Yaliyojiri katika kesi ya Mbowe na wenzake: Kaaya amaliza kutoa ushahidi. Shauri kuendelea 29/10/2021

Suley2019

JF-Expert Member
Oct 7, 2019
1,758
4,307
Salaam Wakuu,

Ile Kesi inayomkabili Freeman Mbowe na wenzake itaendelea katika Mahakama Kuu, Divisheni ya Uhujumu Uchumi na Rushwa, ambapo Ushahidi unaendelea kutolewa.

Fuatilia uzi huu ili kujua kinachojiri katika mchakato mzima wa kesi hiyo kwa siku ya leo 28/10/2021
====

Mawakili upande wa utetezi tayari wameshafika mahakamani na kuketi katika nafasi zao, tayari kuanza kwa kesi.

FCxAQKEXMAMJYS8

Mawakili upande wa utetezi tayari wameshafika mahakamani na kuketi katika nafasi zao, tayari kuanza kwa kesi.

FCxB4RdXEAEz1WI

Shahidi akiwasili mahakamani, akiwa ameambatana na wakili wa Serikali, ambapo leo atakutana na wakili Peter Kibatala anayeongoza jopo la mawakili wa utetezi.

Upande wa utetezi ameongezeka Wakili Niyikiza Seth Jacob, ametokea Bukoba mkoa wa Kagera Kuja kuongeza nguvu katika kesi ya Mbowe na wenzake.

- Jaji ameingia Mahakamani, Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 inatajwa

Wakili wa Serikali Robert Kidando anawatambulisha wenzake
1.Abdallah Chavula,
2. Jenitreza Kitali,
3. Nasorro Katuga,
4. Esther Martin,
5. Ignasi Mwinuka
6. Tulimanywa Majige

Wakili Kibatala anawatambilisha wenzake
1. Peter Kibatala
2. Bonifasia Mapunda
3. Seleman Matauka
4. Sisty Aloyce
5. Dickson Matata
6. Michael Mwangasa
7. Jonathan Mndeme
8. Hadija Aron
9. Evaresta Kisanga
10. Maria Mushi
11. Idd Msawanga
12. John Malya

Wakili wa Serikali: Shauri linalopaswa limekuja kwa a ajili ya Ushahidi na Shahidi namba mbili anaendelea

Jaji: Jana tuliishia kwa Mawakili wa Mshitakiwa wa Kwanza wa Pili, Naomba tuendelee na Wakili wa tatu Mshitakiwa na nakukumbusha Shahidi upo chini ya Kiapo, Naomba sasa.

MATATA: Kwa Niaba ya Mshtakiwa watatu sisi hatuna Maswali

JAJI: Wakili wa Mshtakiwa wa Nne

Wakili Kibatala ameanza kumuuliza Shahidi maswali

Kibatala: kwa Ruhusa yako Mheshimiwa Jaji naomba Kuuliza Maswali yakibakia nitaomba Michael Mwangasa amalizie.

Kibatala: Shahidi unakumbuka Jana wakati wa Ushahidi wako ulitaja namba zako za Simu

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Unaweza kunitajia

Shahidi: 0693006700 na 0754916666

Kibatala: Unajua kuwa Umekuja Kutoa Ushahidi Kwenye kesi Nzito?

Shahidi: sijui Kesi Nzito, Najua Nimekuja kutoa Ushahidi tu

Kibatala: Unakumbuka wakati Unaandika Maelezo yako kwa Inspector Swila ulitoa namba zako za Simu

Shahidi: Hapana sikutoa

Kibatala: kwa Ruhusa ya Mahakama Unaweza Kusoma Hapa

Shahidi: 0754 216170

Kibatala: Je unasemaje kuhusu hizo namba

Shahidi: sijui sasa

Kibatala: Je iambie Mahakama chini ya Kiapo hizi namba Inspector Swila kazitoa wapi

Shahidi: Sijui

Kibatala: Shahidi unaweza kutuambia aliyethibitisha Maelezo ya Inspector Swila kuwa Maelezo ni sahihi ni nani?

Shahidi: Ni mimi

Kibatala: ni Mmoja wa aliyekuwa anawalinda Mahakamani wakati wa kesi?

Shahidi: Hapana

Kibatala: tutarudi hapo baadae

Shahidi: Jana wakati Unatoa Ushahidi ulisema hujawahi kuwa Mwanachama wa Chama chochote cha siasa

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: hujawahi Kushiriki Kura za Maoni kata ya Pili?

Shahidi: Sijawahi

Kibatala: Kama Nikileta Ushahidi ulishiriki

Shahidi: walete Mahakamani

Kibatala: Nimesikia umesema kuwa Umeishi na Sabaya na Ukasema ulikuwa unaishi naye akiwa na Mke wake

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je ulitutajia Jina la Mke wa Sabaya

Shahidi: Nilitaja Jina Moja la Jesca

Kibatala: Je Uliishi na Sabaya Kwa Muda gani akiwa Mkuu wa wilaya

Shahidi: Miezi Mitatu

Kibatala: Unafahamu Mahala anapoishi Mkuu wa Wilaya ni Mahala Nyeti

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Unafahamu Makazi ya Mkuu wa Wilaya ni Ikuku Ndogo ya Hilo eneo

Shahidi: sahihi

Kibatala: Unafahamu Kuwa kuna Baadhi ya Vikao Vya Kiusalama vinafanyika kwa Mkuu wa Wilaya

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Je, wewe ulifanyiwa Vetting na Tasisi yoyote?

Shahidi: Hapana

Kibatala: na Ulikuwa na Access ya Kuachiwa Nyumba na kuingia popote kwa Mkuu wa wilaya

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Nimeona pia una jina lingine la Power Kaaya, umelitoa wapi

Shahidi: Tangu nikiwa Nyumbani

Kibatala: nitakuwa sahihi nikisema Umepewa hilo Jina baada ya Kufanya uhalifu sana Maeneo ya Longido na Arusha..?

Shahidi: Hapana si Kweli

Kibatala: nitarudi eneo hilo baadae

Kibatala: Je, unafahamu wakati Unakutana na Freeman Mbowe ulikuwa unafahamu ni Mwalifu

Shahidi: Sijui

Kibatala: Wakati Unakutana na Mbowe ulikuwa unajisikia Amani Kukutana naye peke yako?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Wakati unampa Majina ulitambua kuwa yanakwenda kutendewa Uhalifu

Shahidi: Ndiyo nilijua kuwa kuna harufu ya uhalifu

Kibatala: Una Elimu gani Shahidi: Kidato cha Nne

Kibatala: Kwa hiyo ukiona Uhalifu wa Madawa ya Kulevya unatolea Taarifa wapi

Shahidi: Polisi

Kibatala: Ukiona uhalifu wa Wizi unatolea Taarifa wapi

Shahidi: Polisi

Kibatala: Je, Wakati Mbowe anakupatia pesa TSh Laki Mbili ulijua ilikuwa kwa ajili ya Uhalifu?

Shahidi: Hapana alisema ilikuwa ni ya Usumbufu

Kibatala: we Uliamini kuwa ni ya usumbufu?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: ulisema baada ya Kukutana na Mbowe ulimpigia simu Mbunge na Sabaya

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Je uliriport polisi?

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je, Kazi ya Mbunge ni Kushughulika na uhalifu

Shahidi: Ndiyo wao ni watunga Sheria

Kibatala: Je, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji baada ya kutoa Taarifa kwa Mbunge ulifuatilia kama amefanyia kazi Taarifa hiyo

Shahidi: Hapana sikufuatilia

Kibatala: Shika Maelezo yako haya Kielelezo D1 uliyoyatoa kwa Inspector Swila kama Ulimwambia Mambo ya Kihalifu aliyokwambia Mbowe

Shahidi: Haipo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa ulitolea Maelezo kwa Tasisi yoyote ya Kiuchunguzi kuhusu uhalifu wa Mbowe

Shahidi: Hakuna

Kibatala: ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa ulimpigia Sabaya Simu, Je ulitaja namba za Simu za Sabaya

Shahidi: Sikuzitaja

Kibatala: Ulimwambia Jaji Kuwa Baada ya Kumkosa Sabaya Ulifanya Jitihada za kumtafuta Sabaya

Shahidi: sikumwambia

Kibatala: ulimwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa Baada ya kumkosa Sabaya ulimtafuta Mke wa Sabaya huyo Jesca kwamba Kuna Taarifa Mbaya ya Sabaya

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Uliowataja Jana ni Walinzi wa Sabaya?

Shahidi: Hapana ni Marafiki zake

Kibatala: hao uliokuwa umewataja Jana ulikuwa umefahamiana nao kwa muda mrefu au Mfupi

Shahidi: Muda Mfupi

Kibatala: Je, uliwataarifu hao Marafiki wa Sabaya

Shahidi: Hapana

Kibatala: Wakati Unakutana na Freeman Mbowe ulihisi uhalifu gani unataka kufanyika

Shahidi: Sikuwa nafahamu

Kibatala: Mkutano wa kwanza unaosema mlikutana na Mbowe, Kama Kweli ilikuwa Lini

Shahidi: mwaka 2020 Mwezi wa Kumi, sikumbuki tarehe.

