Mbinu bora za kivita: Russia and Ukraine war case

Nkerebhuke

JF-Expert Member
Nov 1, 2021
779
1,985
Kuna kundi kubwa sana la watu ambao wanapenda kuona, kusoma na kusikia habari za uwanja wa medani hii inatokana na ukweli kuwa vita ndio jambo gumu sana kufanywa na mwanadamu. Katika dunia ya leo kila jambo lina taaluma yake hata vita pia ni taaluma pana inayohusisha mbinu, mikakati, silaha, propaganda, hujuma, utawala na uchumi.

Katika makala hii naomba kuwakaribisha wajuvi wa mbinu za medani kwa kurejea uwezo wa kimbinu kati ya jeshi la urusi na ukraine. Wajuvi wa mambo ya vita waliwahi kubashiri kuwa russia angeweza kumaliza operation yake ndani ya masaa 72 lakini hali imekuwa tofauti kwani ni miezi mitatu sasa vita inaoendelea na majeshi yanaendelea kujibishana mapigo.

Kutokana na vyanzo mbalimbali vya tv na intelligence blog vimebainisha kuwa russia anatumia mbinu ya ' battalion tactical group'' yaani nikikundi chenye combat unit zote yaani infantry, tank, artillery regiment. Mbinu hii imeonekana kuwa dhaifu kwa maana yakuwa vifaru vingi vitandikwa sana askari wameonesha uwezo mdogo wa kusonga mbele. Hii mbinu ikitumiwa vizuri huleta ushindi wa haraka kweni vikosi vinaweza kusonga mbele kwa haraka sana kwani vinakuwa ensured na fire support.

Takio la kupigwa kwa battalion iliojaribu kuvuka mto ni moja ya udhaifu we hii mbinu, maana inakuwa na mkusanyiko mkubwa wa magari ya logistic, tanks na magari ya askari. Naomba kuishia hapa kuwapa nafasi wajuvi wengine wa mambo ya medani karibuni.
 
... mbinu uliyotaja ni ya kale sana; nakumbuka hata wakati Joshua anatuma jeshi kuuhusuru Yeriko hakutumia mbinu ya kutuma kikosi kizima kama msafara wa harusi.

.., mbinu hiyo iliwahi kutumiwa na wafilisti wakiongozana na Kamanda wao Goliath walichokipata kimekuwa kwenye vitabu vitakatifu hadi leo. Inashangaza nyakati za leo kuna baadhi bado wanaitumia.
 
Hii mbinu ina ubora wake, tuliwahi kuitumia kwenye vita ya kagera wakati huo tunatumia bm 21, tulifanikiwa kuvichakaza vikosi vya amini kwa sababu adui alinyeshewa mizinga kama mvua. Kama nimfuatiliaji mzuri Russia alianza kuinyeshea makombora ukraine kama mvua lakini progress yao ya vikosi vyao imeonekana kuwa poor
 
Kilicho fanya vita hii iwe ngumu kwa Urusi ni msaada wa silaha anazo pata Ukraine kutoka nchi za magharibi tofauti na hapo Ukraine isingezewa kabisa kuhimili ile nguvu ya Urusi iliyo kuwa imeingia nayo.

Mengine tunapoteza muda tu.

Hata rais wa Ukraine jana alisema kuwa bila misaada ya silaha kutoka nchi za magharibi Ukrain haitaweza kupigana kwa muda mrefu na itashwindwa vita.

Siku zote ili ushinde vita inatakiwa kuhakikisha unaharibu silaha za adui yako ili ashindwe kupigana.
Lakini kwa Ukraine ni tofauti kabisa maana kila Urusi anapo haribu silaha za Ukraine zinaingizwa zingine mpya hivyo kuliwezesha jeshi la Ukraine kuendelea kupigana.

Bila shaka nyote mna kumbuka kilicho ikuta Marekani nchini Uvitenam baada Usoviet kuisaidia silaha Vietnam kilicho tokea ni Marekani kushindwa vibaya sana.

Hata vita ya Iraq iwapo Iraq ingepata misaada ya silaha kama ya Ukraine Marekani ingekumbana na maafa makubwa sana na isingeweza kushinda ile vita au ingeshinda kwa gharama kubwa sana ya vifaa na wanajeshi.

