Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Tatizo Sio Kuitoa CCM Madarakani.Tatizo Ni Kua Hakuna Mbadala Wake.Kama Watu Wao Wa Karibu Na Waasisi Wa UKAWA Wameshindwa Kuwaamini.Basi Hata Sisi Hatuwaamini.

Exactly mkuu, hakuna mbadala Wa Ccm! Waliokuwa wanategemewa na wananchi kuwa wangeleta mabadiliko wameishia njiani, wameshindwa kufanikisha Yale yaliyotarajiwa na wengi.
 
Bora nife kuliko nichague chama cha majizi (CCM) wale wale waliopiga escrow, meremeta, EPA, rada, Richmond hii inamuhusu Sana Baba yenu. CCM haufai hata kwa dawa, mnaiba wanyama, meno ya tembo na pembe za ndovu na kuziuza nje !! Huku si wanyonge tunaendelea kutaabika!! Unasign mikataba mibovu ya mafuta na gesi kwa manufaa ya tumbo zako!! Huku elimu duni katika tiba ndiyo usinene!! Rip Ccm chama cha vibaka wa Mali ya umma
 
Huwezi kuziongelea siasa za Tanzania bila kulitaja Jina la Freeman Mbowe.

Mbowe ni kati ya wanasiasa ambao wanaishi katika misingi ya siasa za kibiashara.
He is businessman turned politician and he's not shy away from controversy. He thrives on political controversy and challenge.

Mbowe haiangalii siasa katika jicho la kubadilisha maisha ya wananchi kwenye msingi wa hasara.

Ni kati ya watu ambao wako tayari kubadirika wakati wowote kutokana na mazingira ya kisiasa katika mlengo wa faida ya kisiasa bila kujali ni nani ataumia na maamuzi yake.

Moja ya uwezo wake mkubwa ni kuwakaanga kisiasa wale wote ambao wanaweka uzio wa kupata biashara ya kisiasa kwa mlengo wa faida.

Kuna wakati hakusita kuhudhuria dhifa iliyotayalishwa na Rais Kikwete kwa ujio wa Rais Obama na wafanyabiashara wakubwa wa Marekani pamoja na kwamba, serikali ya Rais Kikwete ilikuwa ni shetani katika macho ya baadhi ya viongozi wa CHADEMA.

Mbowe alihudhuria kwa sababu kulikuwa na faida ya kibiashara. Wanazi walipiga kelele lakini Mbowe yupo mpaka leo.

Zitto alileta kizingiti cha kisiasa katika siasa za faida ndani ya CHADEMA, aliishia kuvuliwa cheo na kufukuzwa ndani ya CHADEMA.

Mbowe baada ya kunusa faida ya kisiasa itakayopatikana kama atamteua Lowassa kuwa Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA, hakusita kumwambia Dk. Slaa akae kando pamoja na kwamba Kamati Kuu ya CHADEMA ilikuwa imemteua awe Mgombea Urais kwa tiketi ya CHADEMA. Dk. Slaa akazira na ''kuingia mitini'', lakini Mbowe hakutikisika katika uamuzi wake, wakati huo huo Dk. Slaa akaonekana kwa baadhi ya wana CHADEMA kama mpinga mabadiliko.

Haitashangaza kumuona akirudi tena ofisini baada ya kugundua kina kirefu cha kisiasa.

Kwa kutambua ulafi wa Prof. Lipumba kwenye ugombea Urais, Mbowe alimwacha Prof. Lipumba ajikaange mwenyewe mbele ya waaandishi wa habari kwa kumsafisha Lowassa bila kutambua kama anayemsafisha ndiye baadaye atachukua nafasi ya Urais anayodhani ni yake ndani ya UKAWA.

Kufumba na kufumbua, Prof. Lipumba akajikuta yuko nje ya matamanio yake na mbaya zaidi, hakufahamu kama Katibu wake Mkuu, Maalim Seif pia amemgeuka baada ya kuongea na Mbowe. Akajiuzuru uwenyekiti na kuondoka nchini wakati huo huo akaonekana kwa wana CUF kama ni msaliti wa mageuzi.

Mbowe ni mwalimu mzuri sana katika siasa za Tanzania zilizojaa wanafiki. Ni mtu anayeongea na mtu yoyote kama anadhani kuna maslahi katika
maongezi.

Ni kati ya mmoja wa wanasiasa ambao hawana marafiki wa kudumu au maadui wa kudumu.

ZITTO, Dk. SLAA na Prof. LIPUMBA hawawezi kuyasahau maamuzi ya Mbowe katika maisha yao.
 
Haa haa haa basi wenzako wajanja wanajua kufanya kinyume na pendekezo lako ndio kuwa na upinzania imara. Lipumba na Zitto ni vibaraka ambao tumeshawajua na katu hatutawaamini tena!
 