Kibatala: nilisikia kuwa Umesema walikufuata na Gari, Je ilikuwa gari ya KUB?

Shahidi: ilikuwa gari ya Kiraia

Kibatala: ulisema alikuwa anaendesha Mwanamke?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Angalia Maelezo yako hapo, Je umeeleza kuhusu huyo Mwanamke

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji kuna Mahala yoyote ulitoa Taarifa, kama Polisi hivi, ndiyo ukaenda Kukutana naye

Shahidi: Sikutoa

Kibatala: Ulipokamatwa 20/08/2020 ulihifadhiwa Gereza gani..?

Shahidi: Ukonga

kibatala: Lakini Ulikutana na Mbowe Longido 0ctober 2020, Okeeeey Kazi yangu Kuuliza Maswali.

Kibatala: haya Mara ya Pili Mlikutana na Mbowe Wapi na lini

Shahidi: Mwanzoni Mwaka 2020

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji ni wapi katika Statement ataona Khalfani Bwire alikwepo Katika Kikao Moshi

Shahidi: Khalfani Bwire alikuwa katika Kikao cha tatu

Kibatala: Sawa Mwambie sasa Katika hayo Maelezo yako, ni wapi ulimwambia Inspector Swila kuwa Khalfani Bwire alikwepo?

Shahidi: Hakuna

Kibatala: Nini kilitangulia kati ya Maelezo yako na Ushahidi wako Mahakamani

Shahidi: Kilitangulia Maelezo

Kibatala: Je wewe ulimtambua Bwire wapi?

Shahidi: Kabla ya Mahakamani

Kibatala: kwa hiyo kumtambua Bwire umefanya Jana Hapa Mahakamani

Shahidi: Nilimtambua Kabla

Kibatala: kwa Hapo Kwenye maelezo ipo sehemu Umemtaja Bwire.?

Shahidi: Hapana

Kibatala: kwa hiyo sisi tunaona umefanya hivyo kwa mara ya kwanza Jana, uliwahi Kuwa nao Pamoja jela

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: mliongea nini

Shahidi: wao ndiyo walikuwa wananielezea walivyokuwa wanamtafuta Sabaya, Wakakurupushwa, wakahisi ni mimi.

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Mambo mazito kama hayo katika Statement hiyo atayaona Ukurasa wa ngapi

Shahidi: Hayapo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Mambo Mazito kama hayo kama uliriport kwa Mkuu wa Gereza

Shahidi: Sikusema

Kibatala: inawezekana wewe na Inspector Swila Mlipitiwa sasa Mwambie Mheshimiwa Jaji kama uliriport Matukio kama hayo popote

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Je Ulizungumzia kuwa Ulikamatiwa wakati unapelekea pesa benki

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ukasema ulikuwa na Dollar na Euro

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ukasema ulikuwa unafanya Biashara na Hotel na Hotel gani

Shahidi: Mount Meru

Kibatala: Je, ulitoa kielelezo Chochote kama Ulilipwa fedha hizo

Shahidi: Sikutoa

Kibatala: ulifafanua kwa Mheshimiwa Jaji kwamba Ulibadili pesa kwa Euro na Dollar kwenda fedha za kitanzania

Shahidi: Nilifafanua Jana Kuwa nilipewa pesa mbalimbali

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kuwa Ulitoa Nyaraka za Malipo za Mount Meru

Shahidi: Sikutoa Kibatala: ulitaja Jina la Afisa aliyekulipa hizo pesa

Shahidi: Sikutoa

Kibatala: Mount Meru hawanunui papo kwa papo wanafanya kazi kwa mkataba na Mzabuni, Je ulitoa Mkataba kwa Jaji

Shahidi: Sikutoa

Kibatala: Ulitoa Risiti za TRA na Zingine, kwamba Biashara ni halali

Shahidi: Sikutoa

Kibatala: Je, unataka Mount Meru Hotel Leo wasikie wanapo fuatilia kesi hii wasikie luxury walikulipa Dollar 1000 cash

Shahidi: Siyo Mount Meru Bali Mtu wa Mount Meru

Kibatala: ooohooo Uliyasema hayo Jana

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Karoti za fedha hizo Nyingi sana, Je ulitoa Maelezo kuhusu Namna ulivyozipeleka, kwa usafiri gani na Risiti zake?

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Polisi walipokukamata Unawakumbuka?

