Petro E. Mselewa
JF-Expert Member
- Dec 27, 2012
- 10,176
- 25,446
Alipokuwa akifungua Mkutano Mkuu wa CHADEMA jijini Dar es Salaam,Mwenyekiti wa Taifa wa chama hicho Freeman A. Mbowe alitoa agizo. Mh. Mbowe aliwaagiza viongozi wa ngazi zote kuhakikisha kuwa hakuna wagombea wa CCM wanaopita bila ya kupingwa.
Kunaripotiwa habari za kuenguliwa kwa mamia ya wagombea wa CHADEMA kwa njia ya mapingamizi. Wagombea wa CCM katika sehemu hizo wameshapita bila ya kupingwa.
Mapingamizi hujitokeza hasa kutokana na uchukuaji,ujazaji na urejeshwaji wa fomu za wagombea. Hatua zote hizo zinasimamiwa na Sheria pamoja na Kanuni za Uchaguzi. Viongozi wanapaswa kujua sheria na taratibu husika na kuzizingatia. Wao walipaswa kuwasaidia na kuwasimamia wagombea wao.
Kuenguliwa kwa wagombea hao kwa mamia kunatia shaka juu ya weledi na umakini wa viongozi katika sehemu husika. Ni usaliti wa wazi wa agizo la Mbowe juu ya kuzuia kupita bila kupingwa kwa wagombea wa CCM. Kwa usaliti wao wanapaswa kuwajibishwa kichama.
Kimsingi,huu si wakati wa kutopingwa. Viongozi wazembe na wasaliti wa agizo la Mwenyekiti Mbowe lazima wachukuliwe hatua kulingana na taratibu za chama chao.