhali nyinyi huko hai umeme mnaupata, tuulizeni sisi tuliopo huku mbinga, umeme ni msamiati vijijini, barabara za lami ni msamiati, sasa hivi bei ya kahawa ipo chini sana na wakulima wanahangaika sana! Na majimbo yetu yanaongozwa na chama tawala tangu uhuru!
Inategemeana na kijiji chenyewe hai si pale mjini tu walitakiwa wawe na umeme vijiji vyote, sasa huyu form wao anavimba tu bungeni bila sababu.
 
Cdm ni chama kivuli na maendeleo ya jimbo lazima yawe kivuli. chagua ccm chama makini cha watu makini kwa maendeleo makini.
 
Last edited by a moderator:
CCM hakuna kitu. Kila mbunge anayeamka anasema CDM. Hivi kama siyo Upinzani, wabunge wa CCM si ingekuwa ni kusema YES to all government bill of laws??
 
Nadhani ni ishara ya wazi ya tatizo la uongozi wa Naibu Spika Huyo kwa kushindwa kusimamia na kujibu hoja chokochoko za Upinzani ambazo zipo katika mabunge yote Duniani yenye vyama vingi!

Sidhani kama Mh huyu anajua kuwa ni kipimo kibaya kinachomshusha hadhi yake?[ Mkuu umenena, inabidi waende shule wakasome Leadership]
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom