Mbeya: Mdude Nyagali apatikana akiwa hai baada ya kupotea kwa siku 4

figganigga

JF-Expert Member
Oct 17, 2010
16,854
2,000
Heshima kwenu wakuu,

C200B541-B702-4D3E-B7A3-A036C0834FAF.jpeg


Taarifa za awali zinathibitisha kuwa Mdude Nyagali amepatikana akiwa hai, sema kapigwa sana. Hawezi kutembea wala kujipandisha kwenye bajaji. Utaratibu wa kupelekwa Hospitali apewe huduma ya kwanza unafanyika.

Mdude amepatikana katika Jimbo la Mbeya Vijijini kata ya Inyara Kijiji cha Makwenje kitongoji cha Mwasho.

Taarifa hizi za awali zimethibitishwa na Diwani wa CHADEMA mkoani humo, Kissman Mwangomale.

Siku ya Jumamosi Tarehe 4 Mei 2019, Mwanaharakati na Mwanachama wa CHADEMA, Mpaluka Said Nyagali (Mdude Chadema) alivamiwa kisha kuchukuliwa na watu ambao hawakutambulika wenye Silaha za moto, akiwa ofisini kwake, eneo la Vwawa, Mbozi, mkoani Songwe, katika tukio lenye dalili za utekaji.

Zaidi, soma;Stay tuned
IMG_20190509_080024_528.jpg
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom