Mbowe amesalitiwa, wapo wa kuwajibishwa

Petro E. Mselewa

JF-Expert Member
Dec 27, 2012
9,756
2,000
Alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa CHADEMA jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Freeman A. Mbowe alitoa agizo. Mh. Mbowe aliwaagiza viongozi wa ngazi zote kuhakikisha kuwa hakuna wagombea wa CCM wanaopita bila ya kupingwa.

Kunaripotiwa habari za kuenguliwa kwa mamia ya wagombea wa CHADEMA kwa njia ya mapingamizi. Wagombea wa CCM katika sehemu hizo wameshapita bila ya kupingwa.

Mapingamizi hujitokeza hasa kutokana na uchukuaji,ujazaji na urejeshwaji wa fomu za wagombea. Hatua zote hizo zinasimamiwa na Sheria pamoja na Kanuni za Uchaguzi. Viongozi wanapaswa kujua sheria na taratibu husika na kuzizingatia. Wao walipaswa kuwasaidia na kuwasimamia wagombea wao.

Kuenguliwa kwa wagombea hao kwa mamia kunatia shaka juu ya weledi na umakini wa viongozi katika sehemu husika. Ni usaliti wa wazi wa agizo la Mbowe juu ya kuzuia kupita bila kupingwa kwa wagombea wa CCM. Kwa usaliti wao wanapaswa kuwajibishwa kichama.

Kimsingi,huu si wakati wa kutopingwa. Viongozi wazembe na wasaliti wa agizo la Mwenyekiti Mbowe lazima wachukuliwe hatua kulingana na taratibu za chama chao.
 
thatha

JF-Expert Member
Apr 29, 2011
15,340
2,000
Siku zote CHADEMA ni watu wa kupuuza taratibu na sheria katika maeneo mengi sana, huo ndiyo mshahara wa dharau zao
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,532
1,195
Tatizo lenu vijana wa BAVICHA, kila kitu ni USALITI, USALITI, USALITI.

Mnatembea mmebeba ndani ya mifuko yenu stamp iliyoandika usaliti.

Usaliti unatoka wapi hapo?.

The bottom line, CHADEMA haina wagombea makini kwa sababu inaokota wagombea barabarani ambao wengine hata hawajawahi kuiona Katiba ya CHADEMA achilia mbali Ilani yake ya uchaguzi ambayo imejaa ulaghai.

Chama cha hovyo hovyo kinazaa wagombea wa hovyo hovyo.

Ulitaka wagombea makini watoke wapi wakati wanachama wanajaa kwenye kiganja cha mkono!.
 
Erythrocyte

JF-Expert Member
Nov 6, 2012
88,413
2,000
mkuu tusubiri kidogo baada ya rufaa ndio tutafute wa kuwajibika , hujuma zinaweza kuwepo lakini wasimamizi wa uchaguzi huu nao si wa kuaminika .
 
Gwallo

JF-Expert Member
Oct 15, 2010
2,992
2,000
Tatizo lenu vijana wa BAVICHA, kila kitu ni USALITI, USALITI, USALITI.

Mnatembea mmebeba ndani ya mifuko yenu stamp iliyoandika usaliti.

Usaliti unatoka wapi hapo?.

The bottom line, CHADEMA haina wagombea makini kwa sababu inaokota wagombea barabarani ambao wengine hata hawajawahi kuiona Katiba ya CHADEMA achilia mbali Ilani yake ya uchaguzi ambayo imejaa ulaghai.

Chama cha hovyo hovyo kinazaa wagombea wa hovyo hovyo.

Ulitaka wagombea makini watoke wapi wakati wanachama wanajaa kwenye kiganja cha mkono!.

Mkuu habari za Lindi na Mtwara? ulikosekana sana jukwaani wakati wa Escrow, kwema lakini????????
 
MwanaDiwani

JF-Expert Member
Mar 22, 2013
5,532
1,195
Mkuu habari za Lindi na Mtwara? ulikosekana sana jukwaani wakati wa Escrow, kwema lakini????????
Ndugu,
Ninakushuku kwa kunijulia hali, sina budi pia kurudisha fadhira.

