Kama maneno haya ni ya kweli basi Chadema nao wanaenda kusambaratika kama ilivyo CCM, Mbowe kwa kumkaribisha maalun huyu Chadema inagawanyika sasa hivi. Mlisema ananuka rushwa leo mmempaka pafyumu gani hadi anukie vizuri? Eti eti mnamwambia ni chama cha watanzania wote basi wakaribisheni akina Chenge, Prof Muhongo, Karamagi, Ngeleja, Rostam na wengine kwa kuwa Chadema ni chama cha Watanzania wote Mbowe please usituharibie chama.
Hutaki sepa,tunamkaribisha aje atubu dhambi zake na kuweka mambo hadharani....
Mie sioni haja ya kuwa na hasira. Ooh! Ntarudisha kadi kwa manufaa ya nani sasa? Hivi hayo mnayowaza mnadhani wao hawajalitazama hilo??!! Wapeni nafasi ya kujieleza kwann wanampokea Lowassa !!!
Kumbuka ndio huyo mungu tulikesha tukimwomba na lowassa akakatwa na ccm lakini kabla walitukebehi kama wewe unachofanya sasa hivi na pesa yote waliotumia lakini bado akashinda aliyetumia hata 10mil haifiki
Ulikesha wewe kumuomba huyo mungu wako, mimi mpaka leo namuomba MUNGU wangu alete mabadiliko TZ
Mimi naona shida yao itakuwa ni kuongeza mtaji wa wapiga kura na si vinginevyo na mtu mwenyewe waliyemuona kuwa anaweza akaja na mtaji mkubwa wa wapiga kura ni Lowassa.
Mwenyekiti wa CHADEMA taifa mh. Freemam Mbowe amemkaribisha Lowassa kujiunga na CHADEMA hakibagui mtu ili mradi tu afuate kanuni na taratibu za chama.
Source: Tanzania Daima, Mwananchi
Mzee Mtei na Ndesamburo wana imani kwa lowasa kuliko babu Slaa
SLAA ni muiIRAQ asili yake ni kutoka Eritrea , mmeru na mchaga ni mtu na binamu yake. Dr SLAA sio mla rushwa hali luwasa ni Mr 20%, hapo mchaga atamkaribisha nani
Wangu nilimwomba na majibu akawa kama nilivyoomba jina la fisadi likakatwa, mabadiliko hayawezi kuletwa na fisadi lowassa na team yake ya akina Rostam, mengi, karamagi, chenge, Tibaijuka. Mabadiliko ya kweli yataletwa na kizazi cha viongozi wasiokula rushwa na wasio na tamaa ya madaraka. Naomba uendelee kuomba mabadaliko ili tupate viongozi wasio na uchu wa madaraka kama lowassa.Ulikesha wewe kumuomba huyo mungu wako, mimi mpaka leo namuomba MUNGU wangu alete mabadiliko TZ