Wakuu,
Mbezi Beach inasifika kuwa kuwa na wadosi watu wazito na viongozi mbalimbali hasa upande wa chini. Lakini kipindi hiki cha mvua Mbezi haitamaniki, barabara za ndani ni mbovu kupita maelezo, yaani utafikiri uko pale urafiki wanapouza kwenye soko la ndizi.
Kwa kwa jinsi Mbezi Beach inavyobeba watu watu wakubwa kweli wanashindwa hata kuweka lami mitaani, au hata kumwaga kokoto. Yaani wao na Mikocheni ni aibu nyakati hizi, au na huko wavamizi wa kwenye kwenye njia za maji wamejaa na sababu ni wadosi basi wanashindwa kuchukuliwa hatua?