Kwa habari zaidi za Lindi na Mtwara pitia kwenye thread hizi,

Hiyo ndiyo CCM katika kazi zake za kila siku.

Karibu sana!
 
Mr.Professional

JF-Expert Member
Oct 4, 2010
1,582
1,195
Hili ni tatizo kubwa sana na hofu yangu ya kila mara. Tumekuwa tukisema mara nyingi chadema kinapaswa kuandaa viongozi makini kuanzia ngazi zote. Sasa hivi tunauongozi karibu kila wilaya na mikoa inakuaje wanashindwa kuratibu mambo madogo kama haya. Hao viongozi wa wilaya na mikoa kazi yao ni nini au wanasubiri mpaka mwenyekiti na katibu mkuu ndio waende kufanya kazi zao. Hapa ni lazima watu wawajibike kwa kujipima kama kweli wanafaa kuendelea na nyadhifa zao tunapoelekea uchaguzi wa mwaka 2015. Otherwise napo tutegemee business as usual kusema tumefanyiwa fitina na ccm wakati sie wenyewe tumebweteka.

Viongozi hawawezi hata kuhamasisha watu waende kujiandikisha kwenye daftari la wapiga kura na bado tunategemea kushinda hizi ni ndoto za alinacha tuamke tuwe watu wa matendo na sio maneno matupu wananchi watatuchoka baada ya uchaguzi ujao
 
Morinyo

JF-Expert Member
Aug 26, 2011
2,795

CCM wana ofisi kila wilaya na kila mwezi ofisi ya wilaya inatumia kiasi cha pesa kwa ajili ya kuratibu shughuli za chama. Ofisi za wilaya za ccm zina uwezo wa kuzunguka vitongoji vyote kuandaa wagombea wao. Vyama vyetu vya upinzani havina utaratibu wa kuziwezesha ofisi za wilaya kifedha, hata kama ruzuku ni ndogo lakini haijulikani ni kiasi gani cha ruzuku kinaenda kusaidia kazi za wilayani. Huwezi ukazunguka wilaya nzima kwa mguu ndani ya mda mfupi kama wa kupitia fomu za wagombea. Pamoja na kua yapo matatizo ya uzembe lakini kabla ya kuwawajibisha watu inabidi tuangalie ofisi zenyewe zina hali gani ili tujue tatizo lilipo, vinginevyo tutakua tunabadili chupa lakini mvinyo ile ile.
 
Katika hili kama uzembe ukiwa ni kwa viongozi wa kitaifa nao inabidi tuwawajibishe. Ni lazima kuonesha utofauti kama kweli tunafanya modern politics sio tunakuwa tunafanya yaleyale tu. kila uchaguzi yaani sie hatujifunzi kila siku hapana chama kifanye tathimini na kuwanyooshea vidole wote wanaohusika hata kama ni viongozi wajuu kabisa otherwise chadema kitakuwa hakina utofauti na vyama vingine vya wachumia tumbo
 
Ghosryder

JF-Expert Member
Jul 6, 2014
10,147
2,000
Alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa CHADEMA jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Freeman A. Mbowe alitoa agizo. Mh. Mbowe aliwaagiza viongozi wa ngazi zote kuhakikisha kuwa hakuna wagombea wa CCM wanaopita bila ya kupingwa.

Kunaripotiwa habari za kuenguliwa kwa mamia ya wagombea wa CHADEMA kwa njia ya mapingamizi. Wagombea wa CCM katika sehemu hizo wameshapita bila ya kupingwa.

Mapingamizi hujitokeza hasa kutokana na uchukuaji,ujazaji na urejeshwaji wa fomu za wagombea. Hatua zote hizo zinasimamiwa na Sheria pamoja na Kanuni za Uchaguzi. Viongozi wanapaswa kujua sheria na taratibu husika na kuzizingatia. Wao walipaswa kuwasaidia na kuwasimamia wagombea wao.

