Mbowe aalikwa kwa Obama

Fidel80

JF-Expert Member
May 3, 2008
21,942
4,410
MWENYEKITI wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Freeman Mbowe, amealikwa kuhudhuria mkutano mkuu wa Chama cha Democratic, ambao utampitisha rasmi mgombea urais wa chama hicho, Seneta Barack Obama.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa na CHADEMA jana na kusainiwa na Kaimu Katibu Mkuu na Mkurugenzi wa Mahusiano ya Kimataifa wa chama hicho, John Mnyika, ilieleza kuwa akiwa nchini Marekani, Mbowe atahudhuria mkutano huo unaofanyika katika Jiji la Denver, Colorado, ambao utamuidhinisha Obama, ikiwa ni pamoja na kutangaza jina la mtu atakayekuwa mgombea mwenza wake.

“CHADEMA inapenda kuutaarifu umma wa Watanzania kwamba Mwenyekiti wetu ameondoka kwa ziara ya siku nne kwenda nchini Marekani, kuhudhuria Mkutano Mkuu wa Chama cha Democratic, ambao utamwidhinisha kuwa mgombea urais wake, Barack Obama, pamoja na mgombea mwenza,” ilieleza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ya Mnyika imesema kwamba, Mbowe amealikwa kuhudhuria mkutano huo muhimu na taasisi ya National Democratic Institute (NDI), yenye dhamana ya kuandaa mkutano huo.

Miongoni mwa viongozi mashuhuri wa Kiafrika walioalikwa katika mkutano huo ni Waziri Mkuu wa Kenya, Raila Odinga, ambaye naye kwa mujibu wa taarifa za vyombo vya habari vya Kenya, amekubali mwaliko huo.

Akiwa huko, Mbowe atapata fursa ya kuhudhuria jukwaa la kimataifa la viongozi (Leadership Forum), ambalo huwakutanisha viongozi waandamizi mbalimbali duniani.

“Katika jukwaa hilo, kunakuwa na watu kama mabalozi, wanaharakati na wanasiasa waandamizi kutoka takriban mataifa 100 duniani,” iliongeza taarifa hiyo.

Taarifa hiyo ilieleza baada ya ziara hiyo ambayo itakamilika Agosti 28 mwaka huu, Mbowe atarejea nchini, na baada ya kurudi atazungumza na waandishi wa habari kuhusu masuala mbalimbali ya mwelekeo wa taifa na chama chake.

Kwa mujibu wa taarifa hiyo, katika mkutano wake na waandishi wa habari, baadhi ya mambo anayotarajia kuyazungumzia ni pamoja na kutathmini kuhusu utendaji wa kazi wa serikali ya Rais Jakaya Kikwete, hasa katika maeneo ya mwenendo wa uchumi, siasa na mwelekeo wa mapambano ya vita dhidi ya ufisadi.

Pia atazungumzia kwa kina mambo ya chama chake katika kusimamia mwenendo wa serikali sambamba na kubainisha kile kilichoelezwa kuwa ni mkakati unaoendeshwa na wapinzani wa vita dhidi ya ufisadi nchini, unaowahusisha viongozi waandamizi serikalini, Chama Cha Mapinduzi (CCM) na baadhi ya viongozi wa vyama vya upinzani.

Aidha, taarifa hiyo ilisema mkakati huo kwa muda mrefu sasa umekuwa unalenga kuichafua na kuidhoofisha CHADEMA, ili kuzorotesha mapambano dhidi ya ufisadi na utetezi wa rasimali za taifa.

source;Tanzania daima
 
Ole wako msishitaki kama mlivyoahidi, sitakuwa na imani na nyie.

Thank you
 
No wonder wanafanya kila wawezalo kumzamisha huyu bwana !

Nilikwisha sema kuwa hawa Mafisadi watafanya kila wanaloweza kuizamisha Demokrasia hii changa inayoanza kuchipua hapa Tanzania, nilisema kama Mbowe atakuwa na utashi wa kisiasa atumia sana busara kuliko akili ya darasani.

