Mbowe amekubali CHADEMA kimfie mikononi

William Mshumbusi

JF-Expert Member
Mar 27, 2012
1,657
2,252
1488314_185131778355725_308368871_n.jpg

Zitto ukiacha kauli zake matendo yake sasa ni sawa na ule wimbo wa kale wa vikosi vya tz zidi ya amini wa "CHADEMA ikifa yeye awezi kulia atajiunga CCM awe mbunge wa kigoma".

Sababu ata mkakati wake wa ushindi hauonesi kwa uyakinifu mbinu mbadala alizotaka kujanazo ili kuijenga Chadema bali umejaa ukosoaji mkubwa kwa mwenyekiti wake tu.

Pili vitu alivyoviona kwenye uongozi wa juu wa Chadema Na kuvikosoa sana kama usiri kwenye matumizi ya fedha na swala la wapi wangepata fedha za uchaguzi 2015 na maamuzi makubwa kuwa mikononi mwa watu wachache ndivyo alivyokopi na kupesti na kuweka kwenye mkakati wake wa ushindi kwani.

Wapi wangepata pesa na zitumikaje kuupata uwenyekiti chadema lilibakizwa liwe siri kati ya MM NA M1 na hawakutaka ata wapambe wajue. Pili halipinga sana kitengo cha usalama kisichoonekana wakati anajua wazi ndicho kinachowaumbua mipango ya CCM dhidi ya viongozi wa chadema kama Kesi ya kugushi za kina Rwakatare, za kugushi za Mnyika aliyotaka kufunguliwa na mwigulu. Vyanzo vya Mabomu wanayopigwa na ndio usalama wa viongozi wa chadema na hajiulizi kwanini usalama wa taifa kwa asilimia nyingi ni invisible.

Kitu kibaya zaidi ata mkakati wa ushindi uliweka wazi mapungufu yake kama kuongozwa na Jazba akibuguziwa. Kutojua kuchagua maneno ya kuongea akibuguziwa lakini habadiliki mpaka sasa kwani toka avuliwe uongozi kauli zake zinakinzana mara.

Ukaguzi wa matumizi ya fedha mara uraisi mara mabilioni ya uswisi Sasa waelewa hatumuelewi. Tunasubili akivuliwa uanachama akamilishe sababu mbili za Mwisho Ukanda na Udini ili akiulie mbali Chadema.

Hata hivyo sababu ninayoielewa sana ata unishikie bunduki. Swala la katiba kubadilishwa kinyemela ili Mbowe awe mwenyekiti wa muda mrefu na kudumu chadema. Kwanini Mbowe afanye haya. Je hana mwingine kabisa anayemwamini ndani ya Chadema ata Afiche aibu zake za uroho wa madaraka. Mbowe ficha aibu zako bwana au waelewa huku mtaani hatukuungi mkono tumewaachia misukule. Kaka Freemani Alkael Mbowe unataka chama kikufie mikononi ili uende zako Uswisi ukamalizie akaunti zako. Siko upande wa zitto wala mbowe. Napenda mabadiliko ya kweli tu basi
 
Wewe mtu wa CCM unahangaika sana.Kama chama kinamfia si unatakiwa ufurahi?
 
hahahaha, hehehe jf bhanaa!!!!
yaani kuitwa CCM ni zaidi ya tusi????

kabisa tena ndilo tusi kubwa linalotumiwa na wapinga Democrasia au watu spesho wa kumtetea Mbowe humu Jf kama vile ni malaika.

Kama ni kupendwa Mandela alipendwa sana lakini alijiuzuru baada ya minne. Nyerere angegombea uraisi mpaka kifo. Lakini walijiongoza
 
Hivi Zitto kuna Kazi nyingine yoyote aliyowahi kufanya zaidi ya Siasa?.Ana uzoefu gani wa Maisha nje ya Siasa?
 
CCM sio mchezo, ile ni mwanzo mwisho, nilikuwa naanza kuwaona wale wanawezad kumbe, ni waigizaji tu, hela tu ndio chanzo, ulaji period tusidanganyane, ila basi Zitto amefanya mengi mbona hawampi nafasi, yaani wawe tu wa kaskazini haiwezekani, kwakweli CCM ndio chama tawala, wengine ni waigizaji, wachanga
 
Nimefanya utafiti juu ya JAMII FORUM; Hali ya Siasa Nchini na Ms Mstakabli wa Tanzania: Majibu ya Utafiti wangu ni Kama ifuatavyo:-

Hali ikiendelea hivi ndani ya jukwaa bila Mods kuchukua hatua, halitakwepa lawama ya kuwa chanzo cha kuivuruga nchi yetu.(Jukwaa limekuwa kilinge cha watu kutumia hoja dhaifu za udini, ukabila na ukanda kwa maslahi yasiyo na afya kwa nchi)

Jukwaa limekuwa ni source ya udaku wa siasa za Tanzania tofuati na miaka kadhaa nyuma ambapo Jukwaa lilikuwa ni sehemu ya kujadili matatizo ya nchi yetu (Elimu, nishati, miundombinu nk)..

Hali ikiendelea hivi, basi JAMII FORUM haitakuwa na muda mrefu na itapoteza sifa yake iliyojijengea...

Ushauri... Moderators lazima mbadilike, role yenu kubwa iwe ni ku-control flow ya topics.. Utakuta kuna topics karibu 30 zinazungumzia kitu kimoja, cha kufanya ni kuziunganisha ziwe kwenye folder moja.... (Epukeni upendeleo)
 
I second it.
 
CDM ikifa CCM si ndo mfurahi au...? Huu mtego CCm waliyowekewa wa siku 14 watasema yote
 
Back
Top Bottom