skendo ya buzwagi iliipaisha sana chadema, kipindi cha zitto hicho. baada ya zitto kusimamishwa bunge kwa muda walizunguka nchi nzima kutoa elimu kwa wananchi kuhusu skendo ya buzwagi.
uhusika wa kalamagi na waziri mkuu lowasa ulielezwa vizuri bungeni na mikutanoni. kalamagi alibeba mihuri ya serikali kwenye briefcase akaenda saini mkataba kwa niaba ya serikali hotelini London, waziri mkuu lowasa nae alijipelekea london akaweka kambi hoteli jirani na hotel aliyofikia kalamagi na wawekezaji hao. wao wajua vyema walichoongea/peana huko ila kalamagi alirudi na mkataba umeshafungwa. mbowe alilisema hili majukwaani nchi nzima.
waziri mkuu wamruhusu waziri wako atie mihuli kwa begi aende hotelini nje ya nchi kufunga mkataba kwa niaba ya serikali. haikutosha akajipeleka mwenyewe London - na kumbukumbu za ofisi ya waziri hazikuonesha kwamba waziri mkuu alienda london kiserikali, pia hakuwa likizo.
leo hii mbowe kabadilika anatuhubiria kwamba lowasa anayesaidiwa pesa na kalamagi ndiye tumaini jipya la watz, atatuvusha na kutufutia umaskini. aenda mbali zaidi na kusema hana kashfa yeyote.
mbowe adhani siye watz ni wasahaulifu sana, afikiri twamjua lowasa kwa richmond tu. twajua mengi mbowe.
kalamagi sasa ndo mfadhili mkubwa wa lowasa - ambaye ukawa watwambia akiingia ikulu atafuta ufisadi.
tutafakari zaidi watz wenzangu. kwa ufupi naweza sema anachokifanya mbowe ni unafiki,unafiki na unafiki.