Mbowe aalikwa kwa Obama

Mkuu wa nchi kualikiwa kuhudhuria mkutano wa chama wapi na wapi? Nijuavyo mimi sana sana anaweza kualikwa kuhutubia huo mkutano lakini sio kubaki kwenye mkutano akisikiliza hotuba za wengine.

Mialiko kama hiyo hutolewa kwa viongozi wa kati au viongozi wa vyama vya upinzani ambao hawana dola ya kuongoza.
Nitashangaa kweli kama kiongozi wa nchi yeyote ataalikwa kwenye mkutano wa CCM au CHADEMA na kukaa hapo akiwasikiliza wengine hata kwa siku moja nzima.

Hivi unajua walioalikwa ni wakina nani?
Hivi unajua ni viongozi wa nchi ngapi ambao wamealikwa ambao wako madarakani?
Acha kuandika kwa hisia fanya utafiti utajua waalikwa ni watu wa kaliba gani na sio kupotosha hapa.
 
MK,

Kama unajua walioalikwa andika hapa na ndio maana tuna JF ili kuweka data zote waziwazi.

Usitegemee rais wa nchi akae kwenye huo mkutano siku nne. Anaweza kuwepo muda mfupi, sana sana siku hiyo ya Obama kutangazwa lakini sio vinginevyo. Pia kama ameshiriki mkutano wa Democratic, what about mkutano wa Republican? Ni marais wachache sana ambao watakuwa na muda wa kuzunguka kwenye hizo conventions. Rais anayejua siasa hachagui upande maana huwezi kujua nani atakuwa rais November.

Wengine tuna miaka mingi sana kwenye kufuatilia hizo conventions kwahiyo nina uhakika na ninachosema.

Hata Odinga aliyealikwa ameamua kutokwenda. Kama unajua politics utaelewa ni kwanini. Huyo ni Mjaluo mwenzake Obama na bado kaamua kutoenda. Jiulize why?

Kwa taarifa zaidi soma hapa chini juu ya watu gani wanaalikwa kwenye hizo conventions na lengo ni nini. Hicho ndio kitu nilikuwa naongelea.

Londoner invited to Democratic convention

Mon, August 25, 2008

By CHIP MARTIN

There's a touch of London, Ont., in the house as the U.S. Democratic party gathers in Denver, Col., to formally elect Barack Obama as its presidential candidate.

Doug Ferguson, the London lawyer who is president of the Liberal Party of Canada, is an invited guest for the event in the Mile High City.

It's his first such foray and, he said, he might just pick up a few tips.

The Democrats have invited what they consider members of like-minded political parties elsewhere to join them at the historic event that opens today and runs until Thursday.

"The Democrats have this International Leaders' Forum where they invite political parties from around the world with similar political philosophies to come out," Ferguson said. "They have workshops and they will put us on the floor at times. It will be very exciting."
 
Mbona unajichanganya kwenye maelezo yako mara useme wanaoalikwa ni viongozi wa kati na upinzani,

Mara useme kuwa Rais ana ama wanaweza kuwepo muda mfupi ,sasa tukuelewe vipi?

Hata kama hupendi Mbowe aalikwe bora ukae kimya kuliko kuandika maneno yanayojichanganya kiasi hicho.
 
Mbona swali ni rahisi sana, kwanini ushindwe kujibu, ni marais gani hao walioalikwa? Mwenzangu umefanya utafiti, toa data basi.

Rudia kusoma tena nilichoandika mwanzoni hasa paragraph ya kwanza. Nitashangaa sana kama kuna rais wa nchi atakaa hapo siku nne kusikiliza hotuba za wengine. Tatizo sio muda tu lakini hata ptotocols za kisiasa, kama amehudhuria mkutano wa Democratic na akashindwa kuhudhuria mkutano wa Republic kama amealikwa pia, hapo kunaweza kuwa na issues.

Mimi kutokumpenda Mbowe inatoka wapi? Mimi simwoni Mbowe kama kiongozi bora wa chama cha siasa, hilo nimeliandika mara nyingi. Kumwona mtu hafai kwenye jambo moja na kutompenda/kumpenda ni vitu viwili tofauti.