Hata Urusi kinacho msaidia na kitakacho msaidia kupigana kwa muda mrefu ni kwa sababu tu ni mtengenezaji wa silaha, lakini angekuwa anategemea silaha za kununua hii vita ingemshinda mapema sana na angekuwa amesha kimbia.

Vita ya ardhini huwa ni ngumu sana tena sana haijalishi unaye pambana ana uwezo kiasi gani.
 
Jeshi la Russia limejengwa kulinda serikali(Raisi) kuliko kuilinda taifa. Hapo utapata ma generali hawawezi toa Ushauri huru badala yake, wao ndo wanapewa ushauri na raisi.

Alafu pia wanajeshi wa Russia morale yao iko chini sana ukizingatia wanampigania mtu mmoja na sio taifa zima.
 
Kilicho fanya vita hii iwe ngumu kwa Urusi ni msaada wa silaha anazo pata Ukraine kutoka nchi za magharibi tofauti na hapo Ukraine isingezewa kabisa kuhimili ile nguvu ya Urusi iliyo kuwa imeingia nayo.

Mengine tunapoteza muda tu.

Hata rais wa Ukraine jana alisema kuwa bila misaada ya silaha kutoka nchi za magharibi Ukrain haitaweza kupigana kwa muda mrefu na itashwindwa vita.

Siku zote ili ushinde vita inatakiwa kuhakikisha unaharibu silaha za adui yako ili ashindwe kupigana.
Lakini kwa Ukraine ni tofauti kabisa maana kila Urusi anapo haribu silaha za Ukraine zinaingizwa zingine mpya hivyo kuliwezesha jeshi la Ukraine kuendelea kupigana.

Bila shaka nyote mna kumbuka kilicho ikuta Marekani nchini Uvitenam baada Usoviet kuisaidia silaha Vietnam kilicho tokea ni Marekani kushindwa vibaya sana.

Hata vita ya Iraq iwapo Iraq ingepata misaada ya silaha kama ya Ukraine Marekani ingekumbana na maafa makubwa sana na isingeweza kushinda ile vita au ingeshinda kwa gharama kubwa sana ya vifaa na wanajeshi.

Hata Urusi kinacho msaidia na kitakacho msaidia kupigana kwa muda mrefu ni kwa sababu tu ni mtengenezaji wa silaha, lakini angekuwa anategemea silaha za kununua hii vita ingemshinda mapema sana na angekuwa amesha kimbia.

Vita ya ardhini huwa ni ngumu sana tena sana haijalishi unaye pambana ana uwezo kiasi gani.
Umesahau 'morale victory'' hii ni segment muhimu sana. St javelin zimechangia sana kuharibu mwelekeo wa vikosi vya Russia. Tactical specification zake inatisha, inapiga kutokea juu sehemu ambayo nidhaifu kifaru kinaungua chote.
 
Russia huwa wanatumia mbinu kuu mbili.
1. Kufurumusha makombora ya masafa ya mbali.
2. Misafara mikubwa ya kijeshi yenye kila kitu.

Ukraine wanatumia mbinu kuu mbili.
1. Kufurumusha makombora ya masafa mafupi mafupi.
2. Kujitawanya katika makundi madogo ya askari wenye silaha ndogo ndogo.

Kila mbinu ina faida na hasara zake, tatizo ni namna unavyoitumia hiyo mbinu. Kwa mfano, Mbinu ya Russia ya kutumia makombora ya masafa ya mbali imeishia kulenga majengo ya kiraia ambayo hayana tena watu ndani yake au kuua raia wasiokuwa na hatia kuliko wapiganaji halisi, kwa kuwa Ukraine ilishajipanga kwa hilo muda mrefu kabla ya vita kuwatawanya wapiganaji wake maeneo yasiyo rasmi.

