masopakyindi
Platinum Member
- Jul 5, 2011
- 17,882
- 13,172
"Jiji" la Mbeya ni 90% squatters.
Hata aliyekuwa mkuu wa mkoa wakati fulani Mateo Qares, aliliita jiji la Mbeya kijiji kikubwa.
Sehemu ambayo imepimwa vizuri jiji la Mbeya ni lile la mkoloni, Uzunguni, Ghana, Soko Motola(alikofikia Mandela) na Majengo na mjini kati.
Lakini sehemu ambazo kuna watu wengi zaidi kama Mwanjelwa, Mafiati, Isyesye, Mabatini, Nzovwe na sehemu nyingi hali ni mbaya sana.
Dr. Tulia sasa tunakutegemea kuanzisha mpango kabambe utakaowezesha kuchonga barabara kati kati ya hizo squatters. Ofcourse lazima watakaobomolewa inabidi walipwe fidia.
Hili lazima lifanyike sasa, maana 50 years later ndio mafanikio yataonekana.
Magufuli ametuonyesha hili, hapo Kimara-Kibaha.
Dr. Tulia hili ukifanya litakumbukwa kwa miaka mingi.