#COVID19 Mbona Serikali imetugawa katika chanjo ya COVID-19?

Leo katika hotuba ya MH Rais amesikika akisema wameshakubalia taasisi mbalimbali kuagiza chanjo za aina wanayoitaka wao, taasisi mojawapo ni ya Mzee Azim Dewji.

Najiuliza mbona suala kama hili la chanjo Serikali inashindwa kuwa na kauli moja ya aina ya chanjo itakayowafaa Watanzania ukizingatia tumeambiwa Chanjo tunanunua kwa fedha zetu za kodi? Mbona Serikali imetuchagulia chanjo ya John & Jonson pekee? Je, Serikali ina maslahi katika hiyo kampuni ya Chanjo?

OMBI
Tunaomba Serikali iwape Watanzania uwanja mpana wa kuchagua aina ya chanjo wanayoitaka maana chanjo zipo za aina nyingi kama Pfizer, AstraZenecca n.k


Tanzania imeshatoa list ya chanjo zinazokubalika hii ni moja tu kati ya chanjo. Hivyo wanaweza kutumia chanjo yeyote iliyo kubalika
 
Hawa akina Dewji wakinunua hizo chanjo watazitoa bure? I doubt it. Na kwanini watu binafsi waruhusiwe kununua hizo chanjo badala ya Serikali kuzinunua!? Sijasikia nchi yoyote ile ya Africa kuruhusu watu binafsi kununua chanjo badala ya Serikali.
mambo ya ajabu kweli nchi hii. Serikali wao wameamua kununua chanjo zenye unafuu wa gharama bila kuangalia ubora, iweje kila mtu aagize chanjo kivyake? ina maana hawana imani na chanjo iliyochaguliwa na Serikali?
 
Hili la chanjo ni sawa na la muuza karanga ukikubali tu offer ya kuonja za bure habanduki mpaka umnunuze.. Tulivyopewa zawadi ile za zile chanjo milion moja nilijua tu kifuatacho ITV... NI HIKI.!
walituambia chanjo ni bure kumbe serikali inazinunua tena kwa gharama kubwa? au walìmaanisha wananchi hatutouziwa mahospitalini?
 
Tanzania imeshatoa list ya chanjo zinazokubalika hii ni moja tu kati ya chanjo. Hivyo wanaweza kutumia chanjo yeyote iliyo kubalika
sasa iweje kila taasisi ina agiza chanjo kivyakevyake?
 
Usikubali mtu yeyote akugawe, kama unataka chanjo tayari ipo nenda kachanjwe tu.
 
Pia Serikali ihakikishe kila anayepata chanjo ajue kapewa chanjo ipi.

Mbele ya safari kuna mambo ya "booster" ambapo kila chanjo itakuwa inayo busta yake.
 
WaTanzania nikama tumelaniwa badala ya kuwaza postive tunashikilia trivial issues, wenzetu wanapambana na covid sasa wako huru kiasi, sisi tunajidili aina ya chanjo, cmna wana sayansi muhimbili tegenezeni ya kwanu.

Watu kama Gwajima wanao tumia udhaifu ya watu kuwa potosha zaid ni hatari kabisa ni kwasabb ni CCM ni basi tu.
huwezi kuwa positive kwa kitu ambacho sio salama kwa afya yako.

UHAI haununuliwi dukani.
 
Wenye dunia yao wakikutaka hutoki vitu vingi kutoka kwao tunatumia hivyo wakidhamiria kufanya ubaya watafanya kwa njia yoyote.
Wewe unajuaje kama hawafanyi huo ubaya ambao unaathiri kidogo kidogo?
 
Azim Dewji!🤔🤔,nimewahi kumsikia wapi vile!..Yes juzi kwA Gwajima

Kumbe jamaa alikua ashaweka mradi sawa sawa😂😂
MJINU HAPA WATU WALISHACHANGAMKIA FURSA YA KUINGIZA CHANJO NDO MAANA JUZI JUZI HAPA ALIONGEA JAMBO. BUSINESS ...
 
Sijui kama ni kukuaminisha au kukuogopesha lakini ninachokuambia kama unafikiri hizo chanjo zimekuja kwa lengo la kudhuru watu unaweza kuacha kuchoma lakini iwapo hao jamaa kama ni kweli wana lengo la kudhuru watu basi hutoweza kukwepa mitego yao maana vingi tunavyotumia vinatoka huko na wanaweza kufanikisha lengo lao kwa njia yoyote.
Huyo anakataa chanjo kwa kisingizio cha kuogopa hujuma za wazungu utakuta amevaa nguo, anapanda magari na ndege, anaongea na simu ya mkononi, amechanjwa chanjo lukuki tangu utotoni na bado anachanja watoto wake chanjo lukuki, anakunywa vidonge na kuchomwa sindano akiugua, anaangalia TV na zote hizi ni za haohao wazungu.
 
Hii JF mbna nikama inaingiliwa kinyume na taratibu? Yaan wale wauza sura wa fb&insta wamehamia uku na kuanza nao kuchangia hoja kwa points mbovu,uhandishi mbovu, na mbwembwe zao za uko waliko toka, ushauri kwa hao moderator wawe wanakaguwa watu wa aina hii watolewe maana wanaharibu ile dhana ya kuita jf the site of great thinkers, sasa imekuwa ni site ya uchafu
 
Kamsikilize tena Rais! Kabla ya Tanzania kukubali ujio wa chanjo, jumuiya na watu binafsi wamekuwa wakiomba utaratibu waruhusiwe ku-process chanjo kutokana na uhitaji wa kusafiri nje, kujikinga.
Mfano wafanya biashara wa kihindi, wachina wana jumuiya zao rasmi.

Sasa Serikali imeridhia chanjo, hizo jumuiya wameruhusiwa kuagiza ili kukabiliana na uhaba pia na kuongeza kasi ya upatikanaji wake.

Acha chuki.
 
Mkuu mbona tumechaguliwa aina ya chanjo wakati chanjo zipo nyingi?
Husomi habari? Hukusikia kuwa hizi ni za msaada kutoka USA? Yaani hakuna malipo. Sasa kama unataka kuchagua upewe msaada wa aina gani hilo unabidi ufanye jambo la ziada.
 
Mimi nakuambiaje serekali ya huyu mama ni dhalimu kabisa katika afya ya watanzania katika hi chanjo wana lao jambo ni Mungu tu aepushilie mbali.

Sichomi na haitoka ikatokea nikachoma.
Mawazo ya kipumbavu tu haya
 
Back
Top Bottom