Mbowe ajibu tuhuma dhidi yake juu ya matumizi ya gari la KUB.

Vipi Zitto naye amerudi na kuchukua posho au? Kama bado Zitto anaendelea na msimamo wake basi huo ndio msimamo thabiti na siyo msimamo wa nataka sitaki.
Zitto anasema tangu mwaka jana hadi leo posho yake inapelekwa kwenye mfuko wa maendeleo ya jimbo!!!!
 
Kufuatia tuhuma zilizo elekewa kwake juu ya matumizi shangingi la kambi ya upinzan mbowe alikua na haya yakusema:

"Mimi nilikataa gari kwa kipindi cha miezi sita na nikawa natumia gari langu kwa shughuli zote za vikao vya bunge,lakini nataka umma uelewa kuwa kwa nafasi yangu natakiwa kulipwa posho ya madaraka sh 200000 kila mwezi,kupewa nyumba ya kuishi ikiwa samani zake.

Ila mpaka sasa sina nyumba ya serekali,wala mlinzi,wala kulipwa fedha za mawasiliano,vyote natumia fedha zangu...kama ningetaka ningedai mambo mengi ambayo natakiwa kupata lakini kulingana na hali ya uchumi wa nchi ni lazima nitumie fedha zangu ili kunusuru uchumi" alisema.

Source: Tanzania daima 22 june, 2012

Enzi za Mwalimu.

Wabunge wa BUNGE la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania wakielekea kwenye VIKAO vya Bunge huko DODOMA mwaka 1984 kwa kutumia usafiri wa Basi . Unaonaje hii Mdau? Wengi Wanafiki Walafi Sasa Hivi...

kama ndiyo aina ya utetezi wenyewe basi naanza kuamini bongo hatuna viongozi wenye kusimamia dhamira zao. Umekataa alafu baadaye unachukua? Kuweni makini sana watz sasa hivi tuko makini na kwa kiasi fulani tumeanza kuwaamini sasa kwa uroho huu ttaanza kuwashuku. Unaulizwa kuhusu kukubali gari mpya tena ya thamani kuliko hata ile ya kwanza unajitetea kwa kukumbushia stahiki zako za awali. Sasa ndo unafidia au?
wabongo bwana hivi mbona mnafuatilia vitu vidogo. Kwanini hamkomai na wezi waliopeleka hela >300bn katk swiss banks?
 
Fikra za mtu duni, hutoa hoja duni zisizo na tija. Nani kakudanganya kuwa penye wakatoliki hakuna maendeleo. Inawezekana maisha yako yote umekulia manzese uwanja wa fisi ndio maana, kwa hiyo sikushangai. Hebu jaribu kufanya tafiti alafu utuletee hoja zenye uzito.

Utuletee picha hapa na tafiti zenye ushahidi wa ukisemacho. Acha udini na kupayuka, hakutakusaidia maishani.
 
nani kakuambia chadema ni chama,historia inaonyesha sehemu yoyote ukiingia mkono wa wakatoriki hakuna maendeleo.

Mkuu MADAYA hii kauli niliwahi kuisikia toka kwa mzee mmoja hivi ambaye ni Mkatoliliki (Nami ni mkatoliki). Alinmiambia kwamba Wakatoliki ni wachoyo na huwa hawasambazi maendeleo kama wamissionari wengine. Wao hujizungushia tu hata kama ni maji wanakuwa nayo mission kwao lakini hawawapi majirani. Utakuta wana umeme lakini jirani wako gizani. Akaniambia Ureno ni ya wakatoliki zaidi na ndio miongoni mwa nchi masikini huko Ulaya. Nikatafakari nikaangalia mission za vijijini kwetu nikaona ka ukweli fulani!
 
Last edited by a moderator:

Vipi kuhusu huduma za jamii znazomikikiwa na katoliki? Mf.shule na hosputali, je zinatoa huduma kwa wakatoliki pekee au? Baada ya kumsikia huyo mzee wako akibweka hivyo we ulifanya utafiti maeneo gani hadi unataka utuaminishe na hoja yako dhaifu isiyo na supportive evidence? Jipange upya!!
 