Kwenye hili ningeandika hivyo hivyo hata kama ambaye angealikiwa angelikuwa Mrema.

Sioni deal yoyote kualikwa kwenye hizo conventions, sana sana inaweza kuwa opportunity kama mhusika anataka kujifunza. Lakini kwa viongozi kama Mbowe, atajifunza lakini kesho anarudi kule kule business as usual.
 
Mtanzania!!!
Unanisikitisha kuwa jina lako ni tamu sana lakini hoja zako ni chungu kuliko shubili.

Ni rahisi sana kujua fungu lako ni lipi hapa JF na pia kwa nchi ya Tanzania.
Kama watanzania wanafikiri kuwa Mbowe ni kamanda wa vita dhidi ya ufisadi wewe unapopambana naye kwa namna yoyote ile unaonekana kibaraka wa mafisadi.

Sithubutu kukuita kibaraka wa mafisadi bali nakutahadharisha kuwa hakuna taswira nyingine inayokuja kwako pale unapopambana na mtu ambaye watanzania wanaammini kuwa anapambana kwa ajili yao.

Hata hivyo sikunyimi na wala sitathubutu kumnyima mtu yeyote humu jukwaani kujitambulisha kuwa yeye ni mtetezi wa mafisasdi. Ninachopinga ni watu kutoa hoja wanazosingizia kuwa za kushauri kumbe nia yao ni kuhujumu vita ya ufisadi bila wao kujitambulisha moja kwa moja kuwa ni watetezi wa mafisadi.

Ni hakika kuwa uzuri wa Dunia ni kuwa shetani amejitambulisha kwa jina na kazi zake. Ninawaomba hata watetezi wa mafisadi wajitambulishe kwa majina na kazi zao. Wasijitambulishe kama wazalendo kumbe ni vijakazi wa mafisadi.

Amina
 
Kamende,

Hapo umenena na kwa kuongezea tupo wengine ambao kipaumbele chetu ni ustawi na maendelao ya Tanzania, period. CCM imeidumaza NCHI YANGU na sisiti kulitamka hili. Tumaini langu ni mabadiliko katika uongozi wa Tanzania kwa sababu tulipofikia lazima tugeuze mwelekeo la sivyo tutazama.

Sitajali kama ni Chadema, NCCR, CUF ama chama gani kinashika hatamu mradi kiwe na uwezo wa kuwawajibisha MAFISADI na si kuwakumbatia. Asiyekubaliana na hili ingefaa akajitangaza bayana tujue tunapambana na nani na si vinginevyo. Either you are with us or against us - na kwenye hili hakuna droo.
 
Onyango nae vipi, kaalikwa? Ingekuwa vyema wakimpiga soap soap na yeye ili ahudhurie nomination ya bro....kwikwikwiiiiiii
 
Nyani Ngabu,

..who is Onyango? umeniacha kwenye mataa.

..Balozi wa Tanzania USA, kwa wadhifa wake, huwa anapata mialiko kuhudhuria national convetions za Democrats, pamoja na Republican.
 
Mtanzania!!!
Unanisikitisha kuwa jina lako ni tamu sana lakini hoja zako ni chungu kuliko shubili.

Ni rahisi sana kujua fungu lako ni lipi hapa JF na pia kwa nchi ya Tanzania.
Kama watanzania wanafikiri kuwa Mbowe ni kamanda wa vita dhidi ya ufisadi wewe unapopambana naye kwa namna yoyote ile unaonekana kibaraka wa mafisadi.

Sithubutu kukuita kibaraka wa mafisadi bali nakutahadharisha kuwa hakuna taswira nyingine inayokuja kwako pale unapopambana na mtu ambaye watanzania wanaammini kuwa anapambana kwa ajili yao.

Hata hivyo sikunyimi na wala sitathubutu kumnyima mtu yeyote humu jukwaani kujitambulisha kuwa yeye ni mtetezi wa mafisasdi. Ninachopinga ni watu kutoa hoja wanazosingizia kuwa za kushauri kumbe nia yao ni kuhujumu vita ya ufisadi bila wao kujitambulisha moja kwa moja kuwa ni watetezi wa mafisadi.

