Mbinu bora za kivita: Russia and Ukraine war case

Unataka wataalamu wa mbinu za kivita wajiunge na uzi wako walete uchambuzi wao.Inabidi wewe mwenyewe kwanza uwe na utaalamu wa hayo mambo lakini inaonekana uko mbali sana na mambo ya kijeshi na mbinu za kivita.Na inaonekana hufai kupewa hata cheo cha kuongoza askari kanzu katika vita kwani unatishwa haraka na propaganda za adui.Una uhakika gani kuwa bataliani ya Urusi imeteketezwa na kwamba huo ndio mwisho wa kuvuka huo mto hata kama walipata kikwazo mara ya 1
Wewe una uhakika kama kuna vita kati ya Russia na Ukraine?
 
Kilicho fanya vita hii iwe ngumu kwa Urusi ni msaada wa silaha anazo pata Ukraine kutoka nchi za magharibi tofauti na hapo Ukraine isingezewa kabisa kuhimili ile nguvu ya Urusi iliyo kuwa imeingia nayo.

Mengine tunapoteza muda tu.

Hata rais wa Ukraine jana alisema kuwa bila misaada ya silaha kutoka nchi za magharibi Ukrain haitaweza kupigana kwa muda mrefu na itashwindwa vita.

Siku zote ili ushinde vita inatakiwa kuhakikisha unaharibu silaha za adui yako ili ashindwe kupigana.
Lakini kwa Ukraine ni tofauti kabisa maana kila Urusi anapo haribu silaha za Ukraine zinaingizwa zingine mpya hivyo kuliwezesha jeshi la Ukraine kuendelea kupigana.

Bila shaka nyote mna kumbuka kilicho ikuta Marekani nchini Uvitenam baada Usoviet kuisaidia silaha Vietnam kilicho tokea ni Marekani kushindwa vibaya sana.

Hata vita ya Iraq iwapo Iraq ingepata misaada ya silaha kama ya Ukraine Marekani ingekumbana na maafa makubwa sana na isingeweza kushinda ile vita au ingeshinda kwa gharama kubwa sana ya vifaa na wanajeshi.

Hata Urusi kinacho msaidia na kitakacho msaidia kupigana kwa muda mrefu ni kwa sababu tu ni mtengenezaji wa silaha, lakini angekuwa anategemea silaha za kununua hii vita ingemshinda mapema sana na angekuwa amesha kimbia.

Vita ya ardhini huwa ni ngumu sana tena sana haijalishi unaye pambana ana uwezo kiasi gani.
Malezo yako yana upungufu fulani. Unashindwa kuelewa kuwa Nchi za Magharibi zimeanza kuisaidia Ukraine baada ya kuona udhaifu wa Urusi na uwezekano wa Ukraine kushinda vita hiyo. Msaada wa kwanza kabisa wa Marekani ilikuwa ni kumpa hifadhi Rais wa Ukraine na familia yake nje ya nchi, lakini yeye akajibu haihitaji ride ya kuondoka Ukraine bali anahitaji risasi za kupambana na mvamizi.

Urusi ilitegemea sana vitisho kwa kudhani kuwa ikija na askari wengi sana na vifaru vingi basi serikali ya Kiev itaogopa na kukimbia, hivyo Putin angesimika serikali ya kibaraka wake Yakunovych aliyepinduliwa miaka tisa iliyopita. Baada ya Ukraine kumobilize raia kupinga uvamizi huo, urusi ikajikuta imeshtukizwa kuwa haikuwa imejiandaa kukumbana na mapigano ya ana kwa ana. Jeshi la Urusi halina mbinu nzuri za kupigana ana kwa ana, linatumia mbinu za kizamani sana za kufyeka kila kitu kwa kutumia mizinga ya masafa marefu lakini wanapokumbana ana kwa ana wanashindwa. Limekuwa ni jambo la kawaida sana kuona jeshi la urusi wanauwawa au kutekwa kwa wingi kwa mpigo kwa sababu ya kutokuwa na mbinu nzuri za kivita. Weakeness hizo ndizo zimesababisha nchi za Magharibi kuona kuwa kumbe Urusi ni paper tiger lakni hawana ubavu wa kupigana, ndiyo maana wakaanza kuipa Ukraine misaada ya silaha.
 
Russia huwa wanatumia mbinu kuu mbili.
1. Kufurumusha makombora ya masafa ya mbali.
2. Misafara mikubwa ya kijeshi yenye kila kitu.

Ukraine wanatumia mbinu kuu mbili.
1. Kufurumusha makombora ya masafa mafupi mafupi.
2. Kujitawanya katika makundi madogo ya askari wenye silaha ndogo ndogo.

