Mbowe ajibu tuhuma dhidi yake juu ya matumizi ya gari la KUB.

Medical Dictionary

JF-Expert Member
Mar 12, 2012
1,057
309
Kufuatia tuhuma zilizo elekewa kwake juu ya matumizi shangingi la kambi ya upinzan mbowe alikua na haya yakusema:

"Mimi nilikataa gari kwa kipindi cha miezi sita na nikawa natumia gari langu kwa shughuli zote za vikao vya bunge,lakini nataka umma uelewa kuwa kwa nafasi yangu natakiwa kulipwa posho ya madaraka sh 200000 kila mwezi,kupewa nyumba ya kuishi ikiwa samani zake.

Ila mpaka sasa sina nyumba ya serekali,wala mlinzi,wala kulipwa fedha za mawasiliano,vyote natumia fedha zangu...kama ningetaka ningedai mambo mengi ambayo natakiwa kupata lakini kulingana na hali ya uchumi wa nchi ni lazima nitumie fedha zangu ili kunusuru uchumi" alisema.

Source: Tanzania daima 22 june, 2012
 
Duh alikataa landcruiser gx standard akapewa V8 akatwaa! Vipi Zitto naye amerudi na kuchukua posho au? Kama bado Zitto anaendelea na msimamo wake basi huo ndio msimamo thabiti na siyo msimamo wa nataka sitaki.
 
Jibu bado halijaonekana hapo sababu ya kulirudia. Ni kwa sababu hajapewa nyumba na samani zake? Ni kwa sababu hjataka hela ya mawasiliano? Ni kwa sababu anatumia ulinzi binafsi?
Nafikiri hapa mwenyekiti wetu ukiri kuwa ni ajali ya kisiasa. Ulirudisha mbele ya waandishi wa habari, ilibidi ulirudie hivo hivo.
 
kama ndiyo aina ya utetezi wenyewe basi naanza kuamini bongo hatuna viongozi wenye kusimamia dhamira zao. umekataa alafu baadaye unachukua? kuweni makini sana waTZ sasa hivi tuko makini na kwa kiasi fulani tumeanza kuwaamini sasa kwa uroho huu ttaanza kuwashuku. unaulizwa kuhusu kukubali gari mpya tena ya thamani kuliko hata ile ya kwanza unajitetea kwa kukumbushia stahiki zako za awali. Sasa ndo unafidia au?
 
Duh alikataa landcruiser gx standard akapewa V8 akatwaa! Vipi Zitto naye amerudi na kuchukua posho au? Kama bado Zitto anaendelea na msimamo wake basi huo ndio msimamo thabiti na siyo msimamo wa nataka sitaki.

Mkuu ni nani dhaifu kati ya aliyelinunua na anayelitumia?
 
Kama ni lingine basi mjanja ila kama ni lile lile kachemka mana alirudisha ili lipigwe bei anunuliwe lingine
 
Gari la Mbowe litamsaidiaje mtanzania mwenye deni la lakini 450,000/- walizokula mafisadi?
 
Hapo tuhuma haijajibiwa; badala yake ameibua malalamiko yake ingawa hajaiweka kimalalamiko zaidi; suala la kutofuatilia stahiki yako ya makazi,Samani na Mlinzi hilo laweza kuwa ni tatizo pia kwa namna mbili tofauti.
Moja ana uhakika gani kama stahiki yake aloiacha inaingia kwenye kusaidia uchumi wa Taifa na hauliwi na walafi kwa maana upo ndani ya utaratibu!!
Pili kwa kutofuatilia haki yake haoni kwamba kuna haja pia ya kuja kututhibitishia kuwa hata House allowance nayo hapokei!!
 
Mh Mbowe anatakiwa atoe maelezo ya kiina ni vipi alirudia kulitumia tena? hii nataka sitaki ina aibisha CDM
 
watanzania makondoo sioni haja ya mbowe kutonufaika walau kidogo na rasilimali zetu!sio wanaccm pekee yao
 
Mwacheni aseme mwenyewe, hilo Gazeti la Tanzania Daima sio msemaji wake ila ni la kwake
Mwacheni aseme
 
Maadam kaamua kujibu. Mbowe pia atueleze kwa nini waandishi wa gazeti lake la Tanzania Daima linalosimamiwa na mkewe hawalipwi mishahara.
Na aseme kwa nini mkewe hivi karibuni aliwajibu wahariri wake kifedhuli kuwa "asiyetaka kazi bila malipo aache! "
 
afadhali aseme ili kuondoa mkanganyiko miongoni mwa kondoo!

ameondoa au ameongeza? We umeelewa nini hapo kuhusu gari? Hayo ya nyumba na posho, mlinzi sijui nini kama hadai kwa7bu za kiuchumi hapa anamwambia nani? Ameulizwa? Kwanini asielezee tu gari ambalo wapinzani wake hawaishi kumsema? Haya ndiyo yanayonifanya nichukie siasa za kibongo, unafiki unafiki sanaa!!
 
kama ndiyo aina ya utetezi wenyewe basi naanza kuamini bongo hatuna viongozi wenye kusimamia dhamira zao. umekataa alafu baadaye unachukua? kuweni makini sana waTZ sasa hivi tuko makini na kwa kiasi fulani tumeanza kuwaamini sasa kwa uroho huu ttaanza kuwashuku. unaulizwa kuhusu kukubali gari mpya tena ya thamani kuliko hata ile ya kwanza unajitetea kwa kukumbushia stahiki zako za awali. Sasa ndo unafidia au?

Mwanawane mbowe jihadhali na tu ccm tulikuchomekea li viagra nawewe ukaingia kichwa, haya timekusamehe sababu titawapeni nchi mjaribu, timelichoka li ccm hii ndo bahati yako ila usitusaliti tena.
 
Back
Top Bottom