Mbeya: Mdude Nyagali apatikana akiwa hai baada ya kupotea kwa siku 4

Welcome back bro Mdude ila yule aliyesema kapelekwa kambi ya jeshi Dar sijui naye nani... kumbe kapatikana Mbeya hukohuko... kweli mbongo mpe picha tu mengine yote anamaliza mwenyewe...bila kelele za umma asingepatikana huyu chalii
Kwani Dar na Mbeya kuna umbali gani kwa muda wa siku 4 mtu umeenda marekani na kurudi.
 
Mwanamke humjui Mdude lakini habari hii inakuuma, ni uchawi wa aina gani? Unaenda kulala saa 6 hii na kinyongo moyoni ukijiuliza sababu ya msingi huna.
 
Sasa hao waliokua wanasema ameletwa dar habari wamezipata wapi. Huyu bila shaka kajiteka kama nondo mpango ukiwa kuwapatia wapinzani tukio kufanya siasa wanazojua.
Tumuogope MUNGU Jamani!!!. Hivi wewe utaishi Mpaka lini?. Kumbuka Dunia Mapito. Hebu tuwe na HURUMA.
 
Kinachosikitisha wapo vijana waliokuwa wanaandika vitisho kwa mdude na hatusikii hatua zozote walizochukuliwa
 
One last chance. Akizingua tena itakula kwake.

Awe smart this time around. Akosoe kwa akili. Aachane na harakati zinazomuumiza na kuwaumiza wampendao.

Sasa afanye harakati zitakazompa heshima ya kweli na recognition huko duniani kama akina Rebeca Gyumi. Sio hizi za kuvuna likes, comments na mateso!
Last chance? wanaweza kutangulia wao wakamuacha Mdude na harakati zake. Mungu si Athuman.
 
Pole yake.
IMG_20190509_005421.jpeg
 
Heshima kwenu wakuu,

View attachment 1092268

Taarifa za awali zinathibitisha kuwa Mdude Nyagali amepatikana akiwa hai, sema kapigwa sana. Hawezi kutembea wala kujipandisha kwenye bajaji. Utaratibu wa kupelekwa Hospitali apewe huduma ya kwanza unafanyika.

Mdude amepatikana katika Jimbo la Mbeya Vijijini kata ya Inyara Kijiji cha Makwenje kitongoji cha Mwasho.

Taarifa hizi za awali zimethibitishwa na Diwani wa CHADEMA mkoani humo, Kissman Mwangomale.

Siku ya Jumamosi Tarehe 4 Mei 2019, Mwanaharakati na Mwanachama wa CHADEMA, Mpaluka Said Nyagali (Mdude Chadema) alivamiwa kisha kuchukuliwa na watu ambao hawakutambulika wenye Silaha za moto, akiwa ofisini kwake, eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, katika tukio lenye dalili za utekaji.

Zaidi, soma;



Stay tuned
hii ni habari njema...
 
Naomba mungu apone ili awataje waliomteka huyu anaweza siyo kama wale waliotekwa kabla yake hadi leo kimya wala hatujui kilichowakuta
 
However, Mungu ndiye anayetawala milele tu, wengine wote wanapita na hata historia zao zitabaki kwenye vitabu vya hukumu vya Mungu tu, kwa ushetani wao wautendao.
 
Back
Top Bottom