Kila mbinu ina faida na hasara zake, tatizo ni namna unavyoitumia hiyo mbinu. Kwa mfano, Mbinu ya Russia ya kutumia makombora ya masafa ya mbali imeishia kulenga majengo ya kiraia ambayo hayana tena watu ndani yake au kuua raia wasiokuwa na hatia kuliko wapiganaji halisi, kwa kuwa Ukraine ilishajipanga kwa hilo muda mrefu kabla ya vita kuwatawanya wapiganaji wake maeneo yasiyo rasmi.

Pili mbinu ya kutumia misafara mikubwa yenye kila kitu ililenga kuyachukua maeneo ya Ukraine na kuyakalia moja kwa moja, lakini lengo hilo limekuwa ni hasara kwa Russia baada ya kukuta baadhi ya maeneo miundo mbinu ya madaraja kubomolewa kabisa kiasi cha kuwafanya kukaa siku kadhaa eneo hilo wakijipanga kuvuka, kuishiwa nishati, chakula, kuzungukwa ghafla na makundi ya askari wa Ukraine kiasi cha kukosa nafasi ya kutorokea nk. Waza tu, kikosi cha Askari 2000 wa Russia, wakiwa na vifaru 30, magari makubwa 60, magari madogo 30 halafu kijikute kimekwama kijiji kimoja ndani ndani huko kwa siku kama saba hivi, hakuna umeme, maji, mawasiliano ya uhakika, hakiwezi kusonga mbele maana daraja la kuvuka mto limesambaratishwa vibaya, halafu kinapata habari kuwa kimezungukwa pande zote na vikundi kama 10 vya wapiganaji wa Ukraine vyenye askari 20 kwa kikundi, wakiwa na bunduki, drones, makombora ya kubebwa begani ya masafa mafupi, na wako kama 3km tu toka eneo walipo. Nini kitafuata kwa Russia? Jibu ni moja tu, askari wote 2000 watatawanywa pande zote, vifaru na magari vitaachwa eneo moja kwanza, na katika hali ya kawaida huenda nusu ya askari wa Russia wataangamia. Na hicho ndio kinaendelea Russia kwa sasa.
Maelezo mazuri na ndo maana vifaru vingi unakuta watu hawapo
 
... mbinu uliyotaja ni ya kale sana; nakumbuka hata wakati Joshua anatuma jeshi kuuhusuru Yeriko hakutumia mbinu ya kutuma kikosi kizima kama msafara wa harusi.

.., mbinu hiyo iliwahi kutumiwa na wafilisti wakiongozana na Kamanda wao Goliath walichokipata kimekuwa kwenye vitabu vitakatifu hadi leo. Inashangaza nyakati za leo kuna baadhi bado wanaitumia.

Imagine msafari wa vifaru mkubwa kama wa kutoka Dar kulekea Chalinze unaongozana kwenda kuiteka Iringa,bila kuwaza je madaraja yakivunjwa watafikaje hata Morogoro na kujiokoa kurudi Dar?
Ndo walichokifanya msafara mkubwa unaelekea tu Kiev kama harusi bila kujali Ukraine wana jeshi pia ,mwisho wa siku mbinu waliyobakiwa ni kurusha tu makombora hovyo kwenye majengo ili kuogopesha raia ili wajiokoe
 
Kilicho fanya vita hii iwe ngumu kwa Urusi ni msaada wa silaha anazo pata Ukraine kutoka nchi za magharibi tofauti na hapo Ukraine isingezewa kabisa kuhimili ile nguvu ya Urusi iliyo kuwa imeingia nayo.

Mengine tunapoteza muda tu.

Hata rais wa Ukraine jana alisema kuwa bila misaada ya silaha kutoka nchi za magharibi Ukrain haitaweza kupigana kwa muda mrefu na itashwindwa vita.

Siku zote ili ushinde vita inatakiwa kuhakikisha unaharibu silaha za adui yako ili ashindwe kupigana.
Lakini kwa Ukraine ni tofauti kabisa maana kila Urusi anapo haribu silaha za Ukraine zinaingizwa zingine mpya hivyo kuliwezesha jeshi la Ukraine kuendelea kupigana.

Bila shaka nyote mna kumbuka kilicho ikuta Marekani nchini Uvitenam baada Usoviet kuisaidia silaha Vietnam kilicho tokea ni Marekani kushindwa vibaya sana.

Hata vita ya Iraq iwapo Iraq ingepata misaada ya silaha kama ya Ukraine Marekani ingekumbana na maafa makubwa sana na isingeweza kushinda ile vita au ingeshinda kwa gharama kubwa sana ya vifaa na wanajeshi.

Hata Urusi kinacho msaidia na kitakacho msaidia kupigana kwa muda mrefu ni kwa sababu tu ni mtengenezaji wa silaha, lakini angekuwa anategemea silaha za kununua hii vita ingemshinda mapema sana na angekuwa amesha kimbia.

