Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Siasa Hazina Rafiki au Adui wa Kudumu; Ndg yangu kwenye Siasa ni Mahesabu, Ukiona Jibu ni Sahihi basi Kinachobaki ni Kuchangamkia fursa.

Kinachotusumbua Watanzania Sio Mtu bali ni Mfumo Mbovu Ndani ya CCM na Serikali yake, So Kama Ikatokea Kuusambaratisha Mfumo

Huo Kwa Njia yoyote ile Wapinzani Hawaewezi Fanya ajizi.
 
Jamani acheni kuwashambulia CHADEMA hawana goli la mkono kama CCM wangekuwa na goli la mkono kama CCM unadhani wangehangaika kuwatafuta hata akina Lowassa?wakati wangepiga chenga za uongo na kweli mtu ana tia mkono wake kama Maradona vile,kitu hichooo tayari kimetinga nyavuni na mtu ana tangazwa kuwa mshindi.
 
Muda huu kikao cha siri kinaendelea makao makuu ya Chadema Mtaa wa Ufipa,mjadala uliobaki sasa ni namna ya kuweza kuwapatia lembeli na Ester Bulaya nafasi za kuwania Ubunge katika majimbo ya Kahama na Bunda mjini.

Katika kikao hiki ambacho Dk Slaa hayupo na tayari ameshakubaliana na uamuzi wa Chama wa kumpokea Edward Lowasa,wajumbe wanaangalia namna ya kuwaruhusu Bulaya na Lembeli kuingia katika kinyang'anyiro ndani ya Chama bila kulitea mgawanyiko na kuonyesha uvunjaji wa kanuni walizojiwekea

Ikumbukwe kuwa kama Chama taratibu za kuchukua na kurudisha fomu tulimaliza julai 19 mwaka huu na muda ambao Bulaya na Lembeli walikuwa bado hawajajiunga nasi.


Tunamshukuru Mungu kila kitu kinaenda sawa na hata kama kutatokea tatizo kwa wale waliotia nia ya kuwania majimbo hayo ya Lembeli na Bulaya tutakuwa na Cha kuwaambia.

Kuhusu Lowasa tumeshamalizana nae ingawa kikwazo kilikuwa kwa upande wa mke wa Katibu mkuu wetu juu ya mumewe kukubaliana na uamuzi huo kwa sasa tunashukuru ametuelewa

Kwa sasa niishie hapa ila jumapili mtegemee mshituko mkubwa wa nchi juu ya kikao hiki
 


mimi binafsi najiuliza maswali haya

1, slaa kwanini alimchafua lowasa na leo hii anayarudia matapishi yake?
2, je leo hii utatwambia nini sisi watanzania na unafiki wako wa wazi kiasi hiki?
3, unafiki ni dhambi na hii dambi slaa utaifutaje machoni mwa watanzania?
4, kumbe mkisemacho mdomoni sio kilichopo moyoni mwenu?
5, je tukiwaita wasakatonge tutakuwa tunawakosea?
6, je tukiwaita wanafiki tutakuwa tunawakosea?


Mimi binafsi nakujibu hayo maswali
1, alimchafua kwa matope na matapishi ni dili
2, mamboooo!
3, ufutio unahusika
4, ni kweli
5, ndio
6, ndio

Maswali mengine tafadhali.

Na mm nina swali moja: Ikiwa kweli Lowassa alikuwa fisadi, ile opersheni ya KUVUANA MAGAMBA ilimkosaje? Na kwa nini hamkumpeleka mahakamani?
 
Chadema darasa chadema chuo
njooni na karibuni cdm mfundishwe uzalendo cdm haikatai mtu karibuni wote tujifunze uzalendo na tujenge nchi yetu.walioshindwa kujirekebisha kwaherini.
 
Kweli Josephine ndo kila kitu hapo ufipa hahaha,,,Maskini Khalid mlinzi wa Silaha alionewa bure tu baada ya kukataa kumpelekea chai babu.
 
Dr. Slaa alikuwa amezila au nini? Please Ukawa be serious,be keen, kusiwe na upande wa kuumia sana katika kipindi hiki cha majeruhi.
 
HATA DHAMBI ZAKO ZIWE NYEKUNDU KAMA DAMU ZITASAFISHWA NA KUWA NYEUPE KAMA THELUJI.ii
 
Kwa Tafsiri hii, ya kuyakumbatia maovu ambayo walikua wanayapinga......


Kwa kumkaribisha yule waliyekua wanamtuhumu majukwaani.....

Kwa kutudanganya tuamini yale wanayotaka tuamini kumbe sivyo.......


Kama ni kweli mmemkaribisha huyu mtu.........


Nyie sio wa kuaminika, hamfai...hamchelewi kutubadilikia mkiwa ikulu.......

Mnapinga nini na kufanya nini????

Uongozi wa ikulu ni muhimu kuliko uhusiano wenu na wanaowaamini...

MMewasaliti Watanzania kwa uchu wa IKULU......

Mtawatawala vipi wale mliowasaliti......

Ina maana mlikua mnatoa tuhuma za UONGO juu ya huyo mtu....

Kama ni tuhuma za Uongo...tokea muanze kutoa TUHUMA mmetoa ngapi za uongo na ngapi za Ukweli....

Tunashindwa kuamini tena hata mkituambia kua yapo ya ukweli mliyotuambia....

Imani juu yenu imepotea.....

CHADEMA hamuaminiki tena...
 
Mkuu we we mshamba hujui siasa ndie nyie ukiacha make akiolewa roho inakuuma
 
Back
Top Bottom