Shahidi: Siwakumbuki

Kibatala: unasema ulihojiwa na Inspector Mahita

Shahidi: Ndiyo Kuhusu tuhuma zote

Kibatala: Mahojiano uliyafanyia wapi

Shahidi: Central Dar es Salaam

Kibatala: Mashitaka yalifutwa na Ukakabidhiwa fedha zako

Shahidi: Ndiyo nilirudishiwa

Kibatala: Walichukua hivi hivi au walikuandikisha na kukupa Karatasi

Shahidi: Walinipa Karatasi

Kibatala: Je jana Wakati Mawakili wa Serikali wakikuongoza walikuonyesha hapa Mahakamani hiyo karatasi

Shahidi: Hapana hawakunionyesha

Kibatala: swala la pesa ni kubwa sana, Je ulionyesha Karatasi kwamba sasa wamenirudishia

Shahidi: Sikuonyesha

Kibatala: Unaweza Kutuambia huyo Wakili wa Serikali ambaye badala ya kukwambia uende kwa DPP badala yake akakawambia uende Central

Shahidi: Simkumbuki

Kibatala: Sisi tunasema kuwa hizo Euro au Dollar hujarudishiwa

Shahidi: Wamenirudishia Kibatala: Sisi tutaamini Vipi

Shahidi: nimesema Chini ya kiapo

Kibatala: Ingekuwa hivyo usingekuwa unahojiwa hapa

Kibatala: haya niambie sasa kuhusu Kukutana na Freeman Mbowe, Je ulitoa Taarifa hapa Mahakamani kuwa Mlinzi wake sikuwa namfahamu Vizuri

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je, Ulimwambia Mheshimiwa Jaji baada ya Kuombwa Majina mara ya Pili Ulichukua tahadhari za Kwenda polisi

Shahidi: Sikusema

Kibatala: zile fedha ulizopokea ulizionaje za Kihalifu au fedha safi

Shahidi: Niliona Fedha safi

Kibatala: baada ya Kuona Siyo pesa Mbaya ndiyo Maana hukumuMwambia Sabaya, Mke wa Sabaya, wala Marafiki zake

Shahidi: Hapana, si kweli

Kibatala: Mwambie sasa Mheshimiwa Jaji hayo Majina Yamo katika Statement?

Shahidi: Hayamo

Kibatala: Kibatala Namba zao za Simu?

Shahidi: Hazimo

Kibatala: hilo gari la KUB uliona lini

Shahidi: January 2020

Kibatala: unataka Mahakama ikuchukulie wewe ni shahidi Muhimu na Umetoka kwa Chumbani wako kuja Kutoa Ushahidi

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je unafahamu January 2020 Freeman Mbowe alikuwa Gerezani Segerea baada ya kufutiwa Dhamana Mahakama ya Kisutu

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Je Mtu akiwa Gerezani Segerea anaweza Kukutana na wewe Longido

Shahidi: Hapana Sifahamu

Kibatala: umezungumzia Joyce Mukya Jana, Nieleze kwenye Statement hiyo Umeandika Wapi

Shahidi: Hakuna mahala nilipoandika

Kibatala: kwetu Muhimu sana sijui Kwa Mahakama

Kibatala: Je kuna Karatasi Umetoa hapa Mhakamani inayoonyesha Ushahidi wa kwamba Namba hii ilimpigia namba hii, Je ulitoa Karatasi hiyo hapa Mahakamani

Shahidi: Hapana sikutoa

Kibatala: Ni kweli Freeman Mbowe ni Mtu Maarufu

Shahidi: Ni sahihi

Kibatala: kwa hiyo hata mtu wa kawaida anaweza Kumfahamu Freeman Mbowe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sawa

Kibatala: Shahidi Jana Ulizungumzia kuwa wewe ni Mkulima, Je Mkulima analipa kodi?

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sasa wewe Ulitoa Karatasi yoyote hapa Mahakamani Kwamba unalipa Kodi

Shahidi: sikutoa kibatala: Jana Ulimtajia Majina ya Kina japhet na wenzake kwamba Je ni Viongozi wa Serikali

Shahidi: Hapana

Kibatala: Je unafahamu Kuwa Sabaya kwa Mujibu wa sheria ni Muhalifu hapa tunavyoongea

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: ila Unajua kuwa amefungwa Miaka 30

Shahidi: Ndiyo nimesikia

Kibatala: Umesikia kafungwa ila hujui kama ni Muhalifu na alifanya uhalifu Miaka ya 2018 Mpaka 2020

Shahidi: sifahamu

Kibatala: Bila shaka hufahamu pia kwamba Freeman Mbowe aliwasiliana na IGP SIRRO Kumfahamisha Matendo ya Kihalifu aliyokuwa anatenda Sabaya

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: bila Shaka hufahamu pia kuwa ni Wajibu wa Raia Mwema Kukusanya Taarifa na Kuzifikisha kwa Mamlaka husika