Niliposema ktk thread yangu kuwa vyama vyenza vimemsaliti, watu wakaniuliza maswali mengi, ila siku si nyingi mtayashuhudia mengi, nilisema CCM sasa haina pa kushika na hivyo kwa kuwa CHADEMA ndicho chama chenye mwelekeo na sura ya kitaifa CCM watafanya kila wanaloweza ili kumchafua Mbowe, watu wakaja juu wakasema nimejuaje,

Kwa sasa nazidi kumuhasa M/kiti ajiweke pembeni ili awatie Ndimu hawa CCM, wazidi kuchanganyikiwa na pia wakose mshiko wa kueemea , watu hamunielewi mnazidi kuendekeza upenzi bila kuzingatia hoja.

Cha kusikitisha ni kuwa hatuna mikakati ya mapema 2010, tunazidi kulalama bila kujiandaa, hii ni hatari kabisa.
 
Hata kualikwa kuhudhuria mkutano tayari ni jambo la maana?

Tunamlaumu JK kwa kuwa Vasco Da Gama, huku Mbowe akialikwa tunaona ni ujiko?

Kiongozi wa TZ atakuwa judged kwa mafanikio yake Tanzania na sio vinginevyo. Tumeona akina prof. Lipumba wakipewa kila nafasi lakini bado wanashindwa hata kuwafikia wananchi wao huko kwenye wilaya za Tanzania.

Tumeona akina JK wakialikwa mpaka kwenye viwanja vya mpira na kuona kila maendeleo ya wenzetu lakini wanashindwa kusukuma gurudumu letu la maendeleo hata kwa hatua kumi.

Kualikwa mikutano ya vyama vya siasa duniani sio issue kubwa kabisa, inabidi muelewe hivyo.
 
Cha kusikitisha ni kuwa hatuna mikakati ya mapema 2010, tunazidi kulalama bila kujiandaa, hii ni hatari kabisa.

Niliwahi kushauri siku nyingi pia kwamba tutumie muda wetu mwingi kuweka mikakati nikianza na ushauri wa kufuatilia na kuhakikisha ccm hawapati hela za kampeni mwaka huu maana wenzetu huko vijijini wataendelea kudanganywa wawapigie ccm maana hawajui kinachoendelea. Hilo litawezekana tu kama watakuwa na pesa ya kampeni, naunga mkono hoja. Tujipange kwa ajili ya 2010 wana-JF.
 
Nenda salama, urudi salama, tunasubiri kuja kusikia utakayosema utakaporudi. Please, usirudie kama hotuba ya Kikwete, ndeeefu isiyo na yale wananchi waliyoyatarajia
 
Nilikwisha sema kuwa hawa Mafisadi watafanya kila wanaloweza kuizamisha Demokrasia hii changa inayoanza kuchipua hapa Tanzania, nilisema kama Mbowe atakuwa na utashi wa kisiasa atumia sana busara kuliko akili ya darasani.

Niliposema ktk thread yangu kuwa vyama vyenza vimemsaliti, watu wakaniuliza maswali mengi, ila siku si nyingi mtayashuhudia mengi, nilisema CCM sasa haina pa kushika na hivyo kwa kuwa CHADEMA ndicho chama chenye mwelekeo na sura ya kitaifa CCM watafanya kila wanaloweza ili kumchafua Mbowe, watu wakaja juu wakasema nimejuaje,

Kwa sasa nazidi kumuhasa M/kiti ajiweke pembeni ili awatie Ndimu hawa CCM, wazidi kuchanganyikiwa na pia wakose mshiko wa kueemea , watu hamunielewi mnazidi kuendekeza upenzi bila kuzingatia hoja.

Cha kusikitisha ni kuwa hatuna mikakati ya mapema 2010, tunazidi kulalama bila kujiandaa, hii ni hatari kabisa.Umeongea kwa uchache ila somo ni kali .Kwa walio wengi watahitaji muda sana kukuelewa .Nasema asante sana Mwita .

Mkuu wangu Mtanzania , nimeona maneno yako .Hapa si neno la ujiko na uvasco dagama.JK na watanzania kuelewa usemalo si leo na wao wanadhani akiwa na Bush nk ni fahari kama kawaida .Na hata kuomba omba kwa CCM na Rais ni utawala bora na kukubalika .