Last edited by a moderator:
Hili suala limevaliwa njuga na wanaCCM. Na hii yote inadhihirisha kwamba Lusinde & company wameegemea kimaslahi zaidi. Simlaumu Mbowe nalaumu serikali yetu kwa kuendekeza anasa huku hali ya mahospitali na shule ipo duni
 
Tatizo la Mbowe ni kuwa kama cdm wakiingia madrakani atadai marejesho kwa kupitia ufisadi.. ufisadi anaoufanyia cdm hujitetea ya kuwa cdm ilipokuwa haina kitu yeye aliifadhili kwa hiyo saa ya malipizi imewadia................mbowe is a the night mare of cdm for he is the face og offical grand graft within the corridors of the opposition...................
 
na bado mtamuona slaa akiingia madarakani,atatafuna kama alivyozitafuna akiwa katabu wa baraza la maaskofu tanzania
Sio kutafuna kama aliyotafuna za kanisa, bali sema kutafuna kama jinsi CCM inavyotafuna utajiri wetu na kutunyonya mchana kweupeee. Kweli CCM ni janga la kitaifa, CCM haikubaliki, tushirikiane kuitokomeza.
 
ndio eti hao wenye msimamo ndo wanaonekana wasaliti,wa chama wakati wao walikubaliana hiv kuto kuchokua posho
 
Kufuatia tuhuma zilizo elekewa kwake juu ya matumizi shangingi la kambi ya upinzan mbowe alikua na haya yakusema:

"Mimi nilikataa gari kwa kipindi cha miezi sita na nikawa natumia gari langu kwa shughuli zote za vikao vya bunge,lakini nataka umma uelewa kuwa kwa nafasi yangu natakiwa kulipwa posho ya madaraka sh 200000 kila mwezi,kupewa nyumba ya kuishi ikiwa samani zake.

Ila mpaka sasa sina nyumba ya serekali,wala mlinzi,wala kulipwa fedha za mawasiliano,vyote natumia fedha zangu...kama ningetaka ningedai mambo mengi ambayo natakiwa kupata lakini kulingana na hali ya uchumi wa nchi ni lazima nitumie fedha zangu ili kunusuru uchumi" alisema.

Source: Tanzania daima 22 june, 2012
Mbowe mnafiki mkubwa wewe umepewa nyumba Dar na dodoma na mlinzi pamoja ofisi na VX, na pia ukimaliza kama kiongozi wa kambi rasmi bungeni utapewa mil200 kama kiinua mkongo lakini ukiachia uenyekiti tu utakosa hiyo fursa
 
Kufuatia tuhuma zilizo elekewa kwake juu ya matumizi shangingi la kambi ya upinzan mbowe alikua na haya yakusema:

"Mimi nilikataa gari kwa kipindi cha miezi sita na nikawa natumia gari langu kwa shughuli zote za vikao vya bunge,lakini nataka umma uelewa kuwa kwa nafasi yangu natakiwa kulipwa posho ya madaraka sh 200000 kila mwezi,kupewa nyumba ya kuishi ikiwa samani zake.

Ila mpaka sasa sina nyumba ya serekali,wala mlinzi,wala kulipwa fedha za mawasiliano,vyote natumia fedha zangu...kama ningetaka ningedai mambo mengi ambayo natakiwa kupata lakini kulingana na hali ya uchumi wa nchi ni lazima nitumie fedha zangu ili kunusuru uchumi" alisema.

Source: Tanzania daima 22 june, 2012

Hahahaaaaa! owwwwkey mh.mbunge,lakini mbona ulikumbuka kunusuru uchumi ukasahau kuinusuru ndoa yako ilhali hilo ndilo lilikua ndani ya uwezo wako zaidi??

Pamoja na majibu mazuri ya mh.mbunge,Nahitaji ufafanuzi zaidi kwenye eneo hilo.

Asante.
 
Hivi sisi kama raia tunachotakiwa kufanya ni nini?! Kumzomea Mbowe au kuishinikiza serikali iache kuudhoofisha uchumi wetu wa kuungaunga kwa matumizi ya magari ya anasa na posho za kifisadi??? Tunaochangia hapa tunaiambia nini serikali ya ccm ambayo ndiyo INALAZIMISHA matumizi ya magari ya anasa na kujigawia posho za kifisadi?! Wabongo tunaelekea kuwa vinara wa unafiki duniani, hivi kweli hatujui wa kumbana kuhusiana na matumizi mabaya ya mapato yetu?!

Hawa viongozi nawabunge wavyama vya upinzani ndio wangekuwa chahchu ya kuupinga huu mfumo dhalimu, lakini wao hawako tayari kukosa hizo posho na malulupu mengine unategemea wewe utapingaje ? tusiwaonee huruma wapinzania kama wamekosea ni kusemwa live kwa sababu wao ni tegemeo la wananchi kwa yale mambo maovu yanayofanywa na chama tawala.

Minashangaa sana kwa mambo ambayo hayawapi tija wapinzania wanajifanya wa kwanza kulalamika lakini yale yanayowapa faidazao binafsi wanaungana na chama tawala mf hizi posho, ruzuku kwa vyama vya siasa pesa ambazo zingeweza kuwa saidia wananchi masikini Tanzania.
 
Back
Top Bottom