Mpaka Kieleweke
JF-Expert Member
- Feb 27, 2007
- 4,132
- 1,571
Mkuu wa nchi kualikiwa kuhudhuria mkutano wa chama wapi na wapi? Nijuavyo mimi sana sana anaweza kualikwa kuhutubia huo mkutano lakini sio kubaki kwenye mkutano akisikiliza hotuba za wengine.
Mialiko kama hiyo hutolewa kwa viongozi wa kati au viongozi wa vyama vya upinzani ambao hawana dola ya kuongoza.
Nitashangaa kweli kama kiongozi wa nchi yeyote ataalikwa kwenye mkutano wa CCM au CHADEMA na kukaa hapo akiwasikiliza wengine hata kwa siku moja nzima.
Hivi unajua walioalikwa ni wakina nani?
Hivi unajua ni viongozi wa nchi ngapi ambao wamealikwa ambao wako madarakani?
Acha kuandika kwa hisia fanya utafiti utajua waalikwa ni watu wa kaliba gani na sio kupotosha hapa.