Programu Tatu Ambazo Zitakusaidia Kuboresha Uwekezaji Kwenye Ardhi Na Majengo

Aliko Musa

Senior Member
Aug 25, 2018
156
240
Habari rafiki,

Naitwa Aliko Musa. Mimi ni mwandishi na mbobezi kwenye mambo ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo. Nimeweka shabaha kwenye kuwezesha watu kujenga utajiri au kutunza fedha zao kupitia ardhi na majengo.

Ninawafikia wateja wangu kwa njia kuu ya kuwashirikisha makala kupitia blogu yangu iitwayo UWEKEZAJI MAJENGO. Kwenye blogu hii unapata masomo ya aina tofauti tofauti bila gharama yoyote.

Pia, nilifungua kundi la whatsapp na Telegram kwa ajili ya kuwakusanya wanaopenda kujifunza, kuwekeza au kujihusisha na mambo ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Ukiwa kwenye familia ya kundi la whatsapp liitwalo TZ REAL ESTATE TEAM utaweza kupata taarifa muhimu zinazoweza kukusaidia katika mambo yako ya uwekezaji kwenye ardhi na majengo.

Programu 3 Unazotakiwa Kujiunga.

Moja.

Programu ya dalali mtaalam.

Moja ya eneo lenye changamoto kubwa sana kwenye uwekezaji wa ardhi na majengo ni huduma za udalali. Hivyo, nimeandaa mifumo ya kumuwezesha dalali wa viwanja na nyumba kuweka shabaha kwenye kazi chache zinazompa matokeo makubwa.

Hii ni kwa kuzingatia kanuni ya 80/20 isemayo matokeo unayopata kwa 80% hutokana na jitihada za 20%. Kanuni ambayo ilianzishwa na Vilfredo Pareto kwa kufanya uchunguzi wa umiliki wa ardhi huko Italy.

Vilfredo Pareto aligundua kuwa 20% ya watu wote wa Italia humiliki ardhi 80% ya ardhi yote ya Italia. Ndipo ikawa mwendelezo wa kanuni hiyo kwenye maeneo mengine ya biashara, maisha na ajira.

Kwa kutumia mbinu bora sana za madalali wenye mafanikio makubwa, utaweza kujenga biashara kubwa ya huduma za udalali wa ardhi na majengo.

Kwenye programu hii utakuwa ukijifunza hatua kwa hatua kwa miezi 6 au zaidi. Je ni akina nani wanafaa sana kujiunga na programu hii ?. Wanaotakiwa kujiunga na programu hii ni;

✓ Madalali wa viwanja, mashamba na majengo.

✓ Mawakala wa bima zote.

✓ Watoaji wa huduma za ardhi na majengo.

✓ Wamiliki na maofisa wa kampuni za kununua, kuendeleza na kuuza ardhi ndani ya miaka 2.

Gharama ya programu hii ni Tshs.50,000 kwa kipindi cha miezi 6.

Mbili.

Programu Ya KUSTAAFU NA MAJENGO YA KUPANGISHA.

Hii ni programu maalumu kwa lengo la kumsaidia mwaajiriwa serikalini au mfanyabiashara mwenye biashara iliyorasmishwa. Kwa kujiunga na programu hii utaweza kumiliki nyumba ya kupangisha inayolipa sana kwa kuzingatia vigezo vya kiuwekezaji.

Tutashirikiana na mimi hatua kwa hatua mpaka umiliki nyumba na wapangaji waingie. Ili uweze kuingia kwenye programu hii unatakiwa uwe na sifa zifuatazo;

✓ Uwe ni mwaajiriwa serikalini au taasisi binafsi kwa ajira ya mkataba wa miaka 5 au zaidi. Hii itakuwa ni chanzo cha kiasi kidogo cha fedha kwa ajili ya kuwekeza kwenye majengo ya kupangisha.

✓ Uwe na biashara iliyosajiliwa na usajili wake ni hai.

Gharama ya kujiunga na programu hii ni Tshs.100,000/=.

Tatu.

Programu ya KUNUNUA/KUJENGA NYUMBA INAYOLIPA.

Hii ni programu maalumu kwa ajili ya kusaidia mambo yafuatayo;-

✓ Uchaguzi wa ramani inayolipa.

✓ Ushauri wa vipengele vya mkataba wa upangishaji hasa hasa kwenye mambo ya kiuwekezaji.

✓ Uchaguzi wa eneo lenye thamani kubwa.

✓ Kujifunza na kutumia mbinu za kutengeneza fedha wakati wa kununua kiwanja au nyumba ya uwekezaji.

✓ Kuhusika kwenye ukaguzi wa nyumba au kiwanja unachotaka kununua.

✓ Kupewa ushauri wa jumla kuhusu uwekezaji katika ardhi na majengo kwenye eneo ulilochagua kuwekeza.

Gharama ya kujiunga na programu hii ni Tshs.100,000/=.

Vitabu Vya Uwekezaji Kwenye Ardhi Na Majengo.

Leo unaweza kupata vitabu vyangu 3 kwa Tshs 10,000 badala ya Tshs.22,000. Vitabu unavyoweza kupata baada ya kulipia kiasi hiki ni;

✓ Usimamizi Wa Uwekezaji Kwenye Ardhi Na Nyumba.

✓ Njia 120 Za Kutengeneza Pesa Kwenye Ardhi Na Majengo.

✓ Lugha Ya Kuzingatia Ya Viwanja Na Nyumba.

Vitabu vyote vitatu (3) unapata kwa Tshs.10,000 baada ya kulipia. Vitabu vyote vipo kwenye mfumo wa nakala tete.

Kundi La REAL ESTATE BEGINNERS.

Hili ni kundi la uanachama wa kulipia. Ni kundi ambalo ninatoa masomo ambayo hayapatikani popote kwenye mitandao yangu. Ukiwa mwanachama unapata nafasi ya kupata ushauri kutoka kwangu.

Ada ya uanachama ni Tshs.30,000 kwa miezi 6 na kwa mwaka mmoja ni Tshs.50,000 tu.

Rafiki yako,

Aliko Musa.

Mbobezi majengo.

Whatsapp; +255 752 413 711
 
Back
Top Bottom