Ni hakika kuwa uzuri wa Dunia ni kuwa shetani amejitambulisha kwa jina na kazi zake. Ninawaomba hata watetezi wa mafisadi wajitambulishe kwa majina na kazi zao. Wasijitambulishe kama wazalendo kumbe ni vijakazi wa mafisadi.

Amina

Kamende,
Leo hii nimekuwa kibaraka cha mafisadi sio? Bahati nzuri mimi siumizwi na vijembe vya namna hiyo na wala hata ufanye nini sina mpango wa kuingia kwenye personal vandetta.

Hivi unaelewa hata maana ya kibaraka? Toa hata proof moja kuonyesha mimi ni kibaraka wa nani?

Ni Watanzania gani hao walio wengi ambao wanaamini Mbowe anapambana kwa ajili yao? Tafadhali toa proof, huwezi kuja na general statement kama hiyo bila hata proof ndogo. Rudia matokeo ya 2005, ni Watanzania wangapi walimpa kura?

Siamini Mbowe ana jipya maana hata mbinu anazotumia kwenye chama hazina tofauti na mbinu za hao CCM. Wala sina haja ya kujificha na nimesema hilo mara kibao. Niko independent na sibabaishwi na mtu yeyote.

Kama wewe unaona anakufaa sawa na toa hoja zako kwanini anakufaa, ila kuanza kuita watu vibaraka huku huna ushahidi wowote ni kuendeleleza zile zile hoja za mabavu ambazo watanzania wengi ni mabingwa. Mnafikiri mtatumia matusi kuwashawishi watu wengine wakubaliane na misimamo yenu? Utakuwa very naive na dunia hii ukiamini vijembe vvina maana yoyote.

Hapa unaweza kuandika chochote na kuita watu chochote unachotaka na wala hutanikosesha usingizi. Hizo ndizo mbinu wanazotumia akina Mugabe kuita kila wenye mawazo na wao vibaraka na bado wamepigwa chini, I hope hutaki kufanana na akina Mugabe.
 
Nyani Ngabu,

..who is Onyango? umeniacha kwenye mataa.

..Balozi wa Tanzania USA, kwa wadhifa wake, huwa anapata mialiko kuhudhuria national convetions za Democrats, pamoja na Republican.

Onyango ni miongoni mwa waigizaji maarufu waliowahi kuwepo Tanzania, kumbuka michezo ya Radio Tanzania wakati ule ikiitwa RTD akishirikiana na wakina mzee Jongo,Pwagu na Pwaguzi n.k.
 
Nyani Ngabu,

..who is Onyango? umeniacha kwenye mataa.

..Balozi wa Tanzania USA, kwa wadhifa wake, huwa anapata mialiko kuhudhuria national convetions za Democrats, pamoja na Republican.

Onyango ni nusu-kaka wa Obama anayeishi kwenye kibanda Nairobi. Jina lake kamili ni George Hussein Onyango Obama. Anaishi kwa chini ya dola moja kwa mwezi. Mzee dizaini umekuwa hufuatilii kabisa kampeni zinazoendelea.
 
Kamende,

Hapo umenena na kwa kuongezea tupo wengine ambao kipaumbele chetu ni ustawi na maendelao ya Tanzania, period. CCM imeidumaza NCHI YANGU na sisiti kulitamka hili. Tumaini langu ni mabadiliko katika uongozi wa Tanzania kwa sababu tulipofikia lazima tugeuze mwelekeo la sivyo tutazama.

Sitajali kama ni Chadema, NCCR, CUF ama chama gani kinashika hatamu mradi kiwe na uwezo wa kuwawajibisha MAFISADI na si kuwakumbatia. Asiyekubaliana na hili ingefaa akajitangaza bayana tujue tunapambana na nani na si vinginevyo. Either you are with us or against us - na kwenye hili hakuna droo.

