Mbeya Mjini: Kiboko ya Sugu 2015 ni Mbuzax

Mbeya Mjini: Kiboko ya Sugu 2015 ni Mbuzax

Mbuza ana phd sugu fom two kwanza ashukulu katiba ya 1977 inamuokoa tungetumia katiba inayotokana na rasimu hii jamaa hana chake mana rasimu inataka fom 4
 
Ivi nyie yan kwakua sugu alishinda basi mnajua nae uyo atashinda! Unadhan uchapakaz unapimwa kwa kuplomoti idadi kubwa ya show? Bora mumuache uyo sugu analeta changamoto kuliko icho kitu mnachotaka kuleta...alafu alikua anatafuta credit ivi alipata???
 
ivi nyie yan kwakua sugu alishinda basi mnajua nae uyo atashinda! Unadhan uchapakaz unapimwa kwa kuplomoti idadi kubwa ya show? Bora mumuache uyo sugu analeta changamoto kuliko icho kitu mnachotaka kuleta...alafu alikua anatafuta credit ivi alipata???

kweli jambo tusilo lijua ni sawa na usiku wa giza
 
Huyo mbuza hadi sasa ana phd we unaongelea credit uliza watu wa mbeya hakuna sehemu ambayo sugu utamfananisha na mbuza kwa mbeya,mbuza ana mchango mkubwa hadi kwenye muziki wa sugu
 
Unajua sugu amejazwa ujinga na neno moja tu RAIS WA MBEYA ambalo nalo lina nguvu kwa watu walio nje ya mbeya,ukweli ni kwamba sugu mbeya hana nguvu ambayo nje ya mbeya wanampa sugu ndani ya mbeya ni MZIGO tena mkubwa sana,na mara nyingi akiwa jukwaani ndani ya mbeya huwa anasema atagombea udiwani ili aje agombee umeya wa jiji ukweli chadema lazima wafanye kitu kunusuru jimbo la mbeya mjini nje ya hapo tutaongea mambo mengine
 
sugu ni zaid ya mbunge ndani ya mbeya city utake us'taje lazima ukae!
 
Amgekuwa zaidi ya mbunge si angekuwa anajaza watu kwenye mikutano yake ndani ya mbeya kama wakina lema kule arusha yeye mpaka Dr slaa aje ndio anakuwa anakubalika HATUMTAKI HATA KWA BURE
 
nimeseme msafwa katika maana ya uzawaa sio kama ni kigezo chakuonyesha ukabila ila kwa ivo ipo wazi hapa nchi yetu kua mzawa ndo anapewa nafasi na watu kumuamini jimbo lazima lirudi kwa mnyakyusa au msafwaa
Nimezaliwa Iyunga,nimesoma Mabatini primary na mimi kabila langu ni mojawapo ya kabila kubwa Mbeya,sidhani kama huyo mtu wako unayempigia debe atachaguliwa na WASAFWA peke yao,ilhali unajua ni wasafwa wachache waliopo Mbeya mjini waliojiandikisha kupiga kura,wapiga kura wengi wa jimbo la Mbeya mjini si wazaliwa wa Mbeya mjini,na hii si Mbeya ni katika majiji yote.Sasa ungekuja na hoja za maana za kwanini huyo MSAFWA wako anafaa ,lakini kwako naona ni ukabila ndo unakutia hofu.Mbeya tuliwahi kuwa na wabunge wasafwa,wamefanya nini? Chagua mtu na sera zake sio USAFWA.
 
Mi nimemuelewa mleta mada amejaribu kumuelezea huyo mbuza kwa ujumla wake usafwa sio issue ni sawa na kusema sugu mkinga sio kosa ila safari ijayo lazima mbunge wa mbeya atoke kati ya mnyakyusa au msafwa kwa majimbo mengine yaongozwe na makabila ya mkoa hao mbeya mjini ndio mseme ukabila uachwe hilo ni angalizo hata kwa chama chadema
 
Nani kakudanganya wasafwa ni wachache ndani ya jiji la mbeya huko ni kujidanganya na kutaka kupindisha mada hii
 
Hata mimi niko huku huku lakini huyu bwana sija wahi kumsikia nadhani ndo anafanya promo hata hii thread labda kajianzishia mwenyewe.You never know.

huyu bwana alikuwa ni promota wa miziki ya bongofravor na anamiliki redio kwa sasa ila uwezo wake wakuongoza jimbo ni mdogo halafu kwa ushindani wa mbeya hawezi hata kidogo.
 
Unaesema uwezo wake mdogo humjui mbuza wewe uchaguzi si mwakani kwa nini tuandikie mate sugu hatakiwi
 
Hatakiwi wakati vijana wa mbeya ndio mwokozi wao 2015,hatuwezi kuwa na mbunge mvuta bangi sugu ukimuona kwenye gari lake yupo na wahuni watupu utafikili ni Wu tang clan wanapita
 
nimeseme msafwa katika maana ya uzawaa sio kama ni kigezo chakuonyesha ukabila ila kwa ivo ipo wazi hapa nchi yetu kua mzawa ndo anapewa nafasi na watu kumuamini jimbo lazima lirudi kwa mnyakyusa au msafwaa
Bado hujajibu hoja.
Mzawa wa Mbeya anaweza kuwa Mhaya, Mkinga, Muha, Msukuma, Mngoni, Mhehe etc, provided amezaliwa na kukulia hapo au ameishi hapo kwa kipindi kisichopungua miaka mitano. Sifa mojawapo ya mbunge ni kukaa mahali kwa muda usiopungua miaka mitano mfululizo. Muda huu ndio unaoainishwa katika katiba. Suala la makabila halina nafasi kwenye ubunge. Sugu ni Mkinga lakini ni mbunge wa Mbeya kutokana na ukaazi. Deo Sanga (Jah People) wa Makambako ni Mkinga, ni mbunge kwa sababu anaishi hapo, si kwa sababu uya Ukinga wake, kwa sababu lile ni eneo la Wabena kiasili.
Kwa mantiki hii basi, huyo 'mbunge' mtarajiwa uliyemtaja hapo juu anatakiwa kuwa mkaazi wa Mbeya kwa muda usiopungua miaka mitano kabla ya uchaguzi, wala sio kwa sababu ya Usafwa wake, wala Ukinga Wake wala Unyiha wake, wala Ungoni wake.
Nawasilisha
 
mkuu sugu ni mngoni cyo mkinga
 
Back
Top Bottom