Soma tena habari ya Mbowe na Ziara then linganisha na JK kutamba kuwa bingwa wa kuomba omba akisema wanatekeleza ilani kwa kuwaacha mafisadi wa EPA .
 
Hata kualikwa kuhudhuria mkutano tayari ni jambo la maana?

Tunamlaumu JK kwa kuwa Vasco Da Gama, huku Mbowe akialikwa tunaona ni ujiko?

Kiongozi wa TZ atakuwa judged kwa mafanikio yake Tanzania na sio vinginevyo. Tumeona akina prof. Lipumba wakipewa kila nafasi lakini bado wanashindwa hata kuwafikia wananchi wao huko kwenye wilaya za Tanzania.

Tumeona akina JK wakialikwa mpaka kwenye viwanja vya mpira na kuona kila maendeleo ya wenzetu lakini wanashindwa kusukuma gurudumu letu la maendeleo hata kwa hatua kumi.

Kualikwa mikutano ya vyama vya siasa duniani sio issue kubwa kabisa, inabidi muelewe hivyo.

kama nimekusoma vizuri post yako ina mambo makuu mawili kama siyo matatu

(a) kualikwa huku kwa mbowe kuna fanana na ziara za kila mara anazozifanya Rais kikwete nje ya nchi.

(b)Ziara za viongozi wa kisiasa nje ya nchi kama hazileti mabadiliko nchini hazina maana

(c) kualikwa kwenye mikutano ya vyama vya siasa siyo dili

Tafakari yangu

(a) Mbowe hatumii fedha za walipa kodi kwenda kwenye huo mkutano alioalikwa, na wala yeye hajazuka tuu kuamua kwenda huko kwa sababu anatamani kumuona Obama akithibitishwa kuwa mgombea urais wa Chama chake. Bali chama chake ndiyo kimealikwa na kwa nasibu, yeye kwa sasa ndiye mwenyekiti wake.

kama hujui mara nyingi kikwete husomba "washikaji' wake wengi tuu kwenda nao Ughaibuni "kutalii" kwa pesa za walipa kodi wa Tanzania

(b) Ziara za wanasiasa wasio na mamlaka ya kidola huwezi kuzifananisha na zile za wale wenye mamlaka ya kidola. Na manufaa ya kimadaraka ya kina Lipumba huwezi kuyaona wewe au mimi kama hatumo kwenye mzingo wa taaluma anayoshughulika nayo (Professional circle)

(c) mikutano ya vyama vya kisiasa inatofautiana kutokana na dhima ya chama chenyewe kwenye jamii na dunia kwa ujumla. Huwezi kusema kualikwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha kikomunisti cha China, kunafanana na kualikwa kwenye mkutano mkuu wa CCM!!
 
kuna watu hapa jf hawajachefuliwa bado na sppeech ya mkwere kikwete. wengine tuna kichefu chefu hadi leo
 
Hivi JK hajaalikwa?

Mkuu wa nchi kualikiwa kuhudhuria mkutano wa chama wapi na wapi? Nijuavyo mimi sana sana anaweza kualikwa kuhutubia huo mkutano lakini sio kubaki kwenye mkutano akisikiliza hotuba za wengine.

Mialiko kama hiyo hutolewa kwa viongozi wa kati au viongozi wa vyama vya upinzani ambao hawana dola ya kuongoza.

Nitashangaa kweli kama kiongozi wa nchi yeyote ataalikwa kwenye mkutano wa CCM au CHADEMA na kukaa hapo akiwasikiliza wengine hata kwa siku moja nzima.
 
kama nimekusoma vizuri post yako ina mambo makuu mawili kama siyo matatu

(a) kualikwa huku kwa mbowe kuna fanana na ziara za kila mara anazozifanya Rais kikwete nje ya nchi.