Shahidi: sifahamu

Kibatala: Mwanzoni ulisema kuwa Mbunge kazi yake ni Kushughulika na Uhalifu

Shahidi: Nilisema Kuwa Mbunge kazi yake ni Kutunga Sheria na anaweza Kushughulika na uhalifu

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa kuwa Wakati Mbowe anakuomba Taarifa alikuwa Mbunge

Shahidi: Alikuwa Mbunge wa Hai

Kibatala: Je, unafahamu Mtu uliye mtajia Jina lake Sylvester Nyegu amehukuliwa Kifungu cha Miaka 30 na Sabaya Kwa Makosa ya Ujambazi

Shahidi: Nafahamu

Kibatala: Huyo ndiyo uliyempatia Freeman Mbowe Taarifa zake

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: na Umesema hujui kuwa Mbowe alikuomba Taarifa zao

Shahidi: Ndiyo sikuwa nafahamu

Kibatala: hufahamu kuwa Hizo Taarifa alizishughulikia

Shahidi: sifahamu

Kibatala: Kama nakumbuka baada ya Kumpatia Mbowe Majina na Namba nimekunukuu Mbowe alisema "Wewe niache Mimi nafahamu nitashughulika nao Vipi"

Shahidi: Ndiyo alisema hivyo

Kibatala: Na Hukusema kama Mbowe alikwambia kuwa anataka kumdhuru Sabaya wala Wenzie

Shahidi: Hakusema

Kibatala: Jana Katika Statement Yako umeeleza kuwa ulimtongoza Helga Mchomvu

Shahidi: Ndiyo ni sahihi

Kibatala: unafahamu Helga Mchomvu Aliyekuwa Mwenyekiti wa Halmashauri Ya Hai kuwa anamiaka Mingapi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Mimi Nakwambia Sasa Ana miaka 60,wewe Unamiaka Mingapi

Shahidi: Miaka 31

Kibatala: na Ulimtongoza

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Jana Katika ushahidi wako ulisema palikuwa na Diwani wa kiboriloni

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kama ulitaja Jina lake

Shahidi: Sikutaja Jina lake

Kibatala: Je unafahamu Kuwa Mwenyekiti wa Chadema jimbo la Hai alitekwa na kumizwa Vibaya

Shahidi: sifahamu

Kibatala: Kwa hiyo unafahamu kuwa Mbowe kama Mbunge alikuwa anafuatilia Taarifa za Uhalifu wa watu waliomdhuru Kiongozi wake

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Jana ulitaja Majina ya SG hotel na Gold Crest Hotel

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je unafahamu sehemu zote hizo Sabaya alikuwa hawezi Kufika kwa sababu ya madeni Makubwa ambayo alikuwa halipi

Shahidi: Sifahamu

Kibatala: Umesema pia ulilala Aishi Hotel

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Ulitaja Jina la Chumba Ulicho Lala..?

Shahidi: Hapana

Kibatala: ulitaja Aina Ya Chakula Ulicho kura pale

Shahidi: Hapana

Kibatala: Nilisikia mara zote ulikuwa unasafiri kwa kutumia public transport

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Na ni sahihi Hukutoa risiti/Ticket yoyote ya Magari uliyokuwa unasafiria

Shahidi: ni sahihi

Kibatala: ni sahihi kwamba Ulikuwa unaendelea kuwasiliana na hao Marafiki wa Sabaya Mpaka Muda Unakutana na Mbowe Mara ya Mwisho

Shahidi: Sahihi Kibatala: na hukumwambia Mheshimiwa Jaji Kuwa mlikuwa mnawasiliana kwa Mambo Mema au Mabaya

Shahidi: Sikusema

Kibatala: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji labda kama Mwenzangu atakuwa na Maswali

Wakili Michael Mwangasa ameanza kuuliza maswali

Michael Mwangasa: unatamani Mahakama Iamini kuwa Ushahidi wako ni wa kweli

Shahidi: Ndiyo natamani

Michael: Je Kuna Mahala yoyote Umesema Mbowe alishiriki Vikao Vya ugaidi

Shahidi: Hapana, Sikusema

Michael: Je kuna sehemu yoyote Umesema kuwa uliwahi kushiriki Vikao Vya Ugaidi na Mheshimiwa Mbowe

Shahidi: Sikusema

Michael: Je uliiambia Mahakama Kwamba ulishiriki Vikao Vya ugaidi

Shahidi: Nilieleza Vikao tu

Michael: Kweli kuwa ulikuwa unafanya Vikao na Mbowe na kushitakiwa, kisha Kuachiwa huru

Shahidi: Nilisema nilishitakiwa nikaachiwa huru

Michael: Ulisema ulimpatia Mbowe namba za akina Japhet, Je ulitaja hizo namba hapa Mahakamani

Shahidi: Sikutaja

Michael: Ulisema Ulimpa Taarifa Mbunge wa Longido Taarifa za Kiuhalifu?

Shahidi: Hazikuwa Taarifa za Kiuhalifu, nilimwambia kuna mtu Mkubwa amekuja Longido kunifuata sikutegemea

Michael: ni sahihi hukusema hapa Mahakamani kuwa walikupa Mrejesho gani?

Shahidi: ndiyo

Michael: nitakuwa sahihi nikisema walikupuuza?

Shahidi: Sijui

Michael: Ni hayo tu Mheshimiwa Jaji
---
Jaji: Re examination?

Wakili wa Serikali: tutaendelea na Re Examination na ataanza Abdallah Chavula kwa Ruhusa yako Mheshimiwa Jaji tungeomba tupatiwe Kielelezo E1

Principal State attorney, Akitaka aweke hayo kwenye final submission.

Wakili wa Serikali: Shahidi Umeulizwa Maswala Mengi sana kuhusiana na Karatasi ya Maelezo uliyoyatoa Polisi dhidi ya Maelezo uliyoyatoa hapa Mahakamani, Wakiwa wanataka Kuonyesha

Kibatala: OBJECTION aende Straight kwenye Re examination, anajua kuwa hairuhusiwi na ni...

Jaji: Wakili wa Serikali Unasemaje

Wakili wa Serikali: Sawa

Wakili wa Serikali: kwanini Kwenye Statement yako uliyotoa Polisi haina Maelezo uliyoyatoa Jana Mahakamani

Shahidi: Kwa sababu Jana ilikuwa naeleza kwa urefu Nilichoandika kwenye Statement yangu polisi.

Wakili wa Serikali: NitaKukabidhi sasa hii Karatasi ufafanue

Shahidi: hapa Nimeona Nimeeleza Kuhusu Kilimo, Nilikuwa nalima Viazi na Karoti. Jambo Lingine ni Mwandishi amekosea Mwaka nilioacha kazi kwa Sabaya. Ambaye Mheshimiwa alinitambulisha kuwa ni Kiongozi wa Ulinzi Kanda ya kaskazini.

Jaji: hapo sasa Mnafanya nini Wakili wa Serikali

Shahidi: anafafanua kilichopo

Jaji: afafanue Sasa

Wakili wa Serikali: Sawa

Shahidi: Swala lingine nilimtaja yule Diwani

Wakili wa Serikali: Kwenye Ushahidi wako ulitaja Diwani wa wapi ?

Shahidi: Diwani wa Kiboboroni

Mallya: OBJECTION hiyo ni fact Mpya kuhusu ni Kiongozi wa ulinzi Kanda ya kaskazini

Jaji: Mimi nilirekodi hivyo

Mallya: kama Mahakama ili Rekodi sina tatizo

Wakili wa Serikali: Kuhusiana na huyo Diwani ulisema nini?

Shahidi: Sikutaja Jina la Diwani

Wakili wa Serikali: sasa Uliambia Mahakama Huyo anaitwa nani

Kibatala: Sasa Ndiyo tunafanya nini, Shahidi ameshasema hakutaja Jina, yeye anataka Shahidi ajibu nini cha ziada.

Jaji: Ngoja tuone swali lake Maana hata Mimi nimerekodi kuwa Hakutaja Jina la Diwani

Wakili wa Serikali: Tueleze kuhusu Majina na Maeneo uliyoyatoa Jana hukutaja.? Shahidi: Sikutaja

Wakili wa Serikali: Tueleze sasa kwanini sasa Katika Maelezo yako Polisi hukutaja na Jana hukataja

Shahidi: Nilichofanya nilifanya ufafanuzi kwa kutaja hayo Majina niliyomtajia Mheshimiwa Mbowe bowe ..wakawa wananichanganya baadae nikakumbuka.

Wakili wa Serikali: Umeulizwa Kuhusu Kukutana na Bwana Mbowe Ukasema ni Mwanzoni mwa October 2020 longido na Baadae Ukasema ni October 2018 fafanunua Mkanganyiko huo

Shahidi: kwa sababu Mawakili wa Upande wa Utetezi walikuwa wananiuliza kwa njia Isiyo sahihi...

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Naomba nimkaribishe Mwenzangu

Wakili wa Serikali Robert Kidando anasimama
Wakili wa Serikali: kuna swali Uliulizwa na Wakili Kibatala Kwamba Mbowe alikuwa wapi kuanzia November 2019 Mpaka January 2020 Ukasema hufahamu hebu tuambie

Shahidi: Ninachofahamu yeye alinitafuta akiwa na Mikutano ya Jimbo

Wakili wa Serikali: Umeulizwa Kuhusu Vikao kama Vilikuwa Vya kigaidi Ukasema Hapana Sasa hoja ilikuwa ni nini

Shahidi: Hoja ilikuwa ni Kuomba Majina ya wale Vijana wanaotembea na Sabaya na Namba zao za Simu

Wakili wa Serikali: Ukaulizwa na Wakili Kibatala Kwamba, Kama ulikuwa na hofu ya kiuhalifu Ukasema Hapana hebu fafanua

Shahidi: nilipata hofu kwa sababu Yeye alikuwa Mbunge na Sabaya alikuwa Mkuu wa Wilaya, nikajiuliza kwanini asitafuti kwa Kiongozi Mwenzie

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuhusu Kule Longido baada ya Kumtafuta Sabaya ukampigia Mbunge na Hukuriport hata Polisi

Shahidi: ni Kwa sababu nilihisi wote ni Viongozi na atamwambia mwenzie nikawa nimeshafikisha ujumbe

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kwamba Neno Bwire ni Msiri na Mlinzi wa mbowe, Elezea Sasa Kule Polisi Ulimtaja kwa namna gani?

Shahidi: Nilitaja kuwa alikuwa na Mlinzi, hapa nikajakutoa ufafanuzi

Wakili wa Serikali: Hebu fafanua kuhusu Biashara yako na mount meru ilikuwa je hukuleta nyaraka za Malipo hapa Mahakamani

Shahidi: Kwa sababu nilikwepo Muda mrefu Gerezani na Nyaraka hizo ni za Muda Mrefu

Wakili wa Serikali: Uliulizwa Kama Ulileta Nyaraka za Mount Meru Ukasema hujaileta, kwa sababu Ulifanya na mtu wao hebu tufafanulie

Shahidi: ni Kwa sababu Kuna watu wanakuja kwa wakulima kwa ajili ya Kupeleka Mazao Mount meru.

Wakili wa Serikali: Uliulizwa kuhusiana kutotaja watu wa Sabaya Pale Polisi

Shahidi: niliulizwa Majina ya watu hao hapa Mahakamani, Hapo kwenye maelezo Siku ya orodhesha

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kuhusiana na Jina Power Kaaya kwamba linatokana na Matendo ya Kihalifu, tufafanulie kwanini unaitwa Power Kaaya

Shahidi: ni Jina langu Ndiyo Maana naitwa Power Kaaya hata kwenye Charge Sheet lipo, tangu kwenye ubatizo niliitwa Power

Wakili wa Serikali: Uliulizwa swali kwamba Ulipewa Laki 2 ndiyo Maana Hukutoa Taarifa polisi

Shahidi: OBJECTION, Sikuwa nimesema Kitu hicho

Jaji: Hata Mimi Siku Rekodi Jambo hilo

Wakili wa Serikali: Kuhusiana na namba hiyo kwenye Statement hukasema siyo Namba yako, kwanini sasa unasema siyo Namba yako

Shahidi: Sijui Sasa Mwandishi aliyeandika

Wakili wa Serikali: Na Ukaulizwa kuhusiana namba zako mbili za Simu na Ukaulizwa kama Ulileta Uthibitisho Mahakamani, elezea Sasa kwanini unasema namba hizo ni zako

Shahidi: kwa sababu Namba hizo ndiyo nazitumia

Wakili wa Serikali: Umeulizwa Swali Kwamba Katika Dhamana ya Mbowe kuwa aliwahi kufutiwa Dhamana, je Ni kitu gani walichokuonyesha kuwa walikuwa na Kesi na ikafutwa Dhamana

Shahidi: Hawajanionyesha Kitu chochote

Wakili wa Serikali: Umeulizwa kuhusiana uhalifu wa Sylvester Nyegu na Ole Sabaya Ukasema Ufahamu, elezea kwanini ufahamu

Shahidi: Kwa sababu wakati wanakamatwa Mimi nilikuwa Gerezani

Wakili wa Serikali: Shahidi Mwingine tuliyekuwa tumemuita hajafika, hivyo tunaomba Hairisho hadi Kesho tarehe 29 Mwezi wa 10 ilituweze kuendelea na Shahidi Mwingine

Jaji: Shahidi Tunashukuru kwa Ushahidi wako, una eza kwenda sasa

Wakili wa Serikali: Mheshimiwa Jaji huyo ndiyo Shahidi tuliyekuwa naye kwa Leo

Jaji: Shauri linahairishwa mpka Kesho saa 3 Asubuhi


 
Repoter wa tweeter anayejiita Martin ameripoti ifuatavyo kwenye moja ya tweet yake;

Hapa mahakamani kuna socket ipo nyuma kabisa, dawati wanaloketi sana waandishi na makarao, ile socket inasaidia sana wadau kuchomeka tronic kubwa na kuchaji simu zetu. Sasa juzi ilikuwepo, jana tumefika mahakamani, tunakuta imeng’olewa na nyaya zimekunjiwa kwa ndani. Roho mbaya!