Hahaha he guy anamacho hayaelewek he clearly sees the opportunities
 
Kama mbowe asingemkubali lowasa na akachukuliwa na Act tungemwajibisha kwa kutukosesha wafuasi wapya milion!
Mbowe amefanikiwa kuipaisha CDM,fananisha na wakati anaingia kuwa mwenyekiti!
Upinzani umeimarika sasa more than ever,hebu waulize ccm ni kipindi gani ambacho wanahofu zaidi na upinzani,utaambiwa ni sasa!
Huoni mwenyekiti wa ccm anavyohangaika kumuuza magufuli,hii ni ishara kuwa sasa upinzani ni moto,ukawa mbele kwa mbele!
 
Ukawa mnajidanganya kwa kujilisha upepo. MTU aliyekataliwa upande mwengine mnajiaminishaje kuwa anafaa upande wenu? Kwa misingi IPI? Name kwa itikadi zipi? Na akishindwa uchaguzi mtakuwa nae tayari kusimamia yale mnayoamini kama chama?

Mmekurupuka sana Ila November 2015 mwisho wenu.
 

pamoja na kujaza madaktari na de profesor wengi mbowe anawajambisha ushuzi mpaka suruali zinawashuka

mbowe=kiboko ya madaktari wa kuchonga na de profesery
 

Hawa jamaa wametuangusha sana na uchu wao wa madaraka .. kuna kura nyingi za hasira atazizoa Magufuli Oktoba na bahati mbaya ndo watakuwa wameua upinzani rasmi
 

mwenye akili timamu hawezi kushabikia ccm,chama kimekosa mwelekeo!kwa taarifa yako lowasa aliwahi kulizungumza hilo kwenye NEC na akampoint moja kwa moja mwenyekiti,issue ikazimwa kwamba itakipasua chama!usiwe unalopoka usiyoyajua!
Ccm must go,tumechoka kuwa watumwa kwenye nchi yetu!mzigo mkubwa wa kodi tunabebeshwa huku hatuoni faida yake zaidi ya kutuongezea umaskini!
 
Sijataka kufikiriwa. ..ninalo sema ni ukweli mtupu. .lazima tupate viongozi watakao kuwa na huruma na taifa na wananchi wake, awe mbowe ama kingwendu lakini isiwe Ccm mana imelewa madaraka sasa

Kwahiyo mnasubiri huruma kutoka kwa yule mzee mwenye uchu wa madaraka kutoka monduli.

Andikeni mmeumia.
 
Mwaka hata ukawa wasipopiga kampeni mnawapigia wenyewe maana usipotaja mbowe,slaa,tundu,mnyika,lowassa na wengine hamtapona ule ugonjwa wenu,kwan hamjui kama mnawakuzia jina maadui?au lumumba hamna kitengo cha propaganda?
 
magufuli kipindi cha babu wa loliondo alienda kunywa kikombe alikunywa kama chai au naye mgonjwa tuu?
 
skendo ya buzwagi iliipaisha sana chadema, kipindi cha zitto hicho. baada ya zitto kusimamishwa bunge kwa muda walizunguka nchi nzima kutoa elimu kwa wananchi kuhusu skendo ya buzwagi.
uhusika wa kalamagi na waziri mkuu lowasa ulielezwa vizuri bungeni na mikutanoni. kalamagi alibeba mihuri ya serikali kwenye briefcase akaenda saini mkataba kwa niaba ya serikali hotelini London, waziri mkuu lowasa nae alijipelekea london akaweka kambi hoteli jirani na hotel aliyofikia kalamagi na wawekezaji hao. wao wajua vyema walichoongea/peana huko ila kalamagi alirudi na mkataba umeshafungwa. mbowe alilisema hili majukwaani nchi nzima.
waziri mkuu wamruhusu waziri wako atie mihuli kwa begi aende hotelini nje ya nchi kufunga mkataba kwa niaba ya serikali. haikutosha akajipeleka mwenyewe London - na kumbukumbu za ofisi ya waziri hazikuonesha kwamba waziri mkuu alienda london kiserikali, pia hakuwa likizo.
leo hii mbowe kabadilika anatuhubiria kwamba lowasa anayesaidiwa pesa na kalamagi ndiye tumaini jipya la watz, atatuvusha na kutufutia umaskini. aenda mbali zaidi na kusema hana kashfa yeyote.
mbowe adhani siye watz ni wasahaulifu sana, afikiri twamjua lowasa kwa richmond tu. twajua mengi mbowe.
kalamagi sasa ndo mfadhili mkubwa wa lowasa - ambaye ukawa watwambia akiingia ikulu atafuta ufisadi.
tutafakari zaidi watz wenzangu. kwa ufupi naweza sema anachokifanya mbowe ni unafiki,unafiki na unafiki.
 
magufuli kipindi cha babu wa loliondo alienda kunywa kikombe alikunywa kama chai au naye mgonjwa tuu?
 

ni ngumu kuchangia hoja yako mkuu kwani ina mwelekeo wa maumivu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…