Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

sasa zile video za dr slaa anazosema Lowassa ni fisadi anaetakiwa kuogopwa kama ukoma zitafutwa kwenye sosho media??
 
Habari za lowassa kwenda chadema sasa no porojo tuu kwanza lowassa mwenyewe kazibwa mdomo Stoke ccm aone
 
Lowassa hawezi kuhama chama,faili lake wataliweka hadharani.
 
My take: Hapo watu wamepiga mahesabu kwamba uli mshiko ambao EL amekuwa akiusambaza huko CCM sasa utakuwa unasambazwa CDM. Jamani watu wanaabudu pesa! Na huyo bwana anaendelea kudanganyika tu kwamba ati anapendwa na walio wengi. Haiji kichwani mwake kwamba wanapenda pesa tu. Watamwaminisha kwamba anashinda, kama alivyoaminishwa kwamba kule CCM hakuna wa kumkata jina. Matokeo yake ni yale yale, kwamba mtandao waliojivunia unawatafuna wenyewe kwa wenyewe. Ni Frankenstein huo mtandao. Busara kwake itakuwa ni kupoa kabisa kama watangulizi wake walivyofanya na wakaishi kwa amani kabisa.
 
Naona unatafuta mme jf
 

Yaani kama kuna kosa la karne watakalolifanya UKAWA au chama chochote cha UKAWA ni kumpokea Lowassa (for whatever reason(s) mwaka wa uchaguzi.
 

JAMAAA AMESHATUBU ,AMESHAUNGAMA - JUMAPILI ATASEMA UKWELI KUHUSU RICHMOND- JK jiandae
 
Na mi rasmi najiondoa chadema kwa kumkaribisha huyu fisadi shame on you chadomo
 
Nani katika ccm hatumii Pesa? Mwaka 2005 Pesa zilitumika 2015 ndio mnashangaa acheni wivu
 
Ukweli kuhusu Richmond tumeupata fisadi anajulikana kamati ya mwakyembe iliagiza wote waliotajwa wafikishwe mahakamani he serikali ya ccm iliwafikisha? Haukuwafikisha kwa sababu sio wahusika lowassa atakuwaje fisaduli acheni chuki za kitoto
 
Hivi aliyewaambia siasa ni kitu real ni nani.Siasa ni kitu hewa tu.Ni kiini macho.The real thing kiko nyuma ya hicho mnachokiita ninyi wadanganyika siasa.Wajinga ndio waliwao.
 
Sasa ni dhihiri kuwa CHADEMA iko kwenye mikakati mizito ya kumshawishi au kuafikiana na Edward Lowassa ili aweze kuhama CCM na kujiunga CHADEMA na hapo hapo apewe nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.
Nikiwa kama mshambuzi wa mambo ya siasa humu JF, mtanzania mpenda maendeleo na mpenzi wa CHADEMA jambo hili limenishtua na kunisikitisha sana.

Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amenukuliwa na magazeti kadhaa ya leo akisema, Lowassa anakaribishwa CHADEMA na hana tatizo lolote, na hapo hapo baadhi ya wabunge na viongozi wa juu wa CHADEMA wamenukuliwa ama wakiunga mkono ujio au kumumunya maneno kuhusu hilo.

Mpaka sasa sijui, ni nini kimewaingia viongozi wa CHADEMA kuanza kukubali jambo hili. Nini msukumo wao?
Ni nani asiyemjua Lowassa? Huyu ni mwanasiasa mchafu, ambaye amewekeza muda, pesa na watu wake wengi sana katika siasa ili afanikiwe tu kuwa rais wa Tanzania.

CHADEMA bado tu humjajifunza kutokana na makosa? Yuko wapi Samweli Sitta, John Shibuda nk?
Mtaacha lini kusubiri makapi ya CCM ili kuyapokea na kuwapa nafasi za ugombea katika uchaguzi?

Hivi mnajua kwanini watanzania wengi waliwapenda na kuwaamini?
Hivi agenda ya kupambana na Ufisadi hamhitaki tena?

Hivi viongozi wa CHADEMA mnatambua siasa itaendelea tu hata baada ya October 25?
Hivi mnajua kwanini watanzania walitoa maisha yao hata kufa kuona CHADEMA inasonga mbele?

Inakuwaje muwe na mawazo ya kupata madaraka tu kiujanjaujanja kwa kutumia mtaji wa Fisadi Lowassa hata kwa gharama ya kuuza Identity yenu ya kisiasa na agenda zenu?
Hivi mnajua athari za kisiasa baada ya October kama mkimpokea Lowassa sasa?
Hivi CHADEMA itakuwaje kisiasa kama Lowassa atagombea kwa tiketi ya CHADEMA na akafanikiwa kushinda au bahati mbaya akashindwa?

Hivi CHADEMA mnajua Lowassa ana malengo gani na huo urais?
Hivi mnajua kwa nini CCM kwa gharama kubwa kabisa ilihakikisha Lowassa hapewi nafasi ya kugombea?

Hivi hamjiamini kuwa nyie wenyewe mnaweza pasipo msaada wa makapi ya CCM?
CHADEMA mnawezaje kuacha mbachao kwa msala upitao?

CHADEMA NI NANI ALIYEWALOGA?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…