Kama akina Kichaka ndio watu hata wa kuona umuhimu wa kutumia quotes zao, kazi ipo kweli kweli.

Watu wengine hatuamini dunia ni black and white (2-dimensional) tunaamini ni three-dimensional.

Unakaribishwa kwenye dunia ya watu wanaofikiri, wenye mawazo yao huru na ambao hawana nia wala sababu ya kuvutwa kwenye kambi za ama sisi ama wao. Ukitaka kuendelea na mawazo ya akina Kichaka, well, hukatazwi ila tu tuambie kama ni mwanasiasa ili tupime matokeo yake 2010.
 
Kamende,
Leo hii nimekuwa kibaraka cha mafisadi sio? Bahati nzuri mimi siumizwi na vijembe vya namna hiyo na wala hata ufanye nini sina mpango wa kuingia kwenye personal vandetta.

Hivi unaelewa hata maana ya kibaraka? Toa hata proof moja kuonyesha mimi ni kibaraka wa nani?

Ni Watanzania gani hao walio wengi ambao wanaamini Mbowe anapambana kwa ajili yao? Tafadhali toa proof, huwezi kuja na general statement kama hiyo bila hata proof ndogo. Rudia matokeo ya 2005, ni Watanzania wangapi walimpa kura?

Siamini Mbowe ana jipya maana hata mbinu anazotumia kwenye chama hazina tofauti na mbinu za hao CCM. Wala sina haja ya kujificha na nimesema hilo mara kibao. Niko independent na sibabaishwi na mtu yeyote.

Kama wewe unaona anakufaa sawa na toa hoja zako kwanini anakufaa, ila kuanza kuita watu vibaraka huku huna ushahidi wowote ni kuendeleleza zile zile hoja za mabavu ambazo watanzania wengi ni mabingwa. Mnafikiri mtatumia matusi kuwashawishi watu wengine wakubaliane na misimamo yenu? Utakuwa very naive na dunia hii ukiamini vijembe vvina maana yoyote.

Hapa unaweza kuandika chochote na kuita watu chochote unachotaka na wala hutanikosesha usingizi. Hizo ndizo mbinu wanazotumia akina Mugabe kuita kila wenye mawazo na wao vibaraka na bado wamepigwa chini, I hope hutaki kufanana na akina Mugabe.

Mtanzania heshima mbele!

Umeongea kitu cha maana na kikubwa sana kinachosumbua watu wengi hapa JF. Nimekuwa sichangii mara nyingi kwa sababu hii, japo hakuna siku inapita bila mimi kupita hapa jamvini. Tatizo ninalozungumzia ni hili la watu kutokubali mtu kuhoji au ku-challenge baadhi ya "wateule" au vyama hapa JF kwa sababu tu ya hisia zao! Ukihoji tu utaambiwa tunajua uko upande gani, au wewe fisadi na maneno kama hayo. Kimsingi sijawahi kuwa mwanachama wa chama chcochote huko nyumbani, na wala sitarajii kuwa, lakini ninaamini kuwa kukosoana na kukubali weakness ndio msingi wa kwenda mbele. Sidhani kama hao viongozi wa vyama vya siasa ni malaika amabao hawana mapungufu, sasa kama mapungufu yapo na yanasemwa kwanini tuchukie badala ya kuyafanyia kazi?! This is the main problem we're facing in Tanzanian politics, kuanzia walioko madarakani, CCM mpaka wapinzani....Take it from my heart, I REALLY HATE CCM BUT SOMETIMES YOU WONDER IF THE OPPOSITION ARE ANY BETTER!
 
Nyani Ngabu said:
Onyango ni nusu-kaka wa Obama anayeishi kwenye kibanda Nairobi. Jina lake kamili ni George Hussein Onyango Obama. Anaishi kwa chini ya dola moja kwa mwezi. Mzee dizaini umekuwa hufuatilii kabisa kampeni zinazoendelea.

Nyani Ngabu,

..man ur crazy.

..naona tunaonyeshwa yule dada yake wanaye-share mama.

..wamtumbukize basi ONYANGO kwenye YOUTUBE tumuone anavyoishi wakati Obama akipeta kwenye private jets.