Kuenguliwa kwa wagombea hao kwa mamia kunatia shaka juu ya weledi na umakini wa viongozi katika sehemu husika. Ni usaliti wa wazi wa agizo la Mbowe juu ya kuzuia kupita bila kupingwa kwa wagombea wa CCM. Kwa usaliti wao wanapaswa kuwajibishwa kichama.

Kimsingi,huu si wakati wa kutopingwa. Viongozi wazembe na wasaliti wa agizo la Mwenyekiti Mbowe lazima wachukuliwe hatua kulingana na taratibu za chama chao.

Maumivu ya kichwa huanza polepole..................
 
wikolo

JF-Expert Member
Oct 19, 2010
801
195
Tatizo lenu vijana wa BAVICHA, kila kitu ni USALITI, USALITI, USALITI.

Mnatembea mmebeba ndani ya mifuko yenu stamp iliyoandika usaliti.

Usaliti unatoka wapi hapo?.

The bottom line, CHADEMA haina wagombea makini kwa sababu inaokota wagombea barabarani ambao wengine hata hawajawahi kuiona Katiba ya CHADEMA achilia mbali Ilani yake ya uchaguzi ambayo imejaa ulaghai.

Chama cha hovyo hovyo kinazaa wagombea wa hovyo hovyo.

Ulitaka wagombea makini watoke wapi wakati wanachama wanajaa kwenye kiganja cha mkono!.

Sawa mkuu wangu ila nikukumbushe tu kwamba tuliwaona pia wawakilishi makini wa CCM wakitoa michango yao bungeni kwenye sakata la escrow. Tuliwaona akina Mariam Kisangi, Hawa Ghasia, Asumpta, Chombo na wengineo. Kweli huko CCM kuna watu makini!!
 
dudus

JF-Expert Member
Feb 28, 2011
15,477
2,000
Hii sheria ya "pingamizi" inatakiwa kutazamwa upya; inatakiwa ku-focus katika issue nzito kama wagombea wasio raia, n.k. Lakini mambo ya kipuuzi kama sijui mgombea kasaini kwa Kiarabu badala ya Kiswahili haina mashiko na wengine wanatumia mianya hii vibaya.

Mgombea atakayejitoa dakika za mwisho au atakayethibitika kusuasua kwenye kampeni au kutoa kauli za ajabu ajabu kwa malengo ya kuunga mkono upande wa pili anatakiwa kwenda jela miaka 10 pasi na kuruhusiwa kugombea tena ndani ya miaka 10 baada ya kutoka jela endapo chama chake kitafungua shauri mahakamani.

Ni lazima dawa ya kupambana na mamluki ipatikane kisheria ili kukuza demokrasia. Lakini, je, magamba ambao ni wanufaika wakubwa wa mamluki watakubali? Hii nayo ni changamoto nyingine.
 
Mr.Mponezya

Member
Dec 1, 2014
33
0

Sheria za kijinga kama hizi ndio tegemeo la magamba , hata hivyo tutapambana hadi tone la mwisho .
 
MUSSA ALLAN

JF-Expert Member
Oct 13, 2013
18,927
2,000
Tatizo lenu vijana wa BAVICHA, kila kitu ni USALITI, USALITI, USALITI.

Mnatembea mmebeba ndani ya mifuko yenu stamp iliyoandika usaliti.

Usaliti unatoka wapi hapo?.

The bottom line, CHADEMA haina wagombea makini kwa sababu inaokota wagombea barabarani ambao wengine hata hawajawahi kuiona Katiba ya CHADEMA achilia mbali Ilani yake ya uchaguzi ambayo imejaa ulaghai.

Chama cha hovyo hovyo kinazaa wagombea wa hovyo hovyo.

Ulitaka wagombea makini watoke wapi wakati wanachama wanajaa kwenye kiganja cha mkono!.

Kweli kabisa Mkuu, Na kingine nilichokishuhudia hapa Arusha, hata wale wagombea waliojaribu kugombea kupitia CHADEMA kipindi kilichopita, sasa wamejiunga na CCM na kugombea kupitia CCM, hivyo kuendelea kukuza ombwe la watu makini ndani ya CHADEMA.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom