SoC02 Mbinu za kuondokana na tatizo la Ajira nchini

Stories of Change - 2022 Competition

Tinov 1998

New Member
Aug 26, 2022
3
4
Tanzania ni moja Kati ya nchi nyingi duniani ambazo zimekubwa na tatizo la ukosefu wa ajira, Hali ambayo imepelekea matatizo ya kiuchumi na kijamii. Ukosefu wa ajira rasmi hupelekea makundi ya vijana wasomi wasio na kazi kuongezeka katika jamii zetu, hali inayopelekea kuongezeka kwa makundi ya kihalifu.

Aidha baadhi ya jitihada ambazo zimechukuliwa na serikali ni pamoja na kuhamasisha vijana kujihusisha na shughuli za ujasiriamali ili waweze kujiingizia kipato na kuepukana na umaskini. Aidha mwitikio umekuwa mdogo kutokana na kukosekana kwa mtaji kwa vijana wengi. Zifuatazo ni mbinu zinazoweza kuleta matokeo chanya kuhusiana na tatizo la ajira nchini:

Mosi, kuwapa vijana maarifa na stadi za kazi pindi wanapokuwa shuleni au vyuoni. Hii ni pamoja na kuwafundisha masomo Kama vile kilimo na biashara kwa vitendo ili waweze kumudu Maisha halisi ya mtaani.

Pili, kuwapa vijana mtaji wa kutosha ili waweze kuanzisha miradi mbalimbali kama vile kilimo na ufugaji.

Tatu, kuwafungulia vijana mwanya wa kufanya kazi katika mashirika mbalimbali nchini, au nje ya nchi, makampuni binafsi na taasisi ile waweze kapata uzoefu, ujuzi na kipato.

Nne, kuunda makundi ya vijana katika kila eneo ili waweze kufikiwa kwa haraka na kupewa msimamizi (mentor) atakayewaongoza.

Mwisho Ila si kwa umuhimu, jamii pamoja na serikali wakishirikiana na mashirika na taasisi binafsi wanatakiwa kukaa kwa ukaribu na vijana ambao ndio kundi kubwa linalokumbwa na ukosefu wa ajira ili waweze kuyatatua matatizo yao na kuwaongoza.

From Tinov
Phone 0688503442
 
Back
Top Bottom