Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

Mbowe amkaribisha rasmi Lowassa CHADEMA

sasa zile video za dr slaa anazosema Lowassa ni fisadi anaetakiwa kuogopwa kama ukoma zitafutwa kwenye sosho media??
 
Habari za lowassa kwenda chadema sasa no porojo tuu kwanza lowassa mwenyewe kazibwa mdomo Stoke ccm aone
 
Lowassa hawezi kuhama chama,faili lake wataliweka hadharani.
 
My take: Hapo watu wamepiga mahesabu kwamba uli mshiko ambao EL amekuwa akiusambaza huko CCM sasa utakuwa unasambazwa CDM. Jamani watu wanaabudu pesa! Na huyo bwana anaendelea kudanganyika tu kwamba ati anapendwa na walio wengi. Haiji kichwani mwake kwamba wanapenda pesa tu. Watamwaminisha kwamba anashinda, kama alivyoaminishwa kwamba kule CCM hakuna wa kumkata jina. Matokeo yake ni yale yale, kwamba mtandao waliojivunia unawatafuna wenyewe kwa wenyewe. Ni Frankenstein huo mtandao. Busara kwake itakuwa ni kupoa kabisa kama watangulizi wake walivyofanya na wakaishi kwa amani kabisa.
 
Kwa Tafsiri hii, ya kuyakumbatia maovu ambayo walikua wanayapinga......


Kwa kumkaribisha yule waliyekua wanamtuhumu majukwaani.....

Kwa kutudanganya tuamini yale wanayotaka tuamini kumbe sivyo.......


Kama ni kweli mmemkaribisha huyu mtu.........


Nyie sio wa kuaminika, hamfai...hamchelewi kutubadilikia mkiwa ikulu.......

Mnapinga nini na kufanya nini????

Uongozi wa ikulu ni muhimu kuliko uhusiano wenu na wanaowaamini...

MMewasaliti Watanzania kwa uchu wa IKULU......

Mtawatawala vipi wale mliowasaliti......

Ina maana mlikua mnatoa tuhuma za UONGO juu ya huyo mtu....

Kama ni tuhuma za Uongo...tokea muanze kutoa TUHUMA mmetoa ngapi za uongo na ngapi za Ukweli....

Tunashindwa kuamini tena hata mkituambia kua yapo ya ukweli mliyotuambia....

Imani juu yenu imepotea.....

CHADEMA hamuaminiki tena...
Naona unatafuta mme jf
 
Muda huu kikao cha siri kinaendelea makao makuu ya Chadema Mtaa wa Ufipa,mjadala uliobaki sasa ni namna ya kuweza kuwapatia lembeli na Ester Bulaya nafasi za kuwania Ubunge katika majimbo ya Kahama na Bunda mjini.

Katika kikao hiki ambacho Dk Slaa hayupo na tayari ameshakubaliana na uamuzi wa Chama wa kumpokea Edward Lowasa,wajumbe wanaangalia namna ya kuwaruhusu Bulaya na Lembeli kuingia katika kinyang'anyiro ndani ya Chama bila kulitea mgawanyiko na kuonyesha uvunjaji wa kanuni walizojiwekea

Ikumbukwe kuwa kama Chama taratibu za kuchukua na kurudisha fomu tulimaliza julai 19 mwaka huu na muda ambao Bulaya na Lembeli walikuwa bado hawajajiunga nasi.


Tunamshukuru Mungu kila kitu kinaenda sawa na hata kama kutatokea tatizo kwa wale waliotia nia ya kuwania majimbo hayo ya Lembeli na Bulaya tutakuwa na Cha kuwaambia.

Kuhusu Lowasa tumeshamalizana nae ingawa kikwazo kilikuwa kwa upande wa mke wa Katibu mkuu wetu juu ya mumewe kukubaliana na uamuzi huo kwa sasa tunashukuru ametuelewa

Kwa sasa niishie hapa ila jumapili mtegemee mshituko mkubwa wa nchi juu ya kikao hiki

Yaani kama kuna kosa la karne watakalolifanya UKAWA au chama chochote cha UKAWA ni kumpokea Lowassa (for whatever reason(s) mwaka wa uchaguzi.
 
Kwa Tafsiri hii, ya kuyakumbatia maovu ambayo walikua wanayapinga......


Kwa kumkaribisha yule waliyekua wanamtuhumu majukwaani.....

Kwa kutudanganya tuamini yale wanayotaka tuamini kumbe sivyo.......


Kama ni kweli mmemkaribisha huyu mtu.........


Nyie sio wa kuaminika, hamfai...hamchelewi kutubadilikia mkiwa ikulu.......

Mnapinga nini na kufanya nini????

Uongozi wa ikulu ni muhimu kuliko uhusiano wenu na wanaowaamini...

MMewasaliti Watanzania kwa uchu wa IKULU......

Mtawatawala vipi wale mliowasaliti......

Ina maana mlikua mnatoa tuhuma za UONGO juu ya huyo mtu....

Kama ni tuhuma za Uongo...tokea muanze kutoa TUHUMA mmetoa ngapi za uongo na ngapi za Ukweli....

Tunashindwa kuamini tena hata mkituambia kua yapo ya ukweli mliyotuambia....

Imani juu yenu imepotea.....

CHADEMA hamuaminiki tena...

