Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Nape lazima afanye sherehe kwani mission yake ni kuimaliza ccm na sasa itakuwa " The mission has accomplished"

Nape ni mtu wa visasi sana, kipindi kile ccm walipomzingua akaenda kuanzisha CCJ akiwa na kina6 na bila kujua ccm wakamrudisha wakizani wameyamaliza kumbe wamerudisha nyoka mwenye sumu kali ndani na sasa keshawauma.
 
Sielewi kama uko makini na unachokiandika, kwani kura alizopata Magufuli alikuwa anashindana na Lowassa au ulitaka apewe nani ili ujue nyingi zilikuwa za wafuasi wa EL.
 

Suala ni kwamba tulikuwa hatujajipanga kwa ajili ya huu uchaguzi? Kama angechaguliwa huko CCM tungemwomba nani aje kwetu? Mkiti tusonge mbele hatumhitaji huyu jamaa kabisa kwani atafanya tushindwe uchaguzi.
 
So kweli kwamba ccm hakuna watu wema tatizo n mfumo lakn unaweza kuwa mcha mungu kuacha madhambi uliyoyafanya.kama kaamua na kuachana n mfumo wa ovyo apokelewe afuate taratibu za chama cha cdm.na ilikupata upinzan mkali n kuibomoa ccm kwa kuunganisha nguvu y kweli vyama vya upinzan vyote . Hakuna lisilowezekana hii hatua y kisiasa tuliyonayo nchi nyingi ziliptia na walifankiwa . N mtazamo wangu tu
 
Wamchukue tu , lakini hii sasa itakuwa vita ya ziwa na kaskazini! Labda awe mwanachama wa kawaida tu! Ina maana UKAWA hawawezi kushinda wenyewe mpaka waazime koti kwa jirani? Hili litakuwa doa na maccm ndo yatakapotupigia!
 

Akija Lowasa automaticaly umewakaribisha Chenge,Rostam,Karamagi nk
 
Wamchukue tu , lakini hii sasa itakuwa vita ya ziwa na kaskazini! Labda awe mwanachama wa kawaida tu! Ina maana UKAWA hawawezi kushinda wenyewe mpaka waazime koti kwa jirani? Hili litakuwa doa na maccm ndo yatakapotupigia!

Mpinzani wa Kweli atatoka CCM.maneno ya Nyerere yanataka kutimia
 
Labda aje kuwa mwanachama wa kawaida vinginevyo narudisha kadi.atasafishwaje huyu fisadi?hapo Zitto atawapigia bao.

Kamanda zzk hawezi kuitisha CHADEMA au UKAWA, yule ni project ya ccm tu not otherwise. Viongozi wa CHADEMA na UKAWA ni watu makini sana kila maamuzi wanayofanya wanatathimini kwanza maslahi mapana ya umma
 
Last edited by a moderator:
Wakati mwingine siasa ni kama mchezo wa karata...

Wakati na mahali sahihi ni jambo muhimu sana...
 
Wafuasi wa Yesu walilalama pale Kahaba alipo busu miguu Yesu na kumpangusa miguu yake kwa machozi wakisema inakuwaje Bwana anakubali kuguswa na Mtenda dhambi. Yesu akawaambia "Mwenye Afya Hamuhitaji Daktari". Kwahiyo ili tulete mabadiliko ya kweli ni lazima kuanza na hawa akina Lowasa.

Watu wanamna hii tukiisha wabadilisha mioyo yao wakaacha kuamini katika ufisadi, kwa nguvu waliyonayo katika jamii ushindi utakuwa umepatikana. Sasa unategemea tutawabadilisha wakiwa CCM? jibu ni hapana! kwanza tuwakaribishe, waje tuwabadilishe halafu tutaona wanafaa wapi!.

Tusitumie nguvu sana kumaintain waumini wetu, nguvu nyingi itumike kubadilisha mioyo ya wasioamini. Peopleeeeeeeeessss!!!
 
Lengo ni kuitoa CCM Madarakani...hata kama angekuwa Chenge au karamagi ndo wanakubalika tungewapokea,,,,lengo la kwanza ni kuitoa CCM madarakani mengine baadae.
 
Juzi Mbowe alisema Lowassa ni bubu, leo anamkaribisha Chadema. Kweli siasa mchezo mchafu.
 

Ukiijua siasa vizuri na kuwajua wanasiasa walivyo, basi mambo kama haya hayawezi kukupa shida sana au kukuumiza kichwa, siasa ni game of chance.

"politics is about who get what,when and how" by Okudiba Nnoli.
 

Vyama vya siasa vimeanza kusamehe dhambi.

Tunatarajia baada ya miaka 10 Zitto anaweza kurudi nyumbani.

Malkia hatakiwi hata kuhisiwa ama kunong'onwa kuwa kataongozwa achilia kufanywa na mtu.
 
Last edited by a moderator:
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…