Mbeya: Watiwa mbaroni kwa kuvunja ofisi ya kijiji na kuiba vifaa vya Mradi wa Umeme-REA

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
2,812
11,989
Jeshi la Polisi Mkoa wa Mbeya linawashikilia watuhumiwa wawili Bahati Geofrey (36) Mkazi wa Kiwira na Emmanuel Mtofu (33) Mkazi wa Karasha ambao wanatuhumiwa kuvunja Ofisi ya Kijiji na kuiba vifaa vya Mradi wa Umeme – REA.

Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga amesema awali mnamo tarehe 22.02.2023 majira ya saa 02:15 usiku huko maeneo ya Kitongoji cha Ishinga, Kata ya Swaya, Tarafa ya Ukukwe, Wilaya ya Rungwe, watuhumiwa walivunja Ofisi ya Kijiji na kuiba vifaa vya Mradi wa Umeme (REA) ambavyo vilihifadhiwa katika Ofisi hiyo.

Mara baada ya Jeshi la Polisi kupata taarifa, lilianza msako na kufanikiwa kuwakamata watuhumiwa na baada ya kufanya upekuzi kwenye makazi yao wanayoishi walikutwa na vifaa vya mradi wa umeme – REA vilivyoibwa katika ofisi ya Kijiji ambavyo ni:-
  • Pin Insulator 44,
  • Gun grip 66,
  • Disc Insulator 54,
  • Cross Arm Angle 15,
  • Bracket for Earth Master13,
  • Polymeric 22,
  • Top make off 22,
  • Stay wire mita 180,
  • Tension for U bolt 39,
  • Tension for Earth Master 26,
  • Danger Plate 70,
  • Socket Clevis 60,
  • Section Straps 10,
  • Tie Straps 02,
  • Eye bolt 13,
  • Stay Insulators 08,
  • Square washer 23, na
  • Bolt 71.
Jitihada za kujua thamani ya vifaa vyote zinaendelea. Aidha Polisi wamesema msako mkali wa watuhumiwa wengine ambao ni mafundi wa mradi huo unaendelea.
 
Back
Top Bottom