Mbia anayejihami kwa nguvu kubwa, mara nyingi si Mbia salama

Crocodiletooth

JF-Expert Member
Oct 28, 2012
18,744
21,145
BAADHI YA VIFUNGU VILIVYOPO KATIKA MKATABA HUU.

1. TANZANIA HAIRUHUSIWI KUJITOA KWENYE MKATABA

Ibara ya 23(4) ya mkataba huo inakataza wahusika wa mkataba ambao ni serikali ya Tanzania na Kampuni mwekezaji DPW kujitoa(Denounce) katika mkataba, Kuvunja, Kuahirisha(suspend), au Kusitisha(terminate).

Na ni masikitiko sana kuwa ibara hii imesisitiza kuwa haturuhusiwi kujitoa kwenye mkataba huu hata kama kuna ukiukwaji mkubwa wa masharti(Material Breach), hata kama kuna mabadiliko makubwa ya kimazingira katika utekelezaji wa mkataba(fundamental change of circumstances), hata kama kuna mgogoro mkubwa wa kidiplomasia(severe diplomatic/condular dispute), au sababu zo,ote zile zinazotambulika na sheria za kimataifa.

2. MKATABA HAUNA MUDA

Ibara ya 23 ya mkataba inasema kuwa ukomo wa mkataba huu ni mpaka shughuli za mradi zitakapokuwa zimekamilika. Maneno haya yameandikwa hivihivi.

Serikali inawajibika kutoa maelezo kuhusu hili. Katika sheria hakuna mkataba usio na muda isipokuwa mkataba wa kuuza au kununua tu.

Ukimuuzia mtu kitu haumwambii tumia mpaka muda fulani, ni moja kwa moja. Je na huu mkataba ni hivyo ??.

3. MIGOGORO KUHUSU MRADI KUTATULIWA AFRIKA KUSINI.

Ibara ya 20 ya mkataba inasema migogoro kuhusu mkataba wa mradi utatatuliwa Johannesburg Afrika Kusini na Sheria itakayotumika ni sheria za umoja wa mataifa UNICITRAL Arbitration Rules.

Kumbuka mwaka 2017 tulitunga sheria yetu kwa ajili ya kulinda rasimali zetu.

Katika sheria hii The Natural Wealth and Resources , Parmanent Sovereignty Act 2017, tuliweka wazi katika kifungu cha 11 kuwa Migogoro yoye inayohusu Rasilimali za Taifa hili itatatuliwa na vyombo vya hapa nchini kwa sheria zetu.

Na hiii ilikuja baada ya kuonekana hawa wanaojiita wawekezaji wanatunyonya kisha tukilalamika wanatuburuza kwenye vyombo vyao tena kwa sheria zao.

Unamshitaki mtu kwenye mahakama yake mwenyewe kwa kutumia sheria alizotunga yeye mwenyewe, halafu unategemea upate haki.

Tulitunga sheria hii kujikomboa na huu ukoloni. Mkataba huu sasa unataka kuturudisha huko.

4. TANZANIA HAINA MAMLAKA YA KUTAIFISHA MALI ZA MWEKEZAJI.

Ibara ya 14 ya mkataba inakataa kabisa Serikali ya Tanzania kutaifisha mali yoyote ya mwekezaji.

Yaani hakuna sababu yoyote iwe ya kimadai au kijinai itakayoifanya serikali itaifishe mali ya mwekezaji.

Mnajua kuwa suala la kutaifisha lipo kisheria hasa inapothibitika jinai. Lakini hii si kwa mwekezaji wa Bandari.

Ibara hii inasisitiza kuwa endapo itatokea mali zao kutaifishwa na serikali basi fidia na stahiki ya kuridhisha italipwa na serikali. Neno STAHIKI YA KURIDHISHA limetumika hivyohivyo kwenye mkataba.

Hatujui hiyo ya kuridhisha itakuwa ni kiasi gani lakini limeandikwa hivyohivyo.

5. KUTUNGA SHERIA MPYA.

Ibara ya 27 inasema baada ya mkataba kusainiwa Tanzania haitakuwa na mamlaka ya kutunga sheria, kanuni mpya ambayo itapingana na mkataba.

Tafsiri yake, kama tuna marekebisho yetu ya kikodi, sera pengine kutokana namabadiliko na mda kupita hatutaruhusiwa.

MAANA YA MKATABA HUU NI KWAMBA HATA UTAKAPOONA YA HOVYO HOVYO UKAE KIMYA KAMA TUMBILI
 
Hivi wanaosapoti wameyaona na kuyasoma haya au ?? Naomba mnisaidie hio kopi ya huu mkataba plz 🙏
 
Haya ndiyo matokeo ya kuwa na Wabunge wengi wa Chama kimoja, hata wale ambao wanajua kuwa Mkataba huu ni wa hovyo wanaogopa kuongea kwa kuogopa kushughulikiwa, wachache sana ndiyo wameamua kujilipua lakini wakiwa nje ya Bunge.
 
Back
Top Bottom