huwezi kuziongelea siasa za tanzania bila kulitaja
jina la freeman mbowe.
Mbowe ni kati ya wanasiasa ambao wanaishi katika
misingi ya siasa za kibiashara.
He is businessman turned politician and he's not shy
away from controversy. He thrives on political
controversy and challenge.
Mbowe haiangalii siasa katika jicho la kubadilisha
maisha ya wananchi kwenye msingi wa hasara.
Ni kati ya watu ambao wako tayari kubadirika wakati
wowote kutokana na mazingira ya kisiasa katika
mlengo wa faida ya kisiasa bila kujali ni nani ataumia
na maamuzi yake.
Moja ya uwezo wake mkubwa ni kuwakaanga kisiasa
wale wote ambao wanaweka uzio wa kupata biashara
ya kisiasa kwa mlengo wa faida.
Kuna wakati hakusita kuhudhuria dhifa iliyotayalishwa
na rais kikwete kwa ujio wa rais obama na
wafanyabiashara wakubwa wa marekani pamoja na
kwamba, serikali ya rais kikwete ilikuwa ni shetani
katika macho ya baadhi ya viongozi wa chadema.
Mbowe alihudhuria kwa sababu kulikuwa na faida ya
kibiashara. Wanazi walipiga kelele lakini mbowe yupo
mpaka leo.
Zitto alileta kizingiti cha kisiasa katika siasa za faida
ndani ya chadema, aliishia kuvuliwa cheo na
kufukuzwa ndani ya chadema.
Mbowe baada ya kunusa faida ya kisiasa
itakayopatikana kama atamteua lowassa kuwa
mgombea urais kwa tiketi ya chadema, hakusita
kumwambia dk. Slaa akae kando pamoja na kwamba
kamati kuu ya chadema ilikuwa imemteua awe
mgombea urais kwa tiketi ya chadema. Dk. Slaa
akazira na ''kuingia mitini'', lakini mbowe hakutikisika
katika uamuzi wake, wakati huo huo dk. Slaa
akaonekana kwa baadhi ya wana chadema kama
mpinga mabadiliko.
Haitashangaza kumuona akirudi
tena ofisini baada ya kugundua kina kirefu cha
kisiasa.
Kwa kutambua ulafi wa prof. Lipumba kwenye
ugombea urais, mbowe alimwacha prof. Lipumba
ajikaange mwenyewe mbele ya waaandishi wa habari
kwa kumsafisha lowassa bila kutambua kama
anayemsafisha ndiye baadaye atachukua nafasi ya
urais anayodhani ni yake ndani ya ukawa.
Kufumba na kufumbua, prof. Lipumba akajikuta yuko nje ya
matamanio yake na mbaya zaidi, hakufahamu kama
katibu wake mkuu, maalim seif pia amemgeuka
baada ya kuongea na mbowe. Akajiuzuru uwenyekiti
na kuondoka nchini wakati huo huo akaonekana kwa
wana cuf kama ni msaliti wa mageuzi.
Mbowe ni mwalimu mzuri sana katika siasa za
tanzania zilizojaa wanafiki. Ni mtu anayeongea na
mtu yoyote kama anadhani kuna maslahi katika
maongezi.
Ni kati ya mmoja wa wanasiasa ambao
hawana marafiki wa kudumu au maadui wa kudumu.
Zitto, dk. Slaa na prof. Lipumba hawawezi
kuyasahau maamuzi ya mbowe katika maisha yao.