Vita ya ardhini huwa ni ngumu sana tena sana haijalishi unaye pambana ana uwezo kiasi gani.
Plan ya Russia ilishafeli ,ndani ya masaa 72 waliyosema wamefeli bila hata nchi za magharibu kutoa silaha ,karibia wiki mbili silaha bado haikuanza kuingizwa Ukraine
 
Kama ukraine ataendelea kupewa siraha anazopewa
hii vita sio yakuisha hivi karibun,
 
Malezo yako yana upungugufu fulani. Unashindwa kelewa kuwa Nchi za Magharibi zimeanza kuisaidia Ukraine baada ya kuona udhaifu wa Urusi na uwezekano wa Ukraine kushinda vita hiyo. Msaada wa kwanza kabisa wa Marekani ilikuwa ni kumpa hifadhi Rais wa Ukraine na familia yake nje ya nchi, lakini yeye akajibu haihitaji ride ya kuondoka Ukraine bali anahitaji risasi za kupambana na mvamizi.

Urusi ilitegemea sana vitisho kudhani kuwa ikija na askari wengi sana na vifaru vingi basi serikali ya Kiev itaogopa na kukimbia, hivyo Putin angesimika serikali ya kibaraka wake Yakunovych aliyepinduliwa miaka tisa iliyopita. Baada ya Ukraine kumobilize raia kupinga uvamizi huo, urusi ikajikuta imeshtukizwa kuwa haikuwa imejiandaa kukumbana na mapigano ya ana kwa ana. Jeshi la Urusi halina mbinu nzuri za kupigana ana kwa ana, linatumia mbinu za kizamani sana za kufyeka kila kitu kwa kutumia mizinga ya masafa marefu lakini wanapokumbana ana kwa ana wanashindwa. Limekuwa ni jambo la kawaida sana kuona jeshi la urusi wanauwawa au kutekwa kwa wingi kwa mpigo kwa sababu ya kutokuwa na mbinu nzuri za kivita. Weakeness hizo ndizo zimesababisha knchi za Magharibi kuona kuwa kumbe Urusi ni paper tiger ndiyo maana wakaanza kuipa Ukraine misaada ya silaha.
Hoja zako zimekaa kishabiki sina haja ya kukujibu.
 
Kama ukraine ataendelea kupewa siraha anazopewa
hii vita sio yakuisha hivi karibun,
... sote tunakubali Ukraine ni very weak by all aspects kwa Russia; hilo halina mjadala. Kwa hiyo ili vita iishe haraka Ukraine isipewe msaada ili kumrahisishia mrusi kazi ya kuiteka na kuikalia kimabavu?
 
Plan ya Russia ilishafeli ,ndani ya masaa 72 waliyosema wamefeli bila hata nchi za magharibu kutoa silaha ,karibia wiki mbili silaha bado haikuanza kuingizwa Ukraine
Punguza ushabiki vita sio mpila kusema ina muda maalumu.
Nyinyi ndio huwa mnaharibu nyuzi za watu kwa kuendekeza ushabiki.

Srovakia,Jamuhuri ya check na Poland ni mataifa ya kwanza kupeleka silaha siku ya pili tu baada ya vita kuanza na hata kabla ya vita Ukraine ilikuwa inapokea maelfu ya tani za silaha kutoka nchi za magharibi karibia kila siku.

Hata jana raisi wa Ukraine alisema kuwa ili Ukraine iweze kupigana na Urusi kwa muda mrefu inategemeana na msaada gani atakao pewa na nchi za magharibi tofauti na hapo hawataweza na watashindwa.
Sasa tumsikilize nani kati yako na raisi wa Ukraine?

Ukraine mpaka sasa imesha pokea silaha zenye thamani ya 30$bilion tangu vita kuanza hivi unajua hizo silaha ni nyingi kiasi gani?
Na je unadhani Ukraine ingekuwa na hali gani iwapo isingewa hizo silaha?
 
Ukraine anatumia shock tactics kivita

Ambayo ni offensive maneuver which attempts to place the enemy under psychological pressure by a rapid and fully-committed advance with the aim of causing Russians combatants to retreat.
 
Punguza ushabiki vita sio mpila kusema ina muda maalumu.
Nyinyi ndio huwa mnaharibu nyuzi za watu kwa kuendekeza ushabiki.

Srovakia,Jamuhuri ya check na Poland ni mataifa ya kwanza kupeleka silaha siku ya pili tu baada ya vita kuanza na hata kabla ya vita Ukraine ilikuwa inapokea maelfu ya tani za silaha kutoka nchi za magharibi karibia kila siku.

Hata jana raisi wa Ukraine alisema kuwa ili Ukraine iweze kupigana na Urusi kwa muda mrefu inategemeana na msaada gani atakao pewa na nchi za magharibi tofauti na hapo hawataweza na watashindwa.
Sasa tumsikilize nani kati yako na raisi wa Ukraine?

Ukraine mpaka sasa imesha pokea silaha zenye thamani ya 30$bilion tangu vita kuanza hivi unajua hizo silaha ni nyingi kiasi gani?
Na je unadhani Ukraine ingekuwa na hali gani iwapo isingewa hizo silaha?
kwani Russia walipokuwa wanavamia hakujua outcomes? Unaingiaje kwenye vita ambayo baadaye unalalamika kuwa mwingine anasaidiwa?hawakujua hayo walipokuwa wanaanza?
 
Naona msaada wa silaha umeshatosha.Sasa wapeleke watu kwa sababu majeshi ya Ukraine ikiwemo kikosi kilichoitwa hatari sana kile cha Azov batallion wameshaangamia.Ukisikia askari 26000 wa Urusi wamekufa ujuwe humo ndani kuna wengi zaidi wa Ukraine na wanawaficha ndani ya hesabu ya maiti wa Urusi.Haya mabomu ya hypersonic unadhani yanatua mbugani.Ni kwenye kambi za waukraine. Na iwapo hawawezi kupeleka watu basi Urusi ikaze kamba tu kiuchumi na makombora ya masafa marefu mwishowe NATO watasambaratika.
 
kwani Russia walipokuwa wanavamia hakujua outcomes? Unaingiaje kwenye vita ambayo baadaye unalalamika kuwa mwingine anasaidiwa?hawakujua hayo walipokuwa wanaanza?
Kwani kuna aliye lalamikia mbona kichwa chako kimejaa maji badala ya akili.

Mtoa mada kaleta hoja ndio tunaijadiri na sio kulalamika.
 
Naona msaada wa silaha umeshatosha.Sasa wapeleke watu kwa sababu majeshi ya Ukraine ikiwemo kikosi kilichoitwa hatari sana kile cha Azov batallion wameshaangamia.Ukisikia askari 26000 wa Urusi wamekufa ujuwe humo ndani kuna wengi zaidi wa Ukraine na wanawaficha ndani ya hesabu ya maiti wa Urusi.Haya mabomu ya hypersonic unadhani yanatua mbugani.Ni kwenye kambi za waukraine. Na iwapo hawawezi kupeleka watu basi Urusi ikaze kamba tu kiuchumi na makombora ya masafa marefu mwishowe NATO watasambaratika.
Kama ilivyo kwa upande wa pili hata wewe pia ni blinded ni Russia military superiority kuliko uharisia wenyewe. Ukiwa na mahaba au chuki basi maoni yako yanakuwa niyakihisia kuliko ukweli wenyewe. Kama ilivyo mabeberu ana tabia ya kumuonea mdogo na kumuogopa mkubwa. Jiulize mbona russia kavamia ukraine na si Poland ambae ni member wa nato, jiulize pia mbona nato members wanapeleka silaha na si askari. Hapa ukileta ushabiki utakuwa muhenga
 
Kwani kuna aliye lalamikia mbona kichwa chako kimejaa maji badala ya akili.

Mtoa mada kaleta hoja ndio tunaijadiri na sio kulalamika.
uwe unajibu kwa staha matusi kila mtu anaweza na siyo kila mtu wa kumtusi
 
Ili ushinde vita Yeyote chino ya anga mzima Usheheni Kindakindaki mambo haya!
1-Watu
2-Uchumi
3-Silaha
Uchumi ni asilimia ndogo sana kwenyevita watu mbinu na silaha ndyo Jambo la msingi alafu Ukrein siyo nchi ndogo kama nchi za kiarabu

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Imagine msafari wa vifaru mkubwa kama wa kutoka Dar kulekea Chalinze unaongozana kwenda kuiteka Iringa,bila kuwaza je madaraja yakivunjwa watafikaje hata Morogoro na kujiokoa kurudi Dar?
Ndo walichokifanya msafara mkubwa unaelekea tu Kiev kama harusi bila kujali Ukraine wana jeshi pia ,mwisho wa siku mbinu waliyobakiwa ni kurusha tu makombora hovyo kwenye majengo ili kuogopesha raia ili wajiokoe
Russia harushi makombora ovyoo makombora mengi yamelenga target ndyo maana unaona jeshi la ukrein nguvu ya anga na mizinga limepunguzwa nguvu Kwa asilimia 70 makosa ya Rusia ni kwenda kwenye vita bila kuaribu miundo mbinu ya msingi Kwa Ukrein mbinu ambayo alikuja kuitumia baadaye. Kwenye phase 2 na yote ni sababu alienda kufanya operesheni bila kujipanga Kwa vita kamili kubadil mbinu na kuchukua maeneo ya mashariki ni Jambo la msingi kwake kuliko kung'ang'ania kuchukua Kiev

Sent from my Redmi Note 8 Pro using JamiiForums mobile app
 
Back
Top Bottom