Pili mbinu ya kutumia misafara mikubwa yenye kila kitu ililenga kuyachukua maeneo ya Ukraine na kuyakalia moja kwa moja, lakini lengo hilo limekuwa ni hasara kwa Russia baada ya kukuta baadhi ya maeneo miundo mbinu ya madaraja kubomolewa kabisa kiasi cha kuwafanya kukaa siku kadhaa eneo hilo wakijipanga kuvuka, kuishiwa nishati, chakula, kuzungukwa ghafla na makundi ya askari wa Ukraine kiasi cha kukosa nafasi ya kutorokea nk. Waza tu, kikosi cha Askari 2000 wa Russia, wakiwa na vifaru 30, magari makubwa 60, magari madogo 30 halafu kijikute kimekwama kijiji kimoja ndani ndani huko kwa siku kama saba hivi, hakuna umeme, maji, mawasiliano ya uhakika, hakiwezi kusonga mbele maana daraja la kuvuka mto limesambaratishwa vibaya, halafu kinapata habari kuwa kimezungukwa pande zote na vikundi kama 10 vya wapiganaji wa Ukraine vyenye askari 20 kwa kikundi, wakiwa na bunduki, drones, makombora ya kubebwa begani ya masafa mafupi, na wako kama 3km tu toka eneo walipo. Nini kitafuata kwa Russia? Jibu ni moja tu, askari wote 2000 watatawanywa pande zote, vifaru na magari vitaachwa eneo moja kwanza, na katika hali ya kawaida huenda nusu ya askari wa Russia wataangamia. Na hicho ndio kinaendelea Russia kwa sasa.
 
Unadhani ni kipi kingetokea iwapo hizo stjavelin zingeiishia Ukraine ?
Ina maana isingeweza tena kuvizuia vikosi vya Urusi kusonga mbele.

Kwa hiyo hoja yangu iko pale pale nchi yeyote ikiwa na uhakika wa kupata silaha kuishinda ni ngumu sana.

Unadhani kwa nn makundi kama alishababu yameshindikana, ni kwa sababu yana pata misaada ya silaha ambayo inawawezesha kupigana.

Hata sisi Tz tukipata huakika wa silaha nzuri kama wanazo pata Ukraine tuna weza kupigana na jeshi lolote lile duniani na kulisababishia hasara kubwa mno.
 
... mbinu uliyotaja ni ya kale sana; nakumbuka hata wakati Joshua anatuma jeshi kuuhusuru Yeriko hakutumia mbinu ya kutuma kikosi kizima kama msafara wa harusi.

.., mbinu hiyo iliwahi kutumiwa na wafilisti wakiongozana na Kamanda wao Goliath walichokipata kimekuwa kwenye vitabu vitakatifu hadi leo. Inashangaza nyakati za leo kuna baadhi bado wanaitumia.
duuh
 
Kilicho fanya vita hii iwe ngumu kwa Urusi ni msaada wa silaha anazo pata Ukraine kutoka nchi za magharibi tofauti na hapo Ukraine isingezewa kabisa kuhimili ile nguvu ya Urusi iliyo kuwa imeingia nayo.

Mengine tunapoteza muda tu.

Hata rais wa Ukraine jana alisema kuwa bila misaada ya silaha kutoka nchi za magharibi Ukrain haitaweza kupigana kwa muda mrefu na itashwindwa vita.

Siku zote ili ushinde vita inatakiwa kuhakikisha unaharibu silaha za adui yako ili ashindwe kupigana.
Lakini kwa Ukraine ni tofauti kabisa maana kila Urusi anapo haribu silaha za Ukraine zinaingizwa zingine mpya hivyo kuliwezesha jeshi la Ukraine kuendelea kupigana.

Bila shaka nyote mna kumbuka kilicho ikuta Marekani nchini Uvitenam baada Usoviet kuisaidia silaha Vietnam kilicho tokea ni Marekani kushindwa vibaya sana.

Hata vita ya Iraq iwapo Iraq ingepata misaada ya silaha kama ya Ukraine Marekani ingekumbana na maafa makubwa sana na isingeweza kushinda ile vita au ingeshinda kwa gharama kubwa sana ya vifaa na wanajeshi.

Hata Urusi kinacho msaidia na kitakacho msaidia kupigana kwa muda mrefu ni kwa sababu tu ni mtengenezaji wa silaha, lakini angekuwa anategemea silaha za kununua hii vita ingemshinda mapema sana na angekuwa amesha kimbia.

Vita ya ardhini huwa ni ngumu sana tena sana haijalishi unaye pambana ana uwezo kiasi gani.
Hapa umemaliza kilakitu ni maelezo mazuri Ila na Mimi naongezea neno dogo kuwa "Russia anapigana na NATO ndani ya Ukraine" Ukraine anapata usaidizi WA silaha,wanajeshi wazoefu,pesa na satellite images (majeshi yote ya Russia wanakopitia wanaonekana mpaka meli zao baharini).
Sikuzote vita vya ardhini ni ngumu Sana na hapa ndipo kwenye ushindi
 
Russia huwa wanatumia mbinu kuu mbili.
1. Kufurumusha makombora ya masafa ya mbali.
2. Misafara mikubwa ya kijeshi yenye kila kitu.

Ukraine wanatumia mbinu kuu mbili.
1. Kufurumusha makombora ya masafa mafupi mafupi.
2. Kujitawanya katika makundi madogo ya askari wenye silaha ndogo ndogo.

Kila mbinu ina faida na hasara zake, tatizo ni namna unavyoitumia hiyo mbinu. Kwa mfano, Mbinu ya Russia ya kutumia makombora ya masafa ya mbali imeishia kulenga majengo ya kiraia ambayo hayana tena watu ndani yake au kuua raia wasiokuwa na hatia kuliko wapiganaji halisi, kwa kuwa Ukraine ilishajipanga kwa hilo muda mrefu kabla ya vita kuwatawanya wapiganaji wake maeneo yasiyo rasmi.

Pili mbinu ya kutumia misafara mikubwa yenye kila kitu ililenga kuyachukua maeneo ya Ukraine na kuyakalia moja kwa moja, lakini lengo hilo limekuwa ni hasara kwa Russia baada ya kukuta baadhi ya maeneo miundo mbinu ya madaraja kubomolewa kabisa kiasi cha kuwafanya kukaa siku kadhaa eneo hilo wakijipanga kuvuka, kuishiwa nishati, chakula, kuzungukwa ghafla na makundi ya askari wa Ukraine kiasi cha kukosa nafasi ya kutorokea nk. Waza tu, kikosi cha Askari 2000 wa Russia, wakiwa na vifaru 30, magari makubwa 60, magari madogo 30 halafu kijikute kimekwama kijiji kimoja ndani ndani huko kwa siku kama saba hivi, hakuna umeme, maji, mawasiliano ya uhakika, hakiwezi kusonga mbele maana daraja la kuvuka mto limesambaratishwa vibaya, halafu kinapata habari kuwa kimezungukwa pande zote na vikundi kama 10 vya wapiganaji wa Ukraine vyenye askari 20 kwa kikundi, wakiwa na bunduki, drones, makombora ya kubebwa begani ya masafa mafupi, na wako kama 3km tu toka eneo walipo. Nini kitafuata kwa Russia? Jibu ni moja tu, askari wote 2000 watatawanywa pande zote, vifaru na magari vitaachwa eneo moja kwanza, na katika hali ya kawaida huenda nusu ya askari wa Russia wataangamia. Na hicho ndio kinaendelea Russia kwa sasa.

huu sasa ndio uchambuzi. based on critical analysis
 
Kuna kundi kubwa sana la watu ambao wanapenda kuona, kusoma na kusikia habari za uwanja wa medani hii inatokana na ukweli kuwa vita ndio jambo gumu sana kufanywa na mwanadamu. Katika dunia ya leo kila jambo lina taaluma yake hata vita pia ni taaluma pana inayohusisha mbinu, mikakati, silaha, propaganda, hujuma, utawala na uchumi.

Katika makala hii naomba kuwakaribisha wajuvi wa mbinu za medani kwa kurejea uwezo wa kimbinu kati ya jeshi la urusi na ukraine. Wajuvi wa mambo ya vita waliwahi kubashiri kuwa russia angeweza kumaliza operation yake ndani ya masaa 72 lakini hali imekuwa tofauti kwani ni miezi mitatu sasa vita inaoendelea na majeshi yanaendelea kujibishana mapigo.

Kutokana na vyanzo mbalimbali vya tv na intelligence blog vimebainisha kuwa russia anatumia mbinu ya ' battalion tactical group'' yaani nikikundi chenye combat unit zote yaani infantry, tank, artillery regiment. Mbinu hii imeonekana kuwa dhaifu kwa maana yakuwa vifaru vingi vitandikwa sana askari wameonesha uwezo mdogo wa kusonga mbele. Hii mbinu ikitumiwa vizuri huleta ushindi wa haraka kweni vikosi vinaweza kusonga mbele kwa haraka sana kwani vinakuwa ensured na fire support.

Takio la kupigwa kwa battalion iliojaribu kuvuka mto ni moja ya udhaifu we hii mbinu, maana inakuwa na mkusanyiko mkubwa wa magari ya logistic, tanks na magari ya askari. Naomba kuishia hapa kuwapa nafasi wajuvi wengine wa mambo ya medani karibuni.
Unataka wataalamu wa mbinu za kivita wajiunge na uzi wako walete uchambuzi wao.Inabidi wewe mwenyewe kwanza uwe na utaalamu wa hayo mambo lakini inaonekana uko mbali sana na mambo ya kijeshi na mbinu za kivita.Na inaonekana hufai kupewa hata cheo cha kuongoza askari kanzu katika vita kwani unatishwa haraka na propaganda za adui.Una uhakika gani kuwa bataliani ya Urusi imeteketezwa na kwamba huo ndio mwisho wa kuvuka huo mto hata kama walipata kikwazo mara ya 1
 
Unadhani ni kipi kingetokea iwapo hizo stjavelin zingeiishia Ukraine ?
Ina maana isingeweza tena kuvizuia vikosi vya Urusi kusonga mbele.

Kwa hiyo hoja yangu iko pale pale nchi yeyote ikiwa na uhakika wa kupata silaha kuishinda ni ngumu sana.

Unadhani kwa nn makundi kama alishababu yameshindikana, ni kwa sababu yana pata misaada ya silaha ambayo inawawezesha kupigana.

Hata sisi Tz tukipata huakika wa silaha nzuri kama wanazo pata Ukraine tuna weza kupigana na jeshi lolote lile duniani na kulisababishia hasara kubwa mno.
Achana na upuuzi wa Alshababu .Hizo silaha wanazipata kutoka wapi ?
 
Unataka wataalamu wa mbinu za kivita wajiunge na uzi wako walete uchambuzi wako.Inabidi wewe mwenyewe kwanza uwe na utaalamu wa hayo mambo lakini inaonekana uko mbali sana na mambo ya kijeshi na mbinu za kivita.Na inaonekana hufai kupewa hata cheo cha kuongoza askari kanzu katika vita kwani unatishwa haraka na propaganda za adui.Una uhakika gani kuwa bataliani ya Urusi imeteketezwa na kwamba huo ndio mwisho wa kuvuka huo mto hata kama walipata kikwazo mara ya 1
Uki general bro ni misconception, kuna mstari mwembamba sana unaotenganisha kati ya fake news na propaganda unless kuna wakati nivigumu kuvitenganisha. Propaganda inaweza kupikwa na taarifa za kweli ila zenye lengo la kuvunja morale. Mimi nimetolea mfano wa battalion tactics ambayo ndio hutumika sana kuteka miji. Hata ile ambush ni mfano wa failure ya hii mbinu na hata kama iliongamizwa haikuwa ni battalion nzima.
 
Achana na upuuzi wa Alshababu .Hizo silaha wanazipata kutoka wapi ?
Mbona una attach maoni ya wenzako bila kuonesha maoni yako kana kwamba unaelewa sana kuliko wenzio. Toa maoni yako watu wayasome na uwe open kuwa criticized.
 
Hapa sijakuelewa unakusudia nini kuhusu maoni yangu na wenzangu.Pamoja na hivyo ngoja nifafanue kidogo. Ukraine inajulikana kutokana na matangazo na wanaohusika na hii vita kuwa wanapata silaha.Sasa ukitaja Alshabab nimeita ni upuuzi kwa sababu haijulikani wako wapi na makao makuu yao ni wapi.Na kama ni silaha nani anayewapatia na kwa madhumuni gani.
 
5 Reactions
Reply
Back
Top Bottom