Waandishi wa habari mliopo mahakamani Kuna ukweli? Mahakama inazungumziaje hii Taarifa ya kuaribiwa kwa jengo la umma lililojengwa kwa gharama za walipa Kodi?
 
Naomba niwaulize swali, hivi kwenye hili Jukwa ni nani hana uwezo wa kuwa Rais, Waziri, Mkuu wa Mkoa, RPC etc?

Mantiki ya swali langu ni kwamba wapo Watanzania maelfu wanaweza kuzihold hizi nafasi. Kwa hiyo wale ambao Mungu amewaweka ama wamejitwalia hizi nafasi wazitumie kwa wema na unyoofu wa moyo.
 
Yaani..kila nikifuatilia mashahidi wa Jamhuri nanusa Harufu ya kuivua nguo Sirikali yao..ujibuji wa maswali ni pasposhaka wa kupikwaaa. Lakini juu ya yote Anaeabika ni Governmentali...Hii kesi Ifutwee vingnevo.

Mungu anaenda kuiangusha Governmentali. Waziri wa Katiba futilia mbali..ukushirikiana na wenzako shauri hili...linatia aibu Wasomi wa nchi hii!
 
"Upande wa utetezi ameongezeka Wakili Niyikiza Seth Jacob, ametokea Bukoba mkoa wa Kagera Kuja kuongeza nguvu katika kesi ya Mbowe na wenzake."

Wapiga mayowe mitandaoni walikuwa wanasema hii kesi rahisi sana, sasa huu utitiri wa mawakili wa nini wakati kesi ni rahisi sana?
 
Yaani..kila nikifuatilia mashahidi wa Jamhuri nanusa Harufu ya kuivua nguo Sirikali yao..ujibuji wa maswali ni pasposhaka wa kupikwaaa. Lakini juu ya yote Anaeabika ni Governmentali...Hii kesi Ifutwee vingnevo..Mungu anaenda kuiangusha Governmentali. Waziri wa Katiba futilia mbali..ukushirikiana na wenzako shauri hili...linatia aibu Wasomi wa nchi hii!!
Hawawezi kuifuta kwa mana hukumu wameshaiandaa
 
Kinacho nikera mimi ni ushahidi huu kuandikwa kwenye lugha ya kizungu!

Mbona hapa ilivyo andikwa kwa kiswahili inaeleweka vizuri sana, tena kila mtanzania anaelewa vizuri tu.

Tunaziomba Mahakama zetu za Tanzania zitoe hukuma na mwendo wa ushahidi kwa Lugha yetu ya Kiswahili.
 
"Upande wa utetezi ameongezeka Wakili Niyikiza Seth Jacob, ametokea Bukoba mkoa wa Kagera Kuja kuongeza nguvu katika kesi ya Mbowe na wenzake."

Wapiga mayowe mitandaoni walikuwa wanasema hii kesi rahisi sana, sasa huu utitiri wa mawakili wa nini wakati kesi ni rahisi sana?
Kwani urahisi wa kesi unapimwa kwa kuwa na mawakili wachache? Huoni huo urahisi ndiyo maana mawakili wanaongezeka maana wanajua ni rahisi kweli ingekuwa ngumu wangeongezekaje
 
Huyu Kaaaya mpaka sasa ni Kihiyo Mwingine ndani ya nyumba ya pilato...sijui hao waliomleta wanajisikiaje kwa sasa, au labda akili zao ni kama zake pia ingawaje ni wanajiita wanasheria wasomi wa serikali...
Siku zote palipo na ukweli, uongo hujitenga. Miaka ya 90 niliwahi kuchanganya maji kwenye mafuta ya taa baada ya kutumia kimakosa hela ya kununulia hayo mafuta!

Kilichotokea baada ya hapo, ilikuwa ni kumbukumbu kwangu mpaka leo.
 
Sasa huyu shahidi mbona kila kitu ni kama fambastic, maelezo yake ya awali kwa maandishi na ushahdi wake vitu viwili tofauti, sasa mahakama ishike yapi? au yajumlishwe, na yakijumlishwa si yatakinzana... kazi kubwa hii.
 
36 Reactions
Reply
Back
Top Bottom