Mbeya: Mahakama imeahirisha kusoma hukumu ya Mdude Nyagali hadi Juni 28, 2021

Sanyambila

JF-Expert Member
Jan 24, 2018
339
457
Kwa muda huu saa10:30 asubuhi msafara wa mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe umewasili hapa katika viwanja vya Mahakama Kuu Mbeya kusikiliza hukumu ya mwanachama wao Mdude, ambaye alishitakiwa kwa makosa ya madawa ya kulevya, uhujumu uchumi nk

Wafuasi wa CHADEMA wamewasili hapa tangu saa 2 asubuhi na kukaa makundi makundi

Lakini mshitakiwa Mdude amewasili hapa katika viwanja vya mahakama mnamo saa tatu 3 akiwa chini ya ulinzi mkali na aliingizwa mahakamani na kupumzishwa kwenye chumba maalum akisubiri kesi yake kuitwa hizi ni picha.

Hizi ni picha za hali halisi mahakani hapa hapa.

=========

Mahakama ya Hakimu Mkazi Mkoa wa Mbeya imeahirisha kusoma hukumu ya kesi ya kada wa Chadema, Mdude Nyangali iliyokuwa itolewe leo Jumatatu Juni 14, 2021.

Hakimu mfawidhi wa mahakama hiyo, Zawadi Laizer amesema ameiahirisha kutokana na sababu zilizo nje ya uwezo wake na kubainisha kuwa hukumu hiyo itasomwa Juni 28, 2021.

Mdude anakabiliwa na shtaka la kusafirisha heroin gramu 23.4 mwaka 2020.

Akizungumza nje ya mahakama mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe amewataka wafuasi wa chama hicho kuwa watulivu mpaka tarehe iliyopangwa.


PIA, SOMA: Hukumu ya Mdude Nyagali ni leo 14|06|2021

Md 1E.jpg

Md 5E.jpg

Md 4E.jpg

Md 6E.jpg

Md 3E.jpg


IMG_20210614_115952.jpg


IMG_20210614_115943.jpg


IMG_20210614_115934.jpg

1623666242320.png
 
Mungu wa Ibrahim na Yakob na amsimamie - tunajua kosa lake ilikuwa ni kumkosoa mtukufu ndiyo kupewa haya makosa makubwa ili kumnyamazisha ili iwe funzo kwake yeye na wengine.
Wewe hakimu?
 
Back
Top Bottom