Mbinu mahiri ya kijasusi ya kukwepa wahalifu na wasiojulikana

Artificial intelligence

JF-Expert Member
Jan 28, 2021
1,262
2,191
Je wewe ni muhanga wa ufuatiliaji (SURVEILLANCE)? Ikiwa wewe ni mtu ambaye unafuatiliwa na wahalifu au watu wengine kutokana na shughuli zake ziwe za kisiasa, kibiashara na hata kimahusiano basi njia hizi nitakazozielezea hapa ukizifuata na kuziishi zinaweza kukufanya uwe salama ikiwa upo under surveillance ya aina yeyote.

Kwenye UJASUSI kuna kitu kinaitwa "COUNTERSURVEILLANCE LIKE PRO", Yaani ni jinsi gani mtu unaweza kukwepa surveillance ya aina yeyote ile ndani ya muda mfupi sana ikiwa unafuatiliwa na wahalifu/wasiojulikana ili kukamatwa au kutekwa.

UFUATILIAJI (SURVEILLANCE) KATIKA UJASUSI NI NINI
Ufuatiliaji kwenye UJASUSI mara nyingi hutumiwa kufuatilia tabia, shughuli au habari nyingine yoyote ambayo inaweza kubadilika kutokana na hali fulani. Ufuatiliaji kwa ujumla hutumiwa kushawishi, kusimamia au kulinda watu na kumpata mlegwa wa operation maalumu(yaani target man).

Kuna aina nyingi za ufuatiliaji ambazo mtu wa kawaida ambaye hata siyo jasusi anaweza kukutana nazo. Wengi wetu tumezoea kuona kamera ambazo zinarekodi shughuli kila mahali kutoka viwanja vya michezo na viwanja vya ndege hadi migahawa, majumbani mwetu, mitaani, taasisi mbalimbali na hata shule na Sote tumesikia juu ya ufuatiliaji unaofanyika kwenye mitandao ya kijamii kama vile Facebook na Twitter ambapo habari hutumiwa kuunda ramani za mitandao ya kijamii na data zinahifadhiwa kwa ajili ya habari muhimu juu ya magaidi au watumiaji wengine wenye kashfa mbali mbali za uhalifu.

Baadhi ya aina za ufuatiliaji ni pamoja na ufuatiliaji wa ushirika, maelezo, angani, na ufuatiliaji wa biometriska.

Uhalifu mwingi ni uhalifu wa fursa(Hii ni sentensi ambayo jasusi yeyote akiwa kwenye mafunzo ya countersurveillance lazima aiweke akilini).
Maana yake ni kwamba wahalifu wanatafuta mazingira kamili ambayo wanaweza kufanya uhalifu wao bila mlengwa kutambua. Hapa unaweza kufuatiliwa hata miezi kadhaa au Mwaka bila wewe kutambua kama unafuatiliwa.

Sasa nizungumzie mbinu tano rahisi ambazo maafisa wa ujasusi hutumia kuendesha uchunguzi ambazo hata raia wa kawaida unaweza kuzitumia muda na wakati wowote. Huna haja ya kuwa jasusi wa CIA, MOSSAD au kuwa na uzoefu wa miaka kadhaa ya ujasusi ili kutumia mbinu hizi zifuatazo;

Mbinu ya Kwanza: The Pause and Turn(Sitisha na Kugeuka)
Wakati mtu anakufuata kwa nia ya kukudhuru unatakiwa kusitisha na kugeuka, njia inaweza kuwa njia ya kusaidia sana kuamua ikiwa uko chini ya ufuatiliaji na kumruhusu mtu ajue unajua kile anachofanya juu yako au ikiwa anakufuatilia. Wakati unatembea utatakiwa kupumzika na kugeuka ghafla huku ukijifanya kufanya kitu—kama vile kuangalia simu yako, kufunga viatu kamba, au geuka kana kwamba unatafuta mtu au kitu mahala fulani na Kisha angalia moja kwa moja mtu unayedhani anakufuata/anakufuatilia. Hali hii umfanye yule anayekufuatilia kujishtukia na kujitoa mwenyewe. Kwa maneno mengine, mtu anayekufuata hataonyesha tabia sawa ya asili kama mtu ambaye anatembea tu barabarani na hana muda na wewe.

Mbinu ya Pili: The Acknowledgment(Kukiri)
Mbinu hii inakuhitaji mara tu unapo ona kuwa unafuatwa ni muhimu kumruhusu mtu ajue kuwa unajua kile anachokifanya/wanachofanya kuhusu wewe. Mara tu wahalifu wengi wanapogunduaga kuwa unafahamu kile wanachokusudia kufanya dhidi yako mara nyingi watakuacha peke yako nakuondoka. Kumbuka wahalifu wanatafuta mtu wao tu na kwa kutambua kwamba unajua uwepo wao na kwamba wanapanga kukudhuru hukufanya uwe mtu usiye weza kudhurika kirahisi. Kugeuka na kuuliza kwa ujasiri, "Je, ninaweza kukusaidia?" kuna uwezekano wa kusababisha mtu kuchagua kukuacha peke yako na asikudhuru kwa wakati huo.
Mbinu ya tatu: Don’t Be a Soft Target(Usiwe Mlengwa laini)
Ikiwa unafuatiliwa mara zote usipende kuwa mlengwa laini ikiwa na maana ya kwamba uonyeshe hisia ya nguvu(kama una silaha tumia kujilinda), tembea mwendo wa haraka kama unatumia gari/miguu na uweke kichwa chako juu usiinamishe kichwa chini, ikiwa utainamisha kichwa chini utapoteza focus. Piga simu kwa mtu na ujadili kwa njia ya wazi kwamba kuna mtu anayekufuata, na usionyeshe hofu yakufanya hivyo. Kumbuka kwamba mara nyingi wahalifu wanapoona una viashiria vya woga unawapa picha ya kukuona wewe ni laini na dhahifu, hivyo ni rahisi kukudhuru.

Mbinu ya Nne: Stay Public (Kaa kwenye umma)
Ikiwa umegundua kuwa mtu anakufuata, ni muhimu usiende nyumbani. Inaweza mara nyingi watu wengi tunafikiri kwamba nyumbani ni sehemu salama lakini sivyo na mara nyingi watu utekwa au uchukuliwa wakiwa nyumbani kwao. Nyumbani ndiyo iwe sehemu ya mwisho kabisa unapaswa kwenda, hii ni kwa sababu wahalifu utaka kujua unapoishi ili iwe rahisi kukudhuru. Mhalifu anaweza kujaribu kuvunja ndani ya nyumba yako, au atakulaghai kwamba amekwenda, wakati mwishowe anajificha na kujiandaa kuvunja nyumba baadaye. Katika mbinu hii Ili kuhakikisha usalama wako ikiwa uko chini ya ufuatiliaji fanya haya yafuatayo:​
  • Kaa katika eneo lenye watu wengi la umma na uombe msaada haraka iwezekanavyo. Maeneo salama ni pamoja na migahawa, maduka yenye shughuli nyingi, na pembeni mwa barabara ambapo kuna watu wengi.​
  • Kamwe usitembee kwenye barabara zilizojificha na ambazo hazina watu wengi wanaotembea.​
  • Ikiwa unafuatwa mahali pa umma kama vile duka la vyakula, usijaribu kuondoka dukani na kuingia kwenye gari lako kwa sababu mara nyingi wahalifu husubiri katika mlango kwa ajili ya wewe kuja nje ya duka na kisha wanaweza kukufuata kwenye gari lako ambapo wanaweza kukudhuru au kukufuata hadi nyumbani kwako.​
Mbinu ya Tano: Slow Down and Mix Things Up(Punguza kasi na uchanganye mambo)

Ikiwa upo unaendesha gari na umegundua kuwa gari lingine linakufuata, endelea kuendesha gari na usirudi nyumbani ikiwa gari linakufuata, badilisha kasi/speed ya gari mara nyingi ili kumruhusu mfuasi ajue unamjua. Wakati unafanya hivyo kwa usalama zaidi kumbuka kunakiri namba ya leseni ya gari au hata alama mbali mbali zilizopo kwenye gari linalokufuatilia ili uweze kutoa habari kwenye vyombo vya ulinzi.

N.B Angalia Viatu Vyao
Ni rahisi kuondoa au kuweka kofia ya baseball, miwani ya jua, au vitu vingine ambavyo vinaweza kufanya iwe vigumu kutambua mtu fulani lakini si rahisi kubeba jozi ya ziada ya viatu. Viatu ambavyo mtu amevaa vinaweza kubaki sawa hivyo ni muhimu kumchunguza yule anayekufuatilia miguuni amevaa nini.

Kwa nyongeza Kama upo katika kiwango cha juu cha hatari(high threat level), kwa usalama zaidi zingatia haya;
Ikiwa una uhusiano mbaya na mume/mke wa zamani au mpenzi ambaye anakusumbua wakati wote-au umekuwa na kutokubaliana na mfanyakazi wa zamani, mlengwa wa kisiasa au mfanyakazi mwenza na unaona kama una kiwango cha juu cha tishio Unapaswa pia kuwa na mashaka sana na juu ya mtu ambaye umekuwa ukigundua mara kwa mara anakufuatilia na hapa jiulize maswali haya kabla hujadhurika Je, una wasiwasi juu ya mtu ambaye anaonekana kupata kahawa/chakula/kinywaji mahali pamoja na wakati huo huo kama unavyofanya? Ikiwa upo kwenye kiwango cha juu cha tishio kuna tahadhari chache za ziada ambazo ni muhimu kwako kuchukua
Badilisha Tabia Yako kwa kufanya hivi,
  • Tofautisha wakati unaondoka nyumbani asubuhi.​
  • Badilisha njia na muda wa safari yako.​
  • Changanya shughuli zako. Usipende kula/kukaa sehemu moja tu ikiwa upe nje ya eneo la kazi yako​
  • Tembelea migahawa ambayo hujawahi kuwa nayo hapo awali.​
  • Chukua njia tofauti kuelekea nyumbani wakati wa kutoka kazini.​
#DONT FORGET, MOVEMENT SAVES LIFE
 
Mbinu mojawapo ya jinsi ya kumfuatilia mtu. Usiwe peke yako. Kuweni kikundi. Anamfuatilia mmoja mpaka mahali fulani kisha anapokea mwingine. Hata kama mnatumia gari au pikipiki. Isiwe moja. Hii inafanya anayefuatiliwa asiwatambue kirahisi. Au mmoja amfuatilie overtly na agundulike, akimtilia maanani huyo, wengine mnapata nafasi nzuri ya kumfuatilia. Anadhani yuko kwenye public kumbe nyie ndiyo public.

Mkisha muweka sehemu nzuri, mnamuingizq kwenye Noah na kwenda kumminya makende, kumtoa kucha, meno na mambo mengine kama hayo.
 
Mbinu mojawapo ya jinsi ya kumfuatilia mtu. Usiwe peke yako. Kuweni kikundi. Anamfuatilia mmoja mpaka mahali fulani kisha anapokea mwingine. Hata kama mnatumia gari au pikipiki. Isiwe moja. Hii inafanya anayefuatiliwa asiwatambue kirahisi. Au mmoja amfuatilie overtly na agundulike, akimtilia maanani huyo, wengine mnapata nafasi nzuri ya kumfuatilia. Anadhani yuko kwenye public kumbe nyie ndiyo public.

Mkisha muweka sehemu nzuri, mnamuingizq kwenye Noah na kwenda kumminya makende, kumtoa kucha, meno na mambo mengine kama hayo.
Daaaah bongo sihami aiseee..!!
 
Huu uzi mzuri sana. Kuna mbinu nyingine inaitwa dry cleaning
 
Back
Top Bottom