Fundi Mchundo
Platinum Member
- Nov 9, 2007
- 13,061
- 11,667
Na mtu mwenye akili timamu atasusia mara ngapi kabla ya kutambua kuwa mwenzake hana nia ya kubadilisha Katiba? Hamtagombea mwaka 2029 kama hapatakuwa na reforms? Na mwaka 2030 kama bado hamna mabadiliko? Hivi mnaamini kuwa CCM wataona aibu kutangaza uchaguzi kwa sababu tu CDM wamesusa?Yaani unataka watu wauawe, wateswe, uchaguzi uchafuliwe mara ngapi ili uone umuhimu wa mabadiliko ya Sheria za uchaguzi na Katiba?
Kama mtu una akili timamu kipi kinakuzuia kutambua kuwa kuanzia mwaka 2019, 2020,2024 uchaguzi uliharibiwa na huo ndiyo utakuwa muendelezo Kwa uchaguzi wa mwaka 2025?
Ni akili za aina gani zinazomfanya mtu kusubiri afanyiwe kosa Kwa zaidi ya mara ya tatu ndipo apambanie haki au utu wake!?
Hebu niambie mtapataje haki zenu nje ya sanduku la kura? Mnategemea EU watawapamania? Au Mahakama ndio itawapa ushindi? Clubhouse ndio zitawapa ushindi? Mpaka sasa hivi mmeshindwa kusema mtahakikishaje uchaguzi haufanyiki. Basi tuambieni mbinu mtakayotumia nje ya sanduku la kura?Hoja ya ajabu kabisa! Yaani watu wamezoezwa na watawala kuwa haki zao watapewa kwa hisani!
Mandela alikataa kwa miaka zaidi ya 27 kuachiliwa huru kwa masharti yasiyo na maslahi Kwa wananchi.Na mtu mwenye akili timamu atasusia mara ngapi kabla ya kutambua kuwa mwenzake hana nia ya kubadilisha Katiba? .
Badala ya kusema CHADEMA wamekata tamaa wewe ndiyo umekata tamaa. Kama CHADEMA wangekuwa wamekata tamaa hiyo mikutano wanayofanya ni ya kazi gani Sasa?Kushindana na chama kilichotawala toka nchi ipate uhuru sio kazi rahisi. Inahitaji uvumilivu na kuto kata tamaa.
Inaonekana CDM imekata tamaa.
Wanachodai CHADEMA ni uchaguzi huru na wa haki. Inawezekanaje kuamini kuwa mfumo wa uchaguzi unaoupinga unaweza kukupa haki?Hebu niambie mtapataje haki zenu nje ya sanduku la kura?
Unamfananisha Lissu na Mandela? Wakati wote ambapo Mandela alikuwa ndani chama kilikuwa vitani na utawala wa makaburu. Hawakusema kwa sababu watoto wao waliuliwa Sharpeville basi mapambano basi!Mandela alikataa kwa miaka zaidi ya 27 kuachiliwa huru kwa masharti yasiyo na maslahi Kwa wananchi.
Badala ya kusema CHADEMA wamekata tamaa wewe ndiyo umekata tamaa. Kama CHADEMA wangekuwa wamekata tamaa hiyo mikutano wanayofanya ni ya kazi gani Sasa?
Swali ni kuwa watafanya nini kama hayo madai yao yatapuuzwa? Wataendelea kukaa pembeni mpaka lini?Wanachodai CHADEMA ni uchaguzi huru na wa haki. Inawezekanaje kuamini kuwa mfumo wa uchaguzi unaoupinga unaweza kukupa haki?
Mantiki ya kushiriki kwenye uchaguzi usioamini mifumo yake ya uendeshaji, ni uwendawazimu!
Naunga mkono hoja. Nimemwelewa sana Mbowe, usipoteze imani na Rais Samia. Alivyo kwa Kauli na Matendo hawezi kuwa ni yeye!Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa ambaye huwezi kuzungumzia siasa za Tanzania bila ya kutaja jina lake. CHADEMA hii ya sasa ina mchango mkubwa sana wa juhudi za Mbowe kuifanya iwe imara.
Pamoja na mitizamo yetu dhidi yake, lakini tumheshimu yeye kama binadamu na mtu aliyechangia sana uimara wa CHADEMA
Mbowe apewe heshima yake!
CUF ipi?Swali ni kuwa watafanya nini kama hayo madai yao yatapuuzwa? Wataendelea kukaa pembeni mpaka lini?
CUF walisusa baada ya kufanyiwa dhulma ya wazi wazi. Leo warithi wao hawataki kusikia neno kususa. Mnatakiwa mjifunze kwao.
Yaani kuna aina ya binadamu kwa reasoning yao nabaki nashangaa kama ni binadamu kamili na timamu.Yaani unataka watu wauawe, wateswe, uchaguzi uchafuliwe mara ngapi ili uone umuhimu wa mabadiliko ya Sheria za uchaguzi na Katiba?
Kama mtu una akili timamu kipi kinakuzuia kutambua kuwa kuanzia mwaka 2019, 2020,2024 uchaguzi uliharibiwa na huo ndiyo utakuwa muendelezo Kwa uchaguzi wa mwaka 2025?
Ni akili za aina gani zinazomfanya mtu kusubiri afanyiwe kosa Kwa zaidi ya mara ya tatu ndipo apambanie haki au utu wake!?
Yaani kuna aina ya binadamu kwa reasoning yao nabaki nashangaa kama ni binadamu kamili na timamu.Ushahidi wa 2020 umesaidia nini?
Ushahidi wa local govt, 2024 umesaidia nimi?
Huo ushahidi unapelekwa wapi?
Kumbe CDM inapigania kizazi kijao cha CDM na sio watanzania wote?CUF ipi?
Bado mawazo ya wengi ni ya kibinafsi kuwa ni lazima wao ndiyo wafaidike na mifumo bora ila wao hawapo tayari kupigania uwepo wa mifumo bora kwa ajili ya kizazi kijacho! CHADEMA ya sasa inapigana kwa ajili ya CHADEMA ya kizazi kijacho.
Leo hii vyama vya siasa vya upinzani vinafaidika na marekebisho ya Sheria ya mikutano ya hadhara yaliyotokana na Christopher mtikila kupeleka kesi mahakamani. Jee Mtikila bado yupo?
Nani amesema kuwa watu hawataumizwa n.k.? Mnatuhakikishiaje vipi kuwa wafuasi wenu hawataumizwa wakati wanafuata njia mliochagua? Mimi sielewi mnategemea kupata mabadiliko vipi kwa kususia uchaguzi huku mkiepuka kuumizwa?Yaani kuna aina ya binadamu kwa reasoning yao nabaki nashangaa kama ni binadamu kamili na timamu.
Kitu kile kile kimetokea mara nne, leo eti unaamini tu kuwa kinawezekana kisiendelee kutokea tena!!??
Watu wameuwawa mwaka jana tu, tena kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa, kipi kitakuhakikishia kuwa kesho hawatakufa wengine kwenye uchaguzi mkuu!!??
Vijana wengi kama Ben Saanane tumpempoteza kwenye mikono ya Mbowe na mpaka mzee Kibao inasemekana Mbowe kuna mkono wake.Freeman Aikaeli Mbowe ni mwanasiasa ambaye huwezi kuzungumzia siasa za Tanzania bila ya kutaja jina lake.
Lakini naona Baada ya uchaguzi wa Januari 21 mwaka 2025, Kuna baadhi ya watu wanapambana kwa kila Hali kuonesha kuwa Mbowe alikuwa mamluki ndani ya CHADEMA na alikitumia chama kwa faida yake.
Mimi nakubaliana na wale wanaosema kuwa baada ya Mbowe kukaa madarakani CHADEMA kwa zaidi ya miaka 20, Kuna mambo alianza kutoyapa umuhimu na umakini wake kwenye kusimamia mambo ya msingi ulipungua.
Lakini ukweli lazima usemwe, CHADEMA hii ya sasa ina mchango mkubwa sana wa juhudi za Mbowe kuifanya iwe imara.