..i would love to see how Chris Mathews,Keith Olberman, Rachel Madden[i hate that lady], will react to that.

NB:

..campaign zimekuwa so boring.

..nimemsikia James Clayburn akisema kuwa Bill Clinton is not a racist!!

..Clayburn ndiyo alimbebea bango Bill na kusema uhusiano wake na Blacks umeingia nyongo.
 
Mzee naona kweli umeboreka na kampeni maana inaelekea hata hukumwona Onyango alivyohojiwa na CNN. Nina hakika ukim-youtube utampata tu. Au m-google....lakini ni vizuri kumwona kwenye video footage. Halafu wanafanana kiaina.....

Cheki hii: http://www.youtube.com/watch?v=Qvo2aBQi6l0
 
Mzee naona kweli umeboreka na kampeni maana inaelekea hata hukumwona Onyango alivyohojiwa na CNN. Nina hakika ukim-youtube utampata tu. Au m-google....lakini ni vizuri kumwona kwenye video footage. Halafu wanafanana kiaina.....

Cheki hii: [media]http://www.youtube.com/watch?v=Qvo2aBQi6l0[/media]

Nyani,

Ndio maana na hate politicians, yaani kweli Baraka ameshindwa hata kutoa pesa za kitabu chake kuwasaidia hao ndugu zake? Shame on him!

Sitaki tena hata kusikia hizo changes zake, social mobility inaanzia nyumbani, kwenye familia yako. Utaisaidia USA wakati umeshindwa kumsaidia ndugu yako?

Imenikumbusha ile kitabu Song of Lowino and Ocol. Unasema uta make peace na dunia huku umeshindwa ku make peace na your own brother?

Hili ni kosa kubwa sana, alifikiri Republicans watashindwa kumpata huyu ndugu yake?

Labda hii habari iwe sio kweli, vinginevyo hii ni balaa kabisa kwa Obama.
 
Unaongea usichokijua. Obama unafahamu life story yake? Hivi ndugu zake Kenya waliwahi kumtafuta alipokuwa lawyer na community organizers? Walikuwa wapi wakati mamake Barack alikuwa on foodstamps because she couldn't afford food for her child???? Kila mtu ataubeba mzigo wake mwenyewe!
Babake alikuwa na wake 4 tofauti na hakumlea wala kumtafuta Barack. Barack alifanya jitihada kumtafuta babake na ndugu zake baadaye ukubwani. Amemsaidia bibi yake na dada na kaka yake ambao wako close naye lakini ana ndugu kibao wengine hana hata uhusiano nayo.
Kama unataka kumsema Obama kuhusu ndugu zake, basi tuangalie Cindy McCain ambaye amerithi ma-bilioni na half sister wake ni maskini na baba yao alimwachia 10,000 USD tu huyu mtoto, urithi wote kampa Cindy! Na zaidi ya Cindy au baba yao kutompa hata senti 5 huyu mama, pia Cindy amemkana na anadai ni mtoto wa pekee wa baba yao!!
Mtanzania: Usidandie kwenye gari moshi la Nyani maana 'my dear friend' ana ajenda yake ya kumwuza babu Makopo ambaye ni senile and major flipflopper.
 
Susuviri,

Tunaupiga vita Ujamaa na Azimio la Arusha na kufurahia ubepari, lakini tunanung'unika kwa mkao wa Kijamaa na Azimio la Arusha!
 
moderator hii ni nukuu ya mwaka kwani humu ndani kama anavyothibitisha Rev. kishoka kuna watu wanafikra chotara. hawajulikani kama wanachukia nini wala wanapenda nini hao watu ni hatari sana na kwa jina maarufu zama zile za mwaka "47" tunawaita ndumilakuwili.
 
Susuviri,

Tunaupiga vita Ujamaa na Azimio la Arusha na kufurahia ubepari, lakini tunanung'unika kwa mkao wa Kijamaa na Azimio la Arusha!

I'm pro-life therefore I care about the well-being of all people. I'm a compassionate conservative.
 
Back
Top Bottom