KipimaPembe
Hoja nzuri kuwa Ukawa watasimamia rasimu ya Warioba. Hata hivyo Lowasa hajawahi kutamka hadharani kwenye suala la Katiba yuko Upande gani
Hiyo tusubiri naimani atatamka tu. Muda bado..
na wanaomjua kwa hulka yake ya kupenda sana madaraka haielekei kuwa Lowasa ndo mtu anayefaa kusimamia hoja hiyo. Tusisahau Lowasa maisha yake yote toka ujana hadi anakuwa mzee yamekuwa ni CCM. Wiki chache kabla ya kuhama alitamka kuwa maisha yake ni CCM.
Hilo la afai, siwezi kuliongelea manake lile SI jambo la mtu mmoja mmoja BALI ni la Taifa zima.
Hilo linathibitishwa na jinsi ambavyo amekuwa akiongea baada ya kuhamia Ukawa. Zaidi sana amekuwa akilalamikia uonevu aliofanyiwa akiwa CCM. Wengi wanaweza kukubaliana naye. Hata hivyo alikuwemo CCM akiwa kiongozi mwandamizi ndani ya chama hicho kwa Miaka mingi mno. Ni vigumu sana kuamini kama Lowasa anaweza akafanya mambo tofauti na alivyofanya akiwa CCM kuliko kuamini kuwa Magufuli anaweza akafanya mambo tofauti. Magufuli hakuwahi hata kuwa kiongozi wa tawi - entirely ni mtu mpya kabisa katika safu za kiutendaji za CCM na anaweza akaja na jipya kuliko Lowasa ambaye kuwepo kwake kwenye "top ranks" za CCM kwa muda mrefu kuna mfanya awe CCM zaidi kuliko hata Magufuli. Litakuja lile swali walilokuwa wakiulizana wana reformation baada ya mpasuko ndani ya Kanisa miaka ile kuwa "is Luther a Lutheran??".
Kumbuka MAkufuli Amewekwa na JK
"Mwenye MWANA". Na Pia Sera za ccm sio sera ya Mgombea Binafsi bali ni ya system NZima,. Kwa maana hiyo Magufuli hana atakchoongeza sana sana na yeye aanze kuuza Twiga na Rasilimali za Taifa kam ilivyo Ada kwa viongozi we CCM. MAgufuli amewekwa PAle ili kuua MAkundi ndani ya CCM. Jambo hili halijawezekana pia.
Pia kupitia huo Mfano wako wa Luther bado utaona Lutheran Ipo Mpaka Leo.. SO changamoto zinaweza kuwepo..
Pia NAfasi ya Lowasa pale Ukawa ni kama amezawadiwa ili atekeleze majukumu ya ukawa na anao UZOEFU MKUBWA SANA KULIKO MAGUFULI.
Baada ya Lowasa kuingia Chadema, anaonekana kubeba hoja za ki CCM CCM zaidi kuliko hata wale waliobaki CCM. Swali litakuwa "Is Lowasa representiing Ukawa ideals??".
Mh hapa sijaelewa ni hoja gani mfano aliyoisema imekaa kisisiemu. nachojua huwa anapenda kusema anayatafuta mabadiliko nje ya ccm. Nachoona EL ana utulivu Mzuri unaoweza kumfanya mtu yoyote aone Kuwa Hatetereki.
Hapo wengi tumejikwaa na hatuoni Lowasa akisimamia hoja za Ukawa. Sana sana kuwepo kwake ukawa kunaifanya CCM iliyobaki iungane zaidi kuliko ilivyokuwa huko nyuma. Jambo hili ni baya zaidi. Mpasuko uliokuwemo ndani ya CCM ndio wengi tulitarajia kiisaidie sana Ukawa. Sasa hivi CCM wana "re-group" wakati Ukawa imepoteza nyota wake wakuu. Hili si jambo la kudharau hata kidogo. Wale wanaopiga makelele tu kuwa Ukawa itashinda si vibaya wakafanya analysis isiyo na chembe ya unafiki huko Majimboni.
lakini bado Mpasuko unaendelea tena kwenye mashina ambao ndio MUhimu zaidi kwani wale ndio wapiga Kura. Japo Viongozi wanapambana kuunganisha Nguvu.
Kimsingi: Yapo mambo ninayoyaona ambayo "yamewekwa/hayajawekwa" kwenye katiba ya UKAWA ambayo CCM walishindwa kuyapitisha na Upo uwezekano kwa Ukawa kutokuafikiana pia. Mambo haya yanatugawa kama taifa na yanabomoa umoja. Nisingependa kuyataja hapa, .. Lakini nadhani utakua umeelewa.. Lowasa katika Ubora wake bado nayaona haya kama yatampa changamoto sana.