Wengine tunaomfahamu Mbowe tangu mwaka 2004 tunajua ni kwa kiasi gani amepambana kuifanya CHADEMA iwe hivi ilivyo.
Pamoja na mitizamo yetu dhidi yake, lakini tumheshimu yeye kama binadamu na mtu aliyechangia sana uimara wa CHADEMA hii ambayo sote ni wafuasi wake!
Kama tunaona Mbowe hakuna jema alilolifanya ndani ya CHADEMA, Iko siku na Lissu naye tutamdharau hivi hivi tunavyomdharau Mbowe.
Tukubaliane tu kwamba ni watu wachache sana waliopambana kama Mbowe ndani ya CHADEMA wakati akiwa kiongozi. Mbowe apewe heshima yake!
Hapa si tunazungumzia CHADEMA? Kwani watanzania wote ni wanasiasa. Au hata hujui mjadala unahusu nini?Kumbe CDM inapigania kizazi kijao cha CDM na sio watanzania wote?
Kwa hili la Lissu wewe ulitaka CHADEMA wafanyeje?Au mnangojea kibali cha serikali ili mumpigania kiongozi wenu aachiwe
Tulisema sana kabla ya uchaguzi hawa sio viongozi bali ni kundi la walalamikaji,hawana kesho hawa,wamejaa ubabe bila uwezo wa ubabeSiasa za visasi havitaisaidia Chadema.Jana Katibu wa Chadema wa Mkoa wa Kilimanjaro Bazil Lema amesimamishwa eti kwa kuandaa mkutano wa wanachadema wanaotaka kuhama chama.
Kwa mujibu wa Lema kikao cha kumsimamisha kingefanywa na kamati ya maadili ya Kanda kwa mujibu wa katiba..Anadai hakuna kikao kilichofanyika na amearifiwa kwa barua tu bila kuitwa.Tuhuma ni kwamba kuna mtu aliripoti kwamba ameambiwa Bazil Lema anaandaa mkutano.
Akihojiwa na Moshi FM Bazil Lema amedai chama kimekuwa kinaendeshwa kwa matamko na sio Katiba.
Kama Lisu na nyie mlisema yeye ndio mharibifu,huyo mharibifu na tapeli mnamtaka wa nini sasa hivi.Mbowe kanyamaza ila kila siku mnamtaja kuliko mnavyomtaja Mungu.Hapo yuko Kimya siku akiongea si ndio mtazimia na hao viongozi wenu watatu Heche,Lema na Lisu.Kwanza Lema kashafunga mdomo baada ya kujua upumbavu aliiofanya.Mbowe alikamatwa kwa ugaidi, Lissu akiwa hoi hospitali hakukaa kimya. Mdude labda ameshauawa, ila Mbowe hajali kabisa
Leo Lissu anataka kunyongwa makengeza utafikiri kafa, hasemi chochote. Kwahiyo kutetea haki siku hizi mpaka uwe na cheo???
Genge lake limepora mpaka akaunti za mitandao ya kijamii ya chama, yuko kimya na makengeneza yake.
Mbowe ni tapeli na alikuwa anaendesha CDM kama kampuni yake binafsi, na huko aliko anatamani kabisa Chama kife ionekane bila yeye mambo hayaendi.
Tapeli la kimachame
Kwa nini G55 sasa? Je, mbowe mnamhusishaje sasa?unajisumbua tu mkuu. BINAADAMU HAWANA SHUKURANI.
Suala la kutukanwa na kudhalilishwa Mbowe limenifanya nipoteze Imani na CHADEMA
G 55?Kama Lisu na nyie mlisema yeye ndio mharibifu,huyo mharibifu na tapeli mnamtaka wa nini sasa hivi.Mbowe kanyamaza ila kila siku mnamtaja kuliko mnavyomtaja Mungu.Hapo yuko Kimya siku akiongea si ndio mtazimia na hao viongozi wenu watatu Heche,Lema na Lisu.Kwanza Lema kashafunga mdomo baada ya kujua upumbavu aliiofanya.
Nafuu kunyamaza kimya. Mi siyo mbowe ila kwani lazima mbowe aseme?G 55?