(b)Ziara za viongozi wa kisiasa nje ya nchi kama hazileti mabadiliko nchini hazina maana

(c) kualikwa kwenye mikutano ya vyama vya siasa siyo dili

Tafakari yangu

(a) Mbowe hatumii fedha za walipa kodi kwenda kwenye huo mkutano alioalikwa, na wala yeye hajazuka tuu kuamua kwenda huko kwa sababu anatamani kumuona Obama akithibitishwa kuwa mgombea urais wa Chama chake. Bali chama chake ndiyo kimealikwa na kwa nasibu, yeye kwa sasa ndiye mwenyekiti wake.

kama hujui mara nyingi kikwete husomba "washikaji' wake wengi tuu kwenda nao Ughaibuni "kutalii" kwa pesa za walipa kodi wa Tanzania

(b) Ziara za wanasiasa wasio na mamlaka ya kidola huwezi kuzifananisha na zile za wale wenye mamlaka ya kidola. Na manufaa ya kimadaraka ya kina Lipumba huwezi kuyaona wewe au mimi kama hatumo kwenye mzingo wa taaluma anayoshughulika nayo (Professional circle)

(c) mikutano ya vyama vya kisiasa inatofautiana kutokana na dhima ya chama chenyewe kwenye jamii na dunia kwa ujumla. Huwezi kusema kualikwa kwenye mkutano mkuu wa chama cha kikomunisti cha China, kunafanana na kualikwa kwenye mkutano mkuu wa CCM!!

Kigarama,

Wacha nitoe comments zangu kuhusu maandishi yako hapo juu:

a)Si unajua hata muda ni pesa? Bahati mbaya muda ni kidogo kuliko mambo ya kutendwa hapa duniani. Ndio maana mwingine anaamua kwenda kwa Obama wakati angelikuwa mwingine angeenda Tarime kukuza chama. Hapo labda ni kuangalia opportunity cost. Hata JK atasema si wakati wote anatumia pesa za Watanzania. Lakini bado anatumia muda ambao angeweza kuutumia kusukuma maendeleo ya Watanzania kama rais.

b)Ninachosema mimi ziara kama hizo kama hazisaidii kuleta mabadiliko ndani ya vyama vyao, ni useless. Mfano Mbowe akienda USA akaona jinsi mama Clinton na Obama wanavyosifiana na kuwa pamoja katika kujenga demokrasia ndani ya chama chao baada ya kushambuliana hasa wakati wa kampeni, halafu yeye anarudi TZ na kuanza kufukuzana na viongozi wenzake wenye mawazo tofauti na yeye, ziara kama hiyo ni useless. Ziara ambayo haiongozani na kujifunza ni kupoteza muda. Ndio maana wengine tunamlaumu JK kwa ziara ambazo haziongezi tija kwa nchi.

c)Kwa taarifa yako kama huna habari ni rahisi kualikwa kwenye mkutano wa Obama au chama cha kikomunisti cha China kuliko kualikwa kwenye mkutano wa Mugabe au CCM. Kuna institutions nyingi ambazo zinakuwa stakeholders kwenye mikutano mikubwa kama ya akina Obama na hao ndio wanajaribu kutumia hizo nafasi kwa mfano kukuza demokrasia duniani kwa kutoa nafasi kwa viongozi mbalimbali toka nchi mbalimbali. Ni tofauti kwenye mikutano kama ya CCM.

Sipingi Mbowe kwenda kwenye hiyo mikutano, naamini kwenda kwake anaweza kujifunza. Ila mimi sioni kama ni deal, naona kama ni opportunity ambayo lazima itumike vizuri kwa lengo la kujifunza na kisha kusaidia kukuza demokrasia ndani ya CHADEMA na nchi kwa ujumla.
 
Niliwahi kushauri siku nyingi pia kwamba tutumie muda wetu mwingi kuweka mikakati nikianza na ushauri wa kufuatilia na kuhakikisha ccm hawapati hela za kampeni mwaka huu maana wenzetu huko vijijini wataendelea kudanganywa wawapigie ccm maana hawajui kinachoendelea. Hilo litawezekana tu kama watakuwa na pesa ya kampeni, naunga mkono hoja. Tujipange kwa ajili ya 2010 wana-JF.

Umeanza vizuri lakini umejisahau kwa kuandika ...Tujipange kwa ajili ya 2010 wana-JF... (ungemaliza kwa kuandika hivi) ...Tujipange kwa ajili ya 2010 wana-CHADEMA. JF haiko hapa kama chama cha siasa.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom