Kwa maoni yangu, linapokuja suala la kutii na kuheshimu sheria ushabiki wa kisiasa tuweke pembeni maana utiii wa sheria ndio msingi wa utawala wa sheria, demokrasia na amani. Mheshimiwa Mbowe kama alivyo Mh Doctor Slaa walifikishwa katika chombo cha sheria kwa tuhuma na kwa kuzingatia taratibui za kisheria. Wakapewa dhamana bila usumbufu wowote. Wakavunja masharti ya dhamana kwa kutohudhuria mahakamanai. Mh DR Slaa na Mh. Lema kwa kujuwa matokeo ya kukiuka masharti ya dhamana wakajisalimisha wenyewe mahakamani na kutoa sababu ya kutohudhuria. MH. MBOWE yeye akaamua kukiuka masharti ya dhamana kwa mara nyingine. Kama kwamba haitoshi akaanza kulumbana na mahakama kwa kutumia majukwaa ya kisiasa na vyombo vya habari. Kali hali kama hiyo jeshi la polisi lisingemkamata tungelielewa vipi? Hiyo si ingekuwa kudhalilisha mfumo mzima wa sheria na uhuru wa mahakama?
Kama MH. MBOWE angekuwa na utetezi kwamba yuko bungeni au ana kinga, angepaswa kujisalimisha mahakamani na kutoa utetezi huo badala ya kulumbana na mahakama katika vyombo vya habari. Pia angeweza kushauriana na wanasheria wake kuona uwezekano wa kupinga amri hiyo katika mahakama kuu kama aliona hakimu mhusika alishawishiwa na serikali.
Picha tunayoipata wananchi ni mbaya sana. Kama waheshimiwa wabunge ambao wenyewe wanaheshimika kwaajili ya kazi yao ya utunzi wa sheria wanakuwa wa kwanza kuzarau sheriia sisi walala hoi itakuwaje?
Magamba Typical!
Hapa wewe unaona ni sheria inafuatwa au ni udharirishaji tu wa wa wapinzani ? UNA AKILI AU MATOPE? Kwa akili yako fupi na wenzako Mbowe anaweza kutofika mahakamani kwa makusidi, mbona amekuwa ikihudhuria toka kesi ianze na kuahirishwa kila mara ili kuwapotezea muda tu?
kwa akili yako fupi unadhani kesi hii ni ya kweli au ni kujaribu kuficha makosa ya uuaji ya polisi.
Damu ya mtu haipotei hivi hivi, polisi waliua na wataendelea kuua maana damu ya watu wale inaendelea kuwasumbua mpaka watakapokili makosa yao na kutubu mbele ya wafiwa.
Nani asiyejua kuwa kesi zote tunazoziona ni politically motivated?
Kuna sheria gani inavunjwa kama watanzania wote wako salama hata kama chadema wakifanya maandamano kila siku na kila mahali?
Endeleeni kuwanyanyasa Chadema lakini mateso yenu yatakuwa makubwa kuliko mnayowafanyia wenzenu maana mnapanda kisasi.
Walikuwepo akina mbaraka,waliokuwa na utawala imara na hata nchi ilikuwa imetulia, leo wako wapi bwana?
kama wananchi wamewachoka ni better ukakubali ukakaa pemebeni wengine wakajaribu kuliko kung'ang'ania wakati nchi imewashinda!
Mtalazimisha kuitawala Tanzania lakini hamwezi kuwatawala watanzania!
Mungu ibariki Chadema
Mungu wabariki viongozi wa chadema
Mungu wabariki watanzania wenye uchungu na nchi yetu
Amen.