JAMAAA AMESHATUBU ,AMESHAUNGAMA - JUMAPILI ATASEMA UKWELI KUHUSU RICHMOND- JK jiandae
 
Na mi rasmi najiondoa chadema kwa kumkaribisha huyu fisadi shame on you chadomo
 
Nani katika ccm hatumii Pesa? Mwaka 2005 Pesa zilitumika 2015 ndio mnashangaa acheni wivu
 
Ukweli kuhusu Richmond tumeupata fisadi anajulikana kamati ya mwakyembe iliagiza wote waliotajwa wafikishwe mahakamani he serikali ya ccm iliwafikisha? Haukuwafikisha kwa sababu sio wahusika lowassa atakuwaje fisaduli acheni chuki za kitoto
 
Hivi aliyewaambia siasa ni kitu real ni nani.Siasa ni kitu hewa tu.Ni kiini macho.The real thing kiko nyuma ya hicho mnachokiita ninyi wadanganyika siasa.Wajinga ndio waliwao.
Nakumbuka mtu wa kwanza kuwambia watanzania waziwazi mchana kweupe alikuwa Slaa akimtaja Lowassa kuwa kwenye list of shame,kama fisadi wa kutisha ktk nchi hii.

Lakini leo hii Slaa na Mbowe ndio hao hao wamekaa meza moja na Lowassa wakimpokea kwa shangwe kubwa,
kitendo hiki ni sawa na kuyarudia matapishi yao ya Mwembe Yanga,na kutuonyesha watanzania kuwa Slaa ni mnafiki maana alimtumia uchafu wa Lowassa kujiimalisha kisiasa na kumchafua Lowassa mbele ya umma kumbe mnafiki,

Mimi binafsi najiuliza maswali haya

1, Slaa kwanini alimchafua Lowassa na leo hii anayarudia matapishi yake?
2, Je, leo hii utatwambia nini sisi watanzania na unafiki wako wa wazi kiasi hiki?
3, Unafiki ni dhambi na hii dambi Slaa utaifutaje machoni mwa watanzania?
4, Kumbe mkisemacho mdomoni sio kilichopo moyoni mwenu?
5, Je, tukiwaita wasakatonge tutakuwa tunawakosea?
6, Je, tukiwaita wanafiki tutakuwa tunawakosea?

Na habari za ndani kwa sasa hata kama hamtampitisha kugombea urais kitakuwa ni kiini macho mkiongopa kuulizwa juu ya unafiki wenu lakini ana ahadi ya nafasi ya uwaziri mkuu mkipata na ndio maana atatoa pesa nyingi kuwasaidia hili kushinda kutoka kwa marafiki zake na yeye.

Huu mpango mnaupanga kwa kushirikiana na mengi katika dhana yenu hile sitaitaja mnaijua wenyewe,lakini nachosema unafiki ni dhambi na dhambi hii inawarudia mwaka huu maana nyie ndo mlikuwa wakwaza kumvua nguo lowasa mchana kweupe na kumuita fisadi papa /nyangumi lakini leo hii ndo mpanga diri zenu.

Nasema unafiki wenu tumeishaujua,na matunda yake mtayavuna mwaka huu,msinge mchafua Lowassa na leo hii kuyarudia matapishi hayo ndio plan b yenu, ukweli wenu kwa mkisemacho uko wapi?



 
Sasa ni dhihiri kuwa CHADEMA iko kwenye mikakati mizito ya kumshawishi au kuafikiana na Edward Lowassa ili aweze kuhama CCM na kujiunga CHADEMA na hapo hapo apewe nafasi ya kugombea urais kwa tiketi ya CHADEMA.
Nikiwa kama mshambuzi wa mambo ya siasa humu JF, mtanzania mpenda maendeleo na mpenzi wa CHADEMA jambo hili limenishtua na kunisikitisha sana.

Tayari Mwenyekiti wa CHADEMA Freeman Mbowe amenukuliwa na magazeti kadhaa ya leo akisema, Lowassa anakaribishwa CHADEMA na hana tatizo lolote, na hapo hapo baadhi ya wabunge na viongozi wa juu wa CHADEMA wamenukuliwa ama wakiunga mkono ujio au kumumunya maneno kuhusu hilo.

Mpaka sasa sijui, ni nini kimewaingia viongozi wa CHADEMA kuanza kukubali jambo hili. Nini msukumo wao?
Ni nani asiyemjua Lowassa? Huyu ni mwanasiasa mchafu, ambaye amewekeza muda, pesa na watu wake wengi sana katika siasa ili afanikiwe tu kuwa rais wa Tanzania.

CHADEMA bado tu humjajifunza kutokana na makosa? Yuko wapi Samweli Sitta, John Shibuda nk?
Mtaacha lini kusubiri makapi ya CCM ili kuyapokea na kuwapa nafasi za ugombea katika uchaguzi?

Hivi mnajua kwanini watanzania wengi waliwapenda na kuwaamini?
Hivi agenda ya kupambana na Ufisadi hamhitaki tena?

Hivi viongozi wa CHADEMA mnatambua siasa itaendelea tu hata baada ya October 25?
Hivi mnajua kwanini watanzania walitoa maisha yao hata kufa kuona CHADEMA inasonga mbele?

Inakuwaje muwe na mawazo ya kupata madaraka tu kiujanjaujanja kwa kutumia mtaji wa Fisadi Lowassa hata kwa gharama ya kuuza Identity yenu ya kisiasa na agenda zenu?
Hivi mnajua athari za kisiasa baada ya October kama mkimpokea Lowassa sasa?
Hivi CHADEMA itakuwaje kisiasa kama Lowassa atagombea kwa tiketi ya CHADEMA na akafanikiwa kushinda au bahati mbaya akashindwa?

Hivi CHADEMA mnajua Lowassa ana malengo gani na huo urais?
Hivi mnajua kwa nini CCM kwa gharama kubwa kabisa ilihakikisha Lowassa hapewi nafasi ya kugombea?

Hivi hamjiamini kuwa nyie wenyewe mnaweza pasipo msaada wa makapi ya CCM?
CHADEMA mnawezaje kuacha mbachao kwa msala upitao?

CHADEMA NI NANI ALIYEWALOGA?